Quantcast
Channel: Makala – ShaffihDauda
Viewing all 676 articles
Browse latest View live

TFF Inapojitekenya na Kucheka Yenyewe

$
0
0

NA ABDUL DUNIA

Tumeshazoea kuwaona watoto wadogo wakicheza michezo tofauti kila kukichwa ikiwemo kujitekenya na kucheka wenyewe. Tunaona kawaida kwa kuwa ni watoto.

KITENDO cha Mtu mzima kujitekenya na kucheka mwenyewe kinaweza kuonekana kama ni mzaha lakini inawezekana kwenye maisha ya kila siku. Sio tu kwa wale watoto wadogo tunaokutana nao mitaani na hata majumbani kwetu.

Nadhani sijakosea naposema Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limeamua kujitekenya na kucheka lenyewe kuhusiana na hili la Kamati ya Saa 72 na ile ya Katiba. Hakuna asiyefahamu hilo.

Hivi Karibuni, Kamati ya Saa 72 iliyoongozwa na Hamadi Yahaya iliipa pointi tatu Simba baada ya kubainika beki wa Kagera Mohammed Fakhi alicheza akiwa na kadi tatu za njano ambazo alizipata kwenye mechi dhidi ya Majimaji, Mbeya City na African Lyon.

Siku chache zilizopita, Kamati ya Katiba, Sheria na Hadhi za Wachezaji chini ya Katibu Mkuu wa TFF, Celestine Mwesigwa ilitoa kauli ya kuwa pointi hizo zilitolewa kimakosa na kurudishwa kwa Kagera. Halikuwa tatizo ni kawaida ya rufaa kukubaliwa ama kukataliwa.

Tatizo ni uamuzi mara mbili uliofanya vichwa vya Watanzania, Mashabiki wa Simba, Yanga na Kagera kutaharuki kutoka na majibu hayo. Kuna pande iliyofurahi nyingine kuhuzunika na nyingine pia kukata tamaa juu ya soka la Tanzania.

Pande hizi zimegongana, TFF imegongana na Bodi ya Ligi imegongana. Kamati ile ya Yahya, Mwesigwa (Katibu) na Malinzi (Rais) pamoja na ile ya Bodi ya Ligi inayoongozwa na Wambura zote zimepishana na uamuzi wao.

Naanza kupata picha ya yule aliyesema kuwa Hakuna watu wanafiki kama wale tunaojiita watu wa Soka au Familia ya Soka. Naungana naye mkono mtu yule. Tuje kwenye Hoja Kuu.

Sipo hapa kuitetea Kagera, Simba, TFF wala Bodi ya Ligi bali nipo hapa kueleza ule ukweli niliouona juu ya zile Kamati zetu zinazoongozwa na Watu tunaojiita ama kuitwa Familia ya Soka.

FAKHI alikuwa na Kadi tatu za Njano (Kwa Sauti ya Mwesigwa). Kwa Mantiki hiyo Kanuni ya Usimamizi na Uendeshaji wa Ligi Tanzania inasema kuwa Mchezaji atakayebainika kuwa ana kadi tatu za njano kwenye michezo mitatu mfululizo na akacheza wa nne, timu yake itapokwa pointi na kupewa timu pinzani.

Mchezaji atakayebainika ana kadi tatu za njano hakuna rufaa itakayotendeka badala yake Bodi na Shirikisho lenyewe litatoa ufafanuzi juu ya hilo.

MSIMU uliopita Azam FC ilipokwa pointi 3 na kupewa Mbeya City baada ya kumchezesha beki wake

Erasto Nyoni aliyekuwa na kadi tatu za njano. Mbeya City haikukata rufaa. Bodi na TFF zilitoa adhabu hiyo baada ya kugundua hilo. Hapo ndipo Tatizo lilipoanzia.

Simba imepokwa pointi walizopewa awali kwa hoja tatu thabiti kutoka TFF ambapo ya Kwanza ilikuwa ni Rufaa kuwasilishwa nje ya muda. Hakuna rufaa kwenye kadi tatu za njano. Bodi na TFF zililazimika kutoa ufafanuzi mbali na rufaa ya Simba. Ni wajibu wao.

Kama Rufaa iliwasilishwa nje ya muda kwanini Kamati halali ya Saa 72 ilikaa? Walipata wapi taarifa, nani aliidhinisha uwepo wa kikao hicho na posho zake?

Kama rufaa ilichelewa ilitakiwa kutupiliwa mbali. Haikutakiwa kusikilizwa kabisa. Kamati ilikaa, wajumbe walialikwa, TFF wakatoa fedha za kugharamia kikao na kulipa wajumbe posho, leo inakuwaje rufaa kucheleweshwa? bila ya kupepesa macho kuna ubabaishaji hapa.

Hoja ya Pili ilikuwa ni Rufaa kutolipiwa Ada au Pesa. Kwa kawaida rufaa isipolipiwa haipaswi kusikilizwa inakuwa sio halali tena ‘Invalid’ (Haijatimiza viwango vya kuwa Rufaa). Zipo nyingi zilitopiliwa mbali ikiwemo ile ya Polisi Dar. Kwa nini hii haikutupiliwa mbali kama ile na kuamua kuijadili?

Hoja ya Tatu, Kamati ya Saa 72 kualika wajumbe kutoka nje ya TFF na Bodi ya Ligi. Kama ni kweli Kamati ya saa 72 ilialika wajumbe kutoka nje kimakosa je, Kamati ya Katiba, Sheria na Hadhi za Wachezaji iliyotengua uamuzi ya ile Kamati ya Kwanza imetoa pendekezo la kuvunja kamati hiyo ili makosa ya namna hiyo yasijirudie tena baada ya kuundwa kwa Kamati mpya? Sijui labda tusubiri.

Turudi nyuma kidogo, Kagera Sugar hawakuandika barua ya kulalamika juu ya Simba kuwasilisha rufaa nje ya muda, Kutolipia Ada Rufaa yao na Uhalali wa ile Kamati ya Saa 72.

Waliandika Barua kupinga kuwa Fakhi hakuwa na kadi tatu za njano, je, Fakhi alikuwa na kadi au hakuwa nazo? Hiyo ndiyo pointi ya msingi kujadiliwa kwenye Kamati.

Sihitaji kuzungumza sana, ngoja niweke akiba ya maneno yangu. TFF ilihitajika kutoa uthibitisho juu ya kadi tatu za Fakhi na kama kweli alikuwa na kadi tatu kama ilivyosema ile Kamati ya Kwanza basi Simba ilikuwa na uhalali wa kupewa zile pointi walizopewa hapo awali bila ya kukata rufaa.

Kwenye hili la Fakhi na kadi za njano. Naamini sijakosea naposema TFF inajitekenya na Kucheka yenyewe.

Sidhani kama Fakhi alikuwa na hizo kadi, maana navyoifahamu Ligi yetu ingekuwa kweli anazo basi uamuzi wake usingechukua siku nyingi. Ungekuwa ni sawa na kumsukuma mlevi kwenye mtaro wa Maji.

 


James Kotei na Kivuli cha Athumani Iddi ‘Chuji’

$
0
0

NA ABDUL DUNIA

HUWEZI kuwataja viungo watano bora wa miaka yote kwenye klabu ya Yanga bila ya kulitaja jina la Athumani Iddi ‘Chuji’.

Chuji ni moja ya viungo bora wakabaji kuwahi kutokea Tanzania na Afrika Mashariki na Kati. Ubora wake, kujituma na bidii alizozionesha uwanjani ndizo zilizomfanya aonekane bora kila siku.

Sahau kuhusu umri wake, kiungo huyu wa ulinzi na amepitia vipindi vingi vigumu katika maisha yake ya soka lakini alihakikisha anaonyesha kiwango cha hali ya juu kwenye klabu zake alizozitumikia hususani Yanga.

Alianza soka katika timu ya Polisi Dodoma, 2005, Chuji alitokea kuwa mlinzi bora wa kati katika soka la Tanzania, alikuwa akipata nafasi ya kucheza mara kwa mara katika timu ya taifa ya vijana ‘ Serengeti Boys’ mwaka huo, akitokea timu za nje ya Dar es Salaam.

Kupata nafasi ya moja kwa moja katika timu ya taifa ukitokea mkoani, bila shaka wewe utakuwa mchezaji ‘usiyegusika’ popote pale nchini.

Polisi Dodoma ndiyo timu iliyomfanya Chuji akaonekana kuwa mchezaji bora na kuanza kucheza klabu kubwa nchini.

Namba sita mwenye sifa za utulivu, mpangaji mzuri wa ngome na kiongozi mwenye kujiamini, ni sifa ambazo zilimfanya Chuji kusajiliwa na Simba, kwa ajili ya msimu wa mwaka 2006.

Chuji,  aliingia Simba na kukuta wachezaji wengine wazuri kama yeye. Katika nafasi ya ulinzi wa kiungo wa kati ambayo alikuwa akicheza katika timu ya Polisi Dodoma, ndiyo alicheza nayo Simba.

Chuji, alitumia mwanya wa matatizo ya kinidhamu yaliyopelekea baadhi ya wachezaji muhimu kuwa kando ya timu. Costa, hakuwa na maelewano mazuri na kocha Neidor dos Santos, hapo ndipo Chuji alipata nafasi ya kuonesha kile atakacho.

Dos Santos, alipendezwa na viwango vya wachezaji vijana wakati huo, Chuji, Henry Joseph na Kelvin Yondan na akaamua kuwapatia nafasi ya kudumu kikosini hapo.

Soka la uhakika akicheza katika idara ya kiungo kwa dakika 120 lilimtambulisha kiungo, mwenye mapafu ya ‘ mbwa’ katika soka la Tanzania.

Chuji alihamia Yanga huku mashabiki wa Simba wakimtupia lawama nyingi na kumuangushia laana za kila aina lakini Chuji aliongeze kiwango zaidi ya kile.

Chuji alikuwa tishio anapokutana na Simba kwenye uwanja wa Taifa, alikuwa na vita uwanjani alipokutana na swahiba wake Haruna Moshi ‘Bobani’ na Juma Nyoso.

Chuji alikuwa tegemezi la Yanga na timu ya Taifa ‘Taifa Stars’ iliyokuwa chini ya kocha Marcio Maximo wakati huo. Kila kipindi kina nyakati zake, Chuji ameshamaliza nyakati zake.

Hakuna shabiki wa soka Tanzania kwa sasa asiyemfahamu kiungo wa Simba, Mghana James Kotei kutokana na uwezo wake wa kuukata umeme wa wapinzani unapowaka langoni mwao.

Kotei anacheza kama Chuji, anakaba, anashambulia na anacheza zaidi ya nafasi moja uwanjani. Anaweza kucheza kama kiungo mkabaji, kiungo wa kati na hata beki wa mwisho kwa wakati mwingine.

Kotei akicheza kama kiungo mkabaji anacheza vyema, kiungo wa kati anacheza vyema na akicheza kama mshambuliaji wa kati pia anacheza vyema pia.

Kotei alionyesha kiwango cha hali ya juu kwenye mchezo dhidi ya Yanga uliochezwa Februari 25, mwaka huu pale kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Alianza kucheza kama kiungo wa kati alitibua mipango ya Niyonzima na kumuondosha nje Kamusoko. Pia alicheza kama beki wa kati na alifanikiwa kupoteza ndoto za Chirwa na Msuva.

Hivyo ndio mchezaji kiraka anatakiwa awe, Chuji alikuwa akicheza zaidi ya nafasi moja kama Kotei anavyocheza sasa. Simba haina hofu tena kwa kuwa ina mtu anayehakikisha lango lao halikai wazi.

Kotei alionyesha kiwango cha hali ya juu kwenye mchezo uliochezwa hivi karibuni dhidi ya Mbao. Alisaidia timu yake kupata ushindi wa mabao 3-2 wakitokea nyuma ya mabao mawili.

Kotei alikuwa mmoja kati ya wachezaji watatu waliofunga bao moja kwenye mchezo wa huo uliochezwa kwenye uwanja wa CCM Kirumba mkoani Mwanza.

Kotei amekuwa muhimili muhimu sana kwenye kikosi cha kocha wao, Joseph Omog kwenye kikosi cha Simba na baadhi ya mashabiki wameanza kumfananisha na kiungo wa zamani wa klabu hiyo Mkongo Patrick Mafisango.

Mafisango alikuwa kiungo mahiri kwenye klabu ya Simba ambapo aliisaidia klabu yake kupata ushindi wa mabao 5-0 dhidi ya Yanga na kufanikiwa kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara mwaka 2011.

Mafisango alifariki kwa ajali ya gari mwaka 2012 akitokea kwenye ukumbi wa starehe unaofahamika kwa jina la Dar Live uliopo Mbagala, Dar es Salaam.

AL OROUBA SC

Msimu uliopita alicheza kwenye klabu ya majaribio kwenye klabu ya Al-Orouba inayoshiriki Ligi Kuu ya Oman.

Akiwa amesajiliwa Orouba SC ya Oman, Mchezaji huyo alifanikiwa kucheza mechi nane za Ligi Kuu nchini humo.

Kotei ameanza kuwasahaulisha machungu mashabiki wa Simba baada ya kuondokewa na Chuji miaka 8 iliyopita.

 

Baada ya kuwanyoosha Zenji, Himid ana haya ya kuwaambia Simba

$
0
0

Azam FC wamekuwa klabu gumzo sana katika siku za usoni, aina ya wachezaji walionao pamoja na uwekezaji ndani ya klabu hiyo, kuelekea pambao la Simba na Azam mtandao huu ulifanya mahojiano na kiungo wao mkabaji Himid Mao.
Kwanza nilitaka kujua kuhusu Mao anauchukuliaje mchezo kati yao dhidi ya Simba ambapo alisema “Simba ni timu kubwa kama ilivyo kwetu sisi na mechi itakuwa ngumu sana kutokana na ukubwa wa timu hizi mbili, haitakuwa mechi rahisi”.

Kwa siku za karibuni Azam wamekuwa wakiisumbua sana Simba ambapo mchezo wao wa mwisho Azam waliifunga Simba katika ligi kuu ya Tanzania na Himid bado anaona Simba itakumbana na upinzani kutoka kwa Azam.
Mao aliulizwa kuhusu ubora wa kikosi cha Simba ambacho wachezaji wa nje kama Laudit Mavugo, James Kotei wamejenga kikosi imara wakishirikiana na wazawa kama Kichuya, Ajib, Mkude na wengineo.
Mao aliambiwa achague wachezaji watatu kutoka kwa wapinzani ambapo alijibu, “Mimi siangaliagi mpira na sijui kuhusu wachezaji wa timu nyingine japo nina marafiki Simba, huwa naangalia kikosi chetu na naamini tutaibuka kidedea dhidi ya Simba”

Mao amesema japokuwa kocha aliyepo Simba kwa sasa Mcameroon Joseph Omog anaijua sana Azam lakini hiyo haitawazuia kuwafunga wekundu hao wa Msimbazi kama walivyofanya mara ya mwisho walipokutana.

Himid ambae anaukumbuka sana msimu wa mwaka 2012 mechi waliyoifunga Simba bao tatu uwanja wa taifa amesema kikosi chao kipo tayari kuwakabili Simba.
Mwisho Shaffihdauda.co.tz ilitaka kujua kuhusu inakuwaje yeye yuko bize na msichana wake wakati timu iko katika maandalizi ya pambano gumu dhidi ya klabu ya Simba ambapo Himid alijibu kama ifuatavyo.
Kwanza yule sio msichana wangu, ni mke wangu wa ndoa na ieleweke hivyo na kuhusu kukaa naye naweza kaa naye muda wowote, picha zinahifaziwa kwenye simu na kupost picha haimaanishi umepiga hapo hapo” alimalizia Himid

Shaffih Dauda: Kikosi changu bora cha Simba na Azam 

$
0
0

Kuelekea pambano la nusu fainali kati ya Simba na Azam, mchambuzi mkongwe wa masuala ya soka Tanzania Shaffih Dauda ametaja kikosi chake bora.
Shaffih ametaja kikosi cha wachezaji anaowaona bora ambao walizichezea timu zote mbili kwa nyakati fulani na wengine wamestaafu soka huku wengine hawapo timu yoyote kati ta hizo mbili.

Golini Shaffih ameamua kumuweka golikipa wa Yanga Deogratius Munishi “Dida” ambaye kabla ya kutua Yanga ameshawahi kuzitumikia Azam na baadae Simba.

Beki wa kushoto ni Mohameid Hussein wa Simba ambaye alikulia wakati flani katika timu ya Azam, huku mlinzi wa kulia ni Shomari Kapombe ambaye sasa yuko Azam lakini hapo kabla alikuwa Simba.

Walinzi wa katikati yupo mkenya Owino na beki wa zamani wa Simba na timu ya taifa ya Tanzania Boniface Pawasa ambaye kwa sasa amestaafu kucheza soka.

Katika mfumo wa Shaffih ambao ni 4 – 3 – 3 katikati ameweka viungo watatu ambapo kiungo wa katikati ni marehemu Patrick Mafisango akizungukwa na Seleman Matola na Shekhan Rashid.

Mbele yao viungo hao kuna washambuliaji watatu ambao wanaongoza na Mrisho Ngassa ambaye kwa sasa anakipiga Mbeya City huku kushoto kwake yupo Ramadhan Singano na kulia yuko Ramadhan Redondo

Upande wa kocha, Shaffih hakusita kumuweka kocha Mcameroon ambaye kwa sasa anaifundisha klabu ya Simba lakini hapo awali aliwahi kuwafundisha Azam Fc Joseph Omog.

Mbeya City Wanavyowashangaa Yanga Na Michango Yao.

$
0
0

ATHUMAN BEMELENGO
0713 094952

Kuna ujumbe nilikutana nao katika mitandao ya kijamii siku za hivi karibuni. Ukiusoma unafurahisha sana lakini umebeba ujumbe mzito sana. Unasema wakati mwanamuziki Diamond Platnumz amefanya hafla kubwa ya kuzindua biashara yake inayofahamika kama CHIBU PERFUME ambayo inauzwa shilingi laki moja na elfu tano (105000) kuna klabu kubwa hapa  nchini zimeshindwa kuweka utaratibu mzuri wa kujipatia hata 20000 kutokana na mauzo ya jezi za mastaa wao.

Maisha ndivyo yalivyo, kupanga ni  kuchagua. Diamond ameamua kuisimamisha Brand yake na wengine wameona kuwarudia wananchi wawachangie ndiyo maisha wanayostahili. Diamond huyu ameamua kuingia kwenye ulimwengu mwingine tofauti na ule wa muziki. Ulimwengu wa kibiashara ambao unahitaji watu makini wanaoweza kuifanya biashara kusimama bila kuyumba. Sio kazi rahisi kama unavyoweza kufikiri unapoitazama ukiwa nje.

Hata kama atakuwa anakutana na changamoto za hapa na pale ila kitu alichokifanya ni kikubwa sana. Ubunifu wa aina hii ndio unaompa Cristiano Ronaldo jeuri ya kumiliki ndege binafsi na kuiishi dunia vile atakavyo. Alishindwa Ngassa, Msuva nae licha ya kuwa na uhakika wa kukutana na mashabiki zaidi ya milioni kumi kwa mwaka bado anahisi hili ni kubwa sana kwake.

Kwa mazingira ya soka letu inawezekana suala hili likawa gumu kwa wachezaji wetu lakini hawana budi kubadilika maana dunia nayo imebadilika. Ni aibu sana mchezaji wa kizazi cha dunia ya leo kuishi katika dunia aliyoishi Sunday Manara au Athuman Machupa.

Sawa inawezekana wachezaji wanahofia ukubwa wa Brand zao lakini vipi kuhusu klabu nazo? Bado nazo zinahofia kuhusu ukubwa wa Brand? Ukitafakari vizuri utakubaliaana na mimi hiki sio kikwazo kwa klabu zenye idadi kubwa ya mashabiki kama hizi za Kariakoo.

Kama umeweza kuamini watu wanaweza kukuchangia fedha bure unashindwaje kuwatumia watu hao hao kuwa sehemu ya mtaji au soko lako? Mpaka hapo unaweza kuamini na mimi tatizo kubwa linaloukwamisha mpira wetu kupiga hatua ni watu wanaouongoza mpira wenyewe.

Rasilimali watu ni kitu muhimu sana katika mustakabali wa maendeleo ya sekta yoyote. Ulishawahi kujiuliza kuwa Yanga wangeweza kuachwa na ndege nchini Algeria kama wangekuwa na mtaalamu wa masuala ya Logistics? Bila ya kuwa na watu sahihi unaweza kuwa na kila kitu lakini bado usifanikiwe.

Nairejea kauli ya Zeben Hernandez aliyekuwa kocha wa Azam fc wakati anaondoka alisema uwekezaji mkubwa bila watu sahihi ni sawa na bure. Wanasema unapoona mdogo anamzidi mkubwa kwa busara na maarifa basi huitaji kufikiri sana kugundua hapo kuna tatizo.

Mbeya City anazidi kuyafanya tuliyotarajia kuyaona yakifanywa na kaka zake siku nyingi zilizopita. Licha ya uchanga wao lakini wanaamini tayari nembo yao ni Brand inayoweza kuwapa fedha kutoka kwa wadhamini na kuwaondoa katika kundi la omba omba.

Mbeya City wametangaza rasmi wamesaini mkataba wa udhamini na kampuni ya vifaa vya michezo ya Sports Master. Udhamini huo utaifanya kampuni hiyo kuwa mtengenezaji na msambazaji mkuu wa vifaa vyote vya michezo vitakavyokuwa vinatumiwa na klabu ya Mbeya City katika kipindi chote cha miaka miwili ya mkataba huo.

Hii ina maana kuwa mbali na timu hiyo kunufaika na vifaa vya michezo vitakavyokuwa vikitengenezwa na kampuni hiyo pia itakuwa imeongeza chanzo kingine cha mapato kwa sababu kampuni ya Sports Master watalazimika kuilipa Mbeya City kutokana na nembo yao kuonekana kwenye jezi ya klabu hiyo.

Hii ni aina mojawapo kati ya zile aina za udhamini wa kwenye jezi ambapo makampuni mbalimbali ya Marekani na Ulaya kama Adidas na Nike huzilipa klabu kubwa fedha nyingi kwa ajili ya udhamini huu.

Kwa sasa Manchester united ndio wanaoongoza kwa kuingiza kiasi kikubwa cha fedha kutokana na udhamini huo ambao wanaingiza kiasi cha Pauni milioni 75 kwa mwaka za Adidas wakifuatiwa na Chelsea watakaokuwa wakiingiza kiasi cha Pauni milioni 60 za Nike kwa mwaka kuanzia msimu ujao. Ni hatua kubwa sana waliyopiga kama klabu kwa sababu wanaweza kuwa wameonyesha mfano kwa kuwa klabu ya kwanza Tanzania kufanya hivyo. Ndio wameweza.

Unafikiri Mbeya City wana nini cha kuwapa shavu kama hili zaidi ya viongozi makini? Ndugu zetu wa Kariakoo wanalitambua hili? Yupo mmoja anavaa jezi zinazotengenezwa na makampuni ya Nike na Kelme na mwingine akivaa zilizotengenezwa na kampuni ya Uhlsport.

Nisaidie hapa Je, klabu zinanufaika na chochote kutoka kwenye makampuni hayo kwa kuzitangaza nembo zao? Jibu la swali hili ni jepesi sana, kama kinapatikana basi kinaishia tusikokujua mimi na wewe. Mbeya City wameonekana kuwa makini sana kwa namna wanavyoingia katika masuala haya ya kibiashara.

Ukiachana na aina hii ya udhamini wa jezi ambao klabu hunufaika kutokana na kutangaza makampuni ya utengenezaji wa vifaa vya michezo, pia kuna aina nyingine ya udhamini kupitia kwenye jezi ambapo klabu inaweza kuwa na wadhamini kadhaa kati ya mmoja au zaidi ambao bidhaa zao zitatangazwa kwenye jezi ya timu husika.

Mdhamini mkuu ndio hukaa sehemu ya mbele au sehemu ya tumbo wakati wale wadogo wakikaa nyuma mgongoni au kwenye fito za mikono. Kwa aina hii ya udhamini Mbey city wanadhaminiwa na Bin Slum kupitia bidhaa yake ya RB Batteries ambayo nembo yake huonekana mbele ya jezi za timu hiyo. Pia Coca Cola ambao wanaidhamini timu hiyo kupitia jezi yao ambapo nembo yao huonekana kifuani kwa size ndogo juu ya nembo kubwa ya mdhamini mkuu.

Wanachokipata Mbeya City kutokana na ubunifu wao wa kutengeneza vyanzo vya mapato unawasaidia kuendesha timu bila ya kuwa na matatizo ya hapa na pale  ambayo yamekuwa ni sehemu ya maisha ya kawaida kwa klabu zetu.

Licha ya udogo wa klabu yao lakini wamefanikiwa kuitumia nembo yao hiyo ndogo kunufaika nayo. Nawaza hapa ingekuwaje kama wao ndio wangekuwa na Brand kama zile za klabu fulani? Wanahitaji nini zaidi ya kuwashangaa wasiojua ukubwa na thamani ya Brand za klabu zao? Sina budi kuwapongeza Mbeya city katika hili.

Ifike hatua tufikiri kutengeneza fedha za kuendeshea klabu zetu kutokana na nembo za klabu zenyewe. Bila kubadilika hatutaisha kutembeza bakuli kuomba misaada. Klabu inahitaji kuwa na watu sahihi kila sekta ili kuendana na usasa. Hili linawahusu watu wa idara ya masoko ambao wanaweza kuhakikisha wanatengeneza mazingira mazuri ya kuwavutia wawekezaji na wadhamini ndani ya klabu.

Hivi kweli kwa ukubwa wa Simba, leo hii wanavaa jezi plain isiyokuwa na hata nembo ya mdhamini yeyote? Najiuliza hapa wadhamini ndio wanakosekana au tatizo ni wao kutokujua thamani ya jezi yao.

Mbeya city hawana la kufanya zaidi ya kuendelea kuwashangaa na michango yao pamoja na madeni yao wanayoendelea kuyatengeneza kila siku maana unaweza kushangaa mmoja anamcheka mwenzie kwa kuamua kutembeza bakuli wakati wao wanaendesha timu kwa mikopo.

 

Barcelona Wanamtesa Messi Waliyeamini Ataishi Milele.

$
0
0

ATHUMAN BEMELENGO
0713 094952

Majuma kadhaa yaliyopita nilipata kuwatazama wachezaji wawili bora zaidi kwasasa ulimwenguni. Lionel Messi na Cristiano Ronaldo. Nilimuona Messi aliyecheza dhidi ya Juventus ambaye kimsingi hakucheza kwa kiwango bora. Pia nilimuona Ronaldo aliyecheza dhidi ya Bayern Munich.

Unaweza kusema walikuwa binadamu tofauti sana na wale tuliozoea kuwaona kila mmoja kwa michezo waliyocheza. Lakini ndio uhalisia. Messi dhidi ya Juventus alikuwa mchezaji wa kawaida sana ambaye usingeweza kuamini kama ndio yeye kama ndio ingekuwa mara ya kwanza kumuona baada ya kusimuliwa maajabu yake.

Cristiano Ronaldo yeye alikuwa na usiku mzuri dhidi ya Bayern Munich baada ya kuiwezesha timu yake kufuzu hatua ya nusu fainali dhidi ya timu bora kama Bayern Munich tena akiwa amefunga magoli matano katika michezo yote miwili. Sio kitu rahisi kufunga magoli matano mbele ya kipa mwenye kiwango cha Manuel Neuer.

Ulikuwa usiku pekee ambao ungeweza kumpata mshindi katika ile debate ya ubora wa hawa wafalme wawili. Mtizame Ronaldo, licha ya kuwa na umri mkubwa lakini anaonekana bado ana uwezo mkubwa wa kucheza na kufunga tofauti na Messi ambaye anaonekana kabisa kasi yake imepungua.

Kabla ya El Classico ungeweza kuamini Messi hana jipya tena zaidi ya ndevu zake kuwa maajabu pekee aliyobakiza. Huu ndio ulikuwa wimbo wa wale waliomdhihaki.

Niliulizwa sana, Ni kweli Messi alikuwa ameisha? Jibu sahihi lilikuwa hapana, Nikaulizwa tena, sasa tatizo ni nini? Na kwa nini Ronaldo licha ya kuwa na umri mkubwa zaidi anaonekana kuwa bora?

Hayo ni baadhi ya maswali niliyoulizwa na waliotaka kujua kwa nini nilikuwa nikisema Messi bado hajaisha na anaweza kuendelea kuwa mshindani sahihi wa Ronaldo wakiitafuta pensheni yao.

Suala ni moja tu, Ronaldo kwa upande wake yeye amejua namna sahihi ya kucheza kwa wakati huu ambao umri umeanza kumtupa mkono. Ronaldo wa sasa hivi hakimbii sana wala hakai sana na mpira. Unaweza usimuone timu ikicheza mpira na ukalazimika kumuona akifunga tu.

Analazimika kugusa mpira mara chache sana hasa pale inapobidi. Real Madrid tayari inao watu wanaoweza kumfanya Ronaldo asilazimike kuuchezea zaidi mpira na akasubiri tu mbele ya goli la timu pinzani ili afunge.

Miguu ya Toni Kroos na Luka Modric inafanya kazi kubwa kuhakikisha inautawanya mpira katika maeneo yote ya uwanja huku Marcelo na Carvajal wakiwa na jukumu la kupeleka mipira salama kwa Ronaldo.

Hivi ndivyo Real Madrid ilivyojiandaa kumfaidi zaidi Ronaldo akiwa anaelekea katika uzee wake. Unafikiri hawakuujua umri wake walipoamua kumpa mkataba mrefu mpaka mwaka 2022? Hawezi kuwa Florentino Perez anayeweza kufanya biashara ya kiuendawazimu.

Wanaweza kuwatumia Isco na James Rodriguez ili Ronaldo apate muda wa kupumzika. Hii ndio njia sahihi ya kuwatumia wachezaji walioanza kuishi mbali na zama zao. Hawahitaji kukimbia sana uwanjani, kufanya kazi nyingi uwanjani au kucheza muda mrefu bila kupumzika.

Madrid tayari wanalijua hili na wameshaona wamefanikiwa na ndio maana wanapata jeuri ya kuamini hawana haja ya kutumia nguvu nyingi kuzipata nyayo za Eden Hazard kuliko mikono salama ya David De Gea.

Ukimuangalia Messi unaweza kudhani ni mkubwa kuliko Roaldo lakini shida yake ameanza kutumika mapema sana. Akiwa na miaka 19 alishaingia katika rekodi ya kufunga hat trick kwenye El Classico.Barcelona wamejisahau sana.

Waliamini kile kizazi alichokitengeneza Pep Guardiola akiwa kocha wa vijana pale Catalunya kingeishi milele. Hakuna kizazi kilichoandaliwa kuja kurithi zama zao.Messi anahitaji kupumzika, kuugusa mpira mara chache katika maeneo hatari zaidi na akiwa hakimbizani tena na mabeki.

Lakini mambo ni tofauti sana. Barcelona ya sasa inamhitaji zaidi Messi kuliko unavyofikiri. Matokeo yake wamemfanya kuwa mtumwa, anateseka sana. Wanamhitaji afunge, aichezeshe timu na ikibidi akabe pia. Unampata wapi tena Messi anayeweza kufanya yote haya wakati hata yule wa ubora wake hakuweza.

Barcelona haina tena mashine zake zilizoifanya kuwa tishio kuanzia kwenye eneo la kiungo. Sergio Bosquets na Andres Iniesta tayari wamejichokea. Huwezi tena kuziona miguuni mwao zile  pasi zilizomtia ‘Degedege’ Sir Alex Ferguson pale Wembley mwaka 2011. Ni vijana wa kiume pekee walioweza kumtetemesha mwanaume Sir Alex Ferguson.

Ni nani anaweza kuifanya ile kazi aliyokuwa akiifanya pass master Xavi Hernandez ambaye alikuwa na uwezo wa kukimbia uwanja mzima akiwa amepiga pasi nyingi zaidi ya timu pinzani?

Sio Ivan Rakitic wala Andre Gomes anayeweza hata kujaribu ila inabaki kuwa kazi nyingine ya Lionel Messi. Unaikumbuka mechi dhidi ya PSG? Luis Enrique alimuanzisha Messi katika eneo la kiungo kuifanya kazi hii huku Rafinha akianzishwa katika safu ya ushambuliaji sambamba na Neymar na Luis Suarez.

Siku ile Messi alikuwa mtu muhimu zaidi uwanjani huku Neymar akiwa mchezaji bora. Sio Iniesta wala Rakitic ambaye angeweza kuwashinda Verrati na Rabiott pale kati ya dimba.Ulimuona Messi dhidi ya Real madrid?

Kupitia kwake utakiona nilichokueleza hapo juu. Alihitajika kumsaidia Iniesta katika eneo la kiungo ili kuiunganisha timu kutoka eneo la kiungo hadi mbele. Ilikuwa kazi rahisi sana kwa uwezo wake. Alimaliza mechi akiwa ametimiza magoli 500 ya La liga na magoli 23 aliyofunga kwenye El Classico.

Messi bado ana uwezo wa kuendelea kucheza kwa muda mrefu tena kwa kiwango kikubwa hata zaidi ya Cristiano Ronaldo kama Barcelona watatafuta namna sahihi ya kumtumia kwa kipindi hiki ambacho anaonekana umri umeanza kuachana na kasi yake.

Njia pekee na sahihi ni kuijenga timu upya itakayomhitaji Messi kutumia zaidi akili yake na ubunifu kufunga magoli bila kutumia nguvu kubwa. Kama wataona hawahitaji kufanya hivyo kutokana na uwepo wa Neymar, basi watakuwa wanajiongopea.

Nani ataweza kuutawanya mpira katika maeneo yote ya uwanja kama walivyokuwa wakifanya Xavi na Iniesta? Neymar pekee? Hatoweza kuifanya hata anayoifanya Messi sasa hivi.

Wanahitaji damu changa kama Thiago Alcantara na Marco Verrati au Hector Bellerin bila kusahau watu imara katika safu ya ulinzi.

Ukiwa na watu wa aina hii, ni lini Messi atalazimika kushuka kwenye  eneo la kiungo kukimbizana? Hii ndio njia sahihi itawafanya Barcelona waendelee kumfaidi Messi kwa muda mrefu zaidi.

Yanga inaposhindwa kujitajirisha yenyewe

$
0
0

Abdul Dunia

Hongera Yanga…Hongera Yanga…Hongera Yanga…Hongera Yanga. Ndio lazima Yanga ipewe pongezi kwa hapa ilipofikia. Ni mara chache sana kwa klabu kubwa kama Yanga kueleza ukweli kwenye matatizo yake. Ni mara chache sana.

Leo napingana na ule msemo unaopendwa kutumiwa na Wanajeshi Vitani unaosema, Usiombe amani wakati wa Vita. Ila nakubaliana na ule msemo wa Mwanafalsafa Voltaire, Usiwe sahihi wakati watu waliokuzidi wanapokosea.

Yanga imeonyesha kutojali kelele za Mashabiki wa Simba na kueleza nia yao juu ya kuhitaji msaaada kutoka kwa mashabiki na wanachama ili kuendesha timu yao kwa sasa. Imekubali kuwa sahihi kwa kipindi hiki kigumu.

Hakuna asiyefahamu kuwa Yanga inapitia kipindi kigumu kifedha kwa sasa, ilikataa kueleza hali halisi mwanzoni lakini hivi karibuni iliamua kuomba amani wakati wa vita na kueleza hali inayowakabili kwa sasa. Pongezi kwao.

Ni ngumu sana kwa timu kama Yanga kuomba mchango kupitia kwa mashabiki wake. Hiyo tumezoea kuona kwenye klabu kama ile yangu ninayoishabikia ya Lipuli FC. Lazima ieleweke hivyo. Lipuli inaweza kufanya hivyo lakini sio Yanga.

Napozungumzia Yanga lazima ieleweke kuwa namzungumzia Bingwa mtetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Timu iliyotwaa Ubingwa wa Ligi mara nyingi zaidi, Timu iliyoifunga Simba mara nyingi na Timu ya Kwanza kuanzishwa Tanzania.

Yanga ni klabu kubwa, ina mtaji wa mashabiki. Hakuna anayepingana nami kwa hilo, lakini Mkwasa na viongozi wengine wasihitimishe mwisho wao wa kufikiria hapa walipofika. Kufikia mwisho huu ni sawa na kufeli mtihani wa Chekechea wakati wewe ni mwanafunzi wa Chuo Kikuu.

Ni ngumu kuamini Yanga hii, ndio inayochangiwa 1000 na lile pandikizi la baba linaloishabikia Simba, Mkubwa Kambi? Sina sababu ya kutokuamini hili.

Sipo hapa kuzungumzia suala la jezi na vifaa vya timu kama wengine wanavyozungumzia, atakayehitaji kujua matumizi ya jezi na vifaa vya michezo anaweza kusogea kwenye lile andiko takatifu la ndugu yangu Athumani Bemelengo. Sipo kwenye vifaa.

Yanga ni jina kubwa, jina hilo linaweza kutumiwa kunufaisha klabu na hata Watanzania wengine. Neno Yanga linaweza kuwepo kwenye kikombe cha Chai, Bakuli na hata kwenye Chupa ya Maji na mashabiki wakanunua ili kuichangia klabu yao na kuinufaisha.

Neno Yanga linaweza kukaa kwenye bidhaa kedekede zinazoambatana na matengenezo yao na wakafaidika kutoka kwa mashabiki wao zaidi ya ile sera ya kuichangia kwenye Tigo, Airtel na Mpesa. Mmewapelekea mfumo huo? Hapana.

Mchango wa mashabiki wa Yanga ni kwenda kwa wingi viwanjani timu yao inapocheza ili wadhamini wajue ukubwa wa Yanga na waipapatikie kuidhamini kama zinavyodhaminiwa Orlando Pirates na Mamelodi Sandowns za Afrika Kusini.

Hakuna mdhamini yeyote anayekataa kuidhamini Yanga leo hii. Kama Bilionea namba moja Afrika na Dunia inamtazama kama mfanya mapinduzi kwenye sekta ya Uchumi, Aliko Dangote anatamani kuidhamini Yanga, matajiri wengine wa kawaida wanashindwaje? Hawashindwi. Yanga yenyewe ni mtaji. Hakuna anayebisha hilo.

Kama Dangote alihitaji kuidhamini Arsenal inayocheza Ligi Kuu ya England na Ligi ya Mabingwa Ulaya, Atashindwaje kuidhamini Yanga inayocheza Ligi Kuu ya Tanzania Bara?

Mashabiki wanapotumia juhudi zao kuipenda Yanga tu, hapo ni mchango tosha wanaotakiwa kuutoa hakuna zaidi ya hapo. Nyingine ni ziada tu.

Mkwasa ana nia thabiti na Yanga, aliipenda, anaipenda na ataendelea kuipenda…Kwa sababu anamapenzi na Yanga na hata Yanga inampenda lakini anatakiwa afikiri zaidi ya hapa alipofikiri.

Mkwasa kwa sasa, anachotakiwa kukifanya ni kujua aina ya kusuka mipango itakayoifanya Yanga kuwa tajiri wa kuendelea na kuacha kumtegemea mtu mmoja au wawili. Lazima ieleweke hivyo.

Mtaji wa Mashabiki wa Yanga hapa bongo ni sawa na ule wa mashabiki wa Man United ama Arsenal pale England. Yanga ya leo inaweza kuanzisha tournement ya siku tano mpaka saba kwa ajili ya kujiandaa na msimu mpya na ikapata pesa.

Yanga inaweza kuzialika timu jirani kutoka Kenya, Uganda na Burundi na hata moja kutoka South Africa ikauza haki za matangazo ya TV kwa pesa kibao na kupata pesa zitakazoifanya iweze kujitegemea.

Yanga haiwezi kukosa wadhamini wa hayo mashindano madogo wanayoweza kuyaanzisha na kupata pesa kibao za kujiendesha kama klabu.

Yanga itapata viingilio vya uwanjani (Gate collection) kupitia kwa mashabiki watakaofika uwanjani kushuhudia hizo mechi. Mkwasa unaandika lakini?

Kwa nini hatujiulizi, Arsenal ya England haijatwaa ubingwa wa Ligi Kuu tangu 2003/2004, haijawahi kutwaa UEFA Champions League katika maisha yake…lakini mbona haijafika huku ilipofika Yanga?

Arsenal ilianzisha lile Kombe la Emirates Cup kwa malengo gani? sidhani kama ilianzisha lile kombe ili kuwafurahisha mashabiki wake kwa kulitwaa.

Arsenal ilianzisha lile Kombe kama njia moja ya kupata pesa, iliwaalika Juventus, Monaco, Inter Millan na klabu nyingine kubwa. Ikapata TV Rights, viingilio vya uwanjani na wadhamini walijitokeza kwa ajili ya kupata pesa.

Kupitia michuano hiyo ya wiki moja Arsenal ilihakikisha inauza bidhaa zake nyingi uwanjani pale Emirates ili kupata pesa. Na mashabiki walinunua. Yanga inashindwaje?

Nihitimishe kwa kusema hongereni Yanga kwa hapa mlipofikia…lakini kuna safari zaidi ya hii mliyoingoja kwa miaka mingi iliyopita. Siku njema.

AD: 0679469044

Ni Ngumu Kumpata Anthony Joshua Huku Kwetu

$
0
0

Na ATHUMAN BEMELENGO
Contact: 0713 094952

Umemuona Anthony Joshua? Naimani ulimuona yeye mwenyewe pamoja na kile alichokifanya pale Wembley mbele ya umati wa watu 90,000.Ulikuwa usiku wa tarehe 29 April kijana wa Kiingereza alipowapa ndugu zake walichokihitaji. Ndio hulka yao waingereza, wanahitaji vyao kuwa bora zaidi siku  zote.

Wameanza kumtukuza tayari, kwao Anthony Joshua ni zaidi ya akina Floyd Mayweather na Bernard Hopkins. Wameamua kumuweka nyuma ya Muhammad Alli. Kwao ndio bondia bora zaidi duniani kwa sasa.

Hii haishangazi sana, tulishawazoea na hao ndio waingereza halisi. Hao hao  ndio waliothubutu kuuaminisha ulimwengu kuwa Wayne Rooney huyu ambaye hana hata magoli 500 ana ubora sawa na Pelle. Walimuita “The White Pelle”. Baadae wakajaribu kutuaminisha Theo Walcot angekuja kumfunika Lionel Messi. Ukiwafikiria wanachekesha sana.

Ila tuachane nao turudi kwa Anthony Joshua ambaye ndio msingi wa andiko hili. Nafikiri tuna jambo la kujifunza kutoka kwake. Ukitaka kuwa bora huna budi kujifunza kutoka kwa waliokuwa bora.Leo hii wote tunafurahia ujio wa kipaji cha Kylian Mbappe, lakini tusisahau huyu alikaa na kujifunza zaidi kwa Cristiano Ronaldo na ndio maana leo hii tunajiandaa kufurahia kipaji kinachochipukia kwenye ukomo wa zama zake.

Baada ya pambano pale Wembley, Eddy Hearn promota wa Anthony Joshua alipata kusema kuwa AJ alifanya mazoezi mpaka akawa anasema anahisi damu. Hii inamaanisha ni kiasi gani AJ alikuwa amejifua vya kutosha kuelekea kwenye pambano hilo. Kwa wanamichezo wenzangu naamini tutakuwa tunaelewa kuna wakati unafikia unapokuwa unafanya mazoezi hadi unatamani kuingia mchezoni. Hii ni kwa mchezo wowote unaocheza.

Katika football, volleyball au Basketball ukifanya mazoezi mengi sana na ukautesa mwili ipasavyo kuna wakati inafikia unausikia kabisa mwili umekolea mazoezi. Hiki ndicho alichokimaanisha Eddy Hearn. Anthony Joshua alikuwa amefanya mazoezi ya kutosha hadi akawa anausikia mwili wake kuwa ulikuwa tayari kwa ajili ya pambano.

Kuna kipindi miezi kadhaa kabla ya pambano Jamie Reynolds ambaye ni kocha wa Anthony Joshua alipost video iliyomuonyesha AJ akiwa mazoezini kujiandaa na mchezo huo.
Mazoezi yake yaliibeba dhamira yake na yakaistawisha ndoto yake ikaishi. Alihitaji kuwa mshindi. Jitihada na maarifa ndio zao la matokeo bora siku zote. Mnamo raundi ya 11 Anthony Joshua alifanikiwa kumshinda aliyemuita role model wake.

Mara kadhaa wakati pambano likiendelea alionekana kuzidiwa kutokana na kukosa uzoefu, lakini alipambana. Unafikiri angeweza kukomaa ulingoni kama asingekuwa na mazoezi ya kutosha?  Wladmir Klitschko alitaka kutumia uzoefu wake kumzamisha AJ lakini maandalizi makubwa aliyokuwa ameyafanya ndio yalibaki kuwa silaha yake.

Licha ya kuingia kwenye mchezo huo akiwa hapewi nafasi kubwa ya kushinda lakini jitihada alizokuwa nazo tangu mwanzo zikaufanya ulimwengu kuandika historia nyingine. Aliamini anaweza kushinda na njia ikiwa ni moja tu, maadalizi bora.

Hivi ndivyo walivyo washindani bora siku zote ambao bahati mbaya ni ngumu sana kuwapata huku kwetu. Ndio namaanisha washindani bora ni ngumu kuwapata huku kwetu.  Unabisha? Niambie ni lini mara ya mwisho ulisikia bondia kutoka hapa nchini ameshinda pambano lolote nje ya nchi?

Kuna bondia alipoteza pambano katika raundi ya pili huko nchini Australia. Hivi kweli huyu nae alikuwa serios alienda kuiwakilisha nchi? Wanatia hasira sana hawa mabondia wanaofikiri mapambano ya kimataifa ni sawa na yale wanayocheza uchochoroni huku Manzese kwetu.

Unapotaka kupambana kimataifa lazima ujiandae kimataifa tena kwa kiwango cha kimataifa. Wangapi tumemiss zile headlines za Francis Cheka alivyokuwa akiwadunda mabondia kibao wa kimataifa? Leo utamsikia Clouds amemuangusha Mchina, kesho utamsikia ITV amemlaza Mcanada.

Binafsi nimemmiss sana Cheka, alikuwa anajua anachokifanya na alikuwa na dhamira inayoishi alipokwenda kupambana. Sina maana nataka kumfananisha na Anthony Joshua lakini alijua alichokuwa anakifanya kwa kiwango chake.

Alifanya mazoezi ya kutosha na kila mmoja wetu anaweza kuwa shahidi katika hili.Unakumbuka enzi zake alipokuwa akifanya mazoezi ya kusukuma tairi la trekta milimani huko Morogoro?
Binafsi niliielewa dhamira yake, licha kuwa na upungufu wa miundombinu ya kufanyia mazoezi lakini alitafuta njia itakayomfanya ajifue ipasavyo. Na alifanikiwa.

Nasikitika kusema akina Cheka wameondoka na ngumi zao bora niendelee kuwashabikia akina AJ na Tony Furry. Sio Juma Fundi wala Kamburuta au Dulla Mbabe anayeelewa anachokifanya.
Mnalalamika migogoro iliyopo katika vyama vya ngumi ndiyo inayowaathiri, kwani kipindi cha akina Japhet Kaseba na Cheka haikuwepo? Simaanishi kuwa migogoro hiyo haina athari ila haiwezi kunifanya niamini ndiyo inamfanya mtu kupoteza pambano kwa raundi mbili tu.

Narudia tena, Anthony Joshua ana kitu cha kutufunza kuanzia namna alivyojiandaa kuelekea kwenye pambano na kwa namna alivyokabiliana na mpinzani wake ulingoni.Unakwenda kwenye pambano bila kujifua vya kutosha halafu unategemea nini. Kipigo tu, tena cha aibu.

Ni wakati wa kubadilika sasa na kuacha kufanya mambo kwa mazoea. Ushindi mtamu huandaliwa mapema tena kwa gharama kubwa sana. Tunahitaji sasa kuuona mcheo wa ngumi ukirejesha heshima yake na nyinyi mabondia ndio watu wa kwanza katika hili maana hii ndio kazi yenu.

 


Kama ulipitwa na Ngumu Kumeza ya Sports Extra Mei 5, 2017

$
0
0

Kupitia kipindi cha Sports Extra cha Clouds FM, kila Ijumaa huwa kuna kipengele cha NGUMU KUMEZA ambacho kimekuwa kikifuatiliwa na wadau wengi wa michezo kutokana na kugusa maeneo mbalimbali bila kujali kinachoma kwa kiasi gani.

Ijumaa ya Mei 5, 2017 Nngumu Kumeza ilijikita kwenye klabu ya Yanga kwa kuangazia suala la utegemezi wa klabu hiyo kwa mtu mmoja.

Kama ulipitwa na Ngumu Kumeza hiyo unaweza kutulia na kusoka kile kilichojiri siku ya Ijumaa ya Mei 5, 2017.

Wakati wakoloni wanajiandaa kuziachia huru nchi za Afrika, tayari walishagundua njia mpya ya unyonyaji iitwayo utegemezi ambayo waliinadi kwa njia ya misaada lengo lilikuwa kutengeneza ngome za kumbukumbu kwenye bongo za watu.

Waliunda benki ya Dunia ambayo inatupa mikopo kwa masharti makali yanayofanya nchi za Afrika kuendelea kuwa tegemezi, ilipotokea kuna viongozi wa bara la Afrika wenye mawanda makubwa, wenye peo za kutafakari unyo nyaji wao waliwekewa vikwazo vya kiuchumi na aliyeonekana anawapinga alishambuliwa na kufupishiwa maisha, Mwenyezi azilaze mahala pema nafsi za viongozi hao akiwemo Muamar Ghadaffi.

Na wapo waafika wanaoamini bila misaada ya wakoloni bara hili halitopiga hatua za maendeleo, siwezi kuwalaumu wenye fikra hizo kutokana na wengi wao bado wamelewa ukoloni mambo leo.

Tuitazame dhana hii ya utegemezi kwa waafrika iliyoshamiri ndani ya klabu ya Yanga iliyopandikizwa tangu enzi zile ingieni bure tiketi kalipa fulani, imemea kwenye vichwa vyao na hata sasa inawatesa hasa kipindi hiki bwana kubwa anapoonekana kutoa talaka rejea.

Katibu anajaribu kupambana na adui asiyeonekana lakini kaptura lile laonekana ni kubwa halijasadifu maumbile yaketofauti na ilivyokuwa kwa Tiboroha ndiyo maana leo Kaunda inadaiwa milioni 300, timu imejaa majina ya fedheha kama Matonya FC, japo Dodoma walipotezea kwenda.

Wengine wanaidhihaki kwa kuiita Njaa FC yote yanakuja kutokana na kuwa tegemezi, muungwana mmoja ananiambia mwenye kilanga haliliwi wala akifa hawekewi matanga, namuuliza una maana gani anaeleza kuwa suala la kufanya harambee hii kutunisha mfuko wa timu ni kitu kilicho asisiwa na Dkt. Tiboroha japo kilipingwa na Mwenyekitienzi zile mpango kazi wa uendeshaji haukuwa kwa staili hii ya Mkwasa.

Dkt. Tiboroha aliafikiana na kampuni za simu zichukue asilimia 20 ya hambee kwa ajili ya matangazo na asilimia 80 iende kwenye klabu, hii ilitokea kipindi kile Mwenyekiti aliponuna miezi mitatu akawa hapokei simu wala barua pepe kule Marekani.

Dkt. Tiboroha alifanya harambee Mbagala, Tegeta, Mbeya na Mtwara akapata pesa ya kulipa wachezaji miezi mitatu ila katibu wa sasa ameruka bila kuagana na nyonga ndiyo maana inaonekana hili suala la uchangiaji ni geni mbele za watu. Lingeendeshwa kisasa lingesaidia kujua idadi halisi ya wapenzi wa Yanga, kwa vile linaendeshwa kwa upeo hafifu ndiyo maana watu wanajiuliza Yanga wakichangisha vile, Mbao, Kauzu na Makumba zifanyaje?

Mwenyekiti tangu mwanzo alikuwa anaonesha anahitaji ategemewe ndiyo maana aliwatimua TBL, akazuga kidogo akajiweka kifuani kwa thamani ya milioni 600 ambayo mkataba haujulikani mbele ya kamati ya utendaji wala wanachama, labda walisainishana mwenyekiti na makamu bila kuhusisha wajumbe.

Hivi karibuni kampuni ya kamari ilitaka kukaa kifuani, mwenyekiti akaibuka toka mafichoni akatoa agizo alipwe milioni 600 kwanza kabla ya yote ili aipishe kampuni ya kamari, sasa jiulize kama kampuni ya mwenyekiti inatoa milioni 600 mbona timu inatanga na njia? Yanga imekimbia mechi ya kujipima nguvu Dodoma lakini inaenda kucheza Katoro, kipindi kile mwenyekiti kanuna mechi hizi zilisaidia kuwapa bonus wachezaji kama unakumbuka ndio mwaka ule Yanga waligomea Kagame TFF wakahofia michuano haitonoga ikawapam ilioni 150 wasijitoe ikiwa pamoja na kuwalipia huduma ya malazi pale Tiffany Hotel, nzi akiacha upuuzi wake anaweza kuvaa viatu vya nyuki na kutengeneza asali.

Hata Yanga wangeacha kumtegemea mtu wakaamua kujitegemea bado basi nadhani leo hii klabu hii ingeweza kupata wafadhili ambao wangejikita kudhamini Nyanja tofauti mfano makazi kwa ajili ya wachezaji, chini ya Dkt. Tiboroha NHC walikubali kuingia makubaliano na Yanga wachezaji wangepata pakuishi. Ukipata nafasi muulize Mchechu nahisi atajibu hajui mpango ule ulifia kwa nani.

Mwambie ukweli mwenyekiti hataki Yanga ijitegemee hata mahoteli kadhaa yalikuwa tayari kuingia ubia wa kambi, leo klabu isingeweza kuishi yatima Kimbiji.

Wakati Mkwasa na wachezaji wake 11 walipokwama Algeria, nilimkumbuka Tiboroha na mipango yake ya Yanga kuingia ubia na Fastjet ambao walikubali kutoa milioni 500 kwa mwaka pia usafiri wa michezo ya kimataifa, kuna shirika moja la ndege la kigeni lilikuwa tayari lakini yote yalikwamishwa na mwenyekiti.

Kupitia vipindi vya Yanga TV mfano matangazo ya milioni saba klabu ingejipatia milioni 3,500,000 na nusu nyingine ingekwenda kwa wamiliki wa king’amuzi chaTING. Muulizeni mwenyekiti wenu kwa nini alipiga chini pesa hizi? Kuna kampuni ilikuwa tayari kurusha mchezo wa Yanga kwa kuwalipa shilingi milioni 194 kwa mwezi ni timu gani bongo inaingiza fedha ndefu kiasi hicho kupitia haki za matangazo television lakini nalo lilikwamishwa na mwenyekiti.

Afisa mmoja wa Straburg       anasema, wakati wanajenga kituo cha mabasi ya mwendo kasi pale Jangwani waliwafuata Yanga wakawaambia wapo tayari kuwajengea uwanja wa Kaunda kwa shilingi milioni 450 tu ikiwa ni pamoja na kupainua juu pasifikiwe na mafuriko. Katibu wa wakati huo Jonas Tiboroha alikubali mwenyekiti alipokuja alikataa wazo hilo na ndio maana bwawa la perege bado lipo pale Jangwani.

Kama mwenyekiti alipiga chini udhamini wa TBL ,NHC Fastjet, SBT, Azam Media, TING, Oryx na G Ozone sitegemei matangazo yako Mkwasa ya zabuni yatakuja kukubaliwa, zaidi endeleeni kuvaa Quality pasipokujua mnapata nini.

Jicho la 3: Kwanza jiulize MO ni nani hasa ndani ya Simba, kwanini anakopesha kwa maandishi?

$
0
0

Na Baraka Mbolembole

MUNGU anawapenda sana watu masikini, angekuwa hawapendi asingekuwa anawaumba wengi namna hii. Mungu anawapa hekima na busara viongozi ili waweze kuwaongoza masikini ili wasitumiwe na ‘mabepari’ na kukandamizwa. Ni dhambi mbaya sana kumkandamiza masikini.

Heshima inaombwa? Uhuru unaombwa?

Yanga SC inasubiri ‘muujiza’ tu kushindwa kutetea ubingwa wa ligi kuu kwa mara ya 3 mfululizo mwishoni mwa wiki hii watakapokuwa ugenini kucheza mchezo wa mwisho vs Mbao FC katika uwanja wa Kirumba, Mwanza. Hili nilitaraji, tangu mwanzo wa msimu huu nimekuwa nikiandika na kusisitiza kuwa Simba haikidhi vigezo vya kushinda taji la VPL msimu huu.

Niliamini hivyo na sikutaka kuvunjwa imani yangu na yeyote yule. Je, nimekosea wapi? Wako wapi wale ambao walikuwa wakipinga hoja zangu kwa kashfa na matusi? Nimekuwa mshindi kwa mara ya tano mfululizo kwa sababu ndani ya misimu mitano Yanga inaelekea kushinda ubingwa wa nne huku timu ‘changa’ katika soka la Tanzania-Azam FC ikishinda taji hilo mara moja.

Simba si nguvu moja

Busara na hekima ni tatizo pekee lililobaki klabuni Simba, na ili wafanikiwe kupata mafanikio ya ndani na nje ya uwanja-Simba kama klabu wanatakiwa kujitazama wenyewe katika vioo vyao na kurudisha kumbukumbu ya mafanikio yao yaliyopita.

Ilifanyaje hadi ikapata jengo ambalo ni makao makuu ya klabu hivi sasa, ilifanyaje ikaweza kushinda mataji 19 ya ligi kuu ndani ya miaka isiyozidi 60, walitumia njia gani kutengeneza kikosi kilichoweka rekodi isiyofikiwa hadi sasa-klabu pekee ya Tanzania kufika nusu fainali ya Caf Champions League (historia tuliyozaliwa na kuikuta ni kwamba timu hiyo kutoka Mitaa ya Msimbazi ilifanikiwa kufika nusu fainali ya klabu bingwa Afrika mwaka 1974)

Ni lazima kwanza ‘wahitaji-mabadiliko’ wajiulize kilitokea nini hadi wakayumba kwa miaka karibia 20 katika soka la Afrika na kurejea hadi kufika fainali ya michuano ya Caf Confederation Cup mwaka 1993? Naweza kuielezea Simba kuanzia hapo hadi sasa yapata miongo miwili na nusu.

Majibu ya maswali ilipotoka Simba unayaweza kuyajibu hata wewe msomaji wa makala haya lakini unaifahamu Simba SC? Siamini katika njia ya mabadiliko inayotaka kutumiwa na ‘kikundi’ cha watu wenye maslahi yao binafsi.

Unawezaje kubadili taasisi iliyojiendesha kwa miaka zaidi ya 80 ndani ya mwaka mmoja baada ya wazo hilo la mabadiliko kuwasilishwa? Unawezaje kubadili mfumo wa uendeshaji ulioifanya klabu kuishi kwa miongo nane mfululizo bila kuwashirikisha waasisi?

Kizazi chetu hiki kina matatizo makubwa sana. Kwanza tunashabikia mambo ambayo hatuyajui kiundani. Tunafahamu njia za mabadiliko kuliko wakubwa zetu.

Mabadiliko gani yanatakiwa?

Nimeshangazwa sana na mwenyekiti wa kamati ya usajili wa klabu Zacharia Hans Poppe kubembelezwa arejee madarakani siku moja baada ya kuwasilisha baraua ya kujiuzulu nyazifa zake klabuni hapo kisa tu uongozi wa Rais wa klabu, Evance Aveva na makamu wake kuingia mkataba mnono hivi karibuni na kampuni ya SportPesa.

Kujiuzulu kwa Poppe kulikuja muda mfupi baada ya Mohammed Dewji kutaka klabu hiyo ya Simba imlipe kiasi kisichopungua bilioni 1.4 ambazo alikuwa akiikopesha klabu hiyo ndani ya miezi isiyozidi kumi iliyopita.

Unakumbuka makala haya niliyowahi kuandika?

Mara baada ya baadhi ya wanachama wa klabu ya Simba kukubali ‘mabadiliko’ katika mkutano mkuu wa mwaka wa klabu hiyo, tajiri/mfanyabiashara na mwanachama wa klabu hiyo Mohammed Dewji ‘MO’ aliusaidia uongozi wa timu hiyo kiasi kisichupungua milioni 100 ili kusaidia usajili wa baadhi ya wachezaji.

Hakuishia hapo, tajiri huyo mkubwa barani Afrika ameendelea kutoa msaada wa kifedha na inasemekana hadi sasa amekwisha saidia zaidi ya milioni 600-fedha ambazo zimekuwa zikisaidia klabu kuwalipa mishahara wachezaji na baadhi ya viongozi walioajiriwa klabuni hapo.

Kumbuka Simba haina mdhamini yeyote hivi sasa baada ya kumalizika kwa mkataba wao na bia ya Kilimanjaro.

Kitu kinachonishangaza ni kwanini uongozi wa timu haufanyi jitihada zozote za kufanikisha klabu kupata wadhamini mara baada ya mkataba wao na Kilimanjaro kumalizika?

Nadhani ‘wamepumbazwa’ au wameridhika na misaada ambayo MO amekuwa akiitoa katika miezi ya karibuni. Inawezekana viongozi wa sasa klabuni hapo wameshindwa kuyashiwi makampuni kujitangaza kupitia klabu yao!

Inashangaza sana, timu kubwa kama Simba kukosa mdhamini hata mmoja na kutegemea misaada kutoka kwa mwanachama kuendesha timu!

Najiuliza, ni kwanini MO anaisaidia sana Simba katika utaratibu wa ufadhili na si kuingia nao mkataba? Nadhani hata yeye anatoa msaada hivi sasa kwa kuwa naye anaamini klabu inakwenda katika mabadiliko makubwa kiuendeshaji.

Nimenukuu sehemu tu ya makala yale yaliyopita, na sasa naamini

Ukimsikiliza MO, sehemu ya mazungumzo yake mara baada ya kuibuka katika vyombo vya habari hivi karibuni utagundua ni ‘mtu mbinafsi, ndiyo maana alisema kuna kampuni ipo tayari kuingia mkataba na Simba SC kwa kiasi kisichopungua bilioni 2 kwa mwaka, lakini hapo hapo anasema-watakuja baada ya klabu kubadili katiba yake na kukubali mabadiliko ya kiuendeshaji.

Aveva anaonekana hataki kubeba ‘msalaba’ ambao wenzake wote waliukwepa ndiyo maana anatafuta wadhamini wenfgine ambao wataendelea kusaidia uendeshaji wa klabu wakati huu suala la mchakato wa mabadiliko likiendelea.

Ningekuwa na mamlaka ya kubadili katiba ya Simba kitu cha kwanza na muhimu ni kuweka kamati ambayo itatambulika kikatiba kama yenye mamlaka ya mwisho kikatiba kukubali jambo kubwa la klabu lililopitishwa na mkutano mkuu wa wanachama. Angalau watu 100 wanatosha kuingia katika kamati hiyo na hawa wanaweza kutoka kila mkoa wa Tanzania mahala ambako Simba ipo kikatiba.

Kuwaacha wanachama tu wapitishe jambo lolote katika mkutano mkuu si vyema kwa sababu wanachama wengi wa kizazi cha sasa hawajui chochote kuhusu Simba zaidi ya kuwa ‘bendera fuata upepo tu.’

Wanachama wengi wa klabu ya Simba hawajui ni kwanini klabu inakwama na hawajiulizi ipi ni njia sahihi ya kuifanya klabu kujiendesha bila kutegemea nguvu ya watu binafsi.

Baada ya MO kutoka hadharani na kusema anahitaji kulipwa pesa alizoikopesha Simba msimu huu kisa tu hakushirikishwa katika mkataba wa SportPesa, kulinifanya nijiulize sana, HUYU MO NI NANI HASWA NDANI YA SIMBA ukiachana na uanachama wake? Eti, msomaji  wa makala haya unaweza nisaidia jibu, MO ni nani hasa ndani ya Simba hadi alalamike kutohusishwa katika mikataba halali ya klabu na wadhamini?

Kwanini MO aliweka makubaliano ya kulazimisha ashirikishwe katika makubaliano yoyote ya klabu na wadhamini watakaojitokeza wakati yeye anaikopesha klabu na ndani ya muda mfupi deni limefikia bilioni 1.4? ni kwanini amechukia baada ya Aveva kumwambia watamlipa pesa zake mara baada ya kuingia mkataba na SportPesa?

Je, wakipatikana wadhamini wengine watatu au wanne wanaokaribia au kupita thamani ya SportPesa Simba haitaweza kujiendesha? MO anataka kuwekeza nini wakati tayari ni mshindwa? Simba inaweza kumlipa chochote anachotaka MO sababu ni tajiri na maarufu zaidi ya MO na hili lingewezekana ikiwa idara ya masoko ingekuwa inafanya kazi kwa ajili ya klabu na si watu binafsi kama ilivyo sasa.

Kabla ya kukaa meza moja na MO viongozi wa klabu wangejiuliza huyu MO ni nani hasa katika klabu? Mimi nafahamu ni mwanachama anayesaidia na kuwakopesha Simba kwa maandishi ili waweze kujiendesha. Anakopesha ili pesa zake zirudi. Kwanini mkataba wake na wadhamini itakuja baada ya mabadiliko? Kabla ya mabadiliko Simba iendelee kumkopa yeye au itafute njia nyingine ya kujiendesha?

Mamadou Coulibaly. Msenegali Aliyechagua Ukimbizi na Njaa Ili Awe Mwanasoka. Somo Kwa Sureboy.

$
0
0

Wangapi wanamfahamu Mamadou Coulibaly? Inawezekana lisiwe jina maarufu miongoni mwa mashabiki lakini ni jina ambalo linawafanya matajiri na makocha kwenye vilabu tofauti waumize kichwa na kutaka kufungua pochi nene kwa ajili ya kumpata. Huyu yupo tayari na historia yake inafanya jambo hili livutie zaidi, naam aliwahi kuwa mkimbizi huyu.

Kiungo huyu mwenye miaka 18 anayechezea klabu ya Pescara alielezea namna ambayo aliweka maisha yake rehani alipoamua kuondoka Senegal na kuelekea zake Ulaya. Na sasa yupo katika njia ya kujiunga na klabu ya Juventus ambayo ipo katika fainali ya klabu bingwa barani Ulaya.

Stori ya Coulibaly ni moja ya vitu vichache ambavyo vinaweza kukupa jambo la moyo wako ambalo llitakufanya uamini hata jabali haliwezi kukwamisha safari yako.

Alifika Ulaya mwaka 2015 baada ya  kuishi katika safari ambayo ilikuwa ngumu kupita kiasi kutoka Senegal akipitia Morocco kabla ya kufika katika bara ambalo baadae alionekana kwa klabu ya Pescara nchini Italia na ikaamua kumtwaa.

Mamadou Coulibaly in action against Juventus, who he could soon join

Akizungumza na mtandao wa jarida la Gazzetta della Sport  alieleza namna ilivyokuwa tofauti na alivyotarajia na kwa kiasi gani msukumo wa kupata kile alichokihitaji ulivyomsaidia katika nyakati ngumu alizopitia.

“Niliondoka na begi la mgongoni pekee.” Nilimwambia rafiki yangu Mamadou pekee, wazazi wangu walifahamu kuwa nitakuwa shule.”

“ Nilizima simu yangu na sikupiga simu kwa muda wa miezi mitatu mpaka minne, na walijua nimefariki.” “Nilikuwa na chakula cha kutosha kula nyumbani, nipo mimi na dada zangu wawili. Baba yangu hakutaka nicheze mpira hata hivyo,” alieleza Coulibaly.

“Kwake kusoma lilikuwa jambo pekee la msingi katika maisha yake kwa sababu familia yetu ni ya walimu. Yeye akiwa ni mwalimu wa elimu ya viungo, shangazi zangu wakiwa ni maprofesa.”

“Aliniahidi kuwa atanipeleka katika timu za Ulaya, lakini ilikuwa katika kunifunga mdomo. He “Niliamua kuweka maisha yangu rehani kwa ajili ya soka, lakini pia nilifanya hivyo kwa ajili yao pia. Muda si mrefu nitaweza kuwasaidia,”  alisema Coulibaly.

Lakini jambo la ajabu kwa Coulibaly ni kuwa inawezekana hilo likawa ni jepesi kati ya mazito aliyoyapitia. Mambo yalikuwa magumu zaidi katika njia yake ya mafanikio.

Mamadou Coulibaly couldn't afford the train ticket to get to Pescara

Kiungo huyo alielezea namna ambayo aliamua kulala mitaani na angeweza kufariki kama boti aliyodandia ingechukuliwa na mawimbi huku hana hata chembe ya mbinu ya kuogelea.

Aliongeza: “Nililipia tiketi ya basi kutoka Dakar mpaka Morocco, haikuwa hatari ila mambo yalikuwa mabaya baadaye.

“Nikiwa Morocco nilikuwa nalala bandarini, sikuwa na fedha za kupanda boti. Kuna mwanaume aliniona hapo kwa siku kadhaa akaniuliza nilikuwa nafanya nini kulala mitaani. Nilimjibu nahitaji kwenda Ulaya.”

“Baada ya siku chache akarudi, alikuwa anfanya kazi kwenye meli iliyokuwa inaelekea Ufaransa na akaniambia tunaweza kwenda.

“Haikuwa boti kama mnazoziona kwenye Tv, ilikuwa kubwa zaidi na inasafirisha chakula. Kulikuwa na wavulana 20 wengine niliokutana nao. Nilikuwa pale kwa ajili ya soka sijui wenyewe walifuata nini, sikufahamu ndoto zao.”

“Hivyo ndivyo nilivyofika hapa na sina tofauti na wengine wote waliofika hapa kwa njia ya boti. Haikuwa hatari sana lakini sijui kuogelea, na kama boti ingezama ningeweza kufa tu.

Mamadou Coulibaly risked everything to make journey from Senegal to Italy

Coulibaly alifika Kaskazini mwa Italia, lakini maisha hayakuwa rahisi. Alikuwa mhanga wa matukio ya ubaguzi na ingekuwa bahati sana kwake kupata japo chakula cha kuhudumia tumbo lake.

Anasema kuna nyakti watu wa Italia wangeweza kumwita “Mtu wa Kwenye Boti” ili kunikashifu lakini sikujali na sikuhamaki. Wakati mgumu kabisa akiwa Livorno. Mtu Yule alinileta hapa ili anitambulishe kwa baadhi ya timu, siku moja nikaamka nipo hotelini na alikuwa ameondoka.”

“Sikuwa na fedha yoyote, sikumfahamu yoyote na sikuwa naweza kuzungumza Kiitaliano. Aliniona nikicheza ufukweni na akanipeleka Livorno kwa majaribio ambayo niliyahitaji lakini sikuwa na vielelezo vinavyotakiwa. Nilikuwa nalala mitaani na kama ningekuwa mwenye bahati ningekula sandwich pekee.”

Coulibaly akaamua kwenda kusini ambako ni mji mkuu wa Italia na mambo mengine yakatokea. Aliendelea kuishi maisha ya kujitoa mhanga akijaribu kufikia ndoto zake.

Akaendelea “wakati nilipofika Rome, wakanieleza kuwa kulikuwa kuna raia wengi wa Senegal Pescara hivyo nikapanda treni bila hata kulipa tiketi. Nikakosea na kushuka Roseto kituo tofauti hivyo ikabidi nilale uwanjani.”

“Maaskari wakanikuta na kunipeleka sehemu ya kulelea huko Montepagano.

“Nilifanya majaribio na Cesena, Sassuolo, Roma na Ascoli lakini wote hawakunichukua. Nilicheza kiasi mpira wa kishule nyumbani Senegal nikiwa mtoto na nilijifunza kucheza soka nikiwa mtaani.”

Mamadou Coulibaly came to Italy by boat, despite not being able to swim

Coulibaly hajaiona familia yake tangu aondoke Senegal na anathibitisha kuwa hawakuwahi kufahamu kama yupo hai.

Anaeleza kuwa: “Baba yangu ni mkali na mwenye misimamo, miaka miwili iliyopita nisingeweza kumwambia kuwa nipo Ufaransa, angefanya kila linalowezekana anirejeshe. Lakini kwa sasa naongea nae kila siku na anasema ana furaha na nimemwomba radhi. Nimemkumbuka mama yangu pia, sijamwona kwa miaka miwili. Nilivyoondoka alilia na hakufahamu kama nipo hai”

Naam kijana mwenye miaka 18 ambaye aliona ana uwezo wa kushinda njaa kwa muda mfupi ili ausake utajiri, huyu ambaye alivuka maji yaliyowameza wengi baharini na leo anaelekea kutimiza ndoto yake.

Nimekusogezea hapa Ngumu Kumeza ya Sports Extra Mei 19,2017

$
0
0

Katika kila kundi la wanyama kuna kiongozi ndani yake, unaweza kustaajabu kuona Nguchiro wanakiongozi lakini ndani ya Simba SC hakuna mtu wa kuwaongoza wenzake. Kama ukweli ni utupu wacha niweke wazi hakuna mtu mwenye mapenzi ya kweli ndani ya timu.

Rais wa timu amewekwa kama kivuli tu, hana kauli mbele ya kina Ben, Kolo, na Kandili nyie mnawaita marafiki wa Simba, hawa hawana lolote ndio maana miaka mitano timu inapiga-dash na pesa zao bado zinanuka.

Viongozi hawajisikii vibaya kuwanyong’onyeza wapenzi wao mtaani, wanaitwa Maandamano FC, Mezani FC, Wa mchangani FC hata wa Matopeni FC. Ni vyema kujifunza mengi sio kujifanya unajua kilakitu, Simba ina viongozi wajuaji bwana, hakuna wa kumsikiliza mwenzie kila mtu anataka lake ndio lisikilizwe yote ni kwa vile wamechoka kufikiria na ndio maana wanahisi wanajua sana.

Mo ametoa pesa nyingi sana tena inazidi hiyo aliyosema kwenye mitandao lakini kila kiongozi anataka proposal yake ndio ifanyiwe kazi ndio maana wanafelishana. Jamaa mmoja anasema, mimi sio mchoyo nitakupa jambo jipya sikioni, Mo alipelekewa bajeti ya mechi za Kanda ya Ziwa ambayo ni shilingi milioni 60, wachumia tumbo kila mmoja akawa anaitaka hiyo pesa hata mipango ya kuzitafuta pointi ikakwama timu ikaambulia pointi nne na ikaanza kupoteza matumaini ya ubingwa.

Kusaka ukweli, sawa na kumenya kitunguu, kila ganda litakutoa machozi na macho yatabaki juu. Wenye sauti ni vijana wa mjini tu ambao kazi yao ni ‘udananda’ na hawa ndio wanaopanga mchezaji gani acheze na yupi akae jukwaani.

Hata suala la kwenda FIFA limegeuzwa ‘kanyaboya’ tu, rage alidhamilia na akatoa maelekezo jinsi kila kitu kinavyoweza kufanyika lakini wakwamishaji wanadai wamepeleka, mpaka sasa sio barua wala dola 15,000 iliyofika FIFA. Hawahawa ndio wamefanya Simba ikose ubingwa kwa kuingilia mipango thabiti ya timu iliyokuwa imepangwa tangu mwanzo.

Timu ilikuwa inakwenda vizuri sana, wakaona pesa za Mo washike wao timu ikaanza kupoteza pointi. Hata huo mkataba wa SportPesa Aveva aliingizwa chaka asaini na hao vijana wa mjini wakiongozwa na mwenyekiti wa fedha na mwenyekiti wa mashindano pamoja na jamaa mmoja ana jina kama la Dogo Aslay.

Kamati ya fedha ya Simba ituambie pesa yote ya Mo imetumikaje kwa nusu msimu? Kama kila mechi tunayocheza tuna group letu la viongozi, humo wapo wabunge, mawaziri, wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya na wanasimba wenye uwezo kipesa, kila mechi tunaweka mezani milioni 5 hadi 10. Mo huyo anaetukanwa sasa ndio alikuwa anaweka kiasi kama hicho wachezaji wakishinda wanapewa, ila nimegundua kikulacho kinguoni mwako.

Wale waliokuwa hawachangii ndio walijifanya wana mipango nyuma ya pazia ndio wanahujumu timu, ikiwekwa milioni 20 na wanachama, Mo anaongeza milioni 20 jiulize timu gani ukanda huu inapata pesa hiyo nje ya mshahara?

Mo katoa zaidi ya pesa hiyo kwa Simba, kama Mo anatoa pesa yote hiyo, je kulikuwa na haraka gani kusaini mkataba na SportPesa? Hasa kipindi hiki bado mechi mbili tu, kwa nini koti la uvumilivu lisitumike ligi iishe?

Simba haina njaa kama wale, ingeweza kukaa na kufanya tathmini ya ligi ikasaini mkataba tayari kwa msimu ujao, kwa nini wanachama wasiamini Simba imepoteza hatua za mwisho kwa sababu viongozi walishindwa kujiandaa kushinda na ndio maana wakajiandaa kushindwa. Walikuwa wanawaza mpunga wa SportPesa na kusahau mipango mikakati ya timu.

Siku ya utambulisho wa jezi ya Simba inajulikana, je Simba ni ya kutambulisha jezi yake ya msimu mpya kwa utaratibu ule? Simba Day itatambulisha jezi gani mwaka huu? Kamba iliyolegea ukiwa na haraka usiivute, je Simba watarudia kuvaa jezi ileile ya msimu msimu ujao kama Aveva alivyoitambulisha kwa kuvaliwa na wachezaji kuchezea mechi kipindi cha pili, si bora angewaeleza SportPesa juu ya nyasi za Simba na uwekezaji kwenye hekaya Simba Arena.

Ufinyu wao wa kufikiri ndio maana wamezidiwa mkataba na Yanga walioishi kwa kupiga miayo msimu mzima. Hivi kuna faida gani Simba kufanya kazi na EAG Group ya kina Kajuna  ambao ni washauri wao wa kibiashara? Wakati Yanga haina mshauri wa kibiashara lakini inawazidi nje na ndani ya uwanja.

Waza tu, toka majadiliano ya dola 700,000 kwa mwaka sawa na bilioni 1.5 hivi mpaka leo wanakula milioni 800 ambayo imegawanywa na sasa inawatawala. Kamati ya mashindano ndio yenye watu wanaojifanya wapaza sauti na kati yao kila mmoja ana macho makubwa pesa ikija. Mwenyekiti wa kamati anataka yeye ndio aifanyie kazi hata kama hana njia za za kusaidia kuleta pointi tatu.

Friends of Simba mlizamisha meli mkasahau na nyie mpo ndani yake sasa pigeni mbizi hadi mwisho, ila kumbukeni uchaguzi haupo mbalina haya yaliyo tajwa mtaulizwa kwenye mkuno mkuu.

Wanachama na wapenzi wa Simba jiandaeni kisaikolojia maana lolote linaweza kutokea Dodoma, wapigisha ‘shoti’ wasio na ajira wapo miongoni mwenu na ipo siku Makala atawataja.

Barua ya Simba kwenda FIFA ni anguko lao jingine, watashindwa…

$
0
0

Na Baraka Mbolembole

INAWEZEKANA ni kweli mlinzi wa kati wa Kagera Sugar FC, Mohamed Fakhi alicheza mchezo wa Kagera 2-1 Simba SC akiwa na kadi tatu za njano, lakini Shirikisho la Soka nchini-TFF wamewapa Simba barua inayoonesha mchezaji huyo hakuwa na kadi tatu za njano-ambazo Simba wanadai ilikuwa hivyo.

MALALAMIKO YASIYO NA MASHIKO FIFA

Simba wamepeleka malalamiko yao FIFA wakiwa na nakala ya barua kutoka TFF ambayo wanadai haikuwatendea haki. Ieleweke Simba wameenda FIFA wakiwa na barua ambayo inaonyesha ‘mchezaji anayelalamikiwa’ hakuwa na kadi tatu za njano.

Kwa hiyo wanachojaribu kufanya viongozi wa Simba hivi sasa ni kuendelea kuwahadaa wanachama wao kwa sababu makosa ni yao wenyewe. Inawezekana makosa yasiwe yale ya kupoteza mchezo wa Kagera sababu bahati nzuri hawajanyang’anywa ushindi wao, bali wanapigania ushindi ambao hawakuupata ndani ya dakika 90.

Kama unaona mbali katika hili unaweza kuona malalamiko ya Simba waliyopeleka FIFA hayana ‘mashiko,’ na nachokiona ni muendelezo wa utawala kutafuta mahala pa kufichia makosa yao. FIFA haiwezi kutengua chochote katika ligi kuu ya Tanzania Bara na hata watakapoulizia suala hilo kwa TFF watajibiwa kama walivyoambiwa Simba-Fakh hakucheza Kagera 2-1 Simba akiwa na kadi tatu za njano. Mwisho.

Unadhani FIFA wataamua lolote bila kuwashirikisha TFF? Labda watajaribu kuomba kumbukumbu tu za mchezaji lalamikiwa-ambazo kimsingi hazipo na zilizopo zinamruhusu Faskhi kucheza mchezo aliocheza dhidi ya Simba.

Je, hizo kumbukumbu zipo? Kwa sisi ambao hatujaona hatuwezi kusema sana lakini tayari wale ambao waliona na kuhusika katika mchezo wa Kagera vs African Lyon hadi kwa wale waliosimamia mchezo huo wanasema ‘hakukuwa na kadi yoyote iliyotolewa na mwamuzi katika mchezo huo.’

‘Barua ya Simba SC kwenda FIFA ni anguko lao lingine, watashindwa kwa sababu barua ya TFF ilisema wazi kuwa Fakhi hakuwa na kadi tatu za njano wakati alipoichezea Kagera dhidi yao. Kama walidhamilia kushinda ‘ubingwa wa mezani’ Simba walipaswa kuvuta subira.

Baada ya katibu mkuu wa TFF kusema mbele ya vyombo vya habari kuwa Fakhi aligundulika kuwa na kadi tatu za njano ila Simba hawatapewa pointi baada ya kuwasilisha malalamiko yao nje ya muda tena bila malipo ya ada ya malalamiko, wao wangesubiri barua rasmi kisha wangeenda FIFA ambako wangepata haki yao.

Lakini kitendo cha ‘kukurupuka’ na kusema wanaenda Fifa kudai haki yao kiliwastua TFF na kuona njia sahihi ya kuwamaliza ni kuwapa barua inayosema Fakhi hakuwa na kadi tatu za njano siku anacheza dhidi yao. Hawana busara na ustahimilivu. Mchezo umeishia hapo.

FIFA husisitiza kuhusu ‘mchezo wa kiungwana’ katika soka na hawapendezwi na mabingwa wanaotokana na pointi za mezani hivyo si rahisi kuona Simba ikishinda ubingwa wa VPL kwa msaada wa ‘meza za FIFA’ baada ya kushindwa uwanjani. Naamini hilo na Yanga ndiyo mabingwa stahili wa VPL msimu wa 2016/17.

LICHA YA KUSHINDWA KUBEBA VPL, SIMBA IMEPIGA HATUA

Kuna sehemu ambazo Simba wameonekana kufanikiwa, lakini bila uwepo wa busara na hekima hata zile sehemu walizofanikiwa msimu uliomalizika wataporomoka tena kama viongozi hawatabadilika.

Mfano sehemu ya timu, ndani ya uwanja Simba wamefanikiwa kuwakusanya wachezaji wengi bora vijana raia wa Tanzania na ni hawa ambao wameisaidia Simba kupanda hadi nafasi ya pili katika ligi baada ya kumaliza nafasi ya nne msimu wa 2012/13 na 2013/14.

Walimaliza nafasi ya tatu mara mbili misimu ya 2014/15 na 2015/16 hivyo kitendo cha kumaliza nafasi ya pili msimu huu huku wakisubiri mchezo wa fainali ya FA Cup ni wazi hayo ni mafanikio makubwa kwao licha ya kutoshinda ubingwa.

Ili kushinda ubingwa wao wa kwanza Simba wanapaswa kujipanga zaidi na kusahihisha makosa yaliyowaangusha kwa misimu mitano iliyopita lakini hilo kwao ni gumu kwa sababu wanaachana na sababu za kweli na kudili na sababu za uongo kama ndizo huchangia kuanguka kwao.

KWANINI SIMBA WANAFELI KILA MSIMU?

Msimu huu uliomalizika Jumamosi iliyopita ilionekana kama vile Simba wangefanikiwa kushinda ubingwa lakini mwishoni wameshindwa kwa tofauti ya magoli tu na ‘watani’ wao wa jadi Yanga SC. Kwa jicho langu la tatu naona sababu iliyowaangusha ni ukosefu wa busara na hekima miongoni mwa viongozi-tena ni wawili au watatu tu ambao wapo pale.

Kama wataamua kufanya mambo kwa hekima na busara wanaweza kufanikiwa lakini kwa hali jinsi ilivyo si rahisi kwao kushinda hata mchezo wa fainali dhidi ya Mbao FC katika fainali ya FA siku ya Jumamosi ijayo. Simba atapoteza mchezo ujao kwa sababu ndani yao wenyewe wanatengeneza ‘hujuma’ ili timu isifanikiwe kwa maslahi ya watu wachache.

Jicho la 3: Manji amekuwa ‘mwanasoka mshindi’, ameiacha Yanga katika uelekeo

$
0
0

Na Baraka Mbolembole

‘TANGAZO la ghafla’ la kujiuzulu kwa mfanyabiashara Yusuf Manji katika nafasi yake ya uenyekiti klabuni Yanga huenda likaichanganya klabu hiyo bingwa mara 27 katika ligi kuu Tanzania Bara, lakini kwa ‘Jicho langu la 3’ naona mafanikio zaidi yanakuja ndani ya klabu.

Napenda kuchukua fursa hii kumshukuru Manji kwa kila alichoifainyia Yanga ndani ya misimu mitano aliyoisimamia klabu hiyo na kuiongoza kama mwenyekiti. Amejiuluzu kwa kile alichosema ni ‘sababu za kiafya.’

Manji amefanikiwa

Mara baada ya wanachama wa Yanga SC kushuhudia klabu yao ikichapwa 5-0 na mahasimu wao Simba, Mei, 2012 huku timu ikimaliza katika nafasi ya tatu katika ligi kuu Bara nyuma ya Simba na Azam FC wengi wao walihitaji kuona aliyekuwa mwenyekiti wa klabu wakili Lyod Nchunga akijiuzulu.

Hilo lilifanikiwa licha ya Nchunga awali kusema hawezi kuachia madaraka  ndani ya miaka miwili  tangu alipochaguliwa katika mkutano mkuu wa uchaguzi katikati ya mwaka 2010-shinikizo lilikuwa kubwa sana kwa utawala wake na atimaye aliamua kukaa pembeni baada ya wajumbe wa Kamati ya utendaji kuamua kujiuzulu.

Kujiuzulu huko kwa Nchunga kulifungua milango ya Manji kuingia klabuni hapo baada ya kushinda kwa kishindo katika uchaguzi wa dharura Julai, 2012. Nakumbuka msimu wa mwisho wa Nchunga kama mwenyekiti wa Yanga, wachezaji walikuwa katika kipindi kigumu sana. Walicheleweshewa mishahara yao mara kwa mara huku malipo ya posho zao yakiwa tatizo pia. Hilo lilichangia kwa kiasi kikubwa klabu kuyumba huku timu ikishindwa kuwa imara ndani ya uwanja.

Wachezaji mastaa wa timu hiyo kama Haruna Niyonzima ilidaiwa walikuwa karibu kutua Simba baada ya hali ya kiuchumi klabuni hapo kuwa si nzuri lakini kitendo cha Manji kuchukua fomu ya kugombea nafasi ya uenyekiti kilibadilisha upepo na nyota wengi wa Afrika Mashariki walitaka kujiunga na klabu hiyo.

Kelvin Yondani alijhiunga Yanga akitokea Simba baada ya kupewa zaidi ya milioni 30-cash, Mnyarwanda,Mbuyu Twite alisajiliwa kwa zaidi ya milioni  60 akitokea APR ya Rwanda licha ya awali kuonekana mlinzi huyo ‘kiraka’ angejiunga Simba. Huo ulikuwa ni mwanzo tu wa harakati za Manji kama mwenyekiti wa klabu hiyo ambayo alianza kuifadhili miaka takribani 12 iliyopita.

Misimu mitano sasa Manji anang’atuka Yanga akiwa ameisaidia klabu kutawala soka la Tanzania. Ameshinda mataji manne ya ligi kuu,  mawili ya Ngao ya Jamii, moja la klabu bingwa Afrika Mashariki na Kati, moja la FA Cup huku akiiwezesha timu hiyo kufika hatua ya makundi katika michuano ya Caf Confederation Cup 2016.

Kwa kiongozi yoyote haya ni mafanikio makubwa hasa ukizingatia yamepatikana ndani ya miaka mitano tu. Yanga wana kila sababu ya kumshukuru Manji kwa sababu amewasaidia kwa kiasi kikubwa kuimarisha ‘uhai’ wa klabu na historia yao ‘isiyoshindika.’

Mishahara ya juu 

Katika soka la kisasa si rahisi klabu kufanikiwa ikiwa wachezaji hawalipwi vizuri. Na licha ya kutokuwa na ufahamu mkubwa katika mambo ya soka wakati anaingia madarakani Julai, 2012, Manji alidhamilia kuifanya Yanga kutawala soka la ndani na kupiga hatua Kimataifa.

Hili afanikiwe kuhusu hilo aliamua kuwapa uhuru makocha na watendaji wa klabu kuwasaini wachezaji bora na hakusita kukubali kuwalipa mishahara mikubwa. Hii imewasaidia kwa kiasi kikubwa wachezaji kuimarisha maisha yao huku wakitoa mchango mkubwa kwa timu ndani ya uwanja.

Haruna Niyonzima, Kelvin, Mbuyu Twite ni baadhi ya wachezaji wa mwanzo wa Yanga kulipwa mishahara minono na sasa mishahara ya nyota kama Mtogo, Vicent Bossou, Mzambia, Obrey Chirwa,Wazimbabwe, Donald Ngoma na Thaban Kamusoko inaisimamisha klabu juu katika ulipaji wa mishahara ya wachezaji.

Wakati nyota hao wa kigeni wakilipwa zaidi ya milioni 7 kila mmoja kuna rundo la wachezaji wazawa pia wamekuwa wakilipwa mishahara mizuri. Ulipaji huu wa mishahara umeifanya klabu kuwa imara katika soka la ndani na hili nampongeza sana Manji kwa kuleta mapinduzi ya kweli katika soka la Tanzania.

Katikati ya mwaka 2008, Manji akiwa mfadhili tu wa klabu alisaidia usajili wa mlinda mlango Juma Kaseja kutoka Simba na kujiunga Yanga. Usajili wa Kaseja ulifungua ‘kufuri’ la wachezaji wa Kitanzania ambao awali walikuwa wakisajiliwa chini ya milioni 15.

Kaseja alisaini Yanga kwa zaidi ya milioni 35 mwaka 2008 na alikuwa mchezaji wa kwanza katika historia ya VPL kulipwa mshahara wa milioni moja. Haya ni sehemu ya mapnduzi ya kweli ambayo Manji aliyaleta katika soka la Tanzania na ningependa kumpongeza kwa kila alichofanya kwa vijana wengi wa kiafrika-kuwapa maisha ya kukidhi mahitaji yako.

Alikubali kujifunza

Ndani ya miezi yake mitatu ya kwanza ya uongozi kama mwenyekiti wa Yanga, Manji aliwaajiri makocha wawili. Mbelgiji, Tom Saintfiet na Mholland, Ernie Brandts na hadi anatangaza kujiuzulu nafasi yake Jumanne hii, Manji alifanya kazi na makocha watano tofauti huku Mholland, Han van der Pluijm akifanya naye kazi kwa vipindi viwili tofauti.

Wengine ni Mbrazil, Marcio Maximo ambaye alifanya kazi kwa miezi isiyozidi sita tu klabuni hapo. Kufanya kazi na makocha watano ndani ya miaka mitano  ndani ya uongozi wake sitazami kama sababu ya kumlamu Manji bali kuna wakati alilazimika kufanya hivyo ili klabu ifanikiwe ndani ya uwanja.

Alimfukuza kazi Tom kwa sababu tu aliambiwa ‘yeye si mfanyabiashara wa kimataifa’, aliwaondoa Brandts na Maximo kwa sababu tu walipoteza michezo ya ‘Nani Mtani Jembe’ dhidi ya Simba, lakini  namna alivyofanya kazi na Hans misimu  miwili ya mwisho  ni wazi alionekana kujifunza mengi na bila shaka ‘ Manji alikuwa mwanafunzi mzuri’ ambaye alijitahidi kusahihisha makosa yake kila alipokuwa akisonga mbele.

Yanga itaendelea kusimama?

Miezi kadhaa iliyopita baada ya taarifa za kujiuzulu kwa Manji zilipotoka wanachama wa klabu hiyo walionekana kuchanganyikiwa sana na walimlaumu Mzee Akilimani na baraza lake la Wazee wa klabu . mzee Akilimali alipinga mpango wa Manji kutaka kuikodisha klabu hiyo kwa miaka kumi na kuwa ‘Yanga Yetu.’

Upande wangu niliwaunga mkono Wazee hao na nakumbuka niliandika makala ( humu www.shaffihdauda.co.tz) iliyokuwa na kichwa cha habari, ‘ YANGA INAWEZA KUISHI BILA MANJI ILA WATAMKUMBUKA, MANJI HAWEZI KUISHI BILA YANGA, ATAIKUMBUKA…’

Huo ndiyo ukweli na wana Yanga hawapaswi kusikitika hivi sasa zaidi ya kutafuta namna nyingine ya kuendelea kuishi, kuwalipa vizuri wachezaji wao na kuisapoti klabu. Jambo la muhimu na la haraka ni klabu kwenda kwenye uchaguzi mdogo na katika hili kaimu mwenyekiti wa klabu, Clement Sanga ni kuhitisha uchaguzi wa haraka wa kujaza nafasi iliyoachwa wazi na Manji.

Huu ni wakati ambnao Yanga inapaswa kuwasaini wachezaji wake bora wanaomaliza mikataba na wale wapya ambao watapendekezwa na kocha Mzambia, George Lwandamina hivyo kwa namna yoyote ile wanapaswa kufanya uchaguzi haraka ndani ya miezi minne kabla ya kuanza kwa msimu mpya.

Yanga inaweza kuishi bila Manji ikiwa tu uongozi wa sasa utaendelea kutafuta wadhamini zaidi. Si lazima wapate mdhamini mwenye uwezo wa kuwapa bilioni moja kwa mwaka,  hapana ili klabu ifanikiwe wakubali kuwafungulia milango wadhamini wengine wenye kipato  cha kati ambao wanaweza kuwapa hata milioni 500 kwa mwaka.

Kuwa na wadhamini wane wenye uwezo wa kuipa klabu walau milioni 500 kwa mwaka itamaanisha Yanga kuingiza bilioni 2 kwa mwaka na hilo linawezekana kama uongozi utaamua kuimarisha idara yake ya masoko na kuwapa nafasi wadhamini wadogo wadogo.

Yanga itamkumbuka Manji kwa mambo mengi kwa maana chini yake klabu ilikuwa ikifanya maandalizi ya uhakika kabla ya msimu, aliisafirisha timu kwa lengo la kujifunza mara kadhaa barani ulaya. Hakika Manji ni ‘mtu wa Yanga’ hasa na uamuzi wake wa kujiuzulu umekuja wakati mwafaka sana.

Amejiuzulu wakati mwafaka

Ingekuwaje endapo Manji angejiuzulu wakati timu ikiendelea kugombea ubingwa wa ligi kuu? Bila shaka ingekuwa tatizo ambalo lingewaathiri  sana wachezaji na kuathiri utendaji wao kama timu ndani ya uwanja.

Kila mwana Yanga anafahamu ni kiasi gani Manji anapitia nyakati ngumu katika maisha yake binafsi lakini kuendelea kubaki  na klabu hadi mwisho wa msimu  ni jambo la kufurahisha sana na kumshukuru pia. Manji amekuwa ‘mwanasoka mshindi’ na ameiacha Yanga katika uelekeo sahihi. Sasa ni wakati wa wanachama kuchagua mtu sahihi wa kushika kijiti kilichoachwa na Manji. Yanga SC-Daima mbele nyuma mwiko.

Hakutanga kuharibu malengo ya timu-kushinda taji la 3 mfululizo ndiyo maana licha kukumbwa na misukosuko  mingi hivi karibuni aliamua kuonyesha yuko nao.  Nadhani watu wa Yanga wanapaswa kumshukuru tu Manji licha ya kwamba kama mwanadamu alikuwa na mapungufu yake. Amejiuzulu wakati ambao anaona Yanga inaweza kupata kiongozi mpya na kusaidia sajili na maandalizi ya msimu ujao.

Kueleka UCL Final: Mambo 6 ya kuitia wasiwasi Madrid – dhidi ya Juve

$
0
0

Real Madrid wanauwinda ubingwa wa 12 wa kihistoria wa Champions League lakini kuna mambo 6 ambayo wanapaswa kuyaangalia kwasababu huenda yakawa kikwazo kwao. 
Mkosi wa bingwa mtetezi 

Endapo watafanikiwa kutwaa ubingwa wataweka historia ya kuwa timu ya kwanza kutetea ubingwa wa CHAMPIONS LEAGUE – na kuushinda mkosi ambao umewahi kuzishibda timu 4 zilizokaribia kuvunja rekodi hiyo. 
Mnamo msimu wa 1993/94, AC Milan waliifunga Barcelona 4-0 katika fainali  kabla ya kuja kufungwa 1-0 na Ajax katika fainali ya msimu uliofuatia. Juventus nao wakaifunga Ajax katika fainali ua 1995/96 kwa mikwaju ya penati – Juventus nao wakashindwa kuutetea ubingwa kwa kufungwa na Borussia Dortmund miezi 12 baadae. 
Msimu wa 2007-08, Manchester United waliifunga Chelsea kwa penati na wao wakaja kupoteza miezi 12 baadae mbele ya Barcelona 

Mabingwa wa Klabu Bingwa ya Dunia

Tangu kuanzishwa kwa mashindanonya klabu bingwa ya dunia, haijawahi kutokea kwa mshindi wa michuano hiyo kwenda kubeba Champions League Trophy katika msimu huo huo. 

Mkosi wa mchezaji wa zamani 

Wachezaji wa zamani wa Real Madrid, Gonzalo Higuain na Sami Khedira, watakuwa katika kikosi cha Juventus na watapambana kwa kila hali kuweza kuidhuru timu yao ya zamani.  

Hata hivyo Juve nao watakuwa na pambano lao dhidi ya mkosi huu kwa Alvaro Morata ambaye aliwadhuru Madrid misimu miwili iliyopita timu hizi zilipokutana katika semifinal ya michuano hii. 
Mwaka Tasa 

Real Madrid hawajawahi kushinda ubingwa wa ulaya katika mwaka ambao haugawanyiki – mwaka tasa katika karne hii ya 21. Mara mwisho  kushinda Champions League ilikuwa mwaka 1959. 

Wapinzani wa Kiitaliano 

Historia inatuambia ni wakati wa kikosi cha kiitaliano kushinda UCL, kwa sababu kila baada ya miaka 7 kikosi cha waitaliano kimekuwa kikishinda Champions League – mara mwisho kwa waitaliano kushinda UcL ilikuwa miaka 7 iliyopita- Milan walibeba 2003 na miaka 7 nyuma mwaka 1996 Juventus walibeba. 

Jezi za Zambarau 
Madrid watakuwa ugenini katika mchezo huu wa fainali, hivyo watavaa jezi za Zambarau na katika msimu huu wamepoteza mechi mbili ambazo walivaa jezi hizo. 


Kuelekea UCL Final: Takwimu 10 za mchezo wa Real vs juve

$
0
0

Zimebaki takribani siku 4 kabla ya ulimwengu wa soka kushuhudia mtanange wa fainali ya ligi ya mabingwa wa ulaya kati ya miamba ya Italia na Spain – Juventus na Real Madrid. 

Kuelekea mchezo huo wa fainali naendelea na mfululizo wa mambo mbalimbali yanayohusiana na mchezo huo.

TAKWIMU 10

• Real Madrid wanahitaji kufunga goli moja zaidi ili kuwa timu ya kwanza kutimiza magoli 500 katika historia ya UEFA Champions League, kuanzia hatua ya makundi mpaka fainali. 
• Dani Alves alicheza mchezo wake wa 99 wa UEFA Champions League vs Monaco. Jumamosi ijayo atakuwa mchezaji wa 31 kutimiza mechi 100 katika mashindano hayo. 

• Kipigo cha Real Madrid vs Atletico katika nusu fainali ya kimewaacha Juventus kuwa timu pekee ambayo haijapoteza mchezo hata mpaka sasa katika michuano hiyo. The Bianconeri wanaiwinda rekofi ya kushinda ubingwa UEFA Champions League bila kupoteza mchezo hata mmoja – na kuifikia rekodi ya Manchester United ya 2008. 

• Madrid na Juve wote watakuwa wanacheza fainali zao za 6 za UEFA Champions League, wanaifikia rekodi ya AC Milan. 

• Madrid wameshinda mechi zao zote 5 za fainali za UEFA Champions League, wana rekodi nzuri kwenye michuano hiyo wakati Juventus wamepoteza mchezo wa fainali za UCL kuliko timu yoyote – mara 4. Ushindi wao pekee ulikuja dhidi ya Ajax kwa mikwaju ya penati mnamo mwaka 1996. 

• Ukiiondoa Madrid ambao wana rekodi 💯 ya kushinda fainali za UEFA Champions League –  Marseille (1993), Porto (2004) na Internazionale (2010) ambao wamecheza fainali ya UCL mara 1 nao wana rekodi hiyo pia. 

• Madrid wana lengo la kuwa timu ya kwanza kutetea ubingwa UEFA Champions League. AC Milan (1989, 1990) chini Ariggo Sacchi walikuwa timu ya mwisho kutwaa ubingwa wa Kombe la Ulaya mfululizo, timu nyingine ziliwahi kusogelea kuivunja rekodi hiyo ni Milan (1994, 1995), Ajax (1995, 1996), Juve (1996, 1997) and Man. United (2008, 2009) – wote hawa walifika fainali baada ya kutwaa ubingwa msimu uliopita lakini walifungwa – Je Madrid atauvunja mwiko huu. 

• Zinédine Zidane anaitafuta rekodi ya kwanza kubeba ubingwa wa UEFA Champions League mara mbili mfululizo – wakati Ramos anaitaka rekodi ya kuwa nahodha wa kwanza kubeba taji hilo mara mbili..

• Bila kuhesabu mwaka 2017, Italy na Spain ndio nchi ambazo vilabu vyake vimeingia fainali mara nyingi zaidi – kila nchi mara 27; Spain wameshinda mara 16 katika hizo mara 27 na Italy wamebeba mara 12 na kupoteza mara 15. 

• Hii itakuwa mara ya 4 kwa vilabu vya nchi hizi mbili kukutana na UEFA Champions League – mara nyingi zaidi kuliko pair nyingine ya vilabu vya nchi nyinginezo – vilabu vya England v .

‘Simba inapaswa kuachana na Omog na kumtazama mkali huyu wa mbinu’

$
0
0

Na Baraka Mbolembole

NAAMINI moja kati ya mabadiliko muhimu katika kikosi cha Simba SC ni kuachana na kocha wake Mcameroon, Joseph Omog.

Licha ya kuisaidia Simba kushida ubingwa wa kombe la FA na kushindwa kwa tofauti ya magoli na mabingwa Yanga SC katika ligi kuu Tanzania Bara 2016/17, makosa binafsi ya Omog yaliigharimu sana timu hiyo na yalikaribia kuwaangusha katika fainali ya FA vs Mbao FC.

Omog inawezekana alifanikiwa kama kocha wakati alipoisaidia AFC Leopard ya Congo Brazaville kushinda ubingwa wa Caf Confederation Cup 2012, na akashinda ubingwa wa VPL 2013/14 akiwa kocha wa Azam FC, lakini Mcameroon huyo ameonyesha wazi udhaifu wa kimbinu huku suala la ufundi likinipa shaka mara kwa mara.

Kupoteza uongozi wa 2-0 walioupata Azam FC vs El Merreikh ya Sudan katika uwanja wa Azam Complex kisha kuondolewa katika Caf Champions League kwa jumla ya magoli 3-2 baada ya pambano la marejeano jijini, Khartoon Machi, 2015 nitaendelea kuamini kulisababishwa na mabadiliko ya kocha huyo ambaye alimtoa mshambulizi Kipre Tchetche katika kipindi cha pili.

Kipre aliwamiliki walinzi wa El Merreikh ambao waliogopa kusogea mbele wakimuhofu Muivory Coast huyo ambaye alipotolewa Azam FC wakapigwa presha kisha wakapoteza mwelekeo na kuchapwa 3-0 na kuondolewa katika michuano.

Mapambano matatu vs Hans, Lwandamina 

Ndiyo, Simba haikupoteza mchezo wowote dhidi ya ‘watani’ wao wa jadi Yanga katika michezo miwili waliyokutana katika ligi kuu na mmoja wa Mapinduzi Cup 2017  lakini kuna sababu kadhaa za kimsingi zinazonifanya niamini kocha huyo hana uwezo wa kuifanya Simba ipate ubingwa wa VPL na kuleta changamoto katika michuano ya Caf Confederation Cup mwaka ujao.

Mfano, katika mchezo wa Oktoba Mosi, 2016 ambao ulimalizika kwa sare ya kufungana 1-1 vs Yanga. Watu wanaweza kuendelea kumlaumu aliyekuwa mwamuzi wa mchezo huo Martin Saanya lakini kwa namna Simba ilivyocheza katika eneo la ulinzi na jinsi walivyopanga mashambulizi ni wazi hawakuwa bora kuliko Yanga.

Upangaji mbovu wa kikosi 

Kuwaacha nje ya kikosi walinzi kama Abdi Banda, Mganda, Juuko Murishid na kumuanzisha Novaty Lufunga lilikuwa ni kosa la kiufundi na liliwagharimu.

Kilichowanusuru Simba na kichapo ni kuwahi kuchoka kwa viungo wa kati wa Yanga lakini bado mbinu zao ndogo zilishindwa kuwapatia nafasi ya kutengeneza magoli na wakasubiri hadi dakika tatu za mwisho kusawazisha kwa mpira wa kona ya moja kwa moja iliyopigwa na Shiza Kichuya.

Kikosi cha Mholland, Hans van der Pluijm kilikuwa katika uchovu baada ya kucheza mfululizo kwa miezi zaidi ya 24 (kuanzia Kagame Cup, Julai, 2015 hadi Makundi Caf Confederation Cup , Septemba, 2016.) Hivyo wachezaji wake wengi walikuwa wakicheza huku wamechoka.

Mashabiki wa Simba waling’oa viti wakati ule na kusahau mapungufu muhimu katika timu yao. Waliamini wana timu iliyokamilika. Game ya nusu fainali Mapinduzi Cup 2017 ilimalizika kwa suluhu-tasa.

Yanga ilikuwa chini ya Mzambia, George Lwandamina tena akiwa ndani ya mwezi wake wa kwanza tangu alipopewa kibarua kilichokuwa kimeachwa na Hans.

Lwandamina hakuwa na kikosi imara kutokana na wachezaji wake wengi kuwa na majeraha lakini aliweza kumtoa jasho Omog na kustahimili pambano ambalo wengi waliamiani Simba ingeshinda rundo la magoli hasa ukizingatia Yanga ilikuwa imetoka kuchapwa 4-0 na Azam FC siku mbili nyuma.

Ushindi wa Mbinde 2-1 Februari, 2017 dhidi ya mahasimu  wao Yanga bado hauwezi kuficha madhaifu ya kocha Omog. Yanga haikuwa na makali lakini walimudu pambano kwa robo tatu ya mchezo.

Makosa yaleyale aliyofanya Omog katika mchezo wa mzunguzo wa kwanza akayarudia tena. Licha ya kucheza kwa dakika zaidi ya 50, Lufunga alionekana wazi kwenye nafasi ya beki wa kati hucheza akiwa na mashaka makubwa.

Lufunga si mzuri katika kucheza ‘tackle’ na anapojaribu kufanya hivyo hucheza faulo. Kasi yake pia ya kukimbia si nzuri ndiyo maana alionekana ‘kumilikiwa’ na Mzambia, Obrey Chirwa. Wakati mechi ikiendelea, Omog akamtoa Lufunga nafasi yake ikachukuliwa na kiungo wa kati nahodha wa timu, Jonas Mkude.

Mcongoman Besala Bokungu akaenda kucheza kati na Banda yalikuwa ni mabadiliko mazuri hasa ukizingatia Lufunga alikuwa na kadi ya njano. Kutokana na kiwango bora kabisa cha Muzamiru Yassin alichokionyesha kabla ya mchezo huo vs Yanga, uamuzi wa Omog kumpeleka Muzamiru katika beki namba 2 ulikuwa ni wa ajabu sana kwa maana aliwaacha Mghana, James Kotei na Mkude katika dimba la kati.

Viungo hao wawili si watengenezaji wa nafasi za kufunga. Kama ni ‘bahati’ basi ilikuwa kwa Omog ila mabadiliko yake ya kumtoa Lufunga na kumpa nafasi Mkude yalipaswa kumbakisha Muzamiru katika eneo la kiungo na si kumpeleka katika beki ya kulia.

Omog alinufaika sana na mbinu ya kushambulia pembeni, lakini mabadiliko yake ya kiufundi mara kwa mara yamekuwa si sahihi. Kwa namna walivyokuwa kikosi cha Omog kisingeweza kufunga magoli mengi kwa sababu alishindwa kutengeneza safu ya kwanza na ile ya pili ya washambuliaji kati ya Ibrahim Ajib, Mrundi, Mavugo, Muivory Coast, Blagnon na Juma Liuzio.

Vs Mbao FC

Kwenye mchezo wa fainali ya FA Cup, Omog aliamtumia Kotei na Mganda, Juuko Murshid katika beki ya kati. Jambo hilo liliwafanya Simba kuwa na nguvu ya ziada na ufundi katika safu yake ya ulinzi.

Mbinu hiyo ya kiufundi iliweza kuleta matunda kwa sababu mwisho wa dakika 90′, Omog aliweza kupata matokeo aliyostahili-kikosi chake kutoruhusu goli. Kotei aliweza kuwaonyesha watazamaji ni jinsi alivyokuwa bora katika beki ya kati, huku akiwa kiunganishi kizuri cha safu ya ulinzi na kuwa msaada mkubwa katika ngome ya mabeki wanne.

Lakini kama kocha angekuwa amejipanga vyema angempanga Kotei katika eneo la kiungo na kumpa nafasi Abdi Banda kucheza na Juuko katika beki ya kati kwa sababu kujipanga vyema katika safu ya ulinzi ni vizuri zaidi kama timu itamtumia Kotei kwenye sehemu ya kiungo kama kweli Omog alitaka kuona timu yake ikienda mbele kushambulia, na hili litamfanya Mkude kupoteza nafasi yake kikosini.

Kwa mechi kama ile ya fainali ambayo timu inahitaji kufunga japo goli moja, Kotei angeweza kuipatia Simba nguvu kubwa ya kushambulia ikianzia kwenye idara ya kiungo. Omog alishindwa kimbinu na kocha wa Mbao, Mrundi, Ettiene Ndayiragije.

Lakini kama kocha angekuwa amejipanga vyema angempanga Kotei katika eneo la kiungo na kumpa nafasi Abdi Banda kucheza na Juuko katika beki ya kati kwa sababu kujipanga vyema katika safu ya ulinzi ni vizuri zaidi kama timu itamtumia Kotei kwenye sehemu ya kiungo kama kweli Omog alitaka kuona timu yake ikienda mbele kushambulia, na hili litamfanya Mkude kupoteza nafasi yake kikosini.

Kocha huyo wa Mbao aliingiza timu yake kuanza mchezo kwa stahili ya kujilinda huku wakishambulia kwa kustukiza. Aliwapanga walinzi wanne, viungo watano na kumuacha mshambulizi mmoja mbele.

Omog ambaye aliwapanga washambuliaji watatu mbele, viungo watatu na walinzi wanne alishuhudia timu yake ikimiliki mpira kwa kiasi kikubwa lakini hawakuwa na mbinu za kupeleka mipira sahihi kwa washambuliaji.

Mbao walikuwa wagumu katikati ya uwanja na ili Simba ipitishe mipira walimuhitaji kiungo kama Kotei ambaye ni mchangamfu, mwenye ubunifu na pasi za uhakika. Mkude ni mzuri lakini stahili yake ya uchezaji inachelewesha sana ushindi huku akihatarisha usalama wa timu yake kutokana na upigaji wake wa ‘pasi mkaa.’

Ettiene alipogundua Simba haina makali akawaruhusu wachezaji wake kushambulia mara baada ya kuanza kwa kipindi cha pili. Jambo hilo liliwafanya Simba kuwa katika presha. Kilichowaangusha Mbao ni kutokuwa na wachezaji wengi wenye maarifa binafsi. Ettiene ameijenga timu yake kucheza kitimu huku ikiongozwa na mbinu zake ndiyo maana walipoona zimesalia dakika 15 kabla ya kumalizika kwa dakika 90′ akairudisha timu yake kucheza mchezo wa kujilinda kwa tahadhari ya hali ya juu.

Akafanikiwa kumaliza dakika 90 kwa suluhu-tasa. Alikuwa makini pia katika ufanyaji wake wa mabadiliko na hakupoteza heshima kwa wapinzani licha ya kuonekana kuwamudu.

Blagnon alipofunga goli la uongozi upande wa Simba dakika ya 109′, Etienne akaamua kuwapa uhuru wachezaji wake kushambulia na baada ya kusawazisha goli hilo wakarudi kujilinda kwa lengo la kuivusha mechi hadi katika hatua ya mikwaju ya penalti.

Kama kocha huyo wa Mbao FC angekuwa na kikosi chenye ubora mpana angefanikiwa zaidi lakini Omog ameendelea kudhihirisha si kocha mwenye mbinu bora zaidi hasa katika michezo muhimu.

Nadhani Simba inahitaji nyongeza ya wachezaji lakini kabla  inapaswa kumuondoa Omog na kumpa kazi mmoja kati ya makocha Mecky Mexime ama Etienne ili kuungana na Mganda, Jaclson Mayanja makocha ambao wana mbinu na ufundi huku vikosi vyao vikicheza vile wanavyotaka.

Azam wataweza kuishi wanachokiamini?

$
0
0

Azam FC imeanza kuboresha kikosi chake baada ya leo Juni 5, 2017 kuingia mkataba na mshambuliaji Waziri Junior kutoka Toto Africans ambayo imeshuka daraja, kwa mujibu wa website ya timu hiyo, Junior alipendekezwa na kocha mkuu Aristica Cioaba na amekuwa mchezaji wa kwanza kusajiliwa na Azam.

Junior alikuwa straika kinara wa Toto Africans ya Mwanza msimu uliopita, akiwa mfungaji wao bora kwa mabao sita aliyofunga.

Azam wamewapa nafasi vijana wengi kutoka kikosi cha vijana na usajili wa mchezaji wao wa kwanza ni mzawa kwa hiyo unaanza kuona wanauvaa uhalisia katika uendesha wa klabu.

Abbas Kapombe, Abdul Haji, Godfrey Elias,  Ramadhan Mohamed na kiungo Stanslaus Ladislaus ni wachezaji ambao wamepandishwa kwenye kikosi cha kwanza kutoka timu ya vijana.

Wadau inabidi wawape muda Azam kwa sababu Azam imeamua kuja na aina mpya ya uendeshaji wa klabu yao kwa kuwatumia wachezaji wanaowalea wenyewe huku wakitumia kiasi kidogo cha pesa katika usajili.

Hawajaanza kupata pesa za kutosha zinazotokana na vyanzo vya klabu kwa hiyo unaweza kuhoji pesa nyingi wanazotumia katika usajili wanazitoa wapi? Hapo ndipo kwa wenzetu Ulaya wanakutana na rungu la Financial Fair Play.

Endapo vilabu vingine vya Tanzania vitafuata nyayo za Azam katika mfumo wao mpya walioamua kuja nao, kuna kitu kikibwa tutavuna baada ya muda.

Ukiangalia timu kama Mbao FC imeweza kufanya iliyoyafanya msimu uliopita huku ikiwa na bajeti ndogo tu, kila mtu anaijua historia ya Mbao kwamba ilipewa taarifa ya kucheza ligi kuu siku chache kabla ya msimu kuanza.

Wakasajili vijana ambao hawakuwa na majina makubwa hapo kabla wakawajenga ili kupambana na moto waliouwasha msimu uliopita kila mmoja ameuona na kuvutiwa na timu hii changa kwenye soka la Tanzania.

Kwa hiyo watu wameanza kuvutiwa kwamba, inawezekana kuwekeza kwa vijana ikiwa watajengwa vizuri na kuaminiwa.

Lakini kikubwa ni suala la malengo ya klabu, kila klabu ina malengo yake na tamaduni zake iliyojiwekea yenyewe. Kuna klabu ambazo malengo yao ni kuzalisha wachezaji na kuwauza huku ikihakikisha haishuki daraja na wala haipambani kupata ubingwa. Kuna klabu ambazo ndoto zao za kila siku ni kunyanyua ‘makwapa’ hapa utazitaja Simba, Yanga pamoja na Azam.

Sasa kama Azam wataamua kuchukua ubingwa isiwe kipaumbele chao kwa kuamua kuwatengeneza vijana wao wenyewe, kuwamini na kuwapa nafasi ili badae washindane bila kutumia gharama kubwa kwa kusajili wachezaji wa bei mbaya na kuwalipa mishahara mikubwa.

Mtego kwa Azam ni kwamba, Je, wako tayari kucheza bila presha ya ubingwa? Hapa ndipo inakuja tofauti kati ya Mbao na wao kwa sababu Mbao wanacheza wakiwa hawawazi ubingwa wanachokifanya wao ni kutengeneza timu na kuhakikisha wanakuwa kwenye nafasi nzuri, kama ubingwa ikitokea wamepata kama ilivyokuwa kwa Leicester City basi ni jambo jema.

Ngasa anaweza kendelea kuibeba Yanga, lakini ni usajili wa Lwandamina au kina Mr. Kazinyingi?

$
0
0

Na Baraka Mbolembole

USAJILI wa Mrisho Ngasa kutoka Mbeya City FC na kujiunga Yanga SC unaweza ‘kufurahiwa’ wanachama/wapenzi wengi wa mabingwa hao wa kihistoria Tanzania Bara, lakini kwa ‘jicho langu la tatu’ naamini, Ngassa hawezi kuleta kipya chochote katika kikosi cha kocha Mzambia, George Lwandamina.

Ngasa licha ya kuwahi kuzichezea Azam FC (2010-2012), Simba SC (2012/13) katika soka la Tanzania kiungo huyo mshambulizi amejitambulisha kama ‘mchezaji hasa wa Yanga’ ambayo amewahi kuichezea kwa mafanikio makubwa katika vipindi viwili tofauti miaka ya nyuma.

NGASA WA SASA SI YULE WA 2006

Wakati anasajiliwa Yanga kwa mara ya kwanza akitokea Kagera Sugar FC mwishoni mwa mwaka 2006, Ngasa alikuwa bado ‘kijana mdogo’ huku kasi yake uwanjani ikiwafanya mabeki wa timu pinzani kupata wakati mgumu kila walipokabiliana naye.

Alikuwa akikimbia vizuri huku akikokota mpira, alikuwa na kasi ya kukimbilia pasi ‘iliyopenyezwa’ katika eneo la wazi. Si hivyo tu Ngasa alikuwa akicheza kwa ‘kuhaha’ eneo lote la mbele huku akiichezesha timu, kutengeneza nafasi za magoli, kupiga pasi za mwisho na kufunga magoli.

Ni wapinzani wake tu ambao hawakupenda kumtazama Ngasa lakini kwa ‘watu wa Yanga’ hadi sasa hawaamini kama timu yao imewahi kupata mchezaji bora na mwenye mapenzi ya dhati kwa timu yao kama Ngasa.

Ndiyo, Ngasa ni kati ya wachezaji bora waliopata kutokea katika soka la Tanzania ndani ya karne hii, lakini kwa sasa yuko mbali na kiwango chake kile ambacho alikionesha katika michuano ya CHAN 2009 Ivory Coast.

Majeraha na maisha ya nje ya uwanja yamepunguza kasi ya Ngasa. Sasa hakimbii mara kwa mara na mpira na amekuwa ‘mvivu’ kukimbilia pasi za kupenyeza ambazo amekua akipigiwa. Ngassa wa sasa ‘anajitafutia kieneo’ kidogo cha kukimbia na kujaribu kufanya ufundi wake lakini bado si mahiri katika upigaji wa pasi za mwisho wala ufungaji.

Wakati, Saimon Msuva akiwa bado hajafikia kiwango alichokionyesha Ngasa miaka ya 2007 hadi 2015, Ngasa wa sasa kwa upande wake anahangaika kufikia walau nusu tu ya uwezo wa sasa alionao Msuva.

SI USAJILI WA LWANDAMINA

Na kama ni usajili wa Mzambia huyo ni ishara ya ‘anguko’ la Yanga. Usajili wa Mzambia, Justine Zulu umekuwa na matokeo hasi hadi sasa na kwa mchezaji anaye ‘umia umia’ kama kiungo huyo wa kati bila shaka, Lwandamina alifanya makosa ya kumsaini mchezaji huyo. Emmanuel Martin alionwa na macho ya Lwandamina mara moja tu wakati Yanga ilipocheza na JKU katika mchezo wa kirafiki. Kiungo huyo mshambulizi wa pembeni hajaongeza kipya katika kikosi cha Yanga na Lwandamina ‘alibebwa’ na kikosi kilichosukwa na Mholland, Hans van der Pluijm.

Hans alikataa kumsaini Ngasa mara baada ya mchezaji huyo kuvunja mkataba wake wa miaka mitano na Free State Stars ya Afrika Kusini, Septemba 2016.

Hans aliondolewa Yanga huku sababu mojawapo ikiwa ni kukataa urejeo wa mara ya tatu wa Ngasa klabuni hapo. Na alisema wazi anatazama zaidi maendeleo ya Yanga ndani ya uwanja na ukuaji wa vijana kama Msuva, Deus Kaseke, Juma Mahadhi na Geofrey Mwashuiya.

Najiuliza kipi kimemvutia Lwandamina hadi kutaka kumsaini ‘Ngasa mkaa benchi’ katika kikosi cha City, au ni usajili wa ‘kina-Mr. Kazinyingi’ unarejea Yanga? Hassan Kabunda, Rafael Daud walifaa zaidi kuchukua nafasi ya Ngasa.

NGASA ANAWEZA KUENDELEA KUIBEBA YANGA

Kama yeye mwenyewe ataitumia nafasi hii ‘inayoweza’ kuwa ya mwisho kwake kuvaa jezi ya Yanga, jambo la kwanza ahakikishe anapambana kuyashinda majeraha yake ya mara kwa mara.

Akiwa fiti walau asilimia 70 anapaswa kupambana kuingia katika kikosi cha kwanza chenye washambuliaji watatu au wawili. Ngasa wa sasa anaweza kukupa faida kama utamuondolea majukumu ya kukimbiza timu na kumpa nafasi ya kucheza karibu na goli.

Ngasa anajua kufunga hivyo si ajabu akaendelea kuchanua katika timu ya ‘ndoto zake’ na kujikita katika mioyo ya wana Yanga.

Karibu tena Yanga, Mrisho Ngasa hata kama ni urejeo wa sajili za Mr. Kazinyingi kuna kundi kubwa la mashabiki linaunga mkono usajili wako, kazi kwako na Lwandamina. Mashabiki wa Yanga wana mapenzi ya dhati ila ‘wana kinai’ haraka.

Kama ilikupita Ngumu Kumeza ya Sports Extra June 9, 2017

$
0
0

Safari ya kwenda Gabon haikuwa rahisi jamani, huenda wale vijana waliyaona aliyoyaona Sinbad kwenye safari zake saba. Waliondoka waliondoka wakiwa na umri mdogo lakini ila wamerejea wakiwa na umri wa wahenga kutokana na kutumikishwa na kwa faida za siasa za mpira .

Timu ilianza kugawanywa hapahapa tangu safari ya kufuzu, ukolono ulitumika kugawanya ili uweze kuwatawala ilitumiwa vizuri sana dhana hiyo na uongozi wa TFF, na hiyo sumu uliwalevya mpaka wachezaji na ndyo maana wakasahau ile silaha kubwa kuliko zote duniani ‘umoja ni nguvu’ ndani ya Serengeti kulikuwa na timu mbili halafu bado tuliamini mtafikia malengo. Hivi kwa mpasuko ule halafu tupate mafanikio kweli?

Team Kim ambayo ilikuwa inaongozwa na Rais wa Shirikisho, alifanya hivyo ili kujivua gamba na kuvaa gwanda si unakumbuka alivyomfukuza Kim enzi zile bila kufikiria, lakini pia kulikuwa na team Shime ambayo iliponzwa na fikra nyeusi. Wao hata kama wangefanya zuri, lilifichwa na rangi ragi yao. Si unajua sifa moja wapo ya giza ni weusi usiong’ara na ndio maana hata mchimbaji mdogo wa Nyamongo hana thamani sawa na mchimbaji mdogo wa toka nje ya bara la watu weusi hata mitaji ikiwa sawa.

Kuna wachezaji wametengenezewa mazingira ya kuchagua upande na hata hilo ni moja ya mambo yaliyoiathiri timu kwenye vyumba vya kubadilishia nguo. Mchezo wa kwanza Kim na Shime walipishana juu ya wachezaji Shabani Zuberi na Mohamed Rashid, Kim akitaka waanze ilhali wanamajeruhi huku Shime akitaka wasicheze kitu kilichosababisha timu kushindwa kufanya mabadiliko ya kiufundi badala yake ikafanya kuwatoa wagonjwa.

Alisikika mjumbe mmoja anasema, kama Shime hatotoka Stars akaenda na Serengeti Boys mi Gabon siendi, ndiyo maamuzi yakachukuliwa vinginevyo ‘Mchawi mweusi’ sfari ya Gabon angekuwa sehemu ya hadhira.

Pamoja na maandalizi ya muda mrefu bado timu iliamini kwenye ushirikina, timu haikuwa na mganga India wala kwingineko, naambiwa tangu awali timu ilianza na Mungu wengi tuliamini safari yetu itaendelea hivyo lakini lakini kuanzia kwenye mchezo dhidi ya Congo waumini wa ushirikina walimleta mganga na kwakweli tulianza kushinda kwa taabu tofauti na kabla hatujaanza kuroga ambapo tulikuwa tunashinda kirahisi.

Siku moja kabla ya mchezo wa mwisho wa makundi mtaalamu wa psychology anarudishwa nyumbani kama sehemu ya kubana matumizi, mdomo wangu ulikuwa wazi unaweza kuhisi mamba anaota jua yote ilikuwa mshangao.

Hivi ni bajeti gani mlikuwa mnabana wakati watanzania walikuwa wanachanga au lengo lilikuwa kubaki na chenchi, bajeti ya mtu wa saikolojia haipo eti tuliweka kwenye maandalizi tu ila ya mganga na masuala ya ushirikina ipo. Kwa joto la jiwe kuelekea mchezo wa mwisho dhidi ya Niger tulimuhitaji mtaalamu wa saikolojia kuliko mganga wala mchawi, wachezaji walipaswa kupunguziwa mzigo wa fikra na sio kutwishwa mzigo wa hirizi.

Mtu mmoja anasema hata mkuu alisikika akisema, wakati huu tunahitaji kuongeza wataalam kuliko wakati mwingine wowote. Wakati watu muhimu wanarudishwa nyumbani, washauri wa rais walibaki kutumbua fedha za wavuja jasho wa Tanzania nchini Gabon. Nikakumbuka shairi la Mohamed Seif Khatib ‘Wenye navyo watubana.’

Mnadanganya pesa pesa za watanzania zimetupeleka kambi Morocco, mnakosea kule kila kitu kiligharamiwa na shirikisho la soka la Morocco. Muda wote wa kambi ya kule wachezaji waliwahi kupewa dola 100 tu kwa safari nzima na kambi ya siku saba timu ilipokaa Cameroon iligharamiwa na wenyeji. TFF iligharamia siku tatu za nyongeza za kukaa Cameroon kuanzia Mei 11 timu ianza kugharamiwa na CAF kwa wachezaji 21 na viongozi saba.

Timu yetu ilikwenda na wachezaji 23 hivyo wawili ndio walikuwa wanagharamiwa na TFF, inamaana matumizi ya wachezaji wawili yalikuwa makubwa kuliko kuwalea wale mapacha wawili wa Rais? Natanika na pacha wake Natandua.

Hamasa bila taratibu za kisayansi ziliiua Serengeti Boys, unajua tulilazimisha kucheza michezo mingi kwa muda mfupi kitu kilichosababisha wachezaji kuchoka kabla ya mashindano na wengine kupata majeraha. Michuano inaanza Rais wa TFF anakwenda Gabon, wachezaji wakamtolea uvivu wanataka walipwe malimbikizo ya madeni yao yote, Rais aliahidi baada ya michuano.

Na kuanzia Mei 11 wachezaji walianza kupikea posho ya dola 20 sawa na 44,000 ya kitanzania ambayo walilipwa mpaka tarehe 21 siku waliyotolewa na Niger, najiuliza kwa nini bajeti ya timu iliishia kwenye makundi au inamaana hakuna kiongozi aliyeamini tutavuka kwenye makundi ndio maana posho ya bajeti ya timu iliishia hapo?

Pamoja na timu kurejea tarehe 26 lakini siku tano kati ya tarehe 21 mpaka 26 hakuna mchezaji aliyepewa posho, timu inarudi Tanzania kambi inavunjwa kwa wachezaji kupewa 20,000 kwa wale wanaoishi Dar, 30,000 kwa wa Morogoro huku wale wa Mwanza wanapewa nauli ya 45,000 bila kupewa malimbikizo ya madeni yao.

Wachezaji wanarudi majumbani mwao wakiwa na masikitiko makubwa, mifukoni jua kali ndiyo maana wengi wao leo wanacheza mechi za vichochoroni, wakati wakiwa kambini walikuwa wanachugua viwanja hata vya kufanyia mazoezi.

Yule mchezaji ambaye alirudishwa kwa kuumia kwenye mashindano Ally Makamba yupo kwao Dodoma ametelekezwa na timu hapewi matibabu yoyote, wachezaji wenzie wa Serengeti Boys wameanzisha harambee maalum ya kumchangia mwenzao japo hata wao hali zao sio njema.

Jamani eeh kwa anayejua namba ya huyu Abdallah Hashim basi aiweke hewani watanzania waanze kumchangia, kama tuliichangia Serengeti Boys wakati ule tutashindwa kumsaidia akiwa pekeake?

Kiufupi wachezaji wa Serengeti Boys hawajafaidika na michango ya wasakatonge wa Tanzania bali pesa ile imewasaidia zaidi wajumbe wa kamati kupishana angani kama watumishi wa serikali wa awamu iliyopita, maana walikuwa hawatulii kama vile kuku anaetaka kutaga mara siku moja mjumbe yupo Rabat siku mbli yupo Tanzania siku ya tatu kaenda Yaund Yaunde.

Watanzania tunapenda maigizo hilo alilithibitisha kiongozi wa msafara ‘mzee wa kuzimia’ aliyafuga machozi, hakulia pale tulipotolewa uwanjani eti kaja kulia alipomulikwa na camera za nyumbani jamani tuacheni masuala ya Kaole kwenye mpira.

Kamati kwa kushirikiana na TFF watanzania wanataka muweke wazi mapato na matumizi ya michuano yote, TFF ituambie ile dola 60,000 ya Serengeti kumaliza nafasi ya tatu kwenye kundi imeshatolewa na CAF au mshaibadilishia matumizi itumike kwenye uchaguzi.

Tahadhari kambi ya wachezaji waliopo Mwanza iangaliwe mara mbili kutokana na michuano ambayo tumetoka kupata somo, hivyo basi tuangalie namna ya kuwaandaa watoto bila kuwadhulumu kuelekea michuano ya mwaka 2019 ambayo sisi ndio wenyeji.

Najua baada ya kuweka uchafu huu hadharani, baadhi ya viongozi wa mpira wanatukana huko ila hivyo ndiyo ndoto ya Gabon mpaka kombe la Dunia ilivyoyeyuka na sasa yamebaki mashimo ya madeni kwenye nyongo za wahusika.

Viewing all 676 articles
Browse latest View live


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>