Quantcast
Channel: Makala – ShaffihDauda
Viewing all 676 articles
Browse latest View live

Usajili: Man Utd imetumia mara 14 ya Bajeti ya mwaka ya Wizara ya Michezo TZ kuunda Ukuta wake 

$
0
0

Klabu ya Manchester United jana usiku ilitangaza kufikia makubaliano na klabu ya Benfica juu ya uhamisho wa beki Victor Lindelof kwa ada ya uhamisho ya £31m ambazo ni zaidi ya bajeti ya mwaka ya WIzara ya Michezo ya Tanzania (Bil 28).

Usajili huo wa Victor Lindelof unaifanya United iwe imetumia zaidi ya Euro millioni 161 tangu Sir Alex Ferguson alipostaafu miaka 4 iliyopita ili kuimarisha safu ya ushambuliaji. Daley Blind, Luke Shaw na Marcos Rojo wote waliwasili Old Trafford miaka 3 iliyopita, kabla ya Matteo Darmian mwaka 2015 na Eric Bailly mwaka 2016. 

Kwa maana hiyo United wamesajili angalau beki mmoja katika kipindi cha misimu minne iliyopita. 


Mpaka sasa usajili wa gharama zaidi katika mabeki hawa 6 ni Bailly, ambaye alisajiliwa akitokea Villareal kwa €38m – akifuatiwa na Luke Shaw ambaye alisajiliwa kwa €37m, Lindelof inaripotiwa ni €31m, kisha Darmian 18m Euros na Blind – United waliilipa Ajax kiasi cha 17.5m, na hivyo United wametumia €161m kuunda ukuta huu – hii ni zaidi ya billion 404 za Kitanzania ambayo ukiigawanya kwa Bil 28 ambazo ni bajeti ya mwaka wa fedha 2017/18 ya Wizara yenye dhamana ya michezo – inaingia takribani mara 14. 


Stars itapigwa nyingi vs Uganga kwa beki ya Banda/Mbonde, Samatta ni namba kumi…’

$
0
0

Na Baraka Mbolembole

WAKATI alipokutana na waandishi wa habari kwa mara ya kwanza baada ya kutangazwa rasmi kubeba mikoba ya kuiongoza timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ mwanzoni mwa mwaka huu, kocha Salum Mayanga aliahidi mabadiliko.

Upande wangu niliamini hivyo pia lakini sikudhani kama mabadiliko hayo yamelenga kumaliza zama za Kelvin Yondan ambaye ni miongoni mwa mabeki bora wa kati waliopata kutokea nchini katika kipindi cha muongo mmoja uliopita.

Kwa namna Abdi Banda na Salim Mbonde walivyocheza katika beki ya kati wakati Stars ilipocheza na Lesotho katika mchezo wa kwanza kuwania kufuzu kwa fainali za AFCON 2019 ni wazi kocha, Mayanga anapaswa kutazama tena uamuzi wake wa kumuacha kikosini, Yondan na kutomtumia mlinzi mwenye uzoefu, Erasto Nyoni katika mchezo wa Jumamosi iliyopita.

Timu ya taifa ni mkusanyiko wa wachezaji bora

Kwa wakati ambao kocha yoyote huteua kikosi cha timu ya Taifa, wachezaji waliofanya vizuri katika klabu zao hupewa nafasi kisha kocha hufanya kazi yake ya kukisuka kikosi kimbinu na kiufundi.

Uteuzi wa kwanza wa Mayanga mwezi April wakati Stars ilipocheza mechi mbili za kirafiki dhidi ya Botswana na Burundi ulikuwa mzuri. Na kikosi alichokiteua sasa si kibaya lakini ukitazama kwa umakini unaweza kuona ni kama kocha huyo ameamua kumaliza nyakati za baadhi ya wachezaji kuichezea Stars licha ya kwamba wanaweza kutoa mchango mkubwa kuliko waliopo sasa.

Kumekuwa na ‘ukiritimba’ mkubwa katika uteuzi wa timu ya Taifa. Kumjumuisha kikosini mshambulizi, Thomas Ulimwengu ulikuwa ni uamuzi mzuri kwa sababu niliamini, Mayanga amefanya hivyo ili kutaka kujua maendeleo ya mchezaji huyo wa zamani wa TP Mazembe hasa ukizingatia Stars itakuwa na michezo mingine dhidi ya Uganda na Cape Verde.

Lakini kitendo cha kumuanzisha na kumpa nafasi ya kucheza kwa zaidi ya saa moja vs Lesotho yalikuwa ni makosa makubwa kwa sababu, Ulimwengu hajacheza mchezo wowote wa ushindani tangu alipoichezea Mazembe vs Yanga SC katikati ya mwaka uliopita.

Mayanga hawezi kukwepa lawama katika hili. Ulimwengu hakucheza katika michezo miwili ya mwanzo ya Mayanga kama kocha wa Stars na hilo lilitoa nafasi kwa Ibrahim Ajib kuanza na nahodha, Mbwana Samatta katika safu ya mashambulizi.

Kuwapanga Samatta na Ulimwengu katika mfumo wa 4-4-2 haukuwa uamuzi sahihi na haupaswi kutumiwa tena. Pia kumpanga Samatta kama mshambulizi wa kwanza katika mfumo wa 4-3-3 pia si sahihi ingawa amekuwa akipangwa mara kadhaa katika nafasi hiyo akiichezea klabu yake ya KRC Genk.

Samatta ana uwezo wa kumalizia mashambulizi, na anaweza kupambana na mabeki wa kati katika mipira ya juu lakini kuendelea kumfanyisha kazi hiyo kwa dakika 90 akiwa Stars inamaanisha kupoteza uwezo wake usio wa kawaida.

Samatta ni namba 10

Hata kama Stars inakabiliwa na mapungufu katika utengenezaji wa nafasi na upigaji wa pasi za mwisho, Samatta anaweza kupewa mpira na yeye akajua cha kufanya ili timu ipate matokeo. Mayanga amepata bahati ya kufanya kazi na ‘mvumbuzi mkubwa’ wa mambo katika timu yake.

Samatta ana uwezo wa kuzunguka nusu ya uwanja na ‘kutumbukia’ katika sehemu ambazo mabeki hawatarajii uwepo wake huku akifanya kazi ya kuichezesha na kuikimbiza timu, huku akipachika magoli kwa mashuti yake ya mbali.

Huyu si tu ndiye mchezaji mbunifu zaidi katika kikosi cha Stars bali ndiye mchezaji ‘mzalendo’ anayejituma zaidi. Ili kunufaika naye na kupata mchango wake mkubwa kwa timu, Mayanga anapaswa kumpa uhuru Samatta acheze anavyotaka.

Kumpanga namba 9 ni kumnyima nafasi ya kufurahia mchezo na kumpanga namba kumi itakuwa ni sawa na kumfanya awe huru kucheza na hilo litaisaidia sana Stars. Mayaoga anapaswa kuanza kufikiria namba bora ya Samatta anapokuwa uwanjani na asijaribu kumuweka katika mfumo utakaomnyima uhuru.

Itakuwa vyema sana kama mifumo ya kiuchezaji ya Mayanga itamwachaitamwacha Samatta afanye chochote anachoweza kufanya akiwa uwanjani.

Tatizo la beki ya kati

Shomari Kapombe na Gadiel Michael walicheza mchezo wa nguvu na kusaidia kupeleka mashambulizi mbele kadri ilivyowezekana wakitokea katika beki za pembeni lakini kwa Banda na ‘patna’ wake Mbonde mambo yalikuwa tofauti sana kwa sababu walinzi hao wa kati walishindwa kumdhibiti mfungaji wa goli la kusawazisha la Lesotho kwa sababu tu ya ‘uvivu’

Walinzi hao walikabia macho kuanzia krosi inapigwa kutokea upande wa kulia wa Stars na kumuacha mfungaji akiwa huru japo kulikuwa na wachezaji watatu wa Stars karibu yake. Ili kucheza vizuri vs Uganda ambao waliishinda 1-0 Cape Verde siku ya Jumapili, Mayanga anapaswa kubadili mfumo wake na huu ni wakati wa kutumia mfumo tofauti ili kupata uimara zaidi katika ngome.

Banda na Mbonde hawawezi kucheza pamoja kwa sababu stahili yao ya uchezaji inafanana na hakuna anayeweza kumtuma mwenzake. Nakumbuka mika ya Mbrazil,Marcio Maximo kocha huyo alitamani sana kuona Victor Costa na Hamis Yusuph wakicheza pamoja lakini wawili hao walishindwa kutoa matunda mazuri kila walipopangwa pamoja katika beki ya kati kwa sababu wote walikuwa wakicheza stahili moja.

Ili kuleta balansi katika timu ni lazima uimara uwe kila idara, katika golikipa Aishi Manula yuko vizuri na alijitolea sana vs Lesotho na kuisaidia Stars isiangushe pointi zote nyumbani. Mayanga anapaswa kutazama upya uwezo wa Kelvin na kumuamini Erasto vinginevyo atapigwa nyingi Namboole Stadium atakapoenda kuivaa Uganga inayoshambulia sana.

Wachezaji ghali zaidi wa kihispaniola – Morata kuandika rekodi mpya ya usajili

$
0
0

Kuelekea kukamilisha usajili wa kujiunga na Manchester United akitokea Real Madrid, Alvaro Morata ataingia kwenye vitabu vya rekodi vya usajili nchini Hispania kwa kuwa mchezaji ghali zaidi katika historia ya wachezaji wa taifa hilo. 


Jose Mourinho anajipanga kuimarisha kikosi chake kwa kumuongeza mshambuliaji huyo katika kikosi chake na ripoti zinaeleza kwamba Morata atasajiliwa kwa ada ya uhamisho isiyopungua Euro million 70.

Tayari imeripotiwa kuna makubaliano binafsi kati ya mchezaji mwenyewe na timu yake pamoja na Manchester United, na kilichobaki na vilabu viwili kumalizana. 

Vyanzo vya habari vya kuaminika vimeripoti kwamba Morata tayari ameitaarifu Madrid mipango yake na ameombwa auzwe – kwa dili ambalo litavunja rekodi ya ada ya uhamisho ya Fernando Torres ya €58.5m iliyolipwa na Chelsea kumsaini El Nino kutoka Liverpool. 

Listi ya wanasoka ghali zaidi wa kihispaniola katika historia inaundwa na Gaizka Mendieta – uhamisho wake wa kutoka Lazio kwenda Valencia kwa ada ya €48m, Juan Mata kutoka Chelsea kwenda United €45m, David Villa na Javi Martinez wote hawa walinunuliwa kwa €40m kila mmoja. 

Liverpool walilipa 38m kwa ajili ya Fernando Torres kwa Atletico, Atletico pia walipokea kiasi kama hicho kwa usajili wa Diego Costa kwenda Chelsea, United iliwalipa Athletic Club €36m kumsaini Herrera na Real Madrid waliwalipa Liverpool 35m kwa ajili ya Xabi Alonso. 

Morata sasa anakuja kuandika rekodi mpya – Juventus ilimsaini kwa €20m na alikuwa na msimu mzuri ambapo aliisaidia timu kufika fainali ya Champions League waliyocheza na FC Barcelona, kiwango chake kiliishawishi Real Madrid kuwalipa waitaliano kiasi cha €30m kumsaini tena Morata – na sasa Los Blancos wana lengo la kutengeneza faida mara ya 2 ya bei waliyomnunua kutoka Bibi kizee cha Turin. 

Mambo 5 ya kuangalia kabla ya kuhukumu mchezaji mmojammoja wa Stars – Shaffih Dauda

$
0
0

Matokeo ya mechi kati ya Stars dhidi ya Lesotho yaliwakatisha tamaa watu wengi sana, baada ya mechi ya nimefuatilia maoni ya wadau wengi sana kila mmoja akiwa na maoni yake tofauti.

Mimi sikustushwa n asana na matokeo yale, kama mtanzania jukumu langu ni kuisapoti timu yangu ya taifa lakini inapokuja uhalisia, nabaki kwenye uhalisia. Kwa nchi yetu ya Tanznia bado kuna mambo mengi inabidi yafanyiwe kazi, wakati mwingine ni vigumu kumhukumu mchezaji mmojammoja, ukiangalia performance ya timu ya taifa halafu ukaangalia mchezaji mmojammoja namna wanavyocheza ukataka uwahukumu kwa ule mchezo mmoja wakati mwingine naona si haki.

Kuna namna ambayo itafika muda wa kumuhukumu mchezaji kama kuna mambo yamefanyika kwa mchezaji mwenyewe, kwa mfano kuna wataalam wengingi ndani ya shirikisho wanajua kwamba ili timu ya taifa ifike kwenye hatua ya kushindana ni lazima kuwe na michakato imefanyika na sio michakato ya kulala na kuamka asubuhi, inahitaji muda.

Tunazungumzia uwekezaji kwenye soka la vijana, ubora wa ligi zetu hususan ligi kuu, hivi ni vitu ambavyo vinahitaji kuviangalia. Sasa watu leo wanatoa wapi ujasili wa kuanza kuhukumu mchezaji mmoja wakati siku chache zilizopita tulikuwa kwenye mijadala ya kuangalia namna ligi yetu inavyokwenda na mambo yanayofanyika kwenye ligi.

Kwa bahati mbaya sisi watanzania ni wepesi wa kusahau, laity kama tungekuwa wastahimilivu na tuna fatilia vizuri, kuna mambo mengi sana ambayo hayajakaa sawa kuanzia kwenye mambo ya kiufundi. Wenzetu wanaocheza na kufanikiwa mipango yao ipo wazi miaka kadhaa iliyopita.

Kwa mfano, siku ambayo Taifa Stars inalazimishwa sare ya  kufungana 1-1 na Lesotho, Afrika Kusini walipata ushindi wa magoli 2-0 ugenini dhidi ya Nigeria, mipango yao ipo hadharani miaka mitano iliyopita na aliyeiweka hadharani ni aliyekuwa Rais wao wa soka Danny Odano wakati anaingia madarakani.

Alikuwa anawashangaa wananchi wa Afrika Kusini wanavyokuwa na hasira kutokana na matokeo mabaya inayopata timu yao, akasema haiwezekani hata siku moja timu ya taifa ya wakubwa haiwezi kufanya vizuri ikiwa timu za vijana hazijafanya vizuri. Alisema timu zao za U17, U20 na U23 bado hazijafanya vizuri kwa miaka 10 hadi 15 iliyopita. Sasa watu wanapata wapi ujasiri wa kutaka kuiona senior timu nafanya vizuri?

Wakakaa chini na wataalam, leo hii timu zao za vijana zimeanza kufanya vizuri na kufanikiwa kushiriki mashindano ya Afrika na Dunia sasa hivi wanaweza kucheza ugenini na wakawa na uhakika wa kuondoka na pointi tatu.

Kwa hiyo na sisi tutengeneze misingi kama hiyo ya kuwa na timu bora za vijana ili twende tukashindane, lakini leo hii ukianza kumpiga maswali kocha ni kumtesa bure. Lazima tuwe na mifumo ya kutengeneza timu ya taifa, tusiwe na klabu ya taifa.

Tunatakiwa tuangalie maeneo matano. Lazima tujitambue sisi tupoje, tukisha tenga muda wa kujitambua na kujitathmini inatupa fursa ya kujua mapungufu yetu na kujua tunatakiwa twende wapi. Tujiangalie sisi tunachezaje kwa sababu inaathari sehemu zote, haiwezekani timu ya taifa inatumia mfumo wa 3-5-2, halafu U20 wanacheza 4-4-2 huku U17 wanacheza 4-3-3 kwenye vilabu kila mtu anacheza anavyojua yeye.

Lazima tujitathmini na kuwa na falsafa moja inayofanana, baada ya hapo tuangalie future ya mchezaji wa kitanzania, lazima tuangalie Msuva baada ya miaka mitano atakuwa ni mchezaji wa aina gani, baada ya hapo tuangalie mifumo yetu ya ufundishaji ipoje, tunafundisha ili iweje.

Halafu tunakuja sisi kama wadau tuna-support kivipi ili kuweza kutekeleza haya mambo, tukifika hiyo hatua tunaweza kumwambia ‘Ulimwengu leo umezingua’ au mchezaji yeyote yule tunaweza kumhukumu endapo atazingua.

Naamini Manula atakuwa na wakati mgumu kuziba pengo la Kaseja Simba

$
0
0

Na Baraka Mbolembole

GOLIKIPA, Aishi Manula, walinzi wa pembeni, Shomari Kapombe na Jamal Mwambeleko, na mshambulizi, John Bocco wamesajiliwa Simba SC wakati huu wa usajili ili kuboresha kikosi chao ambacho kilimaliza katika nafasi ya pili msimu uliopita na kushinda taji la FA ambalo limewapa nafasi ya kuiwakilisha Tanzania Bara katika michuano ya Caf Confederation Cup 2018.

Aishi Manula  

Wakati Azam FC ilipokuwa katika maandalizi ya kuanza msimu wa 2014/15 nilipata nafasi ya kwenda kufanya mahojiano na wachezaji watano wa Azam FC na mmoja wa wachezaji ambao nilifanya naye mahojiano ni golikipa huyu kijana wa timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars.’

Alinieleza chimbuko lake, na jinsi alivyopata nafasi ya kusajiliwa Azam FC. Aishi alinieleza kuwa malengo yake si kucheza klabu za Simba na Yanga kama itatokea yeye kuondoka Azam FC basi ni kwenda kutafuta nafasi ya kucheza na kutengeneza maisha yake nje ya Tanzania. Karibia miaka mitatu sasa tangu nilipofanya naye mahojiano golikipa huyo amesaini mkataba wa miaka miwili kuichezea Simba.

Tangu kuanza kwa tetesi za yeye kujiunga Simba, kukanusha kwake mara kwa mara niliamini Aishi hawezi kujiunga na mabingwa hao wa zamani wa Tanzania Bara.

Lakini tofauti na matarajio yangu kipa huyo amekubali kusaini Simba kwa kile alichodai kutopewa thamani na klabu yake ya zamani (Azam FC) ambao licha ya kuelekea mwisho wa mkataba wake alikuwa tayari kuongeza mkataba wa kuendelea kuichezea timu hiyo iliyomsaini mwaka 2012 na kumuendeleza kielimu akitokea nje ya mkoa wa Morogoro.

Manula anadai alikuwa tayari kuendelea kufanya kazi yake Chamanzi Complex lakini kitendo cha uongozi wa Azam FC kutaka kumsaini kwa dau la chini ya milioni 20 kwake kilimsikitisha sana.

Kweli kabisa, hata kama Azam FC imeamua kuingia katika sera ya kubana matumizi lakini kwa mchezaji mwenye uwezo wa juu, nidhamu isiyo na mfano na kipa namba moja wa timu ya Taifa ni wazi hawakuthamini uwezo wake.

Siungi mkono hoja ya golikipa huyo eti ameamua kuichagua Simba ili kupata nafasi ya kucheza michuano ya kimataifa bali naamini mshahara wa milioni 3 kwa mwezi na dau la usajili lisilopungua milioni 50 ndiyo ‘kichocheo’ cha yeye kusaini Simba.

Usajili huu umekuwa na manufaa kwa kila upande. Simba imekuwa na tatizo la golikipa tangu alipoondoka Juma Kaseja katikati ya mwaka 2013.

Mganda, Abel Dhaira (Mwenyezi Mungu amerehemu,) Ivo Mapundb, Manyika Peter Manyika, Hussein Shariff, Muivory Coast, Vicent Angban na Mghana, Daniel Aggey wote hawa wameonekana kushindwa kuziba pengo lililoachwa na Kaseja ambaye aliachana na timu hiyo kwa kile kilichotajwa na uongozi wa Ismail Aden Rage kuwa ‘amekwisha.’

Katika tuzo za wachezaji bora wa msimu uliomalizika kwa Yanga kutwaa ubingwa wa tatu mfululizo, Aishi alishindana na Kaseja katika tuzo ya golikipa bora wa msimu na kijana huyo akafanikiwa kushinda tuzo hiyo.

Je, Aishi ataweza kuwasahaulisha Simba kuhusu uwezo wa Kaseja? Bila shaka kwa usajili wa golikipa huyu Simba imepata kipa bora na ni wakati sasa wa kijana huyo kuongeza uwezo zaidi na kuisaidia timu yake mpya.

Aishi hawezi kuwa ‘Kaseja Mpya’ lakini anaweza kutengeneza jina lake na kuwa kipa bora zaidi wa timu hiyo katika ‘muongo’ huu wa pili wa karne mpya kama ilivyokuwa kwa Kaseja katika muongo uliopita.

Wasiwasi pekee wa kukua kimchezo kwa golikipa huyo ni uongozi wa timu yake mpya ambao umekuwa ukiwanyanyasa wachezaji katika haki zao za kimsingi, ufanyaji wao kazi umekosa maelewano na kila timu inapoanguka hukimbilia kuwarushia lawama wachezaji hasa magolikipa.

Dhaira, Mapunda, Manyika, Shariff, Angban, na Agyei wote hawa wamewahi kushutumiwa hadharani na uongozi wa Simba ilipotokea wameruhusu magoli ambayo kwao huonekana ni ya kizembe.  Aishi ni kipa bora kwa sasa katika soka la Tanzania lakini ni namna gani ataendelea kuongeza ubora wake katika timu isiyo na umoja hilo ni jambo la kusubiri na kuona.

Agyei  ni kipa mzuri lakini tatizo lake si mzuri katika upangaji wa ngome, na Aishi ni kipa bora katika upangaji wa beki na kucheza mipira inayotokea mbele lakini bado hajakamilika katika uchezaji wa mipira ya krosi na kona hivyo ni jukumu lake mwenyewe kujiimarisha ili awe bora zaidi.

Ataifanyia nini Simba SC isiyo na ‘ustahimilivu’ kwa wachezaji wanaofanya makosa ya kimchezo? Tusubiri na kuona ila hadi sasa naamini kila upande umefanikiwa katika usajili huu.

United watarajie nini kwa Victor Lindelof?

$
0
0

Kutoa kiasi cha euro 30.7m kumnunua mlinzi tena mwenye umri wa miaka 22 sio jambo dogo lakini Manchester United hawakujali na wametoa kiasi hicho cha pesa kumnunua mlinzi Victor Lindelof kutoka Benfica.

Wengine wamefurahia usajili huu huku wengine wakiuliza kwanini beki wakati tayari wana mabeki wengi, lakini kama ulikuwa hujui tu baasi jua kati ya aina wachezaji au walinzi ambao Mourinho anapenda baasi nia aina ya Lindelof.

Unaweza kuona safu ya ulinzi ya United ukiacha Eric Bailly na Dalley Blind klabu hii imekuwa na aina ya mabeki ambao wanajua tu kukaba lakini baada ya kufanikiwa kukaba wanapata tabu kujua sehemu sahihi ya kuupeleka mpira na mara nyingi wanapiga tu mipira mirefu mbele.

Lindelof pamoja na umri wake lakini ni mlinzi mwenye stamina na ana nguvu haswa na kitu cha ziada alichobarikiwa anapenda sana kukaa na mpira na kuanzisha mashambulizi kama ilivyo kwa Eric Bailly ambae nae ana nguvu na ujuzi wa kucheza na mpira.

Jarida moja nchini Ureno limeandika kuhusu mashabiki wa Benfica watakachomiss kwa Lindelof na mmoja kati ya mashabiki wanaoishi karibia na uwanja wa Benfica wa Estadio Da Luz amemuelezea Lindelof kama mchapakazi sana.

Lindelof ni mchezaji ambaye mara nyingi anawahi kufika mazoezini na ni wa mwisho kuondoka na hii ndio aina ya waoiganaji Mourinho anaowataka na kama akiwa katika kiwango alichokuwa nacho Benfica baasi hakika kuna ukuta mgumu sana unaenda kutengenezwa na Lindelof na Bailly.

Benfica walikuw wakimuita “Ice Man” kutokana na aina yake ya ukabaji wa nguvu nyingi sana na akili nyingi na inasemekana Benfica walipata ofa kubwa kutoka Italia lakini Lindelof alitaka kwenda kucheza United.

Tusubiri tuone pacha hii inavyoenda kuwa lakini ni wazi Mourinho anaonekana anataka atengeze ngome imara ya ulinzi kwani msimu uliopita haswa wakati unaanza baadhi ya walinzi waliigharimu United na Mou anajaribu kuzuia hilo lisijirudie.

Kwanini Ronaldo anataka kuondoka Madrid, tetesi za Man United haziepukiki

$
0
0

Wiki hii picha ya Cristiano Ronaldo iliyotumika saba kwenye kurasa mbalimbali za vyombo vya habari ni ile inayomuonyesha akiwa kwenye jezi ya timu ya taifa ya Ureno akiwa ameweka kidole mdomoni. Staili ya ‘shut up’ ambayo amekuwa akiitumia mara kwa mara pale anapohitaji kutuma ujumbe tofauti. 

Tatizo la Ronaldo hakuna atakayenyamaza hasa vyombo vya habari vya Catalan ambavyo siku zote vilikuwa vinasubiri taarifa mbaya kama hii ya kesi ya ukwepaji kodi. Mambo yamekuwa mabaya sasa kwa mchezaji huyu wa zamani wa Manchester United baada ya kutuhumiwa kukwepa kodi ya kiasi cha €14.7 – sawa na takribani billioni 30 za madafu. 

Magazeti ya Catalan yamekuwa yakiandika habari hii kwa upana zaidi katika kurasa zao za mbele na huku wakilinganisha wanavyoripoti kesi hii na ile iliyokuwa ikimhusu Lionel Messi.
Vyombo vya habari vya Catalan mara kadhaa vimekuwa vikivituhumu vyombo vya habari vya jijini Madrid kuwa na upendeleo kwa baadhi ya taarifa zinazowahusu wachezaji wa mji huo. So ilipotokea suala hili la CR7 – Wakatalunya wamekuwa wakiandika habari za kumdhalilisha Ronaldo, huku wakiwatuhumu wenzao wa Madrid kwa upendeleo, na vyombo vya habari vya Madrid ikawabidi waripoti taarifa kwa usawa kadri inavyotatikana. Na upande wa timu ya Real Madrid hakukuwa na kaulinza utetezi na hasira dhidi ya tuhuma za mchezaji wao. 

Wakati wa kesi ya ukwepaji kodi ya Lionel Messi, vyombo vya habari vya Catalan vilikuwa vikiandika makala mbalimbali za kumtetea na kuwashushia lawama wahusika wengine wa kesi hiyo, haikuwa jambo sahihi, na wakati kesi hiyo ilpokwisha, FC Barcelona wakafanya kitendo cha kushangaza zaidi.

Messi alikutwa na makosa matatu ya ukwepaji kodi. Kulikuwa na utetezi mwingi kuhusu kuhusika kwa Messi katika jambo hilo, kwamba alikuwa bado mdogo wakati wasaidizi wake wakifanya kazi ya ku-manage mapato yake, hakuwa anapewa taarifa sahihi na huku akiwaamini sana washauri na wasaidizi wake. Hii ilikuwa njia sahihi ya kusafisha jina la Messi na kauli ya ‘wote tunakosea tunapokuwa tunakua kiumri.’

Lakini haikuwa hivyo, huku klabu ikiwa na wasiwasi wa Messi kutoongeza mkataba (ambao mpaka sasa hajaongeza), wakaanzisha kampeni ya #WeAreAllLeoMessi

Kwa kutumia hashtag ya #WeAreAllLeoMessi wakati wakipost picha au ujumbe wa kumtetea Messi – na huku wakisisitiza mashabiki wa kutumia akaunti zao za mitandao ya kijamii kumpa support mchezaji wao kipenzi. 

Josep Maria Bartomeu, Rais wa  Barcelona, anaonekana kuwa mtu mwenye misimamo lakini lilipokuja suala hili na yeye alijishusha na kuungana na mashabiki wa Barca mitandaoni kumtetea Messi hata kama alithibitika alikuwa na hatia. :

Mashabiki waliungana na kumsapoti shujaa wao, huku wakiwa na matumaini ya kwamba Messi angesaini mkataba mpya haraka. Hiyo ilikuwa July 2016, lakini mpaka sasa hajaongeza mkataba mpya. 

Haya yanahusiana vipi na Cristiano Ronaldo kwenda Manchester United?

 CR14.7 (kama ambavyo vyombo vya habari vya Catalan vinamuita hivi sasa) – anahisi kwamba kesi hii imetengenezwa kumchafua, ameumizwa na jambo hili, anahisi anatumika tu na hathimiwi kama Messi alivyokuwa anajisikia labda. 

Kwa sababu hakuna yoyote ambaye amejitokeza kumtetea inavyopaswa kwasababu mwenyewe amesema hajawahi kutenda kosa hilo. Gazeti la A Bola la nyumbani kwao Ronaldo – Ureno leo limeripoti kwamba mchezaji huyo amechukizwa sana na kile walichokiita uonevu dhidi yake na hivyo ameamua kutoendekea kuishi Hispania. 

Pamoja na mapenzi yake kwa Madrid lakini Ronaldo anahisi analengwa makusudi na mamlaka za Hispania na hivyo ni bora kuondoka katika nchi hiyo. 

Ripoti za Ronaldo kutaka kuondoka Madrid zimezidi kushika hatamu mchana wa leo, MARCA, gazeti lenye ukaribu na Madrid limethibitisha ukweli wa taarifa hizo, Sky Sports na mitandao mingine mikubwa pia imeripoti juu ya taarifa hizo huku vikiripoti kwamba huenda mchezaji huyo akataka kurejea Manchester United ambapo ndipo alipopata jina na kupewa thamani na mapenzi na mashabiki wa klabu kwa siku zote hata baada ya kuhamia Madrid na wengine wakimhusisha na kwenda China au PSG.  

Marca wameongeza kwamba ni kweli kuna jambo hilo la CR7 kutaka kuondoka lakini Madrid wanajaribu kumtuliza kwasababu wanaamini kuhama ni jambo ambalo Ronaldo hajaliamua moja kwa moja na huenda ni hasira tu zinampeleka kutaka kufanya hivyo. 

Sababu za CR7 kutaka kuondoka ni kuumizwa na kesi hii ya kodi, kushambuliwa na vyombo vya habari na kubwa zaidi kutopokea support kubwa kutoka kwa klabu yake ya Real Madrid. CR7 sasa anataka kuanza upya na Marca wanasema huenda huu ukawa wakati wa mchezaji huyo kurejea Old Trafford. 

Je Ronaldo anataka na yeye kutetea mitandaoni na klabu kwa hashtag ya  #WeAreAllCristiano – labda sio hivyo, au support kutoka kwa vyombo habari rafiki vya Madrid? Ni wazi kabisa vyombo vya habari vya Catalunya vimeegemea upande wa Messi kila anapopata matatizo na upande mwingine vikiendelea kumshambulia CR7. Magazeti ya jiji la Madrid Marca na AS, na mengineyo havijakuwa na hali ya kumtetea Ronaldo kama ambavyo vyombo vya Catalunya hufanya kwa Messi. 

Hivyo Ikiwa Cristiano Ronaldo anapima namna anavyotendewa kwa kulinganisha na Lionel Messi alivyo na media za Catalunya, basi ni lazima ajihisi kutengwa. 

Kwa namna yoyote ili CR7 aendelee kubaki Bernabeu – Real Madrid itabidi wafanya kazi ya ziada kuiridhisha nafsi ya Ronaldo, watafute mbinu kuimaliza kesi ya kodi na kisha kuanza kampeni mpya ya Ballon d’Or. 
Endapo watashindwa kufanya hivyo, basi sisi waandishi wa habari na wapenzi wa soka tujiandae na taarifa za usajili wa Ronaldo kwenda Manchester United kwa miezi yote mitatu ya kipindi cha usajili. 

Sports Extra wapishana kuhusu kanuni ya uzoefu wa miaka 5 ili kuongoza TFF

$
0
0

Tayari wadau wameshaanza kuchukua fomu kwa ajili ya kuwania nyadhifa mbalimbali katika shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF) kwa ajili ya uchaguzi mkuu wa kupata viongozi wapya wataoongoza TFF kwa kipindi kingine baada ya uongozi uliopo madarakani kumaliza muda wake.

Rais anamaliza muda wake Jamal Malinzi  alikuwa wa kwanza kuchukua fomu kwa ajili ya kutetea nafasi yake, Imani Magega mwenyekiti wa zamani wa klabu ya Yanga pia ameshachukua fomu kuwania nafasi hiyo ya juu kwenye uongozi wa shirikisho la soka nchini.

Mlamu Ng’ambi na Michael Wambura wao wamechukuwa fomu kwa ajili ya kuwania nafasi ya makamu  wa Rais. Makamu wa Rais wa Simba Geoffrey Nyange ‘Kaburu’ nae amechukua fomu kuwania nafasi ya makamu wa Rais kwa kipindi kijacho.

Nafasi ya ujumbe wa kamati ya utendaji wameshajitokeza watu kadhaa miongoni mwao ni Salum Chama, Efraim Majige, Elias Mwanjala, Golden Sanga, Shaffih Dauda, Athumani Kambi, Kodastian Mkumbu, Samuel Daniel na Mbasha Matutu.

Lakini mjadala mkubwa ndani ya Sports Extra mjada mkubwa umekuwa ni moja ya kigezo cha kuwania uongozi ndani ya TFF, kigezo cha kuwa na uzoefu wa kuongoza mpira kwa kipindi kisichopungua miaka mitano kilijadiliwa huku kila mmoja akitoa mtazamo wake kuhusu kigezo hicho ambacho

Edgar Kibwana

Kibwana anaamini kanuni ya uzoefu wa miaka mitano ndio imruhusu mtu kugombea haina tija na ni kutaka kuweka ugumu kwa watu ambao hawana muda mrefu kwenye uongozi kuingia TFF.

“Kuna kichaka hapa inabidi kichomwe moto, hii kanuni ya kusema kwamba, kama hujawahi kuongoza mpira kwa kipindi kisichopungua miaka mitano ni kichaka kikubwa sana inabidi kichomwe moto. Yani usipokuwa mtu wa mpira kuingia kwenye mfumo wa TFF ni ngumu sana.”

Alex Luambano

Luambano kwa upande wake anaona ni sawa kigezo cha uzoefu wa miaka mitano kuendelea kutumika ili kuwapata wagombea, ametolea mfano kwenye ajira za kawaida ambapo mwajiri hutoa vigezo na masharti kwa waombaji wa ajira husika kabla ya kuomba ili apate mtu mwenye sifa anazo zihitaji.

Lakini akakiri kwamba, wakati mwingine vigezo hivyo vinawaumiza wale wasio na uzoefu na kuhoji hao wasio na uzoefu watapata wapi uzoefu ikiwa kila sehemu wanahitaji mtu mwenye uzoefu?

“Inabidi uanzie ngazi za chini, hata kwenye ajira za kawaida waajiri huwa wanasema wanahitaji mtu mwenye uzoefu wa miaka kadhaa, wanaweka kigezo cha umri. Sasa wale ambao wanakuwa ndio wametoka shule ndio wanakuwa kwenye wakati mgumu kwenye hizo ajira, hivyo ndivyo ilivyo hata kwenye uongozi wa mpira.”

“Kwa hiyo kama wewe ni mpya kwenye uongozi wa soka, unamtihani mkubwa sana.”

Issa Maeda

Maeda hakucheza mbali na Kibwana, yeye pia alisema kigezo cha uzoefu wa miaka mitano ni kufunga milango kwa watu wenye uwezo wa kuongoza ila tu kwa kuwa hawana uzoefu wa miaka mitano basi inabidi wakae nje ya uongozi wa TFF.

Akaongeza kuwa, kwa Tanzania kigezo cha miaka mitano hakina tija labda kwa nchi za wenzetu kinaweza kuwa na mashiko lakini sio Bongo. Maeda akaenda mbali zaidi na kusema inawezekana mtu akawa na uzoefu mkubwa kwenye utawala wa mpira lakini hajafanikiwa katika uzoefu wake huo alionao.

Kwa upande wetu sisi (Tanzania) hicho kipengele hakina tija kabisa, waliopo madarakani wamefanya nini? Tunafunga milango kwa watu wenye uwezo kwa sababu ya kipengele hiki. Ni kweli lazima uanze uongozi katika ngazi fulani ukue uende katika ngazi ya taifa, lakini kipengele hiki kuna namna ya kukitazama.

Kwa nchi zilizoendelea kinafaa lakini sio kwetu. Mfano mtu amekaa madarakani kwa miaka 20 halafu unajivunia inabidi tumuulize kwa mafanikio yapi kwa sababu kila kukicha nafasi yetu ni ya 120 kwa nini tusiruhusu upambane na mtu mwingine ambaye hana uzoefu wa miaka mitano lakini ana uwezo wa kuongoza na kututoa hapo ulipotuweka.

Wewe msomaji uko upande upi hapo baada ya kuona msimamo wa Edgar Kibwana, Alex Luambano na Issa Maeda? Je kigezo cha uzoefu wa maiaka mitano kina tija au hakina mantiki na kimelenga kuwapunguza watu wenye uwezo wanaotaka kuwania nafasi za uongozi pale TFF?

Nipe maoni yako kwa comment yako hapo chini tuone kama kigezo hiki bado kina mashiko au hakina maana yoyote ya kujenga.


Nenda Ally Yanga, nenda, hakika jasho lako halitasahaulika kwenye jezi ya Yanga

$
0
0

Abdul Dunia

NENDA Ally Yanga. Nenda Ally Yanga. Nenda Ally Yanga. Msinishangae kurudia kwangu kauli hiyo zaidi ya mara tatu. Soka limekumbwa na huzuni kubwa nchini. Kifo cha Ally Mohammed maarufu kama ‘Ally Yanga’ kimewagusa wengi sana. Haina jinsi acha iwe tu.

Kila nafsi itaonja mauti. Hakika kila mwanadamu lazima atarejea kwa Mola wake aliyemuumba. Hakika tumeumbwa kwa udongo na lazima tutarejea mavumbini kwa ajili ya kutimiza ufalme wa Mungu muumba. Hakika acha iwe tu, haina jinsi.

Wadau wa soka nchini wamepokea kwa masikitiko makubwa kifo cha shabiki ‘kindakindaki’ wa Yanga, Ally Yanga. Nenda tu kaka, haina jinsi. Ulikuja ukiwa Ally Mohammed na umeondoka ukiwa Ally Yanga. Umeondoka ukiwa kipenzi cha mashabiki wengi wa soka nchini.

Nenda tu Ally Yanga, nenda. Hakika jasho lako halitasahaulika kwenye wino wa jezi ya Yanga pamoja na timu ya Taifa ‘Taifa Stars. Halitasahaulika kamwe. Ulijitoa sana kwa ajili ya Yanga na Stars. Hakika hutasahaulika daima.

Ulikuja mtupu ila umeondoka na kitu Ally. Ulitokwa machozi kwa ajili ya Yanga na Stars. Ulifurahi kwa ajili ya Yanga. Kuna kipindi ulipigwa kwa ajili ya Yanga. Hakika Yanga itakukumbuka daima kwa uliyowafanyia.

Umejulikana na watu wengi kwa ajili ya Yanga. Ulitokwa jasho kwa ajili ya Yanga. Muda mwingine ulilia sana kwa ajili ya Yanga. Umefurahi kuipenda Yanga. Hakika umestahili kuitwa Ally Yanga. Haina jinsi, nenda tu kaka sisi sote tupo nyuma yako.

Kazi ya Mungu haina makosa. Ulikuja kwa kazi ya Mungu na umeondoka kwa kazi ya Mungu. Kwa hakika kazi ya Mungu haina makosa kamwe.

Ajali ya gari huko Mpwapwa mkoani Dodoma ilitafuta sababu tu, lakini Mungu pekee ndiye aliyepanga. Kazi yake Mungu haina makosa hata mara moja.

Mwenyezi Mungu aipumzishe roho yako mahali pema peponi pia utukufu wake uwajalie nguvu na ustahimilivu familia yako na wapendwa wako wote.

Pumzika kwa amani Ally Yanga. Daima klabu ya Yanga na tasnia nzima ya soka nchini itakumbuka mchango wako katika soka kama shabiki mwandamizi.

Kuna wakati niliamua kumpa mkono kila nilipokutana naye baada ya mchezo wa Yanga ama Taifa Stars akiwa kajichafua na rangi za Yanga ama za jezi ya Taifa stars.

Niliwahi kutamani kukutana naye akiwa hana rangi zile za uwanjani lakini mpaka ameondoka sijabahatika kukutana naye akiwa bila rangi zile. Hakika alijulikana kutokana na rangi zile.

Ally alimvutia kila shabiki na mpenzi wa soka. Hakuwavutia watu kutokana na kuishabikia Yanga tu bali ubunifu wake jukwaani ulitosha kuwavuta watu wampende. Sio Mimi tu, sio wewe tu, hata kamera za runinga zilimfurahia kila timu yake ilipokuwa inashangilia goli.

Alivutia wakati wa kushangilia goli kwa staili ya kuchinja lakini pia alivutia zaidi wakati anahuzunika baada ya kufungwa. Ni watu wachache sana duniani wenye moyo kama Ally Yanga.

Namkumbuka Ally Yanga kwenye mechi kati ya Yanga na Simba mwaka 2011 pale kwenye Uwanja wa Taifa. Kichapo cha mabao 5-0 kilimchosha na kumtoa machozi kama mtoto aliyekuwa na njaa. Aina gani ya upenzi hii? Hiyo ndio maana halisi ya kuwa shabiki kindakindaki wa timu fulani.

Nenda ukapumzike Ally Yanga, picha zako ni ushahidi tosha wa ufalme wako jukwaani kwa jezi za Yanga na Taifa Stars katika Sanaa yako. Mwenyezi Mungu aipe faraja familia yako katika kipindi hiki kigumu. Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu mahala pema peponi. Amin.

Yanga yamlilia

Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Yanga, Salum Mkemi alithibitisha kwamba ajali hiyo imetokea na Ally alipoteza maisha kwenye ajali hiyo.

Ally Yanga atakumbukwa kutokana na mbwembwe zake kila Yanga ilipokuwa inacheza. Alipenda kujipaka masizi usoni huku akiweka kitambi cha bandia.

Wasifu wake

Jina lake kamili anaitwa Ally Mohammed maarufu kama Ally Yanga, alizaliwa Machi 1, 1984 mkoani Shinyanga. Ni mtoto wa mwisho katika familia ya watoto sita. Kabla ya umauti wake inafahamika alikuwa anaishi Yombo Vituka, Dar es Salaam.

Aliibukia Ubungo miaka ya nyuma kidogo ambako alikuwa anafanya shughuli ya kusajili laini za simu za mkononi katika vibanda vilivyokuwa pembeni ya kituo kikuu cha mabasi ya mikoani, Ubungo Terminal.

Ally Yanga alianza kuonekana kwenye Uwanja wa Taifa pamoja na kikundi cha mashabiki wa Yanga kilichojulikana kama Yanga Ubungo Terminal, ambako ndipo lilipokuwa tawi lake.

Tangu baada ya uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba 25, 2015, Ally Yanga aliadimika kwenye viwanja vya soka nchini kutokana na kujikita zaidi kwenye shughuli za Chama cha Mapinduzi CCM.

Ally hakuwa shabiki wa Yanga tu, enzi za uhai wake alikuwa akizishabiki pia timu za taifa, kuanzia za vijana na wakubwa za wanawake na wanaume. Hakika alikuwa mtu wa soka.

Alikuwa maarufu Afrika Mashariki kutokana na kwenda kuishabikia Taifa Stars kwenye mechi za Kombe la CECAFA Challenge zilizowahi kufanyika kwenye nchi za Kenya na Uganda.

Ally Yanga alikuwa akisafiri hadi nje ya Afrika Mashariki akiwa akiwa na Yanga na Taifa Stars kwenye mechi za kufuzu fainali za Mataifa ya Afrika na Kombe la Dunia. Mungu ampumzishe kwa amani Ally Mohammed maarufu kama Ally Yanga. Amin.

Simba wanaandaa anguko lao jingine, Okwi, Niyonzima, Bocco, Kapombe si sajili za Omog

$
0
0

Na Baraka Mbolembole

WAKATI mshambulizi Mganda, Emmanuel Okwi anahitaji zaidi ya milioni 100 za kitanzania ili kurejea klabuni Simba kwa uhamisho wake wa tatu, wachezaji walioisaidia timu hiyo kupata ubingwa wa kombe la FA msimu uliopita wanaendelea kuzungushwa kuhusu malipo yao ya mshahara wa mwezi wa tano, pia hakuna bonasi yoyote ile ambayo uongozi wa klabu hiyo umetoa kwa wachezaji.

Viongozi wa klabu badala ya kuboresha kikosi chao wamekuwa ‘bize’ kusaka wachezaji wanaowapenda na si wale waliopendekezwa na kocha Mcameroon, Joseph Omog.

Okwi si chaguo la Omog, na kocha huyo hakupendekeza usajili wa aliyekuwa nahodha wa Azam FC, John Bocco pia alimuhitaji Ally Shomari kutoka Mtibwa Sugar FC kama mbadala na msaidizi wa Mcongoman, Javier Besala Bokungu katika beki ya kulia lakini uongozi umetoa Tsh. milioni 60 na kumsaini Shomari Kapombe kutoka Azam FC.

Huu ni usajili wa kishabiki zaidi ambao umeendelea kufanywa na kina ‘Mr. Kazinyingi’ wakiongozwa na mwenyekiti wa kamati ya usajili, Zacharia Hans Poppe. Kutoa zaidi ya milioni 200 kwa Okwi, Kapombe na Bocco si sawa kwa timu kama Simba hasa ukizingatia wachezaji hao wote watatu hawajapendekezwa na kocha.

Pia kuendelea kung’ang’ani saini yenye thamani ya zaidi ya milioni 100 ya Mnyarwanda, Haruna Niyonzima kutoka Yanga wakati si pendekezo la mwalimu ni sawa na ‘ujinga’ ambao ukuapo huzalisha ‘upumbavu.’

Ni kweli, Simba inahitaji wafungaji wawili wa nyongeza katika kikosi chao hasa baada ya kumpoteza Ibrahim Ajib, pia kikosi hicho kimepatia sana kuwasaini mlinda mlango, Aishi Manula kutoka Azam FC, Ally Shomari na beki namba 3, Jamaly Mwambeleko kutoka Mbao FC.

Pia usajili wa beki ya kati unahitajika licha ya kumsaini, Yusuph Mlipili kutoka Toto Africans ila katika eneo la kiungo, Omog hana upungufu mkubwa ambao unapelekea klabu kuhitaji saini mpya yenye thamani ya zaidi ya milioni 100.

Nahodha, Jonas Mkude, Mghana, James Kotei, Muzamiru Yassin, Mohamed Ibrahim hawa ni viungo wanne wa kati wenye uwezo wa juu.

Ili kujenga timu yenye ubora ni heri pesa aliyotumika kumsaini Kapombe ingefanya kazi hiyo kumleta kikosi Mrundi, Yusuph Ndikumana ambaye si tu ni beki mzuri wa kati bali ni chaguo la kocha Omog ambaye anamuhitaji beki huyo wa kati wa Mbao FC ili kushirikiana na Mganda, Juuko Murishid.

Kuna wakati nilimsikia Hans Poppe akisema hawawezi kumsaini tena Ndikumana kutokana na mchezaji huyo kuhitaji dau la juu ( Tsh. milioni 60) lakini naamini aliamua kumpuuza mchezaji huyo kwa sababu ni chaguo la Omog si yeye wala kamati yake ndio maana licha ya kutohitajika na kocha, Bocco, Kapombe na pengine Okwi ‘wataikwangua’ klabu hiyo zaidi ya milioni 200.

Simba inapaswa kuwasaini, Ndikumana au Salim Mbonde kutoka Mtibwa Sugar ili kuimarisha beki yao ya kati. Wanapaswa kuendelea kuwashikilia Abdi Banda na Juuko huku pia wakisaini wafungaji ambao wamependekezwa na Omog.

Kuendelea ‘kufuja’ pesa ‘wanazokopeshwa‘ na mfadhili wao ni sawa na kuiangusha klabu kiuchumi na kuharibu ufanisi wa timu iliyoanza kujengwa vizuri ndani ya uwanja.

Najiuliza, Okwi, Bocco, Kapombe wa nini Simba SC wakati hawawezi kuziba nyufa zilizowaangusha msimu uliopita.?

Narudia kutolea mfano usajili wa timu hiyo mwishoni mwa mwaka 2002, ambapo aliyekuwa kocha wa timu hiyo, Mkenya, James Siang’a (Mwenyezi Mungu amerehemu) licha ya kusajiliwa kwa wachezaji kwa nyota kama Ulimboka Mwakingwe, Lubigisa Madata, Victor Costa, Christopher Alex (Mwenyezi Mungu amerehemu,) kocha huyo alimwambia wazi aliyekuwa katibu mkuu wa klabu wakati huo, Kassim Dewji,

“Bila kuwasaini Primus Kasonso na Juma Kaseja naacha kazi…”Omog anasubiri nini wakati mapendekezo yake yametimizwa kwa Manula, Ally na Mwambeleko tu? Ndiyo maana nilisema awali kocha huyu hafai Simba SC.

Wakati ule niliposema barua ya Simba kwenda FIFA haikuwa na mashiko zaidi ya kutafuta ‘chaka’ la uongozi kufichia madhaifu yao, kuna baadhi ya wasomaji walipinga sana. Nauliza, vipi kombe la Simba limeshafika kutoka FIFA? Sasa wanawapotezea mbali kwa sajili za Mr. Kazinyingi.

Hakika naona Simba SC wakijiandalia anguko lao jingine, sababu kina Okwi, Niyonzima, Bocco, Kapombe si sajili za Omog…

Miguu ya Ajib inavyopishana na akili ya Niyonzima

$
0
0

Abdul Dunia

Titi la mama ni tamu. Hata likiwa la mbwa. Kiswahili naazimu. Sifayo inayofumbwa. Niimbe ilivyo kubwa. Toka kama chemchem. Titi la mama litamu jingine haliishi hamu. Aliwahi kuandika hayati Shaaban Robert katika moja ya vitabu vyake.

Shaban Robert ni kati ya waandishi walitokea kunivutia kutokana na kalamu yake anapoitumia. Hakuna kama Shaaban Robert. Acha niishie kusema hivyo. Hebu jaribu kufikiria maneno hayo ya nguli huyo katika kalamu kwa utulivu kama unashuhudia ile filamu ya uchaguzi wa Yanga mwaka jana.

Manji anachukua fomu, Msumi anasakwa na wanachama. Unavuta pumzi kisha unaendelea kufikiria. Manji anashinda, Mzee Akilimali anampongeza. Hakika ilikuwa filamu isiyoisha hamu.

Baada ya uchovu niliokuwa nao, nimeamua kuchukua kaseti mbili za Simba na Yanga kwa ajili ya kutazama. Moja kwenye mechi kati ya Simba na Mbeya City na nyingine Yanga na Ruvu Shooting. Zote za msimu uliopita.

Nimetazama kaseti hizo na nimezielewa. Nimeona wachezaji wawili tu. Kwanza nimemuona Ibrahim Ajib alafu nimemalizia kumuona Haruna Niyonzima maarufu kama Fabregas. Hao tu ndio niliowaona katika mechi hizo.

Kufananishwa na mchezaji kama Fabregas sio jambo la kawaida kabisa. Lazima uwe na kitu cha ziada ili kweli ufananishwe naye. Si mlimuona yule Idd maarufu kama Ronaldo wa Misosi FC? Alipiga tano peke yake dhidi ya Buguruni United. Hakika anafaa kuitwa Ronaldo. Ronaldo hana masihara kabisa na nyavu. Anyway.

Kwanza nimemuona Ajib akifunga bao la kusawazisha kwa faulo ya moja kwa moja. Kisha nimemuona Niyonzima akiimaliza Ruvu Shooting kwa pasi yake murua iliyomfanya mmoja wa mabeki kuanguka kama mzigo wa karanga.
Mwisho nimemuona Niyonzima akimvisha kanzu beki. Ghafla nikaikumbuka ile kanzu ya Zinedine Zidane dhidi ya Ronaldo De Lima kwenye fainali ya Kombe la Dunia mwaka 2006.

Kuna vitu wanavyojaribu kuvifanya wachezaji hawa, sio vya kwenye ligi yetu kabisa. Hakika tumewahi kuwashuhudia watu wa kila kanzu miaka ya nyuma sana. Zama za kina Method Mogela na Athuman Chama ndio kipindi cha watu walipokuwa wakipigwa kanzu sio kipindi hiki cha sasa. Tuachane na hilo.

Mwishoni mwa wiki hii kuna taarifa zilizoenea kuwa Ajib amesaini Yanga. Jana, Katibu Mkuu wa Yanga, Boniface Mkwasa alitoa taarifa kuwa klabu yake haitoendelea na Niyonzima. Tukubali tu kuwa kunauwezekano mkubwa Niyonzima kutimkia Simba baada ya kuachana na Yanga. What a football?

Huu ndio mpira wa kweli. Niyonzima Simba halafu Ajib Yanga. Ni nadra sana katika ligi moja wachezaji muhimu kuondoka ndani ya msimu mmoja huku wakibadilishana timu zenye upinzani wa jadi. Hakika ni mara chache sana kwa tukio kama hili.

Katika moja ya maandiko ya mzee Arsenal Wenger aliwahi kusema kuwa “Footballers are Most Hypocrite people in the world” akiwa na maana kuwa wachezaji ni moja kati ya watu wanafiki duniani. Tuliamini kama moyo wa Niyonzima utapokea kelele za mashabiki wa Simba? Akili ya Ajibu itakubali lawama za Simba? Kila kitu acha kimalizike lakini mpira uwepo kwanza.

Hapo awali mashabiki wa Simba walimzomea Niyonzima. Yanga wakamzomea Ajib. Lakini leo kila mmoja anamkaribisha wa kwake. This is Football and that is why, Football is Fair Play Game. Naanza kuiamini FIFA ilipotueleza hilo.

Kama Torres alikubali kutoka Liverpool kwenda Chelsea. Raul Meireles pia. Ajib anaachaje. Niyonzima anaachaje? Huu ndio unafiki aliouzungumzia Wenger.
Ronaldo anamapenzi na United lakini alikwenda Real Madrid. Huwezi kuzuia pesa kwa moyo wa mapenzi. Steven Gerrard hadi leo bado anajaribu kujifariji kwa dhambi aliyoifanya mwaka 2005.

Gerrard kwenye ubora wake. Liverpool inatwaa UEFA pale Instanbul. Real Madrid, Barcelona na FC Bayern Munich zinamtaka. Alichokifanya ni kuweka mapenzi na Liverpool. Akapoteza alichoandikiwa kukipata. Anyway tuje kwenye mada muhimu.

Ajibu anakwenda kuikosa akili ya Niyonzima. Niyonzima anakwenda kuikosa miguu ya Ajibu. Najaribu kufikiria kama wawili hawa wangekuwa kwenye timu moja. Hakika hakuna zaidi ya kupigiwa mpira mwingi. Hakuna zaidi ya hicho.

Hebu jaribu kufikiria zile ‘auta’ za Ajib na chenga za Niyonzima. Umakini wa Ajib na pasi za Niyonzima. Mizungusho ya Ajib na ufundi wa Niyonzima. Ukiwa na watu hawa kwenye timu humuhitaji tena Ngoma wala Tambwe. Chirwa mmoja anakutosha.

Kuwa na watu kama Niyonzima na Ajibu kwenye timu moja. Huitaji uwepo wa Mavugo wala Blagnon. Pastory Athanas ama John Bocco tu wanakutosha. Hakika wanakutosha.

Jaribu kufikiria zile chenga za Ajibu na kanzu za Niyonzima na ule utimamu wa Chirwa wakiwa kwenye timu moja. Najaribu kuufikiria uwezo wa Mohammed Ibrahim ‘Mo’, Haruna Niyonzima na Ibrahim Ajib wakiwa kwenye timu moja. Hakika niliwahi kuomba itokee hii lakini imekuwa ngumu kidogo.

Unaachaje kujisifu unapokuwa na Ajib na Niyonzima kwenye timu yako. Uwepo wa Ajib na Niyonzima ni sawa na ule uwepo wa Zidane na Ronaldo pale Real Madrid. Chenga utapigwa na kufungwa utafungwa tu. Hakika this is football.

Watu hawa wamekosana. Vipaji vyao vimekosana. Uwepo wao pia umekosana. Katika vitu ambavyo nafikiria Ajib na Niyonzima walitakiwa kuviomba ni kuwa kwenye timu moja. Lakini imekuwa ngumu kwao.

Acha nizirudishe hizi kaseti kwenye kabati maana machozi yameshaanza kunilenga. Napomuangalia Ajib halafu Niyonzima naona ule uwepo wa Christiano Ronaldo na Wayne Rooney wakati Manchester United ikitwaa UEFA dhidi ya Chelsea.

0679 469044

Javi Ribalta: Usajili muhimu waliofanya Man United kuliko wa Pogba 

$
0
0

Wakati wa dirisha la usajili lilopita, Juventus walifanya biashara kuhwa zaidi ya mauzo ya mchezaji katika historia ya soka na bado wakaenda kushinda taji la 6 mfululizo la Serie A na kufika fainali ya Champions League pia. Walilipa kiasi cha £800,000 kupata saini ya Paul Pogba mnamo mwaka 2012, kisha Juventus wakamuuza kwa faida ya £89.3 kurudi Manchester United. Fedha hii waliitumia katika usajili wa wachezaji wapya na klabu ikaendelea kushinda na kupata mafanikio. 

Mafanikio haya ya kibiashara yaliyozalisha mafanikio ya uwanjani yalienda kwa kila mtu katika timu lakini sifa za kipekee alipata kijana wa kihispaniola ambaye hufanya kazi nyuma ya pazia, Javier Ribalta. Ijumaa iliyopita Juventus walitangaza kwamba kijana huyo Ribalta ataacha kufanya kazi akiwa kama manager wa timu nzima ya maskauti baada ya kipindi cha miaka 5. Javier sasa anaelekea jijini Manchester kufanya kazi katika klabu ya Manchester United akiungana na Marcelo Bout na Jim Lawlor katika timu ya ‘scouting’ ya United.

Javier Ribalta, ambaye alikuwa anatambulika kama ‘siri bora ya Juve’ kwa sasa sio siri tena, na watu waliokaribu na klabu ya Juventus wanasema kuondoka kwake ni pigo zaidi kuondoka kwa Pogba kwenda United miezi 12 iliyopita.

Ribalta alipata sifa jijini Turin kama mtu aliye nyuma ya ‘mashine’. Katika wachezaji wote wa Juventus ambao walianza mchezo wa fainali ya Champions League dhidi ya Barcelona, watatu tu ndio walioanza katika mchezo wa fainali ya Ulaya vs Madrid mwanzoni mwa mwezi huu — Gianluigi Buffon, Andrea Barzagli na Leornardo Bonucci. Uwepo wa wachezaji wengi katika kikosi cha sasa ulitokana na ubora wa Ribalta kwa kusaidiana na Mkurugenzi mkuu Beppe Marotta na mkurugenzi wa michezo Fabio Patatici. 

Moratta, Paratici na Ribalta walisaidiana katika kuirudisha Juventus katika miongoni mwa timu zenye nguvu barani ulaya — mafanikio yote waliyopata ndani bajeti ya kawaida. Juventus walimaliza nafasi ya 7 mwaka 2011, mwaka huo huo walifungua uwanja wa ‘Juventus Stadium’ baada ya kutumia zaidi ya €150m katika ujenzi. Tangu wakati wameshinda Scudetto mara 6 mfululizo bila kufanya usajili wa kutumia mapesa mengi kama vilabu vingine vya hadhi yao. 

Hata kuondoka kwa Antonio Conte kwenda kuifundisha timu ya taifa ya Italia mwaka 2014 hakukuleta shida katika maendeleo ya timu. Akiwa na network kubwa ya watu mbalimbali katika nchinza Spain na America ya Kusini, Ribalta amekuwa na uelewa wa kina na taarifa za kutosha juu ya vipengele vya mikataba ya wachezaji na mambo mbalimbali kuhusu usajili – taarifa hizi humsaidia sana katika utekelezaji wa mipango ya usajili ya klabu yake.  
Dani Alves alisaini mkataba wa miaka miwili na Barcelona mwaka 2015 lakini Juventus walitumia faida ya kipengele cha kuvunja mkataba na kufanikiwa kumsaini kwa uhamisho huru wakati wa kiangazi uliopita. Sami Khedira aliwasili kwa uhamisho huru akitokea Madrid mwaka 2015. Mwaka mmoja kabla Juventus walilipa kiasi cha £1.2m tu kumsaini Patrice Evra baada ya wiki kadhaa tu nyuma kukubali kuongeza mkataba na United. 

Ribalta pia amepewa sifa katika kuhusika kuisaidia Juventus kukamilisha usajili wa Kingsley Coman, Pol Lirola, Paulo Dybala na Alex Sandro. Juventus alitumia kiasi cha £22.1m kwa Sandro wakati akitokea Porto mwaka 2015, leo hii Sandro anahusishwa kukaribia kukamilisha usajili wa kwenda Chelsea kwa ada inayofikia £60m.

Masiku na wiki ambazo Ribalta amekuwa akitumia kuangalia videos mbalimbali za wachezaji katika kituo cha utafiti cha Juve kilichopo huko Vinovo jijini Turin, jambo hili limemsaidia sana katika kujitengenezea ufanisi katika kazi yake, japo wanaomfahamu kiundani wanasema Ribalta haishii katika kugundua vipaji tu, lakini pia anaijua vyema biashara. Aliwashawishi Juventus kulipa kiasi cha €20m kumsajili Morata mwaka 2014 lakini baba mzazi wa Morata, anasema kazi yake haikuishia tu kwenye kusaidia kukamilisha usajili. 

Javi amekuwa mtu muhimu wa Alvaro hapa Turin. Amekuwa anamuangalia na kumjali na kuhakikisha anakuwa comfortable. Anaujua mchezo wa soka na amemsaidia sana mwanangu kufikia hatua aliyopo sasa.” – Alisema Alfonso Morata. 

Akiwa  United, Ribalta atafanya kazi na Bout na Lawlor katika kumsaidia Jose Mourinho kupata wachezaji anaowahitaji ili kuirudisha hadhi ya United katika kushinda makombe. Wakati katika klabu ya Juventus ulileta mafanikio kuliko wakati wowote katika historia ya kibibi kizee cha Turin na sasa anaelekea United ambapo atapata bajeti kubwa zaidi, moja ya sababu zinazosemekana kumvutia kwenda Old Trafford. 

Soko la usajili ‘kichaa’ linavyoipa Man United wakati mgumu kukamilisha usajili wake

$
0
0

Wakati Jose Mourinho na boss wake Ed Woodward walihitimisha listi ya wachezaji wanaotaka kuwasajili katika dirisha hili la usajili, walifahamu fika kwamba dirisha hili la usajili litakuwa gumu. 
Huku kukiwa na mapato ya £8.3 billion wanayogawana timu 20 za premier league zinazotokana na mauzo ya haki za mtanagazo ya TV duniani kote, pamoja na uwekezaji mpya wa wamiliki wapya vilabu nyumbani na nje ya Uingereza – ushindani wa kusaini wachezaji lazima ungekuwa mgumu sana. 

Sasa, mwezi mmoja ukiwa umekamilika tangu dirisha la usajili liwe wazi, wasiwasi wa Mourinho na Woodward umekuwa ukweli – soko la usajilo limekuwa gumu sana kwa timu nyingi. 

Kwa United, angalia jitihada zao za kumsaini kiungo wa ulinzi. United walikuwa wanaangalia kumsaini Eric Dier lakini pamoja na kwamba wana uwezo wa kumlipa mara 2 zaidi ya mshahara wake wa sasa, Spurs bado wameweza kugoma kumuuza kwa bei ya kawaida na wameamua kubaki nae – yote haya wakiyafanya huku wakiwa wanajenga uwanja mpya unaowagharimu kiasi cha £800 million.

Jose Mourinho alipohojiwa na jarida la France Football mwezi March kwamba United wanaweza wasifanikiwe kupata mchezaji kutoka Tottenham au timu nyingine yoyote ya Top 6 ya Premier League na sasa inaonekana huenda jambo hilo linaweza lisiwezekane katika timu 10 za juu za EPL – kila timu ina pesa na hivyo inakuwa ngumu kuuziana wachezaji kwasababu kila inataka kujiimarisha.
Nemanja Matic anaweza kuwa na upekee kwenye hili kwasababu Chelsea wana utayari kumuachia mserbia huyo ikiwa watafanikiwa kupata saini ya Tiemoue Bakayoko kutoka Monaco. Ikiwa dili hizi mbili za usajili zitakamilika, Chelsea wanaweza kumbadili kiungo mwenye umri wa miaka 28 kwa mwenye umri wa miaka 22 na bado watatengeneza faida ya £5m. Wakati huo huo Mourinho atampata kiungo ambaye anamfahamu vyema, ambaye anaifahamu vyema EPL na kuimudu na ameshaisadia Chelsea kushinda vikombe viwili vya premier League katika kipindi cha miaka 3 iliyopita.

United walikuwa wamepanga usajili wa wachezaji 4 ukamilike kabla ya wachezaji wote kurejea Carrington mnamo July 8, takribani wiki moja na nusu kutoka sasa. 

Lindelof tayari amewasili, hata hivyo uhamisho ulianza kujadiliwa na pande mbili za United na Benfica kutokea mwezi December 2016, ingawa uhamisho wa January ulisitishwa, lakini uliweka mazingira mazuri ya dili hili kukamilika kipindi hiki cha usajili. 

Woodward na timu yake wanapambana dhidi ya timu pinzani ambazo kwa mujibu ya walio ndani ya Old Trafford, wapinzani wao wanakuwa kiuchumi kila mwaka

Mfano Everton, hawajawahi kutazamwa kama wapinzani tangu miaka 1980 lakini hivi sasa kwenye dirisha hili la usajili wameshatumia zaidi ya £55m kwa wachezaji wawili tu – Jordan Pickford kwa £30m na Davy Klaassen kwa £25m. Pia wanakomaa kumruhusu Romelu Lukaku kuondoka isipokuwa timu inayomtaka itakapolipa £85m. Wachambuzi wa mambo ndani ya United wanaamini Everton walioshika nafasi ya 7 msimu uliopita wanaweza kuingia Top 4 msimu ujao ikiwa watafanya usajili mzuri na kubaki na Lukaku kwenye kikosi chao. 

Upande mwingine, vilabu vya nje AC Milan na Inter Milan wana uwekezaji wa matajiri kutoka China. Inter mpaka sasa wameendelea kuisumbua United na kugoma kumuuza Ivan Perisic mpaka United itakapolipa kiasi cha €50m, pamoja na kwamba wanahitaji kukusanya kiasi kichopungua €30m mpaka kufikia Ijumaa hii ili kuepukana na adhabu za kukiuka sheria ya Financial Fair Play. United sasa hawapambani na wakubwa wenzao tu kama Barcelona, Real Madrid, City, Bayern Munich na Chelsea. 
Mourinho alisema hadharani kwamba amemwambia Woodward asijisumbue kuhangaika na usajili wa wachezaji wasiouzika kirahisi na timu zao. Bila kuwataja majina, ilionekana wazi alikuwa akiwazungumzia akina Neymar, CR7, na wengineo wa aina hiyo ambao United imekuwa ikihusishwa nao kila wakati wa usajili. Hata dili za usajili za wachezaji aina ya Dier na Perisic – huko nyuma zilionekana rahisi lakini sasa nao wanaingia kwenye kundi la wachezaji wagumu kusajiliwa. 

Watu kadhaa wanaohusika na biashara za usajili , mawakala, washauri wa biashara, wanasheria, wamekaririwa wakisema soko la usajili limekuwa ‘kichaa’ na hata United wenye sifa ya kuwa klabu tajiri duniani nao wanaiona hali ilivyo ngumu katika kukamilisha uhamisho wa wachezaji kama zilivyo timu nyingine. 

Hii ndio sababu mojawapo katika dirisha hili la usajili wakamsaini mbobezi wa masuala la usajili na mikataba ya wachezaji, Javier Ribalta, ambaye ana sifa kubwa aliyojitengenezea akiwa Juventus. Woodward na Mourinho walitabiri soko gumu la usajili, lakini inaonekana hata wao hawakutegemea kutakuwa na ugumu wa namna hii, na hii ndio sababu mpaka sasa dirisha hili la usajili linaonekana kupooza kwa kutokamilika kwa usajili wa wachezaji wengi mpaka tunaingia mwezi July. 

Alifeli kidato cha pili, sasa anatesa Yanga

$
0
0

Na Zainabu Rajabu.

KILA kilicho na mafanikio hakikosi changamoto huu ni msemo ambao unabeba ujumbe mzito ambao kwa mwanadamu yeyote anatakiwa kuufuata ili aweze kufikia malengo anayokusudia kuyafikia.

Changamoto zipo ili kuweza kumfanya mwanadamu yeyote apambane na kuweza kufikia malengo yake eidha kwa kukwepa vikwazo vingi na baadaye kuweza kufikia kile anachokusudia.

Katika makala haya namzungumzia beki wa kushoto wa Yanga, Hajji Mwinyi Ngwali ambaye anabainisha kuwa hadi alipofikia anamshukuru mungu huku akiweka wazi kuwa sio mwisho bado anaendelea kupambana hadi atakapofikia malengo.

Swali; Ni changamoto gani umefanikiwa kukumbana nazo tangu umeamua kujihusisha na soka?

Jibu; Hadi hapa nilipofika namshukuru sana mungu kwani yeye ndio kila kitu katika maisha yangu nimekutana na vikwazo vingi lakini sikukatishwa tamaa na vikwazo hivyo nikaendelea kupambana navyo hadi nitakapofikia mafanikio.

Napenda sana kazi ninayoifanya lakini nimekuwa nikikwazwa na baadhi ya vyombo vya Habari kuniandika vibaya bila ya mimi mwenyewe kutolea ufafanuzi.

Katika vitu vinavyonikwaza na navichukia ni vyombo vya habari sio vyote lakini kuna baadhi vinafanya vitu kwa kujinufaisha vyenyewe huku wakishindwa kutambua vitu wanavyoviandika bila kuwa na uhakika vinamuharibia kazi pamoja na kumtoa thamani katika jamii mtu wanaemuandika.

Swali; Una malengo gani katika soka?

Jibu; Malengo yangu ni kucheza soka la kulipwa nje ya nchi na kuweza kuisaidia nchi yangu kuongeza idadi ya wachezaji wanaocheza soka nje na kuitangaza Tanzania kupitia soka.

Swali; Ni wachezaji gani anakupa changamoto kutokana na mfumo wao wa uchezaji?

Jibu; Pamoja na kuukubali uwezo wangu mwenyewe katika soka kuna wachezaji wananipa changamoto kutokana na uwezo wao wawapo uwanjani kutokana na uwezo wao mzuri wawapo uuwanjani kwa upande wa wachezaji wa ndani napenda sana uchezwaji wa Agrey Moris anayekipiga katika klabu ya Azam FC.

Moris ni mchezaji mahiri sana na ni mchezaji anayejua nini anakifanya awapo uwanjani huwa namuangalia sana napenda anavyocheza pia naamini uwezo wake unanipa changamoto zinazonifanya niongeze uwezo zaidi.

Kwa upande wa wachezaji wa nje navutiwa na uchezaji wa Cristian Ronaldo ni mchezaji wa kuigwa kutokana na kuhimili vikwazo ambavyo havimkatishi tamaa na kuendelea kupambana lengo likiwa ni kuisaidia timu na kufuirahisha mashabiki.

Swali; Ni vitu gani huvipendi katika maisha yako?

Jibu; Katika maisha ya kawaida na maisha ya soka huwa sipendelei kabisa masuala ya uongo kutoka kwa waandishi na hata marafiki wa karibu wanaomzunguka.

Mimi ni kama kioo kwa jamii inayonizunguka na huwa napenda sana vijana wajifunze kutoka kwangu hivyo nachukizwa sana na baadhi ya vyombo vya habari kuniandika mambo maovu ambayo huwa siyafanyi kitendo ambacho kinanijengea picha mbaya kwa jamii yangu.

Swali: Katika masuala ya vyakula je unapendelea nini?

Jibu: Mimi ni mpenzi mkubwa wa Wali nyama ni chakula ambacho nikila najisikia furaha na kushiba vizuri tofauti na vyakula vingine.

Haji anasema muda wake wa mapuziko mala nyingi anapendelea kukaa nyumbani na marafiki huku akisikiliza muziki ambapo aliweka wazi kuwa yeye ni shabiki mkubwa wa Raper David Genzi ‘Young Dee’.

Swali; Nini ushauri wako kwa Serikali?

Jibu; Naamini kupitia Website hii Shaffidauda.co.tz  ujumbe wangu unaweza ukafika kwa serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais John Pombe  Magufili kwa kumuomba haangalie ata sekta ya michezo kama anavyofanya katika sekta nyingine nyingi.

Pia naiomba serikali hii ijaribu kuinua na kuendeleza michezo kuanzia sekta ya vijana ambao ndio watakaokuwa wawakilishi wa nchi hapo baadaye katika mashindano mbalimbali ya nje na ndani.

Swali; Unaushauri gani kwa vijana wanaopenda mpira?

Jibu; Kila jambo lililo na mafanikio haliwezi kukosa changamoto hivyo wito wangu kwao kutokukata tamaa kama kweli wanaamini katika michezo na wanatakiwa kutumia muda mwingi kufanya mazoezi ili kuendeleza vipaji vyao bila kusubili kusimamiwa.

Swali; Umetokea wapi hadi hapa ulipofikia?

Jibu; Mwinyi kazaliwa Novemba 2, 1991 Visiwani Zanzibar amesoma shule ya msingi ya Wazazi Amani na kuhitimu mwaka 2006 alibahatika kujiunga na elimu ya sekondari ya Mwanakwekwele ambapo alisoma hadi kidato cha pili.

Nili ishia kidato cha pili kutokana na kushindwa kufikisha alama zinazotakiwa ili niweze kuendelea kidato cha tatu hivyo kutokana na kutokupata nafasi ya kuendelea nikaamua kujingia katika soka.

2010 nilianza kujihusisha na soka kwa kuanza katika timu ya Mapunda FC ambayo ilikuwa ni ya mtaani kwetu huko niliendelea kucheza hadi mwaka 2004 niliingia katika ligi ya vijana katika timu ya Necheran Centrel ambapo nilicheza hapo hadi 2011 nilipoonwa na Majimaji ya Zanzibar iliyokuwa inashiriki ligi daraja la kwanza.

Katika klabu hiyo ya Majimaji nilicheza mwaka mmoja na 2012 nilionwa na Chuoni FC ambapo alicheza kwa muda wa miaka miwili na baadaye mwaka 2014 nilisajiliwa na KMKM na baadaye ndipo nilipoonwa na Yanga ambayo naitumikia hadi sasa.

Mtazamo wa Shaffih Dauda kuhusu mchakato wa uchaguzi TFF unavyoendelea

$
0
0

Kamati ya utendaji ya TFF imefanya marekebisho kwenye kamati zake mbalimbali lakini marekebisho makubwa yamefanywa kwenye kamati ya uchaguzi ambapo wajumbe wanne wa kamati hiyo wameondolewa na kubakizwa mjumbe mmoja pekee ambaye alikuwa mwenyekiti wa kamati hiyo na huyu si mwingine ni Revocatus Kuuli.

Wakati hayo yakiendelea, Shaffih Dauda ametoa maoni yake kuhusu mambo yanavyoendelea kuhusu mchakato mzima wa uchaguzi mkuu wa TFF na kushauri wajumbe wanaoteuliwa kuweka mbele maslahi ya mpira wa Tanzania kuliko maslahi ya watu binafsi ambao wamewateua kusimamia uchaguzi.

“Kwa nini kipindi cha uchaguzi ndio kuna kuwa na mizengwe na migongano mingi? Utagundua kuna matatizo sehemu fulani, na mimi huwa sipendi kuangalia mtu alipoangukia, huwa nakwenda mbali zaidi kutaka kuangalia kilichosababisha aangunke ili kuweza kutatua tatizo siku nyingine asijikwae akaanguka tena.”

“Kwa hiyo hizi mamlaka husika wasipambane kufanya mabadiliko au maboresho kwa ajili ya kutatua jambo moja ambalo lipo usoni, waangalie kwa upana waweze kufanya mabadilko makubwa kwenye kanuni za uchaguzi, katiba za vyama na taasisi za mpira kwa ujumla. Hizi katiba na kanuni zina mapungufu mengi sana.”

Kikubwa ambacho kinasababisha mapungufu hayo ni wale ambao wanakuwa na mamlaka kwa kipindi husika kuwa wabinafsi, kutengeneza vipengele ambavyo kwa wakati huo vina wabeba au kutengeneza vipengele ambavyo vitakuja kuwasaidia baadae lakini wanashindwa kuweka mbele maslahi ya taasisi  na mpira wenyewe.

“Kwa hiyo inapofika wakati pande mbili zinapingana kuwania jambo fulani ndio pale ambapo huwa tunaona hayo mapungufu na vita kubwa, inafika mahali kama hili sakata la uchaguzi wa sasa lilipofika. Kama ni mfuatiliaji mzuri utagundua haya maamuzi yaliyofanywa na kamati ya utendaji ambayo ndio ileile iliyoteua kamati zilizopita ambazo zimefanyiwa marekebisho.”

“Wakati ule kulikuwa na mapungufu yaliyopelekea kuziteua hizi kamati, mapungufu yalikuwepo wapi? Kamati aliteua nani? Ukiangalia kwa haraka utagundua kwamba, mtu mmoja au wawili ambao hawakuwepo kwenye kikao cha kamati ya utendaji (kilichofanya marekebisho ya kamati) inawezekana ndio walikaa wakatengeneza hizi kamati? Kwa maana ya Rais Jamal Malinzi na mjumbe wa kamati ya utendaji Geoffrey Nyange ‘Kaburu’.”

“Leo hii hawapo, kamati ya utendaji ya wajumbe wengine wanakaa wanasema kulikuwa na mapungufu makubwa na wameamua kufanya marekebisho. Sasa hapo ndio inakuonesha yale mapungufu ambayo mimi nakuonesha tangu mwanzoni kwamba, inawezekana kuna kipengele kwenye katiba ambacho kinatoa nguvu kwa mtu mmoja au wawili kuweza kufanya maamuzi ambayo mwisho wa siku yanakuwa na athari kubwa.”

“Baada ya haya yanayotokea, wale watakaopata nafasi kwenye chaguzi hizi ambazo zinaendelea, kitu cha kwanza iwe ni kuweka mbele maslahi ya mpira kuliko kuweka maslahi binafsi kwamba tayari watu wameingia kwenye system basi wanatengeneza mbinu za kubaki madarakani kwenye uchaguzi unaofuata. Watengeneze katiba ambayo itakuwa huru kwa watu wote ili huko baadae tusione haya mambo yanayotokea sasa hivi.”

“Kwa mfano, jambo lililofanywa jana na kamati ya utendaji kukaa na kubadilisha baadhi ya wajumbe wa kamati na kuteua wajumbe wapya baadhi yao ni wagombea wa nafasi mbalimbali kwenye mchakato wa uchaguzi ambao unaendelea. Sasa inakuaje kwa wagombea wengine ambao hawapo kwenye kamati ya utendaji ya TFF halafu wanaoteua kamati ya uchaguzi ni wagombea kama wengine, je wagombea wengine wataamini vipi kamati mbalimbali kama zitakuwa fair kwao?”

“Kama zinateuliwa kamati ambazo zitakuwa fair na wasiingie kwenye malumbano kwamba watu wawili ndio wameweka watu wao kwa ajili ya kutetea maslahi yao, waingie wajumbe ambao watatetea maslahi ya mpira hata kama wamewekwa kwenye kamati na watu wanaotaka wawabebe. Wao wanatakiwa kujali kanuni na taratibu, hata kama wagombea waliowateua wakiwa hawana sifa hawatakiwi kuwaangalia usoni badala yake warejee kwenye kanuni zina semaje.”

“Kama mambo yatakwenda hivyo, hutosikia mtu analalamika hata baada ya kuondoshwa kwenye mchakato wa uchaguzi kwa kukosa sifa, lakini hayo yote yafanywe kwa haki bila upendeleo wowote.”


Kwa kasi hii ya Ujerumani, Ulaya na dunia itazidi kupata manyanyaso zaidi ya waliyopata kwa Hitler

$
0
0

Na Salym Juma, Arusha

Ikiwa ni miaka minne tangu Wajerumani wafanye maangamizi pale Brazil, Wajerumani bado wameendelea kutoa dozi katika michuano mbalimbali huku wakiiaminisha Dunia kuwa bado ina vizazi vinavyoweza kufanya makubwa zaidi ya yale waliyofanya kule America hasa kwa kuzitoa timu kubwa za America, Brazil nusu fainali na Argentina fainali. Uwekezaji uliofanywa na Wajerumani haukuja kwa bahati mbaya, ni mipango thabiti iliyoanzia chini na huenda ikadumu miaka mingi ijayo hasa katika michuano iliyochini ya FIFA na UEFA. Wajerumani wamechukua vikombe viwili vikubwa ndani ya siku 4 barani Ulaya.

Uwepo wa mataifa makubwa kwenye michuano ya Mabara kama Chile, Ureno na Mexico haukumuogopesha Joachim Low kuwaacha vijana na badala yake majina mazito kama Aturo Vidali, Vargas, Sanchez, Christiano Ronaldo yaligeuka chachu kwa vijana wa Kijerumani kucharuka na kufanya maangamizi ndani ya ardhi ya Warusi. Ukitizama majina haya Ter Stegen, Ginter, Rüdiger, Kimmich, Goretzka, Süleat, Rudy, Draxler na Werne unaweza kuzani kwamba jamaa labda walitolewa kwenye makundi ila ukiambiwa wameitoa Chile iliyosheheni majina yote unaweza kubaki mdomo wazi.

Wanasoka walibaki midomo wazi kutoitwa kwa Manuel Neuer, Mesut Ozil na Thomas Muller kwenye michuano ya mabara ila mapengo yao yalizibwa vyema na Rudy, Draxler na Werne baada ya Joachim Low kuwapa majukumu na kuwaaminisha kuwa wanaweza. Miaka mingi Ujerumani ilikuwa ikiwategemea Miroslav Klose, Mario Gomez na Muller kwenye idara ya ushambuliaji ila umri na uwezo wao umezidi kudorora hali inayofanya vijana kuanza kupewa nafasi mapema kabla ya jua kuchomoza ili wasije kuaibika kwenye michuano ijayo.

Kiwango kikubwa cha vijana wa U-21 kilichoifunga Hispania ni alarm kuwa Wajerumani wana muda mrefu sana wa kulitawala soka la Ulaya na Dunia. Uimara wa akina Sammy Khedira, Ozil, Neuer na Muller ulianzia humuhumu walipo akina Draxler na Werne hivi sasa. Uwezo huu haukuja kwa bahati nasibu ila ni mipango thabiti iliyowekezwa na watu wenye dhamira ya kweli kwenye mpira na sio siasa kama ilivyo kwa wanaojiita wataalamu kutoka TFF. Kikosi cha U-21 kimechukua ubingwa mbele ya Hispania, England, Italia na Denmark mataifa yanayoaminika kuwa na timu bora za vijana.

DFB {Shirikisho la soka la Ujerumani} chini ya Reinhard Grindel wanajua nini wanachotakiwa kukifanya ili wazidi kulitawala soka la Dunia. DFB ina wanachama {mashirikisho ya ndani} 21 huku kukiwa na vilabu rasmi zaidi ya 25,000 vinavyoshiriki ligi mbalimbali zinazotambuliwa na DFB. Uwepo wa wanachama zaidi ya 6.8 million unalifanya shirikisho hili kuwa la kwanza kwa ukubwa na ufanisi duniani huku mashirikisho mengine yakiendelea kusubiri. Kuwepo kwa karibu timu 171,000 nchini Ujerumani kunafanya idadi ya wachezaji waliopo Ujerumani pekee kufikia zaidi ya millioni mbili.

DFB iliwahi kukaririwa ikisema kuna wachezaji takribani Millioni 6 wanaocheza kwenye michuano rasmi na ile isiyo rasmi huku kila wikiendi kukiwa na michezo rasmi zaidi ya 3000 nchini Ujerumani. Unadhani kwa mipango hii kuna cha kushangaa ukiona wajerumani wanachukua vikombe kwa jinsi wanavyotaka? Ukweli uatabaki daima, mafanikio hayawezi kuja kwa bahati mbaya hata siku moja bali ni mipango inayoeleweka hasa ya kutengeneza vijana na waalimu wa soka kama ilivyofanya DFB kwa ushirikiano wa karibu na serikali ya Ujerumani.

Naamini Joachim Low atakuwa na wakati mgumu wa kuchagua kikosi kwenye michuano ijayo hasa kutokana na uzuri wa wachezaji alionao kuanzia ngazi ya vijana hadi wakongwe. Endapo hatokuwa makini katika uchaguzi atalaumiwa na wajerumani kwani nchi yao ina kila kitu, kila aina ya mchezaji na uzoefu pia. Ni wakati muafaka kwa viongozi wa soka la Bongo kujifunza kitu kutokana na mafanikio ya wajerumani ndani ya siku hizi chache. Kutokana na mipango waliyoweka Wajerumani naweza kusema kwa kasi hii Ulaya na Dunia itazidi nyanyasika zaidi ya ilivyonyanyasika kwa Hitler.

Nidhamu mbovu ya Costa na kiburi cha Conte, kunafanya majaaliwa ya Diego yasieleweke darajani

$
0
0

Na Salym Juma, Arusha

Kiungo mwenye heshima zake AC Milan na Juventus, Andrea Pirlo amewahi kukaririwa akisema kuwa Antonio Conte anapenda kuwa Bosi. Inawezekana watu wengi hawakuelewa kauli hii na kila mtu aliitafsiri kadiri alivyoweza. Kwa maana nyepesi ni kwamba Pirlo alimaanisha Conte huwa hapendi mchezaji fulani kujiona yeye ni bora kuliko wengine. Diego Costa alijikuta anaangukia upande wa pili wa Conte na kujifanya yeye ndie bosi. Costa alifika mbali zaidi na kutaka kumkalia Conte kichwani eti kisa yeye ndiye anaetegemewa baada ya Hazard.

Kutokana na suala hili Conte aliamua kumuandikia ujumbe mfupi wa maandishi Diego na kumtakia kila la heri katika timu atakayokwenda kwani hayumo kwenye mipango yake. Costa anatamani kurudi Atletco ambayo imefungiwa kusajili kwani hawezi kwenda tena nchini China kama alivyokuwa anataka. Leo tujaribu kuchimba sababu ambazo zinamfanya Conte kutomuhitaji kwenye mipango yake licha ya Diego kumpa taji katika msimu wake wa kwanza EPL. Inawezekana kuna vingi ila vichache vinaweza kuwa hivi hapa chini.

Katika mechi iliyochezwa 15 Oct 2016 kati ya Chelsea na Leicester City Diego Costa alionekana kumkaripia kocha wake Antonio Conte akimtaka amfanyie ‘sub’  akihofia kupata kadi ya pili ya manjano hasa baada ya kuwachezea faulu mara kadhaa wachezaji wa Leicester. Costa licha ya kufunga goli la uongozi katika mechi hii alionekana kukaba kwa hasira licha ya timu yake kuongoza magoli mawili hadi wakati huo kabla ya Moses kuhitimisha kwa kufunga goli la tatu. Kitendo hicho hakikumfurahisha Conte hata kidogo japo ‘alinywea’ ila kinyongo hakikumtoka na matokeo yake tunayaona sasa.

Conte ndiye meneja wa timu na yeye anayo mamlaka ya nani aanze nani asubiri. Kitendo cha Costa kumpangia meneja wake kwa kujifanya kaona umuhimu wa mechi dhidi ya United kiliwachukiza wapenzi wengi wa soka kutokana na ukweli kuwa nidhamu ni suala la msingi sana katika mpira. Lugha ya picha aliyoonesha Costa katika mechi hii haikumfanya Conte ampumzishe Costa na badala yake alimuacha hadi mwisho wa mechi, hicho ndicho kiburi cha ‘Dikteta’ Conte cha kutotaka kukawaliwa na mchezaji.

14 Jan 2017 Conte alisafiri takribani kilometa 143 na washambuliaji watatu watakaoanza, Willian, Hazard na Pedro  huku jina la Costa likibaki London. Sababu kubwa ya Costa kuachwa ilielezwa na Conte kuwa ni majeraha yaliyokuwa yanamkabili mshambuliaji huyu kitu ambacho kilikinzana na magazeti ya London. Sababu za kuaminika ni kwamba Conte aligombana na Costa mazoezini hadi kufikia hatua ya Costa ‘kumkusanya’ Conte shingoni. Ili kuboresha morali ya timu na kuepusha migogoro kwenye mapambano, Mtaliano huyu aliamua kulifunika suala hili na kumtetea Costa kwa kigezo cha majeruhi.

Katika kipindi hicho Conte aliangalia morali ya wachezaji wake na shabaha yake kwa msimu hivyo hakupenda kuzungumza suala hili kwenye vyombo vya habari. Conte alijifunza kwa yaliyomtokea mtangulizi wake (Mourinho) ndio maana ilikuwa rahisi kumvumilia Costa ili amalize salama hasa ukiangalia hadi wakati huu Costa ndiye aliyekuwa ameonekana kuibeba timu hadi kuongoza ligi. Uongozi wa klabu pia ulimsihi Costa kutoongea chochote juu ya jambo hili ‘Proffesional player’ anavyopaswa kuwa.

Tianjin Quanjian ni miongoni mwa timu ambazo zilitangaza dau la kumng’oa Costa pale London katika majira ya January. Chelsea chini ya Conte haikuwa na mkakati wowote wa kumuuza Costa kwa kipindi hiki baada ya kuwakosa Washambuliaji iliyokuwa inawahitaji katika dirisha dogo (Morata na Lukaku). Hali hii ilimchanganya Costa kwani aliahidiwa mshahara mnono na timu za China. Tangu kutangazwa kwa habari hizi mwezi January Diego hakuonekana kucheza vizuri kama alivyokuwa anacheza mwanzo kutokana na kuharibika kisaikolojia.

Matatizo makubwa ya Conte na Costa yalianzia hapa kwani Costa hakutaka kucheza kwa moyo wote kuhofia kupata majeraha ambayo yangehatarisha uhamisho wake wa kwenda China kwani alijipa matumaini ya kukamilisha uhamisho kwenye dirisha kubwa kumbe sheria za usajili na malipo ya mishahara kwa vilabu vya China zitakuja kubadilika ila hakuna aliyejua hili kabla. Conte aliamini Costa ni msaliti kwani alitaka aisaliti Chelsea katikati ya mapambano kisa pesa.

Mechi baina ya Manchester United na Chelsea ilikuwa mbaya sana kwa Conte hasa baada ya mchezaji wake wa kutegemewa, Eden Hazard kukabwa vilivyo na kiungo wa Man United, Ander Herera. Kuna wakati Hazard alikabwa na Herera na Eric Bail kwa wakati mmoja. Diego Costa alikuwa ni miongoni mwa watu waliolaumiwa sana kwenye mechi hii kwani alipaswa kuonesha uzoefu wake baada ya mabeki wa Man U muda mwingi kuwa bize na Hazard badala yake muda mwingi alionekana kujiangusha na kunyang’anywa mipira wakati timu ilikuwa inahitaji kusawazisha na kurudisha morali ya mechi.

Conte japokuwa alizidiwa kimbinu na Mou ila naamini ‘kimoyo moyo’ aliishia kumlaumu Costa kwani hakuna alichokuwa anakifanya zaidi ya ‘kui-cost’ timu. Uzembe huu ulimfanya Conte aanze kumpa muda wa kucheza Mich Batshuay kwani aliamini Costa anahitaji changamoto ili arudi kwenye mstari jambo lilifanikiwa kwa kiwango fulani kwani Batshuay ndiye aliyewapa Chelsea ubingwa dakika za mwisho kwenye mechi dhidi ya West Bromwich.

Sababu hizi ndizo zinamjia kichwani Conte kila akilala kwani miongoni mwa makocha wenye viburi na wakorofi katika dunia ya sasa huwezi kumuacha Antonio Conte. Conte anajiamini ana uwezo mkubwa hivyo jambo ambalo limedhihirika msimu uliopita hivyo Costa hawezi kuwa mkubwa kuliko yeye hata mara moja. Pesa aliyopewa inatosha kumnasa mshambuliaji wa kiwango cha Dunia kwa kipindi hiki na tayari yupo kwenye hatua nzuri ya kukamilisha hilo.

Kauli ya Waziri Mkuu ni faraja kwa michezo Tanzania

$
0
0

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amemwagiza Waziri wa Michezo Dr. Harrison Mwakyembe kulifanyia mapitio Baraza la Michezo Tanzania (BMT) na iwapo hatoridhika na utendaji wake alivunje.

Waziri Mkuu ametoa agizo hilo katika hotuba yake ya kuahirisha mkutano wa saba (7) wa Bunge mijini Dodoma.

“Serikali imeazimia kusimamia, kuimarisha, vyombo vya michezo nchini ila kila mwenye dhamana awajibike ipasavyo, kwa msingi huo, leo hii naelekeza kwa Waziri mwenye dhamana ya michezo nchini kulifanyia mapitio na kutathmini upya Baraza la Michezo Tanzania ili kujiridhisha na usimamizi wake wa shughuli za michezo nchini pale itakapothibitika usimamizi sio makini, anayoruhusa ya kulivunja na kuunda baraza jipya.”

Pia Waziri Mkuu amempongeza Mh. Rais Dkt. John Magufuli kwa kuunga mkono jitihada za michezo nchini kwa dhamira yake ya kujenga uwanja wa michezo mkoani Dodoma.

“Nimpongeze Mh. Rais kwa kitendo chake cha kuunga mkono jitihada za michezo nchini kwa dhamira yake ya kujenga uwanja mkubwa wa michezo hapa Dodoma makao makuu ya nchi kwa kushawishi mataifa rafiki kama Morocco ambao wameahidi kujenga uwanja mkubwa hapaDodoma.”

Namuunga mkono Waziri Mkuu na ifike mahali hizi taasisi za michezo zifanye kazi ipasavyo na sio kufanya kazi kwa mazoea kwa sababu wanabeba dhamana kubwa ya watanzania nyuma yao, kwa hiyo wanapoamua kuingia huko ndani basi wakafanye kazi kwa nia njema ya kusaidia maendeleo ya michezo hapa nchini.

Waziri Mkuu anazungumza sio kwakuwa ni kiongozi wan chi, ni mtu ambaye anajua na amekaa kwenye masuala ya michezo kwa hiyo hadanganywi kitu, anazungumza kitu anachokifahamu na ana uhakika nacho.

Kwa upande wa Mwakyembe yeye ni mtu ambaye amejizolea sifa nyingi sana kutokana na misimamo yake, ni mtu ambaye hayumbishwi, kwa hiyo naamini atafanya kile ambacho ameagizwa na Waziri Mkuu.

Hata ukiangalia sheria zake ni za zamani sana mwaka 1967 sheria ya kwanza inatungwa halafu inafanyiwa marekebisho mwaka 1971, ukiangalia kutoka muda huo hadi leo 2017 kuna vitu vingi vimebadilika kwenye michezo. Siku hizi michezo ina wigo mpana hadi imekuwa biahara, leo hii taifa linaweza kunufaika kupitia michezo, kwa hiyo ni muhimu kutazama kwa mapana namna gani BMT litaendana na kasi ya mahitaji ya michezo kwa wakati huu.

Tumekuwa watu ambao tunailaumu serikali kwamba hai-support michezo, lakini hata kama ungekuwa wewe lazima ungejiuliza unatoa vipi hiyo support bila kujua kile unachotaka kukisaidia hakitakwenda hakitafanya vila inavyotakiwa. Serikali jukumu lake ni kusaidia baada ya jitihada za awali kuoneshwa na wahusika.

Mfano, hivi karibuni baada ya bajeti ya Wizara inayosimamia michezo kutajwa na kuonekana ni kiasi kidogo, watu wengi walikuwa wakiilamu serikali kwamba haisaidii, lakini serikali inatakiwa kupokea mapendekezo kutoka kwenye vyama vya michezo (chama cha mpira wa miguu, ngumi, basketball) wanatakiwa wachukue bajeti zao na kuzipeleka Wizarani wawaoneshe kwamba serikali inaweza kusaidia kwa namna fulani.

Serikali itaangalia namna ya kusaidia na kuziingiza hizo bajeti kwenye bajeti kuu ya Wizara, lakini kama hawashirikishwi halafu mwisho wa siku tunawalaumu, tutakuwa tunawaonea.

Tupa kule akina Pogba na Mbape, tazama majembe yaliyostaili zaidi ya €95 ila bahati mbaya yamestaafu

$
0
0

Na Salym Juma, Arusha

Dunia ya soka imeelekeza macho kwenye usajili huku Magazeti na Blog mbalimbali ikitawaliwa na tetesi za usajili pamoja na taarifa kamili za nani kaenda wapi na nani kavutwa wapi. Cha kushangaza ni kwamba kuna baadhi ya Wachezaji wanathaminishwa kwa pesa kubwa tofauti na uwezo na mafanikio yao pia. Leo hii vijana kama akina Mbape wanatajwa
kuwa na thamani ya paundi zaidi ya 100 jambo ambalo nitakuwa wa mwisho kulikubali.

Binafsi nilibahatika kutazama viwango vya baadhi ya wachezaji ambao walikuwa na uwezo mkubwa ila thamani kipesa ilikuwa ya kawaida labda kwa sababu ya nyakati pia.

Thiery Henry ni moja kati ya washambuliaji wachache ambao Dunia inawamisi kwa kipindi hiki ambacho akina Mbape ndio wanaonekana watu hatari katika eneo hili. Mzee Wenger huenda anajuta kumjua Henry kipindi kile kwani huu ndio ulikuwa wakati sahihi wa Henry kuwepo Arsenal kwa maana kubwa mbili, moja ni kwamba Arsenal haijapata mshambuliaji wa kueleweka tangu aondoke ‘Mheshimiwa’ Robin Van Persie na hii imefanya heshima ya Arsenal kupotea kabisa, pili kwa jinsi ‘Professor’ Wenger alivyo mchumi angeweza kutengeneza pesa chafu kwa kumuuza ‘Chogo boy’ kwingineko.

Henry aliyeichezea Arsenal mechi 254 kuanzia mwaka 1999 hadi 2007 aliweza kufunga magoli 174 huku dunia ikinyoosha mikono juu ishara ya kumpa heshima kama miongoni mwa ‘icon’ wachache wa Arsenal. Naamini uwezo wa Henry kwenye eneo la hatari la timu pinzani ulistahili mchezaji huyu kuuzwa zaidi ya paundi milioni 90 kama zama zile zingekuwa sasa. Ila cha ajabu ni kwamba Henry aliuzwa Barcelona kwa €24 million.

Ronaldinho ni zaidi ya mchawi wa mpira aliyepata kuonekana katika zama zake. Wakati nyie mkiwa bize kubishana ni nani bora kati ya Messi na CR7 mi nacheka kwa dharau maana nilibahatika kumfaidi Mchawi huyu aliyekuwa anatukosha kwa tabasamu lake muda wote wa mchezo. Gaucho alipiga chenga zote ambazo Messi kazipiga, Gaucho alifunga magoli yote
ambayo CR7 kafunga. Heshima anayopewa sasa pale Barcelona ni ndogo sana kulingana na shughuli nzito aliyoifanya kipindi yupo katika ubora wake.

Naamini hata Okocha alikuwa anajaribu kuyafanya yale ambayo Gaucho amesha yafanya.
Unadhani ingelikuwa zama hizi bei halisi ya Gaucho ingekuwakiasi gani? Wallah naapa bei ya chini kabisa ingekuwa £200 millioni anaebisha aje kwa hoja yenye mashiko na sio ya kishabiki. Thamani pekee ya goli la free-kick kutoka yadi 40 alilowafunga England chini ya mlinda mlango David Seaman ni takribani paundi 20 millioni. Gaucho alicheza Barca kuanzia 2003 hadi 2008 huku katika michezo 145 akifunga magoli 70 ila kumbuka huyu alikuwa kiungo mshambuliaji. Baada ya kuipiga chini ofa kutoka Man City, Gaucho alisaini Milani kwa  €22.05 millioni.

Raúl González Blanco. Teh teh teh teh najikuta nacheka nikisikia Mbape ana thamani ya paundi 100 millioni. Hivi ni nani aliyekuwa anamjua mshambuliaji huyu ambaye ilifika kipindi wahispania walitaka wamaubudu?  Raul alishinda mataji mengi sana na aliweza kudumu kwenye kikosi cha Madrid licha ya kuwepo kwa washambuIiaji hatari kama Ronaldo de Lima. Kiwango cha mshambuliaji huyu hakikuwahi kufikiwa na mshambuliaji yoyote wa Hispania japo Tores alijaribu kwa kadiri alivyoweza katika ngazi za vilabu na timu ya taifa. Raul nyavu zilikuwa zinamuogopa kwani hakuwa na masikhara langoni.

Raul angekuwa zama hizi zenye utani na pesa naamini bei yake ingekuwa zaidi ya paund 95 million na hili halina shaka hata kidogo. Kiwango chake kilimfanya atajwe na FFHS  kama mshambuliaji bora mwaka 1999, huku pia akitajwa kama mshambuliaji bora wa UEFA mara tatu mfululizo 2000, 2001 na 2002. Unadhani heshima hii ni mshambuliaji gani wa zama hizi kapewa? Leo hii kijana mdogo ambaye ana uwezo wa kawaida anauzwa paundi 100 millioni.

Ronaldo de Lima alimaliza karia yake kwa kufunga magoli 352 katika michezo 518. Ni mtu anayestahili heshima na lau kama anaona vijana kama akina Mbape wanatajwa kuwa na bei ya paund zaidi ya 100 atakuwa anashika mdomo kwa mshangao mkubwa huku akitamani zama za nyuma zirejee sasa na yeye aonekane kijana mbichi aliyemtungua Oliver Khani pale Japan mwaka 2002. Mikasi aliyokuwa anapiga CR7 inawezekana Ronaldo alikuwa anaitazama kwenye luninga huku akicheka kwa kejeli kwani hakukuwa na jipya kwa CR7. Ronaldo alikuwa na uwezo ambao hadi kesho Brazili itajivunia jina lake.

Licha ya nyota yake kuonekana mapema, Ronaldo hakulewa sifa, alikuwa na uwezo wa ‘ku-driblle’ uwezo wa kupiga chenga, kasi na mmaliziaji mzuri. Niambie ni mshambuliaji gani wa sasa mwenye sifa hizi.

Inawezekana Messi na CR7 wakajaribu ila bado wamekopi vitu vingi kutoka kwa Jembe hili ambalo liliichezea Brazil mechi 98 na kufunga magoli 62. Real Madrid ilimnunua kwa kiasi cha €46 milioni kutoka Inter huku mauzo ya jezi yake yakivunja rekodi. Nadhani angekuwepo leo thamani yake ingekuwa zaidi ya  €150.

Kwa leo namalizia na fundi mwingine ambaye anayo heshima yake pale Ufaransa. Zinedine Zidane hawezi kusahaulika milele pale Ufaransa na Madrid. Zidane alikuwa na uwezo mkubwa mno na angekuwepo leo hii naamini mshahara anaopokea CR7 ungekuwa halali yake. Zidane angekuwa na thamani kubwa zaidi ya Pogba. Goli alilowafunga Levekusen kwenye fainali ya UEFA bado vijana wa sasa wana deni la kulipa licha ya kupewa thamani kubwa wasiostahili. Kiungo huyu mchezeshaji alikuwa na chenga za dharau na uwezo mkubwa wa kushambulia timu pinzani.

Japo hakufunga sana katika vilabu alivyocheza ila alifanya makubwa ambayo daima tutaiheshimu thamani yake. Zidane hatojilaumu sana kwani €77.5 million alizonunuliwa akiwa Juve kwenda Madrid hazikuwa haba ila naamini angelikuwepo leo tungekuwa tunazungmza mengine. Uwezo wake akiwa kocha hautofautiani sana na alivyokuwa uwanjani.

Kwanini nyota ya Verratti inang’aa hata kukiwa na mawingu mazito?

$
0
0

Na Salym Juma, Arusha

Jezi namba 6 ndiyo iliyokabidhiwa na PSG kwa kiungo mkorofi aliyezaliwa miaka 24 iliyopita pale Pescara. Hii ilikuwa baada ya kuwaniwa na vilabu kadhaa kama Napoli, Roma na Juventus mnamo mwaka 2012. Uwezo wake wa kutawala kuanzia chini (mbele ya mabeki) hadi eneo la ‘final third’ la timu pinzani uliwafanya Pescara kushinda taji la Serie B mwaka 2012. Kujiunga kwake PSG kumemfanya kupevuka na sasa, mbali na Barcelona, vilabu kadhaa vilitajwa kuwania saini yake kabla hata ya dirisha kufunguliwa na leo hii tujaribu kutazama kwanini Marco Verratti amekuwa akiwaniwa…

Kabarikiwa uwezo wa kuwa kiungo wa kati Mchezeshaji. Verratti ni miongoni mwa viungo wachache wenye kipaji hiki kwani tumezoea kuwaona viungo wengi wa kati wakiwa na kipaji kimoja cha kukaba ila linapokuja suala la kukaba na kuichezesha timu kwa wakati mmoja hauwezi ukawakuta viungo wengi, bila shaka wapo wachache na katika hao wachache Verratti ni miongoni mwao, kumbuka viungo wengi wachezeshaji hukaa juu kidogo ya eneo la katikati ila kwa Verratti ni tofauti. Uwezo huu unamfanya ‘afiti’ katika timu nyingi kama Barcelona, Arsenal na hata Chelsea.

Uwezo mkubwa wa kukokota mpira. Kimombo wanaita ‘dribbling skills’. Ni viungo wachache sana wanaomudu kazi hii ambayo ni nyepesi kwa washambuliaji kama akina Neymar, Hazard, Messi, CR7 na Dybala. Verratti ni mwepesi wa kupiga vyenga na ushahidi wa hili wanao Chelsea na Barcelona. Uwezo huu ni rahisi kuibeba timu hasa pale ambapo timu yake inapokuwa imetawala eneo la kiungo kwani Verratti hugeuka kiungo mshambuliaji na hapa ndipo alipotoa zile ‘assist’ na hata kufunga pia. Kipaji hiki ndicho kinamtofautisha na mkongwe Andrea Pirlo ambaye amekuwa akifananishwa naye.

Maamuzi ya haraka na uwezo mkubwa wa kuudhibiti mpira katika eneo lake. ‘Control’ ni uwezo ambao wachezaji wengi wanaocheza Ulaya wamejaaliwa ila kuwa na uamuzi wa haraka tena chanya ambao unainufaisha timu uwanjani ni jambo ambalo viungo wachache wamebarikiwa. Maamuzi ndiyo yaliyowafanya akina Xavi, Pirlo, Lampard na Gerald kuwa na heshima waliyonayo hivi sasa. Verratti ni mwepesi wa kumnyang’anya mpinzani mpira eneo lolote tena bila kucheza faulo. Marco pia anaweza kutoa pasi yenye madhara kwa wapinzani sehemu ambayo hukuitarajia.

Ni mzuri wa kupooza mashambulizi na kurudisha umiliki wa timu. Bila shaka eneo hili wengi wanalimudu. Siwezi kumuacha Herera, Wanyama au Kante katika kufanya kazi hii ila nahitajika kumzungumzia Verratti kwani shughuli aliyoionesha dhidi ya Barca haikuwa ya kawaida. Vilabu vya League 1 vinaujua uwezo wake hasa pale PSG inapokuwa katika hali ya kushambuliwa. Niliwahi kumuona akiwatesa Chelsea, Barca, Monaco na Lyon katika anga hii kwani ni mwepesi wa kumnyang’anya mpinzani mpira na kupiga vyenga hadi timu ikapunguza presha na kurudi katika hali ya kawaida.

Macho makali ya kupiga pasi ndefu na kuwatengenezea wenzake nafasi ni jambo lingine linalomfanya Verratti kucheza popote. kupiga pasi ndefu zenye madhara ni kazi ya watu wachache kama akina Fabregas, Alonso, Carick au Pirlo ila Verratti ni mtu sahihi katika eneo hili ambalo Barcelona wanahangaika kumtafuta Xavi wa zama hizi. ‘Assist’ 7 alizotoa katika michezo 31 na magoli mawili ni ishara tosha kuwa Macho yake hayahitaji miwani uwanjani. PSG imeshinda mara 9 katika michezo 10 ya mwisho huku Verratti akionekana kama mhimili mkubwa katika ushindi huu.

Japokuwa amekuwa na mapungufu kadhaa katika mipira ya juu na nidhamu mbovu ila mapungufu ni machache kuliko ubora wake uwanjani. Uwezekano wa Verratti kubaki PSG ni mdogo mno kutokana na kutajwa kuwa mrithi wa Cazola pale Emirates au kwenda kuboresha eneo la katikati pale Camp Nou. Usajili wa Bakayoko kwenda Chelsea utapunguza nguvu ya Verratti kuwaniwa darajani ila bado soko lake ni kubwa sana barani Ulaya kwani licha ya majina ya viungo wengi kutajwa kipindi hiki, Verratti anaweza kuwapiku kwa bei endapo atasajiliwa katika majira haya.

Viewing all 676 articles
Browse latest View live


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>