Quantcast
Channel: Makala – ShaffihDauda
Viewing all 676 articles
Browse latest View live

Liverpool Wasikosee, Coutinho Hana DNA Ya Ubingwa.

$
0
0

Waliwahi kuishi Steven Gerrard ambaye aliiweka klabu ya Liverpool mabegani na kuhakikisha kuwa haizami kwenye kina chochote cha bahari, alikuwepo siku zote na alikuwa mtakatifu nyakati ambazo Liverpool ilinuka dhambi. Pale kwenye daraja analotamba Antonio Conte aliwahi kuletwa kijana mdogo Frank Lampard ambaye aligeuka kuwa mwanaume wa klabu hiyo mpaka siku anayoondoka. Huyu aliibuka mafichoni siku zote ili kuzima moto utakaoshika nyumba anayoishi inayoitwa Chelsea.

Usitaje kuhusu Ronaldinho ambaye maamuzi yake kwenye soka yalikuwa jirani na akili za Sir. Isaac Newton aliyewafanya wengi kujivunia vyombo vya usafiri katika dunia ya leo. Huyu ambaye wale mashabiki watata wa Madrid maarufu kama Ultra Sur walisimama kupiga makofi baada ya kufanya mambo ambayo ungeenda kumkagua kama ana mbawa yaani pengine ni malaika anayecheza na binadamu wengine.

Pengine Zidane hakubarikiwa kuwa mfungaji bora kama hao waliotajwa, lakini huyu alikuwa Yusufu, mfalme aliyeaminiwa zaidi na Mungu na akamtuma aje kuuamrisha mpira na kila shuruti yake ulitii. Alifanya kila lililokuwa jema, alijifika kofia na wengine wakasujudu, vinywa kuwa wazi ilikuwa sifa ya washabiki waliotembelea uwanja ambao angechezea siku hiyo.

Sayansi inasema dunia inazunguka kwenye mhimili wake huku ikizunguka jua, hii inatoa nafasi kwa wana kukua na kufika utu uzima. Shukuru Mungu hatimaye umemwona Eden Hazard ambaye anaweza kuwa winga mbunifu zaidi kwa sasa, sujudu kuwa umemtizama Neymar, winga aliyekamilika zaidi kwa dunia ya leo, kisha mtizame Coutinho na weka goti lako chini na sema asante kuwa yupo kwenye mboni safi za macho yako. Sahau yote kuhusu waliopita, hawa wapo katika kizazi chao cha tofauti.

Wakati Iniesta akilipisha giza lishike hatamu, wamezaliwa akina Coutinho wengi. Huyu anaishi ndani ya Anfield, anabeba nembo ya ndege ambayo inathaminiwa na mashabiki wa Liverpool duniani kote. Huyu pia ndiye mchezaji wao ghali zaidi kwenye soko la sasa na ndiye wanayemlipa mshahara mnono zaidi. Wanampenda na safari ya maisha yake inampa sababu ya kuwathamini zaidi kwa sababu wameishi nae tangu akiwa jiwe tu mpaka sasa ni dhahabu yao.

Huyu ndiye anayebeba jina la mchawi ndani ya Anfield huku akiwa ndiye mchezaji wao mbunifu zaidi. Liverpool haijawa kwenye muonekano wa kuwa klabu iliyokuwa tayari kushindani ubingwa kwa kipindi kirefu sasa, tangu Suarez akiwa amiri jeshi wao mkuu. Kipindi hiki chini ya Klopp wanaishi wakiamini timu inatakiwa kuwa na muunganiko wa pamoja na ndicho kinachotakiwa kuamua matokeo yao.

Kwa kiasi kikubwa mwanzo wa msimu huu mfumo ulikuwa “mujarabu” kwa sababu Coutinho alifanya kila kitu kiwe rahisi kwa wenzie. Alimfanya Lallana asikimbie sana, alimweka Firmino kwenye nafasi sahihi ya kuwasumbua mabeki na hata Mane angeweza kukimbia kwa uhuru zaidi na kuwaweka wapinzani katika hali joto. Kipindi hiki chote alifikisha mabao 5 na pasi 5 kabla ya mwaka kuisha na kabla hajaumia, huku Liverpool ikiwa na safu hatari zaidi ya ushambuliaji.

Lakini ni huyu Coutinho ambaye wakati anatua Inter Milan, Ronaldinho aliamini kuwa kuna mchezaji bora wa Serie A amezaliwa, likuwa na miaka 18 tu. Lakini maisha hayakumwendea sawa kwa sababu hajui kuwa na mwendelezo “consistency.” Hii ndio sababu iliyofanya Ricky Alvarez na Mateo Kovacic waweze kumwondoa mapema kikosini na akaanza kuzurura kwa mkopo kabla ya kuokolewa na Brendan Rodgers.

Hata Liverpool ameshindwa kuivua kofia hii, kashindwa kuiacha na ni vazi analolipenda. Liverpool yote inakwama kwa sasa mpira unapofika kwake, amesahau kila kitu na ni kama hata macho yake yamepoteza nuru ya kutizama mbele. Na ni huyu ambaye Liverpool ilitegemewa kujengwa kumzunguka yeye. Hili ni tatizo ambalo hata Hazard amekuwa nalo kwa muda kadhaa ingawa ana bahati na kikosi kinachokuwa kimemzunguka na ndio tofauti yao wote na Neymar, yaani kukua na kukomaa na wakati. Kwa Coutinho ni kubwa zaidi na kwa Hazard inaisha.

Kwa umri wa miaka 25 sasa, Coutinho alitakiwa awe amejifunza hili. Lakini kuwa na moyo wa ushindi mtu anazaliwa nayo. Hii huwa DNA, na ndio maana usingejiuliza mara mbili kwa Gerrard au Lampard. Miguu ya Zidane, moyo na sura yake vingezungumza ushindi siku zote. Hili hata Ozil hana ndio maana ni rahisi kumtafutia Sanchez kuwa kiongozi wake. Mashabiki wa Liverpool hawataki kuamini hili, ila ukweli ni mchungu. Ukweli kuwa hawatakiwi kuamini ndani ya Coutinho kwa sababu hawezi kuwa mwanaume wa timu, na hawezi kuongoza timu kama mfano.

Mpaka sasa anaonekana kuishi maisha ya “supporting cast” yaani msaidizi, hana Ufirimino ndani yake. Anaweza kukufaa sana ukimpata aina ya Costa au mshambuliaji yoyote ambaye ataingia kwenye mfumo wa Liverpool na msaada wa Firmino, lakini timu isimzunguke yeye. Na kama akiona hana furaha kupunguziwa majukumu, njia sahihi ni kumuuza maana analipa kweli.  Lakini Liverpool haiwezi kuwa mshindi kama huyu atawaongoza, hana DNA ya ushindi na hana DNA ya ubingwa. Anafaa sana kucheza nyuma ya kivuli kingine.

Nicasius Agwanda “Coutinho”

Instagram @Kotinyotz

 


Ushahidi wa kitakwimu unaonyesha Pogba ni zaidi ya Kante

$
0
0

Umekuwa mwaka wa matukio mengi kwa kiungo wa Manchester United – Paul Pogba.
Jambo la kwanza lilimuhusisha na biashara iliyochukua muda mrefu zaidi wakati wa dirisha la usajili la kiangazi kabla ya kukamilisha uhamisho wa  £89million kwenda Old Trafford.
Tangu wakati huo, dunia ya wapenda soka ilitegemea kuona akiendeleza kiwango chake alichokuwa nacho Juventus – akifunga magoli mengi, na kutoa assists nyingi zilizoisaidia Juve kuiteka Serie A.

Pamoja na mategemeo makubwa, lakini mashabiki na wachambuzi wa soka bado hawajaridhishwa na kiwango cha Pogba katika msimu huu unaoendelea.

Kiungo huyo mfaransa bado hajaonyesha thamani ya fedha aliyosajiliwa.

Wakati huo huo, ulimwengu wa soka umekuwa hauishiwi sifa kwa kiungo wa Chelsea – N’Golo Kante, ambaye kiwango chake kimeonyesha dhahiri fedha iliyolipwa na Chelsea ya £30m kama ada ya usajili ilistahili.

Hata hivyo, kuna jambo watu wengi hawafahamu – Pogba amemzidi Kante karibia katika kila sekta ya kitakwimu msimu huu.

Vijana hawa wawili wa kifaransa wote wamecheza mechi nyingi msimu huu – japo Kante amemzidi Pogba takribani dakika 80, katika mashindano yote.


Pamoja na kucheza dakika nyingi zaidi ya Pogba, Kante amezidiwa idadi ya magoli ya kufunga, assists, mashuti yaliyolenga goli, kutumia nafasi, kutengeneza nafasi kwa wachezaji wenzao, dribbling(kukokota mipira) na jumla ya pasi zilizofanikiwa, n.k.

Sehemu pekee ambayo Kante anamzidi Pogba, kwa kufanya tackling (kupora mipira), interception (kuingilia mashambulizi ya wapinzani), na kukimbia kwa eneo kubwa dimbani.

Pamoja na hayo, takwimu hizi hazibadilishi ukweli kwamba Kante ana msimu mzuri – lakini inashangaza kuona watu wanamkosoa sana Pogba, lakini wanamsifia sana kiungo huyo wa Chelsea.


Labda tatizo linalomzuia Pogba kufanya vyema zaidi ni kwa sababu ni kupewa majukumu mengi na Jose Mourinho- kusaidia safu ya ulinzi, kutengeneza na kumalizia mashambulizi.

Wakati Antonio Conte anampa Kante uhuru wa kufanya majukumu kutokana na uwezo uwezo wake – kufukuza washambulizi, kusafisha uchafu golini na kuipeleka mipira hiyo kwa viungo watengenezaji akina Eden Hazard.

Huenda Pogba akafanikiwa zaidi kama ilivyokuwa Serie A ikiwa atapewa majukumu tofauti na ilivyo sasa.


Ikiwa Mourinho atafanikiwa kuwasajili wachezaji anaowahitaji – kama Fabinho – kiungo wa kibrazil anayekipiga Monaco, Pogba anaweza kuruhusiwa kufocua zaidi kwenye kufanya dribbling zake kwenye eneo la wapinzani na kuwatawanya walinzi na kutengeneza nafasi nzuri zaidi kwa washambuliaji au kwenda mwenyewe kufunga.

Kwa hakika Pogba hajafanikiwa kuwaridhisha hata baadhi ya mashabiki wa Manchester United kulingana na mategemeo waliyokuwa nayo juu yake. Lakini endapo Mourinho atafanikiwa kupata mchezaji wa kumpunguzia Pogba majukumu – mchezaji aina ya Kante – dunia itamuona Pogba ambaye ataenda kuiteka dunia.

Jicho la 3: ‘Ni lazima Lwandamina ashinde vs Azam FC vinginevyo  atakuwa si kocha sahihi Yanga’

$
0
0

Na Baraka Mbolembole

NI ALAMA za nyakati ambazo kocha George Lwandamina anatakiwa kuzisoma kuhusu ubora wa wachezaji wake.

Baadhi ya watu wanasema nyota wengi wa kikosi cha Yanga SC umri ‘umewatupa’ lakini wanasahau kuwa ni kikosi hikihiki kinacho-pepesuka chini ya Lwandamina ndicho kilichoshinda mataji mawili ndani ya Tanzania na kufika hatua ya 16 bora katika ligi ya mabingwa Afrika kisha kufuzu kwa hatua ya makundi katika Caf Confederation Cup msimu uliopita chini ya Mholland, Hans van der Pluijm.

Lwandamina hatakwepa lawama ikiwa Yanga itashindwa kutetea ubingwa wake wa ligi kuu, FA Cup na kushindwa kuifikisha timu hiyo katika hatua ya makundi ya Confederation Cup walipoangukia baada ya kutolewa hatua ya 32 bora katika ligi ya mabingwa na timu isiyo na uzoefu-Zanaco FC katikati ya mwezi huu.

Kuelekea mchezo wa Jumamosi hii kati ya Azam FC vs Yanga, Lwandamina anapaswa kusimama kama kiongozi mkuu wa vita huku akitambua kushindwa kupata ushindi kwa namna yoyote ni pigo katika mbio za ubingwa.

POINTI 18 ZA ‘KUFA NA KUPONA’

Ikiwa imesalia michezo 6 kabla ya kumalizika kwa msimu-inamaana kila timu ina pointi 18  muhimu za kuisaidia kutimiza malengo yao, Yanga wako nyuma kwa alama mbili zaidi dhidi ya mahasimu wao Simba SC ambao watakuwa Katiba Stadium kucheza na Kagera Sugar siku ya Jumapili.

Ushindi dhidi ya Azam FC kesho utaipeleka Yanga kileleni kwa alama moja zaidi, na hilo litapeleka presha kwa Simba kuhakikisha wanaishinda Kagera Sugar ili kuwaengua Yanga kileleni siku ya Jumapili.

Yanga hawapaswi kujilaumu kwa kushindwa kuifunga Mtibwa Sugar wiki tatu zilizopita na kukwea kileleni baada ya Simba kuangusha pointi mbili katika uwanja wa Taifa walipocheza na Mbeya City FC siku moja kabla ya Mtibwa v Yanga.

Bali wanapaswa kuchukulia matokeo ya kupoteza mkwaju wa penati kwa winger Saimon Msuva katika suluhu-tasa vs Mtibwa kama funzo litakalowaongezea umakini na nidhamu ya mchezo katika mchezo mgumu zaidi watakapocheza dhidi ya Azam FC wikendi hii.

Katika historia yao VPL, Azam FC pekee ‘inayoisumbua zaidi’ Yanga, na mabingwa hao wa kihistoria wa Bara hawawezi kupinga hilo kwa maana katika mipambano yao 17 iliyopita katika VPL kila timu imefanikiwa kupata ushindi katika michezo mitano huku michezo 7 ilimalizika kwa sare.

AZAM FC WANACHEZA KITIMU ZAIDI TOFAUTI NA YANGA

Azam FC huenda wana kikosi kipya zaidi ya Yanga na licha ya kutokuwa na msimu mzuri katika ligi na kuondolewa raundi ya kwanza katika Caf Confederation Cup lakini bado Azam FC inacheza kitimu hasa katika mipambano mikubwa.

Wachezaji wazoefu kikosini kama Shomari Kapombe, Erasto Nyoni, David Mwantika na Aggrey Moris katika safu ya ulinzi wameweza kuwapokea vizuri nyota wa kulipwa kama Mzimbabwe, Bruce Kangwa na raia wa Cameroon, Yakub Mohamed ambao wameingia msimu huu na kufanya vizuri.

YANGA WANAPASWA KUCHEZA KITIMU  

Wachezaji wa Yanga wanapaswa kucheza kitimu, walikuwa wakicheza hivyo huku wakiajiamini chini ya Hans lakini ndani ya miezi mitatu chini ya Mzambia, Lwandamina si wale walioshinda mataji ya VPL na FA msimu uliopita.

Wamepunguza hamasa yao ya kusaka na kulazimisha matokeo, na sasa wanapaswa kujituma zaidi ili kushinda ubingwa wa tatu mfululizo. Kwa namna walivyocheza hadi kufika walipo sasa, wanaweza kutimiza matarajio yao.

Kufunga magoli 49 katika michezo 24 hakuwezi kuwapa matarajio makubwa mbele ya Azam FC ambao wameruhusu nyavu zao mara 15 na kufunga magoli 29 tu katika game 24 walizokwisha cheza.

Endapo Donald Ngoma atarejea uwanjani kwenye mechi ya kesho ni habari njema zaidi kwa kikosi cha Lwandamina, hata kama atamkosa Amis Tambwe bado kocha huyo anaweza kuwapanga Ngoma, Msuva na Mzambia, Obrey Chirwa kama washambuliaji watatu katika mfumo wa 4-3-3.

MAHUNDI, SINGANO vs KESSY, MWINYI NI TATIZO

Beki ya Azam imekuwa ikiimarika tangu kuanza kwa mzunguko wa pili lakini inaweza kupitika ikiwa timu pinzani itashambulia kwa kasi. Ugumu ambao unamkabili Lwandamina ni namna gani safu yake ya ulinzi itaweza kuendana na kasi ya viungo wa pembeni wa Azam FC, Joseph Mahundi na Ramadhani Singano ambao watacheza kumzunguka Mghana, Yahya Mohamed.

Si shaka kuhusu uwezo wa Rambdhani Kessy ambaye alipata umaarueu mkubwa nchini Novemba, 2014 baada ya kumzima Singano katika mchezo uliowakutanisha wakiwa timu za Mtibwa (Kessy) na Simba (Singano).

Lakini wasiwasi ni lazima utakuwepo kuhusu mbinu za kujilinda za Mwinyi Hajji  katika  beki namba tatu, hasa  akicheza  dhidi  ya Mahundi mwenye  kasi,nguvu  na  uwezo  wa kukimbia  na  mpira. Hajji  amekuwa  akipoteza mipira  mara  kwa  mara  na  mbaya  zaidi  amekuwa akipoteza mipira  hiyo  akiwa  katika  eneo  lake  la  ulinzi.

HIMID, DOMAYO, SALUM vs NIYONZIMA, ZULU, KAMUSOKO

Mechi  hii  inaweza  kuamuliwa  zaidi  na  namna  safu  za  viungo   zitakavyocheza. Azam FC wamekuwa  wakiwatumia Himid Mao, Salum Abubakary  na Frank Domayo  katikati ya uwanja na watatu hao katika ligi ya Bara wamekuwa wakitawala mechi.

Ili kujaribu kuizuia Azam FC katikati ya uwanja kocha Lwandamina  anaweza kuwapanga Mzambia, Justine Zulu katika eneo la kiungo wa ulinzi, Mzimbabwe ,Thaban Kamusoko na Haruna Niyonzima  wakiichezesha  timu. Hawa ni viungo watatu wa Kimataifa na Yanga inawahitaji kuonyesha uwezo wao  sasa ili timu inufaike.

Kucheza hawa watatu  inasaidia  kwa maana  watakuwa  na mtazamo  mpana wa kulinda na kushambulia, lakini  haitawarahisishia  kwa maana Himid, Domayo na Salum ni wagumu  na wana ustahimilivu mkubwa ndani ya uwanja.

Azam hupasiana pasi fupifupi za uhakika na mara chache  Domayo  amekuwa  akipiga pasi  ndefu za uhakika ili kutawala mechi Yanga italazimika kupeleka mipira mirefu pembeni ya uwanja ambako Zulu  na Msuva  watakuwawepo.

AZAM FC BILA BOCCO

Ni faida kubwa kwa Yanga kwa maana kutokuwepo kwa ‘kiboko’ yao nahodha John Bocco  huenda wasikutane  na makali zaidi  ikiwa angekuwepo. Vicent Bossou na Nadir Haroub inaweza kuwa beki sahihi ya kucheza dhidi ya Yahya katika safu ya kati.

Azam wamekuwa wakikabiliwa na tatizo katika ufungaji na kitendo cha kumkosa Bocco  aliyefunga magoli nane kati ya 29 waliyofunga katikaligi ni tatizo ambalo linaweza kuwaangusha zaidi. Wanaweza kutegemea mashuti ya mbali kutoka kwa Domayo, Salum,Mahundi na Himid na kama  ikitokea wakatangulia kupata goli itakuwa rahisi kwao  kupata matokeo.

Ni lazima Lwandamina ashinde vs Azam FC vinginevyo  atakuwa si kocha sahihi Yanga hasa ukizingatia tayari ameshindwa kuifunga Simba katika michezo miwili, ameshindwa kuifunga timu ya kawaida Zanaco FC, amepoteza 4-0 mbele ya Azam FC na ameshindwa kuzifunga timu kama Mtibwa, African Lyon katika nyakati ambazo timu ilipaswa kuchukua pointi.

Kagera inaweza kuifunga Simba ikiwa Mexime, Mbaraka Yusuph, hawatokuwa na kikomo…

$
0
0

Na Baraka Mbolembole

WAKATI ushindi wa aina yoyote dhidi ya Azam FC  leo Jumamosi utawapeleka mabingwa watetezi Yanga SC katika kilele cha msimasmo wa ligi kuu Tanzania Bara, Simba SC kesho Jumapili watakuwa uwanja wa Kaitaba, Bukoba katika kibarua kigumu watakapowavaa wenyeji Kagera Sugar FC.

Kagera iliyo katika nafasi ya nne na alama 42 baada ya kucheza michezo 24 ilitolewa katika michuano ya FA Cup baada ya kuchapwa 2-1 na Mbao FC katika mchezo war obo fainali uliopigwa katika uwanja huo wa Kaitaba wiki iliyopita.

MBARAKA YUSUPH

Kocha Mecky Mexime anajivunia ‘utitiri’ wa washambuliaji katika kikosi chake, lakini ataendelea kumtegemea mfungaji wake namba moja kijana Mbaraka Yusuph ambaye tayari amefunga magoli kumi hadi sasa katika VPL.

Ame Ally alifunga goli lake la kwanza akiichezea Kagera katika kichapo dhidi ya Mbao na huenda mshambulizi huyo wa zamani wa Mtibwa Sugar, Azam FC na Simba akaanza katika safu ya mashambulizi sambamba na Yusuph ambaye alifunga goli lake la kwanza la kimataifa katika mchezo wake wa kwanza akiichezea Taifa Stars Jumanne iliyopita.

Danny Mrwanda, Ibrahim Twaha, Themi Felix, Edward Christopher na Paul Ngwai wote hawa ni washambuliaji ambao wanaweza kuibeba Kagera ikitokea wakapata nafasi katika mchezo wa kesho.

Kagera hutafuta bao kwa nguvu zote wanapocheza nyumbani, hucheza mchezo wa kuvamia lango la wapinzani wao ndiyo maana licha ya kuchapwa 6-2 na Yanga katika mchezo wa raundi ya kwanza katika uwanja huo lakini bado walionekana kucheza kwa kushambulia muda wote wa mchezo.

Yusuph atawasaidia sana katika mchezo dhidi ya Simba, anachotakiwa kufanya ni kutokuwa na ukomo wa kufanya vizuri, na kama ataendelea kucheza kwa umakini uleule uliomfikisha hapo alipo anaweza kufanya kitu kinachoweza kumng’arisha zaidi. Yusuph anapaswa kuongeza bidii zaidi na hilo litasaidia kuifunga timu yake ya zamani ambayo alikataa kujisajili nayo msimu huu.

Kagera wamefanikiwa kufunga magoli 26 na kuruhusu magoli 21. Si wastani mzuri sana katika kuzuia lakini bado wanaweza kumtegemea kipa mzoefu Juma Kaseja na safu ya walinzi wazoefu kama Mohamed Fakhi, Anthony Matogolo na George Kavila ili kuhakikisha Simba wanaangusha pointi.

LAUDIT MAVUGO, IBRAHIM AJIB

Inaonekana kocha wa Simba, Joseph Omog amekwisha pata safu yake ya mashambulizi. Katika michezo ya karibuni amekuwa akiwapanga washambuliaji Mrundi, Laudit Mavugo na kijana Ibrahim Ajib. Wawili hao wamefanikiwa kufunga magoli kumi kati ya 40 ambayo timu yao imefanikiwa kufunga hadi sasa katika ligi.

Ili Shiza Kichuya aanze ni lazima Juma Ndanda Liuzio aanzie benchi. Wakati Fulani mwanzoni mwa michezo ya mzunguko wa pili Omog alikuwa akiwapanga washambuliaji wake watatu-Liuzio, Mavugo na Ajib lakini hakukuwa na matokeo mazuri upande wao. Timu ilionekana kushindwa kufunga magoli na hata kukosa ‘balansi’ katika eneo la kiungo.

Lakini baada ya kuwarudisha kikosi cha kwanza Kichuya na Said Ndemla angalau unaweza kuona uhai katika safu ya ufungaji ndiyo maana hata yule ‘aliyekuwa hafungi-Mavugo’ ameanza kufanya hivyo kwa sababu amekuwa akipasiwa pasi nyingi anazozitaka.

BEKI YA SIMBA

Pamoja na mabadiliko yote hayo bado hakuna kazi rahisi dhidi ya Kagera na licha ya kuruhusu magoli kumi bado wanaweza kujikuta wakiadhibiwa na Kagera ambao pia wana kikosi kizuri na kocha bora nchini.

Kumkosa Method Mwanjale katika michezo ya karibuni kulionekana kuathiri uwezo wa beki ya Simba lakini sasa amerejea Mganda, Juuko Murishid ambaye atacheza sambamba na Abdi Banda katika safu ya ulinzi wa kati.

Wawili hao wanaweza kukutana na wakati mgumu mbele ya Yusuph, Ame, Themi, Mrwanda ambao wana kasi na uwezo wa kumiliki mpira. Ili kupata kikosi kilichobalansi nguvu, ufundi na mbinu ingekuwa vizuri kwa kocha Mecky kutumia mfumo wa 4-3-3 ambao utawaruhusu kushambulia zaidi.

Kwa aina ya walinzi wa pembeni wa Simba (Besala Bokungu-beki namba mbili na Mohamed Hussein ‘Zimbwe Jr-beki ya kushoto) Kagera haitakuwa na wakati mzuri wakitumia mfumo wa 4-4-2 kwa maana hawana wing walio fiti ambao watawafanya Bokungu na Zimbwe Jr kutoshambulia mara kwa mara.

Ili kuiweka hatarini beki ya Simba, Mecky angewapa nafasi ya kuanza mchezo Mrwanda, Yusuph na Themi  kama wachezaji hao wapo fit. Kucheza kwao watatu kutawafanya walinzi wa Simba kutoshambulia sana na hilo litaisaidia Kagera ambao hawana-cha kupoteza hadi sasa.

MUZAMIRU, NDEMLA, KOTEI, KICHUYA

Omog anaweza kuwaanzisha viungo hawa wane katika mfumo wa 4-4-2 ambao umekuwa ukimpatia magoli. Ili kuuvuruga mfumo huu Mecky atahitasji wachezaji wake kumiliki sana mpira na kupitia katikati ya uwanja ambako si rahisi ila ni salama zaidi kwao kwa sababu Simba inategemea kasi ya Zimbwe Jr kupeleka mashambulizi wakipitia upande wao wa kushoto na Shiza Kichuya katika upande wa kulia.

Naamini uwepo wa viungo watatu katikati ya uwanja upande wa Kagera utamfanya Ndemla kutopiga pasi zake za hatari mara kwa mara na watapunguza nafasi ya Muzamiru kusogea zaidi hadi katika eneo lao la hatari na kuwatengenezea nafasi washambuliaji wake au kufunga yeye mwenyewe.

Simba wana viungo wazuri katika makaratasi lakini hilo si jambo litakalowafanya watawale mchezo. Walisumbuliwa sana katikati ya uwanja na timu ya daraja la chini Madini FC katika robo fainali ya FA Cup, hivyo Kagera wanaweza kutumia nafasi ya kucheza nyumbani na uzoefu wa wachezaji wake kushinda mechi hii.

Takwimu za Kagera Sugar vs Simba katika mechi saba zililizopita za ligi kuu Tanzania bara

02/04/2017 Kagera Sugar ?? Simba

15/10/2016 Simba 2-0 Kagera Sugar

07/02/2016 Kagera Sugar 0-1 Simba

20/09/2015 Simba 3-1 Kagera Sugar

06/04/2015 Kagera Sugar 1-2 Simba

26/12/2014 Simba 0-1 Kagera Sugar

05/04/2014 Kagera Sugar 1-1 Simba

31/10/2013 Simba 1-1 Kagera Sugar

Takwimu za Kagera na Simba katika msimu huu 2016/17

Simba mechi 24 – Kagera mechi 24

Ushindi: Kagera Sugar 12 – Simba 17

Sare: Kagera Sugar 6 – Simba 4

Walizopoteza: Kagera Sugar 6 – Simba 3

Magoli ya kufunga: Kagera Sugar 26 – Simba 40

Magoli ya kufungwa: Kagera Sugar 21 – Simba 10

Mechi bila kuruhusu goli: 14 – Simba 16

Points: Kagera Sugar 42 – Simba 55

Nafasi: Kagera Sugar 4 – Simba 1

Jicho la 3: Jerry Murro aliipeleka ‘Yanga moja’ uwanjani, Manara anawagawa Simba kila mechi

$
0
0

Na Baraka Mbolembole

“Uwezo wa Kamusoko ni sawa na viungo watatu wa Simba…” ni kauli iliyoendana na ukweli, na mtamkaji (Jery Muro) alimaanisha kile alichokiona Februari 2016 wakati kiungo huyo raia wa Zimbabwe, Thabani Kamusoko alipowavuruga Simba SC na kuisaidia timu yake ya Yanga SC kushinda 2-0 dhidi ya mahasimu wao hao na kujikita kileleni mwa msimamo wa ligi kuu Tanzania Bara msimu uliopita. Alikuwa sahihi asilimia 100.

“Baada ya Diamond na Ally Kiba, Ibrahim Ajib ndiye anayefuata kwa utoaji wa burudani nchini…,” ni maneno ya mkuu wa kitengo cha habari klabuni Simba, Haji Manara mara baada ya kumalizika kwa mchezo wa kimataifa wa kirafiki kati ya Tanzania Bara na Burundi siku ya Jumanne iliyopita. Alikuwa sahihi asilimia 0.

Kwanini nimenukuu kauli hizi? Kuzaliwa katika familia ya soka kuna faida na hasara zake. Na wakati mwingine mtu alinayetokea mahala kusiko na historia ya kimpira anaweza kukupatia faida kubwa zaidi kuliko yule anayetokea familia ya soka.

Kuanzia wakati wa Louis Sendeu na Baraka Kizuguto, Yanga imefanikiwa kupata watu sahihi katika kitengo cha habari, lakini misimu miwili ya Jery Muro kama Ofisa habari wa klabu hiyo, klabu imejengeka kama timu. Jery japokuwa alibezwa sana na kuambiwa hajui chochote kuhusu soka alitumia-taaluma yake, ushawishi wake na kipaji chake cha uzungumzaji kuifanya Yanga kuwa ‘timu moja.’

Wakati huu akiwa anatumikia adhabu ya kutojihusisha na soka kwa muda wa mwaka mmoja, naiona Yanga ikikosa huduma yake. Mwenyeji huyo wa Kilimanjaro aliwafanya wapenzi na hata wale wasio wafuatiliaji wa soka kutazama TV/kutegea sikio – radio zao na kumsikiliza kila anaposikika ama katika Tv wakati anapofanya mahojiano na wanahabarii. Hata wana-habari walipenda kufanya mahojiano na Jery
kutokana na kutoa maneno yaliyoleta ‘mshawashwa’ kwa mashabiki wa soka.

Alipokuwa akizungumza kuhusu kikosi cha timu yake, Jerry alizungumza kishabiki sana, lakini maneno yake mengi yalijaa hamasa-akiwahamasisha mashabiki, wanachama, wachezaji, benchi la ufundi na uongozi. Alirusha ‘madongo’ mazito kwa wapinzani wao na bila kujali Yanga ilikuwa ikiienda kucheza na timu gani yeye alipendelea kuzungumzia ‘uelekeo’ wa mchezo husika.

Hakuacha ‘kuikejeli’ Simba, ila alifanya dhihaka kwa mahasimu wao hao baada ya kuchunguza madhaifu yao. Aliwakejeli kwa kushindwa ‘kupanda ndege’ kwa misimu minne mfululizo-akimaanisha kushindwa kuiwakilisha Tanzania katika michuano yoyote ya Caf baada ya kushindwa kufanikiwa katika michuano ya ndani.

Wakati aliposimama katika taaluma yake,Jerry alikuwa ‘mtu smart sana’ na alizungumza kiuweledi-mfano wakati ule ilipotangazwa kufukuzwa kwa kiungo Mnyarwanda, Haruna Niyonzima ksha kurudishwa kwake Jerry alisimama kama mkuu wa kitengo cha kuwajuza habari wana-Yanga na jamii kwa ujumla kuhusu kila kilichokuwa kikifanywa na uongozi.

Aliikingia Yanga kifua tena kwa hoja zenye mashiko kila TFF ilipoijia juu klabu hiyo. Muro alifungiwa mwaka mmoja na TFF kwa sababu tu alitetea kitendo cha klabu yake kuingiza watazamaji 40,000 bila malipo katika pambano la Confederation Cup June, 2016 kati ya Yanga v TP Mazembe.

Kwanini Jerry ni pengo kwa Yanga hivi sasa? Ni pengo kwa maana Yanga inakwenda kucheza michezo yake hivi sasa huku shabiki, mwanachama, mchezaji, kocha na kiongozi akiwa na mtazamo wake kuhusu uwezo wa timu yao.

Nakumbuka mara baada ya Yanga kuchapwa na Coastal 2-0, kisha kulazimisha sare ‘tata’ dakika za mwisho vs Tanzania Prisons, na hata pale walipokuwa nyuma kwa alama zaidi ya 7 dhidi ya Simba msimu uliopita lakini bado Yanga hawakupoteza umoja, hamasa, matumaini na uaminifu kwa kikosi chao kutokana na maneno ya kutia moyo kikosi chao.

Wakati wa usemaji wa Murro klabuni Yanga kuanzia mashabiki, wanachama, wachezaji, benchi la ufundi na viongozi wote walikuwa wakienda kuitazama timu yao wakiwa katika lugha moja “tutashinda.” Na mara nyingi walifanikiwa, na walikuwa wamoja na tumaini moja kutokana na hamasa ambazo zililetwa na Muro.

HAJI MANARA

Historia ya soka la Tanzania inamtaja Sunday Manara kama mchezaji wa kwanza wa Tanzania kucheza soka barani Ulaya, kwa wale waliopata kumuona Sunday akicheza wanamtaja kama mchezaji bora zaidi kuwahi kutokea Tanzania na alipewa jina la ‘Computer’ hata kabla hazijaanza kuingia nchini-sijui kwa maana nimasimulizi tuliyoyakuta.

Sunday ndiye baba mzazi wa Haji Manara ambaye sasa ni msemaji wa klabu ya Simba tangu Julai 2014. Haji alichukua nafasi ya Asha Muhaji ambaye alikaimu kwa muda nafasi iliyokuwa imeachwa na Ezekiel Kamwaga. Cliford Ndimbo ndiye msemaji wa kwanza wa klabu hiyo na hadi sasa Haji ni mtu wa nne kushika wadhifa huo.

Tofauti na Ndimbo, Kamwaga, Asha Muhaji, huyu Manara  ni mtu anayetoka familia ya mpira zaidi na iliyopata mafanikio makubwa, nasikia naye alipata kucheza soka katika wakati wake. Lakini mbona sioni mchango wake kwa klabu tofauti na ule wa Muro, Ndimbo, Kamwaga, Asha ambao hawajatoka katika ‘familia staa za soka?’

Niwe mkweli, sijawahi kushabikia maneno yake ya nje ya uwanja, hamasa zake na uwezo wa kuiunganisha Simba kuwa timu moja-kwa maana kuanzia kwa mashabiki, wanachama, wachezaji, benchi la ufundi na uongozi wote wanakuwa katika ‘mwelekeo mmoja.’

Nadhani hata baadhi ya wakereketwa wa klabu ya Simba HAWAPENDEZWI NA UTENDAJI KAZI WA Manara kwa maana ya kutoa taarifa zenye mwelekeo sahihi wa mchezo unaohusu timu yao. Manara amekuwa maarufu kwa kutengeneza picha za watu na kuwafananisha na baadhi ya wachezaji wa Yanga kuliko kufuatilia mapungufu yaliyopo katika timu nyingine.

Huwezi kuwa na ‘cha-kuwabeza’ Yanga hivi sasa kwa maana wapo katika mwelekeo sahihi kwa msimu wa nne sasa. Kuisema vibaya ni sawa na ‘mtu avuae nguo na kushindwa kuchutuma kwa maana atajitukanisha mwenyewe kwa kwenda uchimbele za watu.’

Yanga wapo katika wakati mgumu hivi sasa kutokana na kumkosa Muro, timu kuandamwa na majeruhi, huku hamasa na viwango vya baadhi ya wachezaji wao vikiwa vimeshuka. Lakini kama timu iliyokuwa kwenye ubora inajitahidi kupambana kumaliza ligi  katika mwelekeo  mwingine lakini kwa nia ileile ya kushinda ubingwa wa watatu mfululizo.

Huu ulikuwa wakati sahihi wa Manara kujaribu kuwashawishi wana-Simba na kuwahamasisha katika ukweli ili wawe na tumaini moja. Kuwashutumu hovyo waamuzi, kuzungumza maneno yasiyo na ‘kichwa/miguu wala mwelekeo wa mechi’ ni baadhi ya mambo ambayo yanashindwa kutengeneza umoja wa klabu na Manara hawezi kukwepa kuwa kinara wa hili.

‘Kuiga si ujinga’ hasa pale unapoiga kizuri kinachoweza kukujenga, Haji amuige Muro ambaye aliwapa jeuri wana-Yanga na Yanga ilimpa jeuri kutokana na meneno ya hamasa yaliyokuwa yakisambnazwa na Muro.

Simba bado wana safari ndefu kufikia kushinda ubingwa wa kwanza wa VPL tangu msimu wa 2011/12 na kwa kuwa haina mwendelezo mzuri katika kupata ushindi hasa michezo ya mwisho wa msimu, Haji anapaswa kuhamasisha timu yake na si kutoa kejeli ambazo haziendani na Yanga licha ya kwamba ni ‘Watani.’

Muro aliipigania Yanga ili mechi zake zisogezwe mbele na TFF kutokana na ratiba ya Caf, licha ya kubezwa kuwa si mtu wa mpira lakini mawazo yake yaliendana na hali halisi. Manara yeye amekuwa akiishinikiza TTF kusimamisha mechi zao wakati timu inashinda mfululizo kwa sababu tu walingane michezo na Yanga na Azam FC.

Kwa mtu wa mpira hii ni aibu kwa maana anaonekana hajui kuwa timu inaposhinda mfululizo hujiamini zaidi na wapinzani wao kujenga hofu. Manara amekuwa mstari wa mbele kushinikiza TFF ipange waamuzi sahihi katika mechi zao kama vile timu nyingine zina waamuzi wao!

Manara ni tatizo Simba na Jerry ni pengo kubwa katika klabu ya Yanga japokuwa wanajitahidi kuliziba. Jerry Muro aliipeleka ‘Yangamoja’ uwanjani, Manara anawagawa Simba kila mechi kwa kuwaaminisha mambo yasiyokuwepo, yasiyotarajiwa na yasiyo na mwelekeo wa mechi husika. Kuna wakati anapaswa kuzungumza kiuweledi.

Jerry aliwafanya Yanga kuwa wamoja lakini ukichunguza kauli za Manara, mfano Januari mwaka huu aliposema Emmanuel Okwi atacheza vs Yanga Februari 25 ni kielelezo tosha kuwa licha ya kutoka familia ya soka, Haji si mtu mwenye uwezo wa kuutazama mpira na kung’amua mapungufu ya timu yake na wapinzani. Amuige Jerry Murro.

Jery aliwaaminisha Yanga na mchezaji husika kuwa ‘Kamusoko mmoja ni sawa na viungo watatu wa Simba kiuwezo’ lakini Haji anawaaminisha Simba kuwa Ajib ndiye mburudishaji bora zaidi nchini baada ya wanamuziki Diamod Platnum na Ally Kiba!!!

Mbaraka Yusuph, Singano, Mkude na nyota hawa watano wataipaisha zaidi Yanga…

$
0
0

Na Baraka Mbolembole

KABLA ya kuanza ‘kutupa macho’ sehemu nyingine, kocha George Lwandamina anapaswa kuangalia ni wachezaji gani wanapaswa kusajiliwa tena na Yanga SC miongoni mwa wale waliopo kikosini hivi sasa.

Kwa mtazamo wangu, Yanga inahitaji kufanya usajili wa beki namba tatu, viungo wawili wa mashambulizi, mmoja wa ulinzi, viungo wawili wa pembeni-kulia na kushoto, na washambuliaji wawili watakaokuwa na uwezo wa kucheza eneo lote la mbele kwa usahihi.

Lakini kabla ya kusaini wachezaji wapya ningependa kuona kocha Lwandamina akiwasaini tena mlinzi wa kati, nahodha Nadir Haroub ambaye ameendelea kuonesha uwezo wake wa kuzuia, kuipanga safu ya ulinzi na kuongoza mchezo.

Licha ya umri wake wa miaka 33, Nadir ni mchezaji ambaye anatengeneza umoja wa ndani na nje ya uwanja kwa timu yake na kiwango chake katika kila mchezo anaopata nafasi kimekuwa juu. Anajituma muda wote na hajaonesha kuridhishwa na mafanikio na aliyopata klabuni hapo tangu alipojiunga 2006 akitokea Zanzibar.

Kuna wachezaji wengine ambao mikataba yao inamalizika mara baada ya msimu huu kumalizika.
Naamini kocha huyo raia wa Zambia atakuwa anafuatilia kwa umakini viwango vya Mwinyi Haji, Oscar Joshua, Mtogo Vicent Bossou, Said Juma Makapu, Mnyarwanda, Haruna Niyonzima, Mzimbabwe, Thaban Kamusoko, Matteo Anthony.

Pia , Geoffrey Mwashuiya, Deus Kaseke, Mzimbabwe, Donald Ngoma, Mrundi, Amis Tambwe, Malimi Busungu ambao mikataba yao inakaribia kumalizika na ni yeye atakayeamua ni wachezaji gani wasajiliwe tena na wapi waachwe.

GADIEL MICHAEL

Yanga haina tabia ya kusaini wachezaji kutoka Azam FC lakini wanaweza kuimarisha beki yao kwa kumsaini mlinzi huyu wa kushoto wa Azam FC.

Gadiel anauwezo wa kupeleka mashambulizi mbele, pia ni mwepesi kurudi katika nafasi yake. Hapotezi hovyo mipira na amekuwa na umakini mkubwa kila anapokuwa uwanjani. Huyu ni mchezaji ambaye ataimarisha safu ya beki wa kushoto ambayo sasa inashikiliwa na Mwinyi  na Oscar Joshua. Lwandamina anapaswa kumfuatilia kijana huyu.

JONAS MKUDE

Bado hajasaini mkataba mpya katika klabu yake ya Simba SC na kufikia mwisho wa msimu atakuwa huru kujiunga na timu yoyote atakayokubaliana nayo. Kuwa na Justine Zulu na Makapu ni vizuri lakini Mkude ataongeza nguvu, ufundi na uwezo wa idara ya kiungo kupanga mashambulizi ya uhakika wakitokea katikati ya uwanja.

Naamini Lwandamina ameshamwona mara kadhaa nahodha huyu wa Simba, kama anapatikana kiurahisi Yanga inapaswa kumsaini katika usajili ujao ili kuimarisha kiungo chao chenye mapungufu. Mkude ameshapevuka kimchezo na sasa yuko katika kiwango kizuri. Ataimarisha sehemu ya kiungo mlinzi na Yanga inamuhitaji mchezaji mkomavu kama nahodha huyu wa Simba.

RAFAEL DAUDI, KENNY ALLY  

Wanacheza vizuri katika kiungo cha timu ya Mbeya City FC. Wachezaji hao wawili wanaweza kuongeza ubunifu katika timu ya Lwandamina endapo watasajiliwa. Wote wawili wana uwezo wa kucheza
nafasi zote katika eneo la kiungo na kufanya vizuri.

Niyonzima, Kamusoko ni viungo wazuri ila wanapokosekana timu imekuwa ikiyumba sana eneo la kiungo. Kuwasaini nahodha wa City, Kenny na Alpha si tu kutaongeza viungozi katika timu bali uimara na ubora. Lwandamina anaweza kuwatazama vizuri wakati atakapokutana na kikosi cha City katika mchezo wa marejeano mwezi huu.

HASSAN KABUNDA

Ni kiungo mzuri wa pembeni na amekuwa na misimu miwili ya kuvutia katika kikosi cha Mwadui FC. Licha ya uwepo wa Juma Mahadhi na Msuva katika wing ya kulia, Kabunda ni mchezaji ambaye anaweza kuifanya Yanga kutengeneza nafasi nyingi zaidi za kufunga kutokana na uwezo wake wa kupiga pasi
sahihi katika wakati mwafaka.

RAMADHANI SINGANO

Katika michezo ya karibuni kiungo huyu mshambulizi wa kushoto wa klabu ya Azam FC amekuwa katika kiwango bora sana. Atakuwa huru mara baada ya kumalizika kwa msimu huu. Lwandamina ameshamuona Singano na ukitazama kikosi chake utaona kabisa kuwa Yanga inamuhitaji mchezaji kama Singano ili kuleta balansi ya mashambulizi kutoka kila upande.

Mwashuiya ni mchezaji mzuri lakini bado Yanga inamuhitaji kiungo aliyepevuka zaidi katika wing yao ya
kushoto na Singano ndiye mtu sahihi kwa wakati huu.

IBRAHIM AJIB

Anamaliza mkataba wake klabuni Simba mara baada ya msimu kumalizika. Yanga hawapaswi kujivunga zaidi ya kujitosa kuwania saini ya mshambulizi huyo kijana mwenye uwezo wa kufunga na kutengeneza nafasi nyingi za kufunga magoli. Ajib atakuwa msaada mkubwa kwa Tambwe, Ngoma na Mzambia, Obrey Chirwa kama Lwandamina atapendekeza watatu hao wote kuendelea kuichezea Yanga msimu ujao.

MBARAKA YUSUPH

Si kutokana na magoli yake matatu katika michezo mitatu vs Yanga na Simba, bali uwezo wake wa kufunga, kumiliki mpira, kutengeneza nafasi na target yake anaposhuti mpira kuelekea golini. Yusuph ameshafunga magoli 11 katika VPL msimu huu. Huyu anaweza kuibeba Yanga na anakidhi vigezo vya kuvaa jezi ya timu hiyo.

Naamini wachezaji hawa nane niliowataja wanaweza kuifanya Yanga kuwa moto zaidi msimu ujao na wanapatikana kiurahisi kutokana na kwamba mikataba yao inafikia tamati mwishoni mwa msimu
huu.

Jicho la 3: Kabla ya kwenda ‘uwanja wa moto’, Lwandamina aitumie kauli yake Taifa kumaliza ‘uteja’ wa Yanga kwa Waarabu

$
0
0

Na Baraka Mbolembole

WAKATI ‘anachukua kazi’ iliyokuwa wazi baada ya Mholland, Hans van der Pluijm kubadilishiwa majukumu klabuni Yanga SC mwezi Disemba, 2016 kocha Mzambia, George Lwandamina alitamba ujio wake klabuni hapo ni sawa na ‘kufikia ukomo’ wa Yanga kunyanyaswa na timu za Kiarabu katika soka la Afrika.

Katika misimu kumi ya mwisho kuelekea mchezo wa ‘play oof’ kuwania kufuzu kwa hatua ya makundi Confederation Cup 2017, Yanga imetolewa katika michuano na timu nyingi za Kiarabu. Walitolewa na Waarabu wa Sudan, El Merreikh mwaka 2007 katika ‘play off’ ya Confederation Cup ambako waliangukia baada ya kuondolewa hatua ya 16 bora katika Champions League na Esperance ya Tunisia.

Walitolewa na Al Akdar ya Libya katika Confederation Cup mwaka 2008, wakatolewa na ASl Ahly ya Misri  katika ligi ya mabingwa mwaka 2009, 2014, na 2016, pia timu kama Zamalek ya Misri, Etoele du Saleh ya Tunisia pia zimewahi kuitoa Yanga katika michuano ya Caf miaka ya karibuni. Pia walishindwa kutamba mbele ya MO Bejaia katika mchezo wa ugenini msimu uliopita katika hatua ya makundi-Confederation Cup.

Lwandamina kama kocha alijipa mwenyewe ‘alama ya mapinduzi’ kufuatia matokeo yake mazuri katika Caf Champions League 2016. Wakati akiwa kocha wa Zesco United ya Zambia msimu uliopita kocha huyo alifanikiwa sana, pia alivuka kundi ambalo alipangwa na timu za Kiarabu (Zamalek ya Misri, Whydad Casablanca)

Lwandamina na Zesco walifanikiwa kufuzu nusu faioali kama kinara wa kundi ambalo kwa timu iliyokuwa ikicheza michuano yake ya kwanza katika hiyo ilionekana isingekuwa na ubavu wa kuvuka mbele ya mabingwa mara tano kihistoria-Zamalek na timu zinazofanya vizuri katika miaka kumi ya sasa katika michuano ya Caf-Wydad.

YANGA v MC ALGER ( play-off CCC 2017)

Ni wakati sasa wa Lwandamina kuitumia kauli yake mwenyewe ili kuleta mapinduzi klabuni Yanga. Hans ni kati ya makocha waliofanikiwa sana katika klabu ya Yanga-rekodi zake zinazungumza zenyewe.

Ndani ya miezi isiyopungua 30 aliisaidia Yanga kushinda mataji mawili ya ligi kuu ( 2014/15, 2015/16,) taji moja la Ngao ya Jamii, lingine moja la FA Cup ( 2015/16,) aliipeleka Yanga hadi hatua 16 bora katika ligi ya mabingwa Afrika 2014, pia aliifikisha timu hiyo katika hatua ya 16 bora ya Confederation Cup 2015.

Hans aliisimamia tena Yanga na  akaifikisha hatua ya 16 katika michuano hiyo mikubwa zaidi barani Afrika upande wa klabu-2016, na baada ya kuondolewa katika ligi ya mabingwa raia huyo wa Holland aliangukia katika michuano ya Confederation ambako aliwaondoa Waangola-Esperanca katika ‘play off’ na kuipeleka timu hiyo kwa mara ya kwanza hatua ya makundi.

Hans hakupata tu mafanikio ya kushinda mataji, hadi anapewa nafasi ya Ukurugenzi wa klabu kutokana na ujio wa Lwandamina, Mholland aliifanya Yanga kuwa timu imara kufungukia huku ikicheza mchezo mzuri wa kushambulia na kufunga magoli ya kutosha.

Swali la kujiuliza ambalo pengine litakuwa kichwani mwa Lwandamina, je, anaweza kufanya vyema vs MC Alger na kuwaondoa Waarabu hao akiwa na rundo la majeruhi kikosini mwake? Tayari imethibitika kuwa Mzambia, Justine Zulu ambaye alifunga goli la kwanza kati ya 7 yaliyofungwa na Yanga katika michezo minne ya Caf msimu huu hatokuwepo kutokana na majeraha aliyopata katika mchezo wa ligi kuu vs Azam FC siku ya Jumamosi iliyopita, Mzimbabwe, Thaban Kamusoko pia hatatumika katika mchezo wa Jumamosi hii. Hawa ni wachezaji wawili muhimu wa idara ya kiungo ambao Lwandamina atawakosa katika mchezo huo dhidi ya MC Alger. Washambuliaji, Mrundi, Amis Tambwe na Mzimbabwe, Donald Ngoma wameanza mazoezi wiki hii baada ya kusumbuliwa na majeraha katika wiki za karibuni.

Wakiwa ‘fiti’ kwa mchezo, Ngoma na Tambwe itamsaidia Lwandamina. Lakini ili kuwalinda na kuwafanya wawe na makali washambuliaji hao wanapaswa kucheza karibu karibu na mfumo mzuri utakuwa ni ule wa 4-4-2.

Msuva wing ya kulia, Obrey Chirwa wing ya kushoto, Mnyarwanda, Haruna Niyonzima na Said Juma Makapu katika idara ya viungo wa kati.

MC ALGER IMEFUNGA MAGOLI 6 KATI YA NANE IKICHEZA ‘UWANJA WA MOTO’

Uwanja ulijengwa mwaka 1935 kama uwanja wa nyumbani wa “Chama cha Mtakatifu Eugene” uliojulikana kama jumuiya ya mtakatifu Eugene. Baada ya Uhuru wa Algeria mwaka 1962,uwanja wa mtakatifu Eugene uliitwa ‘Bologhine’ jina jipya la mji huo.

Eneo la juu la jukwaa la uwanja huo liliharibika vibaya sana mnamo mwaka1980 katika ‘tetemeko la asnam’ na liliendelea kubaki wazi kwa watazamaji na baadae taratibu shughuli zikasimamishwa mnamo mwaka 2003.

Mwaka 1998 uwanja ulibadilishwa jina na kuitwa’uwanja wa moto wa Bologhine wa Omary Hamad’ kiongoz wa zamani wa klabu  hiyo na mwanamapinduzi wa kwanza aliyehukumiwa kunyongwa katika harakati za Mapinduzi ya ñchi hiyo ambaye aliuliwa vibaya pamoja na watoto wake wawili katika Bouzareah ( Algeris) na kundi la magaidi mwaka 1995.

MC Alger imefanikiwa kufunga katika kila mchezo wa Confederation Cup msimu huu. Walifungwa 2-1 katika mchezo wa awali ugenini dhidi ya Wanigeria Becham United, wakashinda 4-1 katika uwanja wao wa Omari Ahmad.

Raundi iliyopita walianza nyumbani kwa ushindi wa 2-0 dhidi ya FC Renaissance ya DR Congo, wakapoteza 2-1 katika mchezo wa marejeano Kinshasa. Hawa Waarabu ni wanaonekana kuwa hatari sana wanapocheza nyumbani kwa maana katika michezo yao miwili wamefanikiwa kufunga magoli 6, huku wakionekana kufanya kila linalowezekana kufunga walau goli moja katika mechi ya ugenini.

Kati ya magoli yao nane waliyofunga katila michezo yao minne, ni magoli mawili tu wamefunga ndani ya dakika 45 za mwanzo.

Hii inamaanisha timu hii ni hatari kuanzia dakika ya 50. Mfano, katika mchezo wao dhidi ya Becham, hadi mapumziko matokeo yalikuwa 0-0. Becham wakapata goli la kuongoza dakika ya pili baada ya kuanza kwa kipindi cha pili, lakini Mohamed Seguer akasawazisha dakika ya 64.

Walikuja kufungwa goli la pili dakika ya 75 na wakalala 2-1. Katika mchezo wa marejeano MC Alger wakiwa nyumbani, Seguer akafunga dakika ya pili tu, kisha Abdurahmane Hadoud akafunga la pili dakika ya 39. Hadoud akafunga goli lingine dakika ya 84 kisha Zakaria Mansour akafunga la nne dakika ya 89.

Katika mchezo huu MC Alger iliruhusu goli dakika ya 60 wakati wakiongoza 2-0. Mwisho wakashinda 4-1. Katika mchezo wao wa kwanza dhidi ya Renaissance, wakicheza nyumbani hadi mapumziko matokeo yalikuwa 0-0.

MC Alger walifunga magoli yao kupitia kwa Ahmed Aoued dakika ya 57 na Bouhenna dakika ya 81, wakashinda 2-0. Mechi ya marejeano Kinshasa, Mehdi Kacem aliwafungia MC Alger goli la kuongoza dakika ya 50, likiwa goli la kusawazisha kufuatia kufungwa mapema dakika ya nane. Waarabu hao wakaruhusu goli la pili dakika ya 80 na kupoteza 2-1.

WANACHOPASWA KUEPUKA YANGA…

Kwa maana hii kikosi cha Lwandamina kinatakiwa kucheza kwa umakini mkubwa muda wote wa mchezo kwa maana MC Alger wamefunga magoli yao 6 kati ya dakika katika michuano hii kuanzia dakika ya 50 na kuendelea.

Ni muhimu wachezaji wa Yanga kubadilisha rekodi yao isiyovutia wanapocheza katika uwanja wa Taifa. Watambue katika soka la Afrika timu nyingi zilizofanikiwa ni zile zinazofanya vizuri katika michezo yao ya nyumbani.

Katika michezo miwili ya Caf Champions League, Yanga wamefunga magoli mawili tu na kuruhusu magoli mawili. Wamefunga magoli matano katika michezo miwili ya ugenini dhidi ya Wacomoro, Ngaya Club na hawakufunga vs Zanaco FC ya Zambia.

Kitu kizuri ni kwamba, wakati MC Alger ikifunga magoli 6 kati ya nane kuanzia dakika ya 50, upande wa Yanga wamefanikiwa kufunga magoli manne ndani ya dakika 6 za mwisho kabla ya kumalizika kwa kipindi cha kwanza.

Katika ushindi wa 5-1 dhidi ya Ngaya ugenini, Zulu alifunga dakika ya 38, Msuva akafunga dakika ya 45. Katika mchezo wa marejeano Hajji Mwinyi aliisawazishia Yanga dakika ya 43 baada ya kutangulia kufungwa dakika ya 20.

Katika mchezo wa kwanza dhidi ya Zanaco uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, Msuva aliifungia Yanga dakika za 39, baadae dakika ya 78 wageni wakasawazisha na mechi ikamalizika kwa sare ya 1-1.

Lwandamina bado ana nafasi ya kuifundisha Yanga lakini ni lazima athibitishe uwezo wake kwa kuifanya timu isonge mbele zaidi ya pale alipoifikisha Hans. Ni wakati wake KAMA KOCHA kuitumia ‘kauli yake’ kumaliza ‘uteja’ wa Yanga vs Waarab.

NAFASI YA KILA TIMU KATIKA LIGI

Haiwezi kuwa kipimo sahihi cha kusema ipi timu bora zaidi. Katika soka la ndani ya Tanzania, Yanga ndio ‘wafalme’ na kuelekea mchezo wa Jumamosi hii katika Cofederation Cup mabingwa hao mara 25 wa kihistoria katika ligi kuu Bara wanasaka taji la 3 mfululizo huku wakiongoza ligi ya VPL wakiwa na alama 56 baada ya kucheza michezo 25.

Kikosi cha Lwandamina kimefunga magoli 50 na kuruhusu 11 tu na hiyo ni dalili kuwa wapinzani wao watakuwa wamewafuatilia vya kutosha. Yanga imeshinda michezo 17, imepoteza mitatu na kutoa sare game tano hivyo wanaingia uwanjani wakiwa bora zaidi ya wapinzani wao ambao wameachwa pointi 11 na Entete Setif wanaongoza ligi kuu Algeria wakiwa na alama 47.

Katika michezo yao 21 ya ligi, MC Alger wamefuoga magoli 23 na kuruhusu nyavu zao mara 17. Hawana wastani mzuri wa kufunga na hata katika kuzuia. Wamekusanya alama 36 wakiwa nafasi ya 3 katika msimamo baada ya kushinda mechi kumi, kupoteza tano na kutoa sare 6.

Huyu ndio Hassan Kabunda anayetamani kucheza na CR7

$
0
0

Na Zainabu Rajabu

JINA la Hassan Kabunda linaweza kuwa geni masikioni mwa watu, lakini wapo wanaomkumbuka beki wa zamani wa Tukuyu Stars, Yanga SC na timu ya taifa ya Tanzania Bara, Kakakuona, Salum Kabunda ‘Ninja’ au Msudan.

Beki huyo alijulikana kwa kucheza kibabe sana uwanjani mpaka ikafikia wakati washambuliaji kuanza kumuogopa.

Ninja au Msudan ndiye baba mzazi wa Hassan Kabunda anayeitumikia Mwadui FC ya Shinyanga.

Hassan Kabunda yeye ni mshambuliaji na si beki kama ilivyokuwa kwa baba yake, kijana huyu amekuwa katika kiwango kizuri na msaada mkubwa kwenye timu yake ya Mwadui FC hali iliyosababisha Kocha wa Taifa Stars, Salum Mayanga amjumuishe kwenye kikosi chake kilichocheza mechi mbili za kirafiki hivi karibuni.

Shaffihdauda.co.tz Ilipata  nafasi ya kuzungumza na kinda huyo aliyeibuliwa na michuano ya Copa Coca-Cola.

ALIPOANZIA KUCHEZA SOKA

Nilianza kucheza mpira wa makaratasi (chandimu) katika timu ya mtaani kwetu inaitwa Jabari na mpaka naanza masomo shule ya msingi nilikuwa naendelea kucheza soka.

Nilipomaliza shule nikachukuliwa na mtu mmoja anaitwa Aluko Simango ambapo alikuwa na kituo chake cha soka kinaitwa DUWC nikawa nacheza hapo na wakawa wananilea kama mtoto wao.

Nilikaa hapo kwa takribani miaka minne ambapo pia walikuwa wakinisomesha.

Baadaye nikafanikiwa kuchaguliwa kuiwakilisha timu ya Mkoa wa Temeke kwenye michuano ya Copa Coca Cola.

Baadaye nikaitumikia timu ya vijana ya  African Lyon chini ya miaka 20 na tukashiriki michuano ya Uhai Cup. Baada ya mwaka mmoja nikaenda Ashanti United kwenye kikosi cha vijana chini ya miaka 20 baadaye nikapandishwa timu ya wakubwa.

Nikiwa na Ashanti ya wakubwa, tulicheza Ligi Kuu msimu mmoja, kwa bahati mbaya tukashuka daraja. Nikiwa nashiriki Ligi Daraja la Kwanza, nikafanikiwa kukutana na Jamhuri Kihwelu ‘Julio’ akanichukua na kunipeleka katika kikosi chake cha Mwadui ambapo nipo mpaka sasa huu ni mwaka wa tatu.

Awali nilipofika Mwadui, Julio alikuwa ananipa nafasi lakini wachezaji wazoefu wengi walikuwa hawaniamini kitendo ambacho baadaye kilikuja kusababisha baadhi ya mechi niishie benchi.

Hali hiyo ilikuwa inaniumiza lakini nikawa najipa moyo kwamba siku moja nitafanikiwa tu kwani mara kadhaa Julio alikua ananiambia nisikate tamaa.

Nakumbuka kuna mechi moja tulikuwa tunacheza na Coastal Union, niliweza kufunga mabao mawili, kuanzia hapo nikaanza kuaminiwa mpaka leo nacheza kikosi cha kwanza.

NANI ALIMSHAWISHI KUINGIA KATIKA SOKA?

Hakuna watu wengine zaidi ya kaka zangu ambao nilikua nikiwaona wanacheza mpira wa makaratasi nafurahi sana.

ANAZUNGUMZIAJE KUITWA KATIKA KIKOSI CHA TAIFA STARS
Kwanza namshukuru Mungu kwa nafasi hiyo niliyoipata kwani naamini juhudi zangu pia zimesababisha hayo yote.
Nakumbuka Kocha Julio na wachezaji wenzangu kama Jabir Aziz ‘Stima’ walikuwa wananishauri mambo mengi sana huku wakisema nafasi ya kucheza popote ninayo hivyo nisibweteke na nifanye mazoezi kwa sana bila ya kusahau kujitunza.

UMEJIFUNZA NINI KUTOKA KWA SAMATTA NA FARID MUSSA?

Nimejifunza mambo mengi sana na kunipa hamu ya kujituma zaidi kwani nataka siku moja na mimi nikacheze Ulaya kama wao.

MCHEZAJI GANI ANAYEKUVUTIA WA KIBONGO NA WA NJE YA BONGO?

Kwa Bongo ni Mbwana Samatta napenda uchezaji wake lakini nje ya Bongo nampenda Cristiano Ronaldo ambaye ananivutia kiasi kwamba natamani siku moja nicheze naye timu moja.

KITU ASICHOKIPENDA

Sipendi kuona nimewekwa benchi halafu mchezaji yupo ndani anacheza vibaya halafu mwalimu  bado anamng’ang’ania wakati kuna uwezekano kabisa wa kumtoa na kumuingiza mwingine, kitu kama hicho kinanikera sana.

UNA MALENGO YA KUCHEZA SOKA LA KULIPWA NJE?
Ndiyo

NCHI GANI UNAPENDA KWENDA KUCHEZA?

Nchi ambayo napenda kwenda kuchezea  soka langu ni Spain, Italy, na Belgium anapochezea Mbwana Samatta.

NJE YA SOKA UNAPENDELEA KUFANYA NINI?

Nikiwa nje ya soka napendelea kukaa na marafiki zangu, ndungu zangu, na kutoka na kwenda beach.

MSANII GANI UNAEMKUBALI ?

Mwanamziki ninamkubali ni dada yangu Tammy ze baddest napenda kusikiliza Nyimbo zake na pia ana mashairi ya kuelemisha.

BEKI GANI UNAMKUBALI ?

Namkubali sana Juma Abdul, David Luhende, Shomari Kapombe, Mohammed Hussen “Zimbwe Jr”.

UNA SHABIKIA TIMU GANI HAPA TANZANIA?

Mimi ni shabiki wa Asanti United

NJE YA TANZANIA UNASHABIKIA TIMU GANI?

Zamani nilikuwa nashabikia Manchester United lakini nimehama kutoka na kuwa na matokeo mabaya lakini kwa sasa naishabikia Real Madrid.

UMEJIPANGA KUFUNGA MAGOLI MANGAPI KATIKA MSIMU HUU WA MWISHO WA LIGI KUU?

Katika msimu huu nimefanikiwa kufunga  mabao 6 ila kwa uwezo wa Mwenyenzi Mungu nimepanga nifikishe mabao 10 na nina amini kutoka na juhudi zangu na ushirikiano ninao upata kwa wachezaji wenzangu nitafanikisha.

UNAPENDA CHAKULA GANI?

Napendelea kula Wali na Maharage .

KATIKA KINYANGANYIO CHA MFUNGAJI BORA, WEWE KARATA YAKO UNAIWEKA KWA NANI KATIKA YA SAIMON MSUVA NA SHIZA RAMADHANI KICHUYA.

Siwezi kusema nampa nani kutokana na Kichuya kuwa na mabao 11 huku na Msuva  akiwa 12 pale lolote linaweza kutokea tuwaachie  wote wazidi kupambana.

JE USINGEKUWA MCHEZAJI UNGEKUWA UNAFANYA KAZI GANI?

Nisingekuwa mchezaji ningekuwa mchezaji wa pool table kwa kuwa nalijua sana ilifikia kipindi hadi nilikuwa nagombana na mama angu kwa kunikataza kucheza.

RAFIKI YAKO KIPENZI NDANI YA TIMU YA MWADUI NI NANI?

Rafiki yangu mkubwa katika timu ninayo chezea ni Mchezaji wa Zamani wa Yanga  Jerryson Tegete amekuwa kama mshauri mkubwa sana kwangu .

UMEOA

Sijao lakini nina mchumba wangu nampenda sana siwezi kumuweka wazi kwa sasa ila muda ukifika nitamuweka hadharani.


Kuna Messi Mmoja, Maradona Mmoja, na Dyabala Mmoja tu. Paulo Dyabala Na Ndoto Ya Baba Yake.

$
0
0

Kama ilivyokuwa kwa kila mtu nchini Italia, Paulo Dyabala aliathirika kwa kiasi kikubwa na balaa la Edoardo Di Carlo na Samuel Di Michelangelo, vijana wawili waliobaki yatima kutokana na maporomoko ya barafu maarufu kama Rigopiano yaliyotokea Januari 18 na kuchukua maisha ya watu 29.

Baada ya kusikia kuwa watu hao walikuwa mashabiki wa Juventus, Dyabala aliwapigia kwa njia ya video na kuwakaribisha Vinovo akiwa na imani kuwa atawaonyesha kuwa hawapo peke yao.

Stori zao hazikufanana nae lakini bado Dybala angeweza kufananisha hisia za hasara hiyo na upweke.

Akiwa na umri wa miaka 15, alimpoteza baba yake kutokana na saratani ya kongosho. Mdogo wa mwisho kati ya wavulana 3, ambaye ni Paulo hakushirikishwa na familia yake, akaachwa asijue lolote.

“Ili kunilinda hawakuniambia kila kitu”, aliweka wazi. “Nilikuwa nina imani atapata nafuu na kupona. Leo, ninamwota na ninaamka nikiwa mwenye machozi kila mara”.

Ukizingatia umuhimu aliokuwa nao baba yake na kifo chake, inaonyesha ni ajabu kwa namna ambayo Dyabala amefanikiwa kufika mbali hivi kwenye soka.

Hata hivyo, alikuwa ni Adolfo ambaye alikuwa ndiye msukumo kwenye kukomaa katika maisha ya soka ya mwanae. Wakati Paulo akienda kucheza soka katika klabu ya Newell Old Boys akiwa na miaka 8, baba yake hakuridhika na klabu hiyo. “Tutakaa nyumbani,” alimwambia mwanae.

Paulo hata hivyo alijiunga na Instituto de Cordoba and na ni baba yake aliyekuwa anamwendesha kwenda na kutoka mazoezini.

Baada ya Adolfo kufariki, Paulo hakuwa na namna zaidi ya kuondoka alikolelewa Laguna Larga na kwenda Cordoba, umbali wa saa moja kwa gari, na kuishi kwenye nyumba ya wageni ya klabu hiyo, hali iliyopelekea kupata jina la utani la ‘El pibe de la pensión’.

“Kilikuwa kipindi kigumu maishani mwangu, haikuwa rahisi,” alikiri Dybala huku akisema familia yake ilikuwa mbali sana.

“Nilikuwa najikuta nikijifungia bafuni na kulia sana. Lakini sikunyanyua mikono, sikufa moyyo.”

Ni kweli, Dyabala anasema kuwa kifo cha baba yake “kilimpa ngubu na kumjenga.” Hali iliyomkomaza na kumkuza.

Hili lilimfanya kuwa na malengo zaidi zaidi ya kipindi chochote akiamini atafanikiwa. “Baba yangu alikuwa na ndoto,” alielezea, “kuwa walau mmoja kati ya wanae aje kuwa mchezaji wa soka.

“Gustavo, ambaye ni mkubwa zaidi, hakufanikiwa lakini hata Mariano, ambaye kila mtu alisema alikuwa bora zaidi kuliko mimi lakini ambaye aliugua ugonjwa wakukumbuka nyumbani unaofahamika kama homesickness.

“Hivyo ilibidi nifanye hivyo ili kumtunza na kumpa heshima kwa kumbukumbu za baba yangu ambapo ningezifikia ndoto.”

Alifanya hivyo tu. Lakini miaka isiyozidi miwili baadae akiwa na umri wa miaka 17, Dybala  alikuwa mfungaji mdogo zaidi wa Cordoba  akivunja rekodi ya Mario Kempes.

Msimu uliofuata alifunga mabao 17 kwenye michezo 38 na ikamfanya apate jina linguine la utani, ‘La Joya’ (Kito), na akauzwa kwa kiasi cha Euro milioni 11.8 (€11.8) kwenda Parlemo.

Ilikuwa ni katika mji wa Sicily ambapo alikuja chini ya uangalizi wa Maurizio Zamparini. Wnaomfahamu Raisi wa zamani wa Palermo wanafahamu fika kuwa fikra zake inabidi zifikiriwe vyema, maneno yake yalibeba maana kubwa kama ilivyokuwa kwa mikataba aliyowapa makocha wake

Hivyo, pale ambapo Zamparini alipodai kuwa Dybala angekuwa mrithi wa Lionel Messi wakati akichomoza kwenye msimu wa 2014-15, wachache ambao hata walimtizama.

“Nilipomuuza kwenda Juventus kwa kiasi cha Euro milioni 32 (€32) ikiwemo na bonasi ya €8m, walilizungumzia hili kama jambo la ajabu,” Zamparini alikumbushia mapema mwaka huu.

“Sasa hivi wanasema Marotta ana akili za kipekee. Dybala ana thamani kiasi gani kwa sasa? Walau kiasi cha €100m; ni Messi mpya!”

Ni wazi wachezaji kama Gonzalo Higuain wamesema kuna ushabihiano: akili na mbinu za kukokota mpira, mgandamizo wa chini kutokana na kimo, aina ya kipekee ya kugusa mpira na mguu wa kushoto wa kipekee.

Lakini pia muhimu zaidi, Dybala anafanana na Messi katika kuamini kwa kiasi kikubwa kwenye uwezo wao.

Ilikuwa ni ajabu alipofika katika klabu ya Juventus hakuonyesha kushitushwa na mazingira mapya. Aliamini kuwa anastahili kuwepo kwenye moja ya vilabu vikubwa duniani.

Ni kweli, ikiwa Andrea Pirlo anaondoka katika msimu ule wa majira ya kiangazi, alichukua maamuzi ya kuwa anapiga mipira ya adhabu, akijaribu kufanana na Messi akiondolewa katika mchezo wa kwanza wa Argentina.

Hata hivyo kuendelea kufananishwa nap engine mchezaji bora wa muda wote ni msalaba mkubwa.

Gerard Deulofeu karibuni alikiri kuwa aliona ana mzigo mkubwa baada ya kupata nafasi ya kuingia kwenye kikosi cha kwanza cha  Barcelona mwaka 2011.

Dybala, hata hivyo yupo tofauti, hawazi thamani atakayonunuliwa nayo, na wala hafanyi mambo kwa sababu anataka kuwa Messi mpya.

“Mimi ni Dyabala, nataka kuwa Dyabala pekee ingawa natambua kumekuwapo ufananisho. Kutakuwa na Messi mmoja tu, kama ilivyokuwepo Maradona mmoja.”

Ni wazi kuwa jambo pekee ambalo linaweza kuwa linamsumbua Dyabala ni kumuenzi baba yake. “Magoli yote ninayofunga ni zawadi kwake, soka limenisaidia sana na nimekuwa mchezaji kwa nguvu zake zaidi ya nguvu zangu.”

“Alinifunisha kupigana na kutokukubali kushindwa, ndoto yake ilikuwa kuniona uwanjani nikicheza. Najua leo baba ana furaha juu yangu.” Na hilo ndilo jambo ambalo Dyabala amekuwa akilihitaji siku zote

 

Jicho la 3: Si kila timu inaweza kununuliwa, ila nilichokiona Mbao 2-3 Simba ni…

$
0
0

Na Baraka Mbolembole

KWANZA niwapongeze Simba SC. Kutoka nyuma 2-0 hadi dakika nane kabla ya kumalizika kwa mchezo, kisha kushinda 3-2 baada ya dakika 90 ni jambo la kujivunia kama timu. Hasa ukizingatia walikuwa ugenini dhidi ya Mbao FC ambao tayari walishawaangusha vigogo kama Azam FC na Mtibwa Sugar katika uwanja wa Kirumba, Mwanza.

MBAO FC

Walikaribia kupata ushindi wao wa nane msimu huu baada ya kuongoza 2-0 hadi dakika ya 82, lakini mbinu zao za kujilinda katika kipindi cha pili hazikusaidia kutokana na kukosa ‘ustahimilivu.’

Katika kipindi cha kwanza timu hiyo ya Mwanza ilifanikiwa kudhibiti kiungo na jambo hilo lilipelekea Simba kushindwa kucheza mchezo wao uliozoeleka-kutafuta goli wakitokea katikati ya uwanja huku wakipasiana pasi fupifupi.

Salmin Hoza, mfungaji wa goli la kwanza, George Sangija, Boniface Maganga na Pius Buswita waliweza kucheza mchezo wa nguvu na pasi za uhakika kwa dakika 30 za mwanzo na kuwafanya viungo wa Simba, Mghana, James Kotei, Mzamiru Yassin na Mohamed Ibrahim kutumia muda mwingi kukaba badala ya kupanga mashambulizi.

Mchezo wa nguvu kuanzia kwa walinzi, Mghana, Asante Kwassi, Mrundi, Yusuph Ndikumana, Vicent
Phillipo na David Mwasa ulikisaidia sana kikosi cha kocha Mrundi, Ettiene. Nawasifu Mbao kwa mchezo mzuri wa kushambulia na kuzuia kwa uhakika.

Na siwezi kuwalaumu kwa kushindwa kupata walau alama moja katika mchezo huo kwa maana walicheza kadri ya uwezo wao, walijitolea lakini mwisho wa siku wakapoteza mechi kutokana na ubora wa kimbinu wa wapinzani wao.

SIMBA SC

Nilishangazwa na uamuzi wa kocha Joseph Omog kuwaanzisha nje washambuliaji Ibrahim Ajib na Laudit Mavugo. Kitendo cha kuruhusu goli la kwanza dakika ya 19 na aina ya mchezo waliokuwa wakicheza Mbao nadhani kulimshtua kocha huyo wa Simba na yeye mwenyewe alijutia kosa lake la kuwapanga Pastory Athanas na Juma Liuzio katika safu ya mashambulizi.

Washambuliaji hao walishindwa kufanya jambo lolote, walishindwa kukaa na mpira, walishindwa kujipanga katika maeneo ambayo yangewarahisishia kutengeneza nafasi za kufunga. Walikuwa wakimya sana uwanjani na utulivu wao ukawapa uhuru walinzi wa Mbao kuanzisha vizuri mashambulizi ya timu yao wakitokea nyuma.

Kumtoa Pastory na kumpa nafasi kiungo Said Ndemla mara baada ya kufungwa goli la kwanza ulikuwa ni uamuzi mzuri lakini haukusaidia kitu kwa sababu Mbao waliendelea kucheza kwa kasi ileile tu, huku
Simba ikionekana kukosa mshambuliaji ambaye angeweza kuwafanya walinzi wa Mbao kutopanda mara kwa mara ndiyo maana wakaruhusu goli la pili dakika ya 34.

Kumpumzisha mlinzi wa kulia Ahmad Juma dakika ya 36 na kumpata nafasi Mavugo ilikuwa ni badiliko sahihi lakini bado mipira ilishindwa kukaa mbele na jambo hilo liliwapa wakati mgumu viungo na walinzi wa Simba.

Omog alikosea katika upangaji wa timu yake lakini badiliko la mwisho alilofanya robo saa ya mwisho ya mchezo kwa kumpumzisha Liuzio na kumpa nafasi Muivory Coast, Blagnon liliimaliza Mbao.  Nadhani aligundua ugumu wa timu yake kupata goli kama wangeendelea kucheza mchezo wa pasi fupifupi.

Kwa kutambua uwezo wa mshambuliaji wake huyo katika uchezaji wa mipira ya juu ndio kulimpa mafanikio.

Blagnon alifunga kwa kichwa cha kuparaza akimalizia mpira mrefu uliopigwa na
Kotei dakika ya 83, na akamalizia kwa ustadi mpira ulioshindwa kudhibitiwa na golikipa wa Mbao, Erick Ngwegwe dakika ya pili ya nyongeza kufuatia mpira mwingine mrefu uliopigwa na mlinzi, Besala
Bokungu.

Mipira ya juu ilionekana kuwasumbua sana Mbao ndio maana kila walipookoa haikuwa ikienda mbali. Mzamiru akatumia faida hiyo kufunga goli la ushindi katika dakika ya 6 ya nyongeza baada ya walinzi wa Mbao kushindwa kuondoa vizuri mpira uliokuwa ukizagaa katika eneo lao la hatari.

SI KILA TIMU INANUNULIWA

Wakati mwingine inabidi tukubaliane na ukweli kuwa soka ni dakika 90. Msimu wa 2011/12 Manchester United walitumia dakika 30 za mwisho kutoka nyuma 3-0 na kutengeneza sare ya 3-3 vs Chelsea katika uwanja wa Stamford Bridge, Simba ilitoka nyuma 3-0 na kutengeneza sare ya 3-3 vs Yanga SC msimu wa 2013/14 na hakuna aliyewahi kusema mechi hizo ziliuzwa zaidi ya kuwasifu Manchester United na Simba kutokana na kusawazisha magoli yote matatu.

Sasa kipi kinawafanya baadhi ya watu kusema kipa wa Mbao aliibeba Simba? Makosa ya wachezaji ndani ya uwanja ndio yanaleta tofauti katika mechi na lazima yafanyike. Mbao hawawezi kuuza mechi huku ukizingatia wapo katika nafasi mbaya katika msimamo.

Ni matokeo tu ya mchezo na hata Yanga walifanya makosa wakati walipofungwa na Simba pungufu mchezaji mmoja wakati waliongoza mechi kwa dakika 70. Je, Yanga nao waliwauzia Simba?

Si kila timu ina uza mechi, matokeo mengine yanatokea kwa sababu za kimpira tu. Simba walijituma sana na kuboresha mbinu zao katika kipindi cha pili ndiyo maana wakapata matokeo.

Kisima Cha Barcelona na Miguu Ya Neymar Ndani Yake.

$
0
0

Ndani ya ubongo wa kocha wa timu ya Taifa ya Brazil, Tite anaamini kuwa hakuna mchezaji aliyekuwa kwenye kiwango bora zaidi ya Neymar kwa sasa. Kwake miguu ya mchezaji huyu ndiyo yenyewe thamani kubwa kwa sasa na ambayo inafanya vitu ambavyo wengi wanaweza kuita ni bidhaa zisizopatikana sokoni yaani adimu.

Ni Neymar huyu ambaye wakati Messi ameamua kuchukua likizo yake ndani ya uwanja dhidi ya Paris St Germain aliamua kubeba msalaba wa moto na kuivusha Barcelona kwenda ng’ambo inayofuata. Kiwango alichokihamishia timu ya Taifa mpaka wanakuwa timu ya kwanza ya Taifa kufuzu kwenda kombe la dunia kule Urusi.

Inawezekana asionekane kwa kiasi kikubwa kwenye orodha ya juu ya wafungaji kwenye ligi kuu ya nchini Hispania, La Liga msimu huu, lakini pia unaweza kumtaja kama mchezaji muhimu zaidi wa klabu ya Barcelona kwa sasa na usipingwe.

Huyu ndiye haswaa aliyeshikilia funguo za Barcelona kama tu watataka kufungua mlango wa paradiso na huyu ndiye maji sahihi kwenye udongo wenye rutuba pale Camp Nou. Haipingiki kuwa hakuna binadamu mwenye kofia kichwani kwake ndani ya Barcelona zaidi ya Lionel Messi, huyu ndiye Daudi wao yaani mfalme wa wafalme wengi wanaopatikana hapo ndani.

Upofu pekee ndio unaoweza kumfanya mtu asitizame miguu ya Neymar ndani ya uwanja kwa sasa. Pamoja na Messi na Suarez kuwa na wastani mzuri wa mabao, bado Neymar ndiye anayeamua sumu yao hawa wawili isambae kiasi gani kwenye mwili wa adui. Neymar ndiye anayeamua kasi ya timu na namna ipi timu inaondoka kuelekea mbele.

Bahati mbaya ni kuwa usajili wa Barcelona uliopita ambao ulishuhudia Andre Gomez ambaye alitegemewa kuja kupunguza mzigo wa Iniesta, Pablo Alcacer ambaye angeweza kushusha pumzi za Messi na Suarez na pia Denis Suarez ambaye alikuwa mtoto anayetegemewa kukua haraka wote hawajaweza kufikia matarajio na maswali yaliyokuwa kwenye karatasi zao yalikuwa mtihani mgumu usiojibika kirahisi kwao.

Usingizi aliolala pono siku zote hutakiwa kuwa manufaa kwa mvuvi kwa sababu hatumii nguvu nyingi, lakini kwa Barcelona kwa siku za karibuni imekuwa tofauti. Walikuwa Simba waenda pole lakini nyama aliyoamua kuiacha Real Madrid wala hawajataka kusumbuka kuitafuna, na ndio kwanza Malaga walionekana klabu kubwa isiyokabika.

Baada ya Real Madrid kupata sare dhidi ya waliozaliwa nao pamoja Atletico Madrid, ilikuwa ni kazi iliyozoeleka ambayo Barcelona walitegemewa kuifanya dhidi ya Malaga. Lakini maisha yakawa tofauti, na ugumu wake ukapelekea Neymar kupewa kadi nyekundu aliyostahiki.

Punda ukimtuma sana hulala akiishiwa nguvu, ndivyo unavyoweza kutafsiri maamuzi ya Neymar, katika hatua muhimu kama hiyo, ni wazi presha ilikuwa juu yake na akashindwa kumuda mchezo. Lakini mdomo huponza kichwa, kitendo cha kuonekana kumdhihaki mwamuzi maana yake kimemfanya afungiwe michezo 3, ikimaanisha atakosekana dhidi ya Real Madrid kwenye El Clasico, huku ikiwa na tafsiri pia kuwa, Barcelona watacheza mchezo huo na mguu mmoja.

Inawezekana kabisa hii ikawa chungu kwa klabu lakini shubiri kwa mashabiki, dozi yao haitofautiani sana. Kumkosa Neymar kwa kipindi hiki kwa Barcelona ni kuepuka kutumia mwiko katika kuivisha ugali, tena msukuma ndiye mpishi. Kuuivisha inaweza kuwa tatizo kiasi lakini kuupika nao ni uamuzi mgumu.

Kwa sasa inaonekana kuwa tatizo la kawaida, inaonekana kuwa jambo lisilokuwa kubwa lakini hii ni furaha ndani ya Real Madrid. Adui kapata njaa na vita yake inakuwa ngumu kiasi, hii inamaanisha kuwa Lionel Messi itabidi abebe mzigo kwa sababu huwezi kumtuma Suarez kufanya kazi ya Neymar.

Kasi ya Neymar, ubunifu na wingi wa mabeki anaoweza kuwavuta upande wake imekuwa silaha ambayo inamfanya asifunge kwa kiasi kikubwa lakini ndio inayomfanya kuwa mchezaji aliyepewa alama nyingi zaidi kwenye michezo mingi kwa sababu anafanya kazi kuwa rahisi kwa pacha wenzie waliosalia.

Hii ndio sababu pia katika michezo ambayo haonekani kucheza vyema basi na Barcelona wanapoteza ubora wao. Juventus walilijua hili na wakahakikisha hachezi, na Barcelona ikafa. Messi hawezi kuwa yule wa siku zote wa kuisukuma timu. Miguu ya Neymar inahitajika.

Umefika muda ambao watu inabidi washike tama, umefika muda amabo mashabiki wa Barcelona wanaweza kuanza kununua dawa za maumivu. Kama machozi yapo jirani basi unaweza kuwa muda sahihi wa kuyaachia yatiririke. Ondoa machungu yamalizike kwa sababu Neymar kachafua kisima na Barcelona inaweza kuwabidi kukata kiu kwa maji yasiyokuwa safi na salama. El Classico haiwezi kuwa nyepesi bila Neymar, amekuwa chumvi katika kila mboga iliyopikwa na Barcelona msimu huu.

 

 

 

Jicho la 3: Kwa nini 4-5-1 itawamaliza Waarabu? Kessy, Msuva katika wings, Abdul, Oscar…

$
0
0

Na Baraka Mbolembole

KUJIONDOA kikosini kwa kiungo-mshambulizi, Mzambia, Obrey Chirwa kuelekea mchezo wa Caf Confederation Cup siku ya Jumamosi hii sidhani kama ni tatizo katika kikosi cha Yanga SC. Kwa msaada wa Chirwa, Thabani Kamusoko alifunga goli pekee katika mchezo wa kwanza wiki iliyopita wakati Yanga iliposhinda 1-0 vs MC Alger katika uwanja wa Taifa.

Chirwa hawezi kuwa tatizo katika kikosi cha kocha Mzambia, George Lwandamina, bali tatizo linaweza kuwa wachezaji wengine kama watashindwa kulinda goli lililofungwa na mchezaji huyo mahiri zaidi kwenye eneo la kiungo katika ligi ya Tanzania Bara.

KUJILINDA

Lwandamina ni kocha mwenye uzoefu sasa katika michuano ya Caf na kitendo cha kuifikisha Zesco United katika hatua ya nusu fainali Caf Champions League 2016 ndiyo sababu kubwa iliyowashawishi
Yanga kumpa kazi aliyonayo sasa.

Kama ataenda Omary Hamad ‘Uwanja wa Moto’ kuichezesha timu yake katika usawa kama ilivyokuwa katika game ya ligi ya mabingwa-ugenini vs Zanaco FC mwezi uliopita, sitakuwa na shaka, naamini Yanga watafuzu kwa mara ya pili mfululizo hatua ya makundi katika michuano  ya Confederation. Soka la kujilinda bila mbinu haliwezi kuleta matokeo bora.

MBINU ZA KUJILINDA VIZURI…

Yanga wanapaswa kufahamu matokeo yaliyopo sasa yanawapeleka hatua ya makundi kama watajilinda vizuri na kulinda ushindi wao katika mchezo wa Jumamosi hii. Imezoeleka kwamba timu nyingi za kiarabu barani Afrika hucheza mchezo wa kushambulia zikiwa katika viwanja vyao vya nyumbani, Omary Hamad.

Kwa namna MC Alger walivyocheza katika mchezo wao wa kwanza jijini Dar es Salaam hasa baada ya Yanga kufunga goli pekee dakika ya 61 ni wazi Waalgeria hao wamejenga imani kuwa wanaweza kupindua kiurahisi kipigo cha 1-0 wakicheza nyumbani.  Njia pekee ya Yanga kusonga mbele ni mbinu, ustahimilivu, uwajibikaji, makosa yanaweza kutokea lakini yapo yale ya kuepukika hasa katika uchezaji wa beki.

Nahodha, Nadir Haroub na Mtogo, Vicent Bossou ndiyo wachezaji wenye umri mkubwa zaidi katika safu ya ulinzi wa kati na wamekuwa wakiibeba sana timu yao tangu kocha Lwandamina alipoanza kuwachezesha pamoja katika mchezo wa ligi kuu Tanzania Bara dhidi ya Mtibwa Sugar FC mwezi uliopita. Kwa bahati mbaya, Bossou ataukosa mchezo huo kutokana na majeraha yanayomkabili hii ni kwa mujibu wa klabu ya Yanga.

Ni vyema kama Lwandamina ataamua kumpanga Kelvin Yondani kutokana na uzoefu wake katika mashindano ya kimataifa lakini pia amecheza kwa muda mrefu na Cannavaro hivyo itatengeneza utulivu na kusikilizana katika safu ya ulinzi wa kati.

KESSY, MSUVA WACHEZE WINGS, JUMA ABDUL, OSCAR KATIKA FULLBACKS…

Hassan Kessy na Juma Abdul ningependa kuwaona walinzi hawa wa kulia wote wakianza mchezo. Kessy katika wing, Abdul katika beki namba 2. Mwinyi Hajji ni beki mzuri wa kushoto lakini tayari amejijengea uoga wa kushindwa kuwahimili Waarabu wanapoamua kushambulia mfululizo kupitia upande wake.

Lwandamina hapaswi kuwapa uhuru wa kusogea mbele mara kwa mara walinzi wake wa pembeni na ili afanikiwe ingekuwa vyema Oscar Joshua kuanza katika beki namba 3 huku mbele yake katika wing ya kushoto akimpanga Saimon Msuva.

Hii ni mechi inayohitaji nidhamu ya kiwango cha juu ya kimchezo. Timu inahitaji kulinda zaidi na kushambulia kwa stahili ya kushtukiza. Faida ya kuwa na Kessy katika wing ya kulia na Msuva upande wa kushoto ni kwamba timu itakuwa na uwezo wa kupeleka mashambulizi timilifu na kuleta balansi ya ulinzi katika beki za pembeni.

Joshua ni mzuri katika kukaba na uwezo wake wa kuanzisha mashambulizi ya haraka unachagizwa na kipaji chake cha upigaji pasi ndefu zinazofika kwa walengwa. Juma Abdul tayari ana uzoefu mkubwa na kitendo cha kumpanga pamoja na Kessy kutaifanya Yanga kuwa imara katika beki zote za
pembeni.

Waarabu wanategemea zaidi wings kumaliza mechi lakini watakutana na wakati mgumu ikiwa Juma na Kessy watapangwa kwa wakati mmoja katika upande wa kulia na Msuva na Joshua katika upande wa kushoto.

4-5-1

Ni mfumo sahihi wa kuanzia mchezo. Katika mfumo huu ili kupata kikosi kitakachoshambulia na kukaba vizuri kuanzia upande wa eneo la wapinzani, Lwandamina anaweza kuwatumia Juma Abdul, Oscar, Nadir na Yondani walinzi wanne mbele ya golikipa Deogratius Munishi.

Mzimbabwe, Thaban Kamusoku, Said Juma Makapu na Mnyarwanda, Haruna Niyonzima wakiunganishwa na Kessy katika wing ya kulia na Msuva upande wa kushoto kutafanya timu kuwa na viungo imara katikati na pembeni mwa uwanja.

Mmoja kati ya washambuliaji Mrundi, Amis Tambwe na Mzimbabwe, Donald Ngoma akianza kama mshambulizi pekee. Makapu amekuwa akizuia vizuri katikati ya uwanja lakini staili yake ya ‘uchapaji viatu’ wapinzani wake hugeuka tatizo hasa kwa zile faulo za karibu na lango lake.

Kwa kawaida timu za kiarabu zinaposhindwa katika mbinu zao za kumaliza mechi wakitokea pembeni mwa uwanja, huanza kusaka mipira ya adhabu hasa kuanzia umbali wa mita 25 kuelekea lango la wapinzani wao.

Ili kuepuka faulo za karibu ni vyema Kamusoko acheze karibu na mabeki wa kati, Makapu mbele yake na Niyonzima akitandaza pasi pembeni au katikati kuelekea kwa mshambuliaji wa kati. Naamini Yanga itafuzu, wana mtaji mzuri, kikosi kizuri, kilichosalia ni mbinu za kocha na jinsi wachezaji watakavyozitimiza.

Siwezi kumbeza Chirwa kwa kitendo chake cha kugoma kusafiri na timu akishinikiza kulipwa kwa stahiki zake anazoidai klabu. Yuko sahihi na amejitolea kwa kila alichoweza kuifikisha Yanga hapa ilipofikia.

Anaweza kuonekana ‘msaliti’ kutokana na ukweli kila mdau wa soka nchini anafahamu klabu hiyo inapitia wakati gani sasa kiuchumi. Kamusoko ameshafunga goli la kuongoza sasa ni wakati wa timu kulilinda, kimbinu, kiufundi, ambako kunatimilishwa na uwajibikaji.

Simba wameshaanguka, TFF hatari zaidi kwa Yanga katika mbio za taji la 3 mfululizo VPL

$
0
0

Na Baraka Mbolembole

KAMATI ya masaa 72 inajaribu kuingilia matokeo ya ndani ya uwanja na kumaliza mbio za Simba SC kurejesha ubingwa wa ligi kuu Tanzania Bara baada ya kuukosa kwa misimu minne mfululizo.

Ni ‘aibu’ kwa watu wa Kamati hiyo kutoa uamuzi wa upendeleo kwa timu ya Simba na kuyageuza matokeo ya ndani ya uwanja Kagera Sugar FC 2-1 Simba na kuwa Kagera 0-3 Simba.

Kwa jinsi suala hili la Kagera kupokwa ushindi wao katika ‘kamati ya kahawa’ lilivyo hakuna sababu ya kujisumbua kuhusu kuzungumzia kanuni kwa maana kanuni zilishavunjwa na ‘kamati hiyo ya mama nibebe mwanao.’ Kinachopaswa kufanywa na wadau wa mpira ni kupaza sauti zao na ‘kusema Kagera hawajatendewa haki.’

Nini maana ya kamati ya masaa 72?

Kama mwenyekiti wa kamati hiyo atatoka hadharani na kusema kwanini kamati yake ilishindwa kutoa uamuzi wa malalamiko ya Simba ndani ya saa 72 kuhusu mchezaji Mohamed Fhaki kucheza mchezo wao dhidi ya Kag era akiwa na kadi 3 za njano atakuwa ‘matatizoni.’

Nadhani uamuzi wa malalmiko ya Simba ulipaswa kutolewa uamuzi ndani ya siku tatu baada ya malalamiko kufika mezani kwao. Siku 3 ni sawa na masaa 72 na maana halisi ya kamati ya masaa 72 pale TFF ni kutoa uamuzi wa haraka kuhusu malalamiko yanayowasilishwa kwao.

Kama ripoti ya mwamuzi wa mchezo inapaswa kuwasilishwa Bodi ya ligi ndani ya masaa 48-siku mbili baada ya mchezo, kulikuwa na ulazima gani sasa kwa kamati ya masaa 72 kushindwa kutoa uamuzi?

Jibu ni kwamba ripoti hizo hazikufika Bodi ya ligi ndani ya muda ambao waamuzi na wasimamizi wa mechi walipaswa kuwasilisha. Mwamuzi kushindwa kuwasilisha ripoti yake ndani ya siku mbili baada ya mchezo husika, kikanuni ni makosa na Bodi ya ligi inapaswa kumuondoa katika orodha ya kuchezesha.

Kwa nini waliendelea kuchezesha? Lakini hilo halikufanyika kwa waamuzi hao walioshindwa kuwasilisha ripoti ya michezo lalamikiwa ndani ya masaa 48.

Niwaambie tu, ‘Muosha, huoshwa’. Kama ‘mlishangilia’ sana wakati ule Polisi Dar FC waliponyimwa ushindi wao wa haki dhidi ya Simba baada ya Novalty Lufunga kuchezesha mchezo wa hatua ya 32 bora katika FA Cup akiwa na kadi nyekundu, suala lililowanyima haki ni ‘MUDA.’

Japokuwa Maafande hao walipaza sauti zao katika vyombo vya habari na kusema walipeleka rufaa yao kudai ushindi dhidi ya Simba ndani ya muda mwafaka. Lakini majibu ya kamati iliyowahuku walisema rufaa ya Polisi Dar FC ilishindwa kutokana na muda. Simba wakashinda kesi na kuendelea mbele ya michuano kutokana na ushindi wao wa 2-0 walioupata ndani ya uwanja.

Wakashangilia sana kuishinda haki ya timu nyingine. Sasa ni wakati wao wa kushindwa, na muda ni suala la kwanza. Muda ambao ripoti za waamuzi wa michezo lalamikiwa ziliwasilishwa Bodi ya ligi mara baada ya michezo husika kumalizika.

‘Kamati ya Mama nibebe mwanao’ inasemekana ilifanya ujanja katika tarehe za rufaa ya Polisi Dar FC na mtindo huo ndiyo ulipelekea kamati ya masaa 72 kushindwa kufanya kazi yao ndani ya muda.

Bila Yanga kuwahi kusema hadharani mchezo uliokuwa ukichezwa amini Kagera ingepoteza pointi lakini sasa Simba haiwezi kuzipata tena, huku suala la ‘MUDA’ likiwaangusha japo liliwabeba vs Polisi Dar FC.

Kuyumbishwa kote huku kwa kanuni kuna maana ya ‘RUSHWA.’ Kuna upande unarubuni upande mwingine ili mahala fulani wapate faida. ‘Kama rais wa TFF ni msafi’ atoe ruhusa ya TAKUKURU kuchunguza kuhusu kukiukwa mara kwa mara kwa kanuni maana ndiyo kuna haribu mchezo wa soka.

Yanga nao wanapaswa waelewe wanapambana na timu mbili na zote haziko tayari kuona wanashinda taji la 3 mfululizo la VPL. Simba ni washindani wao wa karibu ‘wanaoonekana’ na timu ya ‘Kamati fulani ya kahawa’ inayopenda kujifungia katika ofisi za TFF.

Timu hii haionekani uwanjani na inaongoza ligi kwa alama tano zaidi, haijulikani inapofanyia mazoezi lakini inavaa jezi zinazoshahabiana na zile wanazotumia wapinzani wao wa karibu wanaoonekana machoni mwetu.

Matokeo ya Kagera 2-1 Simba yanapaswa kubaki kama ilivyokuwa Polisi Dar FC 0-2 Simba japo Simba wanapaswa kuwa mshindwa wa kila mechi.

Simba wameshaanguka, TFF hatari zaidi kwa Yanga katika mbio za taji la 3 mfululizo. Hawataki kuona Yanga inashinda taji hilo moja kwa moja wakati si kitu kigeni. Endeleeni kughushi email na PiiiPiii wenu.

Mjadala ndani ya Sports Extra kuhusu utata unaoendelea kufunika pointi 3 za Simba

$
0
0

Jana April 17, 2017 katika kipindi cha Sport Extra cha Clouds FM uliibuka mjadala mkubwa wakati Alex Luambano na Shaffih Dauda wakijadili kuhusu Kamati ya Katiba Sheria na Hadhi za wachezaji kukutana leo April 18, 2017 kwa ajili ya kupitia uamuzi uliofanywa na Kamati ya Usimamizi na Uendeshaji wa ligi Tanzania maarufu kwa jina la Kamati ya saa 72.

Kamati hiyo inakutana kutokana na ombi la timu ya Kagera Sugar ambayo imeomba kupitiwa upya uamuzi uliofanywa na Kamati ya Saa 72 ambayo kwa mujibu wa kanuni, ilitoa matokeo mapya ya mchezo kati ya timu hiyo na Simba uliofanyika Aprili 2, mwaka huu huko Uwanja wa Kaitaba mkoani Kagera.

Katika mchezo huo, Kagera Sugar ilishinda mabao 2-1, lakini Simba ilikata rufaa ikidai kuwa Kagera Sugar ilivunja kanuni ya 37 (4) ya Ligi Kuu ya Vodacom kwa kumchezesha mchezaji Fakhi Mohammed ambaye alidaiwa na Simba kuwa alikuwa na kadi tatu za njano katika mechi tofauti za Liku Kuu ya Vodacom. Hivyo, ikaadhibiwa kwa mujibu wa kanuni ya 37 (37) ambayo ilitoa pointi tatu na magoli matatu kwa Simba.

katika mjadala huo huo, liliibuka swali kwamba, kwanini masuala yanayovihusu vilabu vya Simba na Yanga ndio hutatuliwa kwa haraka kuliko vilabu vingine vya ligi kuu?

U-Simba na U-Yanga ndio unasababisha mambo mengi yanapindishwa hilo lazima tukubali, watu wengi wenye mahaba juu ya hizi timu wanatumia nafasi walizonazo kufanya maamuzi ambayo wakati mwingine yanakwenda kinyume na taratibu.

Jiulize kuna mashauri mangapi ya malalamiko na rufaa pale TFF? Mfano mzuri ni sakata la Ludovic, ni kamati hii ya katiba, sheria na hadhi za wachezaji ndio inatakiwa itoa uamuzi lakini ipo kimya hadi leo, lakini limetokea suala ambalo lina maslahi kwa vilabu vya Simba na Yanga kamati inakutana haraka kujadili.

Kwa nini suala la Ludovic pia lisijadiliwe leo na kutolewa maamuzi kwa haraka kama ilivyo kwa masuala yanayo vihusu vilabu vya Simba na Yanga?

Kwa nini vikao ni vingi wakati kanuni zipo? Suala la mchezaji kuwa na kadi tatu za njano au kutokuwa nazo ni la kikanuni vikao vingi vya kamati vinatoka wapi? Mechi ya Kagera Sugar na African Lyon ndiyo inayoleta utata kwa sababu ndiyo inayo mhukumu mchezaji huka kwamba ndiyo ilikuwa mechi ya tatu mfululizo anaoneshwa kadi ya njano. Mechi hiyo hiyo ndio Kagera wanasema mchezaji hakuoneshwa kadi lakini wanakubali kuwa kabla ya mechi hiyo ni kweli alikuwa na kadi mbili za njano.

Sawa wanasema mechi haikuoneshwa na Azam TV wala haikurekodiwa, hebu tujiulize maswali kadhaa hapa. Waamuzi wa mechi husika (Kagera Sugar vs African Lyon) wanasemaje? Taratibu zinasemaje kuhusu mwamuzi kutuma ripoti baada ya mechi kumalizika, je ripoti ilitumwa ndani ya muda?

Waamuzi wa hiyo mechi, fourth official pamoja na msimamizi wa kituo wanajua kama hiyo kadi ipo au haipo.

Kwa upande wao Kagera Sugar wanasema kwenye rekodi zao hakuna hiyo kadi inayolalamikiwa na Simba. Kwa utafiti uliofanywa kwa baadhi ya wachezaji wa African Lyon waliocheza mechi dhidi ya Kagera Sugar wanasema hawakuona tukio lolote alilofanya Mohamed Fakhi lililopelekea kuoneshwa kadi ya njano na hawakuona mwamuzi akimuopnesha Fakhi kadi ya njano.

Sababu 5 kwanini Barca anaweza kugeuza matokeo na kufuzu vs Juventus

$
0
0

Barcelona wanahitaji historia nyingine leo usiku ili kuendelea kubaki katika michuano ya ulaya – ni ngumu lakini kuna sababu za kuamini kwamba kikosi cha Luis Enrique kinaweza kufanya maajabu tena msimu huu.

“Tuna asilimia 1 ya kufuzu, 99% zipo pande zote, tukiwa na imani na kuomba Mungu, magoli yatakuja tu.” – alisema Neymar ambaye aliiongoxa Barcelona kugeuza matokeo dhidi ya PSG na sasa anasisitiza kuna uwezekano wa kufanya hivyo tena. Barca wamekuwa na uwezo wa kubadili matokeo lakini pia wamekuwa wakipokea vichapo vikubwa. 

Pamoja na ushindi wa 3-0 jijini Turin wiki iliyopita, Juventus wana kumbukumbu ya ushindi wa Barca dhidi ya PsG vichwani mwao. “Barca ni kama Papa baharini, pindi tu wanaponusa damu.” Alisema Giorgio Chiellini ambaye pia amesisitiza haiwezekani kuondoa uwezekano wa Barca kugeuza matokeo. Sasa tuangalie sababu zinazotajwa kwanini Barca wanaweza kugeuza tena matokeo. 

 

Messi
 
Watu walio karibu na Messi wanasema amepania kubadilisha matokeo na kuisaidia timu yake kufuzu nusu fainali. Kama alivyoonekana kwenye mchezo dhidi ya Real Sociedad,  moyo wake wote upo katika mchezo wa usiku wa leo. 
Katika La Liga tayari ameshafunga magoli 29 na anaongoza kwa ufungaji katika ligi ya mabingwa wa ulaya akiwa na magoli 11, ana upungufu wa magoli 11 tu kutimiza idadi ya magoli 500 akiwa na Barcelona. Kama Barcelona watataka kutimiza mageuzi mengine ya matokeo katika msimu huu basi watahitaji Muargentina huyu kuwa katika kiwango chake bora kabisa – na akiwa kwenye kiwango chake cha juu hakuna wa kumzuia. 
Sergio Busquets IS BACK 
Bila uwepo wake, Barca walikuwa dhaifu jijini Turin, asipokuwepo dimbani timu inakosa kiungo muhimu katikati. Safari hii atakuwa na uwezo wa kumuweka Dyabala kwenye ulinzi na kuipanga vizuri timu ambayo safu yake ya ulinzi imeruhusu magoli 7 katika mechi za hivi karibuni. Busquets anajua vyema namna ya kuilinda safu yake ya ulinzi tofauti na Mascherano aliyecheza katikati wiki iliyopita.
The Blaugrana watahitaji kutoruhusu goli na kuwahi kufunga la mapema ili kuweza kuiongezea Juve presha na kupata magoli mengine na ili kufanya hivi wanahitaji mtu aina ya Busquets anakuwa kiungo muhimu kati ya safu ya ulinzi na ushambuliaji.  

Mbinu za kiufundi

Je tutaona mfumo wa 3-4-3 au mwingine au tuliozoea wa 4-3-3? Barça wanaweza kuwashtua Juve na mfumo wa uchezaji watakaouchagua. Kule Turin, waitaliano walitumia udhaifu wa mbinu ya Enrique kupanga mabeki watatu nyuma wakimtumia mchezaji kama Cuadrado.

Jordi Alba anaweza kurejea kikosini, huyu anaweza sana kuleta matatizo akishirikiana na Neymar – hili litampa shida sana Dani Alves. Sergi Roberto, pia kama ilivyokuwa katika mchezo vs Real Sociedad, anaweza kuwa na mchango mkubwa katika mfumo wa 4-3-3. 

Kumbukumbu za nyuma

Kwa mara 3 Barcelona wamewahi kufanikiwa kubadilisha matokeo ya magoli 3-0 katika mashijdano ya UEFA. Mara ya kwanza ilikuwa msimu wa 1977-78 dhidi ya Ipswich Town ambapo walipoteza mchezo wa kwanza wakaenda Camp Nou kushinda kwa penati. Mara ya pili ilikuwa msimu wa 1978-79 vs Anderlecht hapa pia walisawazisha na kisha wakaenda kushinda kwa penati. Halafu ukaja mchezo mwingine ambapo walitanguliwa 3-0 na Gothernberg kisha wakaenda kushinda mchezo uliofuatia msimu wa 1985-86 kwa penati tena. 
Halafu kuna huu mchezo wa majumaa kadhaa yaliyopita vs PSG ambapo walitanguliwa 4-0, kolichotokea Nou Camp ni historia……. 
Machinjoni Camp Nou 
Kama kuna sehemu ambayo Barca wanaweza kukufanyia unyama wa kisoka basi ni Camp Nou – ushahidi pekee ni takwimu za msimu huu tu katika mechi za ulaya zilizopigwa katika dimba hili msimu huu: Matokeo yote waliyopata Bsrcelona dhidi ya timu zote walizocheza nazo katika Champions League msimu huu yangetosha kabisha kuwaondoa Juventus katika michuano, Celtic alikufa 7, Monchengladbach alipigwa 4 na Guardiola na City nao walikula 4, PSG akapigwa 6, leo waitaliano watagongwa ngapi? 


Van De Sar Anapanga Aly Mayay na Boniphace Pawasa Wanachagua.

$
0
0

Kiungo wa zamani wa vilabu vya Simba, Yanga na timu ya Taifa, Athumani Idd “Chuji” aliwahi kusema kwenye kipindi cha Sports Xtra cha Clouds Fm kuwa alishangazwa walipoenda kucheza mechi za klabu bingwa Afrika nchini Misri, kuanzia Rais mpaka meneja wa vifaa vya michezo klabuni hapo ni wachezaji wao wa zamani.

Kwa Chuji ilikuwa sahihi kushangaa kwa sababu ni nadra kuona hili barani Afrika. Lakini pengine yanayoendelea kutokea inaweza kuendelea kuwa elimu kwa akina Chuji wengine waliokuwepo ambao hawafahamu katika utaalamu wa kielimu baada ya soka.

Mchezaji na golikipa wa zamani wa vilabu vya Ajax, Manchester United, na timu ya taifa ya Uholanzi, Edwin Van Der Sar atakuwa mmoja kati ya wazungumzaji wa mkutano mkubwa wa masuala ya soka maarufu kama  Soccerex Global Convention.

Mkutano utakaofanyika 4-6 Septemba, katika jiji la Manchester. Van Der Sar atakuwa sehemu ya ujumbe wa wazungumzaji wakuu ambao ni watendaji wakubwa wa vilabu wakijadili umuhimu wa kuwa na taratibu zinazofahamika ndani ya vilabu vya soka; namna ya kuanzisha na kuendeleza taswira ya klabu na vitu gani vinahitajika kuhakikisha haya mambo yanaendelea kusimamiwa na kuendelezwa.

Akiwa kwa sasa huyu ni mkurugenzi mtendaji wa klabu anayoipenda siku zote ya Ajax, Edwin ameweka machoni kwetu uwezo wake mkubwa kwa zaidi ya miaka 21, akishinda mataji na vilabu mbalimbali ikiwemo Juventus, Ajax na Manchester United. Lakini pia ni huyu ambaye amechezea timu ya taifa mara 13, Van Der Sar anahesabiwa kama moja ya makipa bora wa kizazi chake.

Baada ya kuachana na soka, Van Der Sar alienda kusomea shahada ya uzamili (masters) ya usimamizi/uongozi wa michezo na chapa kwenye taasisi ya Johan Cruyff kabla hajajiunga na Ajax, November 2012 akiwa mkurugenzi wao wa masoko.

Huyu amekuwa sehemu ya timu ambayo imebadili kabisa mfumo na mtinfo wa udhamini kwenye klabu ya Ajax na kukuza mwenendo wa chapa ya klabu hiyo duniani kote, na kusambaa kwenye masoko mengi kama bara la Asia. Kwa sasa akiwa kama mkurugenzi mtendaji wa klabu, Van Der Sar ni sehemu ya kundi la wachezaji bora waliochukua nafasi kwenye klabu hiyo pamoja na Dennis Bergkamp na Marc Overmars tangu waamue kustaafu.

Kwenye mkutano huo mkubwa wa kidunia, Edwin atatumia uzoefu wake mkubwa ndani na nje ya uwnaja kutoa elimu kubwa yenye thamani na muhimu kwenye ugeni utakaokuwepo.  Kazi kubwa aliyoifanya kwa miaka ya karibuni akiwa na Ajax imeegemea zaidi kwenye chapa ya klabu hiyo.

Lakini pia akihakikisha anatoa sifa na kusambaza sifa za filosofia ya klabu hiyo duniani.Ajax imekkuwa sehemu ambayo inasifika kwa ubora wa kufundisha mbinu bora, kukuza vipaji na Edwin atafundisha namna haya yanavyofanikiwa.

Hili ni jambo moja la msingi ambalo ni nadra kwa wwachezaji wetu wa ndani, jambo halipatikani na ambalo halijawahi kutiliwa mkazo. Ni aibu kuona kuwa sehemu kubwa ya uongozi wa soka letu upo chini ya watu ambao hawakuwahi kuwa wachezaji, kuanzia makocha, viongozi wa klabu mpaka timu ya taifa.

Lakini bahati mbaya ni kuwa wachezaji nao wamebweteka hakuna anayehitaji kuwa Van De Sar mpya au Giorgio Chiellin ambaye majuzi tu ametoa kuchukua shahada ya Uzamili huko Turin akifanya utafiti wa chapa na masoko ya Juventus. Aibu iliyoje, lakini inatakiwa tujifunze kutoka kwenye aibu hii.

Wachezaji wetu wa zamani wanatakiwa wakaongeze elimu, wasimamie vilabu hivi. Elimu zinazohusisha masoko na michezo, uongozi na michezo zipo nyingi na inaweza kusaidia kuondoa vilio vya kila siku vya soka letu kukosa watendaji sahihi.

Leo tungekuwa na akina Aly Mayay, Pawasa, Sekilojo Chambua wanaoongoza soka letu vyema. Bahati mbaya kupanga ni kuchagua. Alichopanga Van De Sar, Girogio Chiellin sicho walichoamua kuchagua akina Mayay na Pawasa wetu.

 

Njaa na Kilio cha Neymar, Shibe ya Kulevya ya Messi na Iniesta

$
0
0

Wakati mchezo kati ya Barcelona dhidi ya Juventus ukiendelea wengi walikuwa wanatizama na kusikiliza filimbi ya mwamuzi Bjorn Kuipers itaaamua nini. Wengi walikuwa wanasubiri baraka za waamuzi na namna zinavyofanya kazi na vilabu vya Hispania na wengi walikuwa wanasubiri maajabu mapya wa Barcelona baada ya yale yaliyofanyika kwa PSG.

Kwenye kichwa chake Neymar aliamini inawezekana, kwenye moyo wake Messi aliamini ni bora zaidi na angeweza, kwenye imani yake Suarez aliamini ni mhuni sana na angeweza kusababisha yote yawezekane. Unazungumzia klabu iliyofunga amabao 3 ndani ya dakika 7 dhidi ya PSG iliyokuwa imejihakikishia kufuzu mpaka dakika ya 85 ya mchezo wa pili.

Imani kwenye mioyo ya mashabiki ilikuwa kubwa na ndio maana haikuwa ajabu kuona mmoja wao akiwa na abango lililoandikwa Safari Kuelekea Cardiff ilikuwa bado inawezekana. Hizi ni fikra ambazo zilimfanya Simao Sarbrosa kuamini Anfield ulikuwa uwanja wa kipekee kwa mashabiki kutokukata tamaa.

Benfica walikuwa wameiondoa Liverpool na washabiki wake wa wakati huo walikuwa wakiimba muda wote achana na hawa wa sasa wanaomkimbia Klopp uwanjani mechi inapokuwa imekwenda kombo. Hiki ni kitu kinachotengenezwa na kocha na wachezaji kisha washabiki wanaamini ndani yake, akiibuki ghafla. Barcelona waliandika tayari.

Aliyeongoza hili bahati nzuri alikuwa ni kijana bishoo tu, kijana ambaye ugumu haukuwahi kuwa jadi yake na kijana ambaye muda wote angependa kucheza ili akukere, anaitwa Neymar. Sio Messi kama ambavyo wengi wangeweza kutegemea, huyu amekuwa silaha yao msimu huu hata asipofunga, anarahisisha kazi ya Barcelona kwa kiasi kikubwa sana.

Inawezekana usiweze kumlaumu Messi kwa sababu ametumika kwa nguvu kubwa tangu akiwa na umri mdogo, hana tena muda wa kuibuka na mbinu mpya mambo yanapokuwa kombo kwa sababu nyingi alizitumia akiwa kijana. Kwa sasa Messi ni kama Askofu tu, hafanyi misa nyingi lakini akifanya inakuwa kubwa zaidi na wala hajisumbui sana. Neymar ndiye paroko ama mchungaji wao na anatoa mahubiri yote kwa sasa.

Huu ni wakati wake na Barcelona wanatizama anachokifanya timu ya Taifa na wanaridhika. Lakini kuna tofauti moja kati ya Barcelona na timu yake ya taifa. Pamoja na kuwa ni mchezaji wao muhimu kwa sasa, bado Barcelona hawajaamua kukubali kuondoa makali ya upanga wa Messi kwa kiasi kikubwa, naam Messi huyu ambaye hana kasi yake tena na hawezi kuuamua mchezo kutokea katikati.

Inakuwa rahisi zaidi timu kumuwinda Neymar kwa sababu wachezaji wengine wanasubiri atende, ili wanufaike. Kipindi cha Nyuma, dawa ya MSN ilikuwa haikupatikana na eneo la kiungo lilikuwa bora hivyo hawakuzuilika.  Msimu huu eneo lao la kiungo limekumbwa na ukame na mwenye rutuba amebaki kuwa Sergio Busquets peke yake. Huyu ambaye alienda kumpokea Neymar aliyekuwa analia na kumpeleka kwenye vyumba vya kubadili nguo.

Ndani ya Barcelona kuna Messi atakayefikisha miaka 30 mwezi Juni akiwa ameshachukua kila alichotaka ndani ya Barcelona zaidi ya mara tatu, Kuna Iniesta ambaye hana haja ya kujifunza mbinu mpya, Suarez ambaye haufahamu utamaduni wa hapo na ambaye unaweza kukubali hawakilishi nembo yao kwa kiasi kikubwa na Sergio Busquets aliyeshinda kila kitu akiwa bado kijana.

Hivyo uti wa mgongo wa Barcelona wote una ugonjwa mmoja isipokuwa kwa Neymar. Wote wameogelea dimbwi la mafanikio na wote wamejikuta wanazeeka kabla ya umri wao na wala hawajisumbui kuhangaika sana. Katika hili Neymar atakuwa yatima, atalia peke yake na Messi hatojali sana. Kilio cha Messi kwenye Copa America baada ya kukosa Penalty hawezi kukitoa tena Barcelona, kule timu ya Taifa bado ana deni.

Neymar anaamini baada ya Messi na Ronaldo anafuata yeye. Anaamini kuwa hakuna kijana wa umri wake kushuka chini anayeweza kufanya anayoyafanya, ambaye anaweza kuamua maisha ya timu ya Taifa na klabu kwa ujumla kama yeye. Hii ni akili aliyojengewa tangu akiwa Santos mpaka timu ya taifa na kisha Barcelona na ndio iliyomkomaza kuliko wachezaji wengine wa umri wake kama Hazard, Dybala, Griezmann na hata Bale.

Kilio chake dhidi ya Juventus kilikuwa na ujumbe. Alikuwa ndiye mchezaji anayeuhitaji ushindi kuliko wengine kwenye kikosi cha Barcelona. Unaweza usimlaumu Suarez, lakini Messi na wengine wameshiba ndani ya klabu, matumbo yamejaa na la Neymar peke yake bado lina nafasi kubwa. Bado anautamani mpira na bado hajaweza kutwaa uchezaji bora wa dunia.

Barcelona hawajawa tayari kumbebesha timu, sio kwa sababu hastahili lakini kwa sababu wataanzaje kuitoa kwa Lionel Messi ambaye bado ana uwezo wa kufunga mabao mengi zaidi ya Neymar na Suarez kwa sababu bado timu imemzunguka yeye? Neymar ana njaa, Messi ana shibe, Iniesta na Busquests wamevimbiwa kabisa.

Bahati mbaya hata Usajili wao umekuwa mbaya msimu uliopita, hawakuleta mtu ambaye anaweza kuamua matokeo nje ya waliokuwepo. Sio Paco Alcacer wala Gomez au Dennis Suarez wanaoweza kuamua timu ishinde inapohitajika. Msimu ndio umekwisha kwa Neymar kwa sababu hata El Clasico hatokuwepo, hatopata sehemu ya kuonyesha Ulimwengu maajabu ya PSG.

Kilio chake dhidi ya Juventus kilikuwa chake peke yake, na ndio maana aliyemsaidia kulia alikuwa Mbrazil mwenzie na mpinzani wake kwa usiku huo Dani Alves. Huyu alimpa kumbatio la kiundugu tu. Najua msimu ujao atakuja tofauti, atakuwa mchoyo ikibidi, atakuwa hatari kivyake huku pia akikumbatia uwepo wa MSN. Hivyo ndivyo Messi alivyofanikiwa, pamoja na uhatari wa Barcelona alijijenga kuwa hatari zaidi ndani ya mchanganyiko huo.

Pole Neymar kilio kilikuwa chako peke yako, njaa ilikuwa yako peke yako, Suarez hawezi kupewa hii timu, yeye ataendelea kuwa kiungo muhimu kwenye pishi hili. Bahati mbaya kwako Messi kashashiba, msimu ujao njaa yako ikuongoze, kilio chako kikuongoze huku ukinufaika na Messi kujazilizia sehemu ya wazi ya tumbo iliyobaki. Kwa kiasi kikubwa mwezio keshashiba, akina Iniesta ndio kabisa kwa sababu wana mpaka Kombe la dunia, shibe imewalevya.

By Nicasius Nicholaus Agwanda (Coutinho)

Insta @kotinyotz

 

Tulipomhukumu Nyosso kwa jezi zake alizovaa

$
0
0

Na Abdul Mkeyenge

TANZANIA ina Juma Said Nysso mmoja tu yule ambaye hajawahi kubadilika matendo yake uwanjani na nje ya uwanja. Nyosso wa Ashanti United wa Manyema wa Simba wa Mbeya City wa Friends Rangers ni Nyosso yule yule wa siku zote ambae hajawahi kubadilika na sijui lini ataamua kubadilika. Amezaliwa vile alivyo. Nasikia mwenyewe huwa hajali.

Mtemi kwa wenzie, mshindani asiyetaka kushindwa. Mara nyingi naamini kando ya George Oseh wa Ruvu Shooting ya kaka yangu Masau Bwire, Nyosso anabaki kuwa mlinzi katili uwanjani kwa miaka ya hivi karibuni. Unahitaji nguvu na maarifa kupambana nae, bila kujali akizidiwa nini huwa anakifanya kwa washambuliaji.

Nyosso ana sifa nyingi ambazo walinzi wa kati wa kileo hawana. Walinzi wengi wa kileo wanatumia muda mwingi kukaa mbele ya vioo kusokota nywele zao. Ukiachana na mambo yake nje ya uwanja, ndani ya uwanja anakupa vitu vingi ambavyo hawa mabeki wetu wa timu ya taifa hawana. Nyosso jasiri, sidhani kama kuna mwanaume jasiri kwenye ukuta wa Stars anayefikia robo ya ujasiri wa Nyosso. Sidhani. Kama yuko niambieni.

Sifa zote hizi lukuki, lakini hachezi ligi yuko kifungoni kwa utovu wa nidhamu. Taarifa nzuri ni kuwa anakaribia kumaliza kifungo na kurejea uwanjani tena. Sijui akirudi atajivisha ngozi ya kondoo, wakati yeye ni chui. Sijui. Wacha tuusubiri urejeo wake.

Kitendo alichomfanyia John Bocco si kitendo kinachoweza kusahaulika kirahisi. Kile ni kitendo ambacho hata mwanae Moza akikua anaweza kumtazama mara mbili baba yake kwa kitendo kile. Kama Moza hatakuja kumshangaa baba yake kwa tukio lile atakuja kumshangaa kwa tukio gani jingine?

Wakati Nyosso amesimama nyuma ya Bocco na kukikunjua kidole chake cha kati kwa umaridadi wa hali ya juu na kumshika nacho Bocco sehemu ya makalio na baadae kamera za Azam TV kumuumbua, Nyosso hakujua kitu kimoja. Hakujua jezi alizovaa hazikuwa za Simba, Yanga wala timu za Taifa Stars ambazo Wajumbe wa kamati za fungia fungia wangepata shida kumpa adhabu. Hili ndiyo kosa lake kuu.

Jezi ya Mbeya City haina uzito mbele ya jezi za Simba, Yanga na Taifa Stars. Kama Nyosso angefanya tukio lile angekuwa anachezea timu za Kariakoo, ndani ya Wajumbe wa kamati za fungia fungia kwenye mkutano wa kutoa maamuzi ya adhabu yake vikombe vya kahawa vingegongana na korosho zingemwagika na kifungo chake kisingekuwa rahisi kama kilivyokuwa.

Kingine asichokijua Nyosso. Ndani ya kamati za fungia fungia ni aghalabu kumpata mtu wa Mbeya City mwenye sauti kubwa ambaye akisema kitu viongozi wa Simba, Yanga, Azam watamsikiliza na kuiunga mkono hoja yake. Unadhani Nyosso kiongozi wake angekuwa wa Simba, Azam, Yanga afungiwaje miaka miwili kirahisi na kungeacha kutokea kitu?

Jezi ya Mbeya City haina uzito huku mitaani kwetu na siku hizi ndiyo haina uzito kabisa na timu yenyewe ishaonekana kuwa ya kawaida. Nyosso alifanya ujinga wake bila kujua nani atakayemkingia kifua mambo yakiharibika. Ndio maana amesimamishwa miaka miwili na amerudi nyumbani kulia na familia yake. Hana wa kumsaidia kulia, analia na Moza wake.

Utovu wa nidhamu uliomtenganisha na soka la ushindani na sasa kucheza viwanja vya mchangani hauna tofauti kubwa na utovu wa nidhamu wa rafiki yangu Abdi Banda aliyegeuka ‘bondia’ siku hizi. Banda ni bondia wa kwenye viwanja vya soka na sio bondia wa ulingoni. Ananifurahisha anavyowatawala washambuliaji, lakini akizidiwa anaacha kucheza kwa miguu, anacheza kwa mikono.

Matukio yake mawili ya kuwapiga ngumi Said Juma Makapu, George Kavila, ni matukio ambayo kila nikirudia kuyatazama nabaki kutabasamu mwenyewe, huku nikimkumbuka Nyosso. Aibu iliyoje Banda ameitwa mbele ya kamati za fungia fungia na kusamehewa.

Sikumbuki vizuri baada ya tukio lile la Nyosso kama aliitwa mbele ya kamati kujieleza, kujitetea, kukiri kosa, kuwaomba radhi wachezaji, timu na kuendelea kucheza kama ilivyo kwa Banda. Sikumbuki jamani, anayekumbuka anikumbushe na mimi.

Kamati ile ile iliyomfungia Nyosso ndio iliyotoa msamaha kwa Banda. Sababu yao ni nyepesi tu, mchezaji ameitika wito. Hapa Nyosso anaweza kuwa mkaidi na hajaenda alivyokuwa ameitwa. Sina hakika lakini. Sababu nyingine ni kuomba radhi, kukiri kosa kuwa alichokifanya ni kibaya. Hivi mtu kama kakosa akiomba radhi ndiyo anasamehewa kirahisi namna hii?

Uko wapi usawa wa haki usiokuwa na kona kona? Kufanya kosa na kukiri kosa hivi ni vitu viwili tofauti. Ina maana tukawatoe Jela wale walioua watu kwa maana walilia hadi kusaga meno chini kuonyesha wanajutia makosa yao? Hapa ndipo inapokuja tofauti ya mchezaji wa Simba na mchezaji wa Mbeya City.

Tukio la Nyosso limemezwa na jezi alizozivaa wakati anafanya tukio lenyewe ndio maana ndani ya adhabu yake hakuna aliyeshituka wala kumsikitikia. Ameshituka mwenyewe na amesikitika mwenyewe. Hakuna aliyeshituka nae wala kumsikitikia.

Jicho la 3: Kama ningekuwa katika nafasi ya Aveva/MO Dewji ningefanya tafakari kuhusu ‘kauli mbaya’ ya Manara

$
0
0

Na Baraka Mbolembole

Geofrey Nyange Kaburu ana nyadhifa ngapi katika soka la Tanzania? Tatizo la soka la Tanzania linaanzia hapo na msemaji wa klabu ya Simba SC, Haji Manara yuko sahihi kabisa kumshinikiza rais wa TFF kujiuzulu katika moja ya nafasi zake mbili za uongozi wa soka. Malinzi ni mwenyekiti wa Chama cha Soka mkoa wa Kagera pia ndiye rais wa Shirikisho la Soka nchini (TFF).

SIMBA SC

Kuelekea michezo mitatu ya kumaliza msimu, Simba wameshapoteza ‘dira’ ya kushinda ubingwa na kinachofanywa sasa na uongozi wa klabu hiyo ni kuwaaminisha wanachama na mashabiki wa klabu hiyo ‘wameshindwa’ kwa sababu ya watu fulani waliopo katika Kamati mbalimbali za TFF. Kumbe Sivyo.

Simba imefanikiwa kuchukua alama nne kati ya sita dhidi ya washindani wao wa ubingwa msimu huu-Yanga SC (Simba 1-1 Yanga, Yanga 1-2 Simba). Wamefanikiwa kuchukua pointi tatu kati ya sita vs Kagera Sugar FC (Simba 2-0 Kagera, Kagera 2-1 Simba), wamefanikiwa kuchukua alama tatu mbele ya Azam FC (Simba 1-0 Azam, Azam 1-0 Simba), wakachukua alama nne dhidi ya Mtibwa Sugar FC (Simba 2-0 Mtibwa, Mtibwa 0-0 Simba), pia wameshachukua alama Tatu vs Mwadui FC (Mwadui 0-3 Simba)

Kwa mlolongo wa matokeo ya ndani ya uwanja dhidi ya timu 6 za juu katika msimamo wa ligi kuu ni wazi Simba ndiyo timu iliyofanikiwa zaidi kuliko Yanga, Azam FC, Kagera, Mtibwa na Mwadui katika mipambano iliyowahusisha wenyewe kwa wenyewe. Je, ni timu gani imebebwa kuliko nyingine kati ya timu hizi 6 za juu zaidi ya Simba?

Haji si mtu mwenye ufahamu kuhusu soka ndiyo maana amekuwa aki-ropoka bila mpangilio wala kuwa na kumbukumbu. Simba ndiyo timu yenye wanachama wengi hai ndani ya kamati za TFF.

KUHUSU POINTI 3 ZA KAGERA

Ndani ya uwanja Simba wameshapoteza mechi, wakakimbilia mezani kurudia mechi, wakashinda chini ya Kamati ya saa 72 ambayo naiita ‘Kamati ya Kahawa’ kwa sababu ni kamati iliyoshindwa kufanya kazi yake vile ilivyopaswa.

Ikumbukwe pia ndani ya Kamati hii ya saa 72, Wanakamati wengi ni wanachama/wapenzi wa Simba hivyo ni wazi Kagera isingeweza kupata haki hasa ukizingitia ‘umuhimu’ wa pointi 3 ambazo Simba wanazitaka bila ‘kuvuja jasho’

Ni aibu kubwa sana, kuona Simba ikizunguka na uongozi wote wa juu Kanda ya Ziwa na kuambulia pointi nne tu! Labda hili ndiyo linawauma lakini hawawezi kubadilisha ukweli kuwa walifungwa 2-1 na Kagera japokuwa ‘Wana-kamati wa saa 72’ walitumia ‘utashi’ wao kuwapa Simba pointi ambazo hazikustahili.

NILITABIRI SIMBA ITACHEZA MISIMU 6 MFULULIZO BILA TAJI LA VPL, NA BADO MSIMU UJAO

Kabla ya kuanza kwa msimu huu niliandika sababu Tatu ambazo nilisema ‘nitazitumia kama fimbo ya kuichapa Simba msimu wa 2016/17’ na fimbo hizo zote zinafanya kazi niliyotaraji. Naendelea kuichapa timu ambayo sikupaswa kufanya hivi lakini imenibidi niichape tu ili mambo yajerejee kama ilivyokuwa miaka ya nyuma.

Sababu ya kwanza nilisema, Hamis Kiiza. Kumuacha mfungaji bora wa klabu aliye ndani ya mkataba kwa sababu tu alidai pesa zake za mshahara, kwa jicho langu la 3 niliona ni kosa kubwa. Lakini Zacharia Hans Poppe ambaye ni mwenyekiti wa kamati ya usajili klabuni hapo aliamini Simba inaweza kuziba pengo la Mganda huyo aliyefunga magoli 19 katika michezo 22 ya VPL msimu uliopita na nakudhani Mrundi, Laudit Mavugo atafaa kuziba nafasi ya Kiiza.

Poppe na hata tarajio lenyewe Mavugo wote wameshafeli. Na kufeli kwao ni kufeli kwa timu ndani ya uwanja. Katika magoli 43 waliyofunga Simba msimu huu huku wakisalia na michezo mitatu kabla ya kumalizika kwa msimu, mfungaji anayeongoza kwa ufungaji ni kijana Shiza Kichuya.

Huyu alisajiliwa akitokea Mtibwa Sugar na wakati wa tetesi za usajili wake June 2016 niliandika Simba inapaswa kumsaini winga huyo wa kulia na uwepo wa Kiiza ulikuwa ni sawa na kumaliza tatizo ambalo liliwaangusha kwa kiasi fulani wakati Mganda huyo alipokosekana katika baadhi ya michezo msimu uliopita.

Niliamini uwezo wa Kiiza katika ufungaji na kwa kweli kati ya wafungaji mahiri wa kigeni ambao nimepata kuwaona VPL, Kiiza ni mfungaji wa hatari hasa pale timu yake inapocheza kwa kushambulia. Kiiza alikuwa na njaa ya magoli na alijua kujipanga akiwa ndani ya eneo la hatari. Alifunga ‘hat-tricks’ mbili msimu uliopita akicheza katika timu isiyotengeneza nafasi nyingi za kufunga kama hii ya sasa.

Mavugo amekosa ‘msukumo’ japo wengi wana mtetea kwa kusema apewe muda. Atapewaje muda wakati kila msimu klabu inasajili mshambulizi mpya?

Kiiza aliingia Simba na kufunga magoli 24 katika michezo isiyozidi 30 msimu uliopita na alifanya hivyo akiwa mchezaji mpya kikosini. Ila hakupewa muda kwa sababu ya kudai stahiki zake ilikuwa ni kosa kwa watawala wa klabu na kumjumuisha katika ‘wahujumu klabu’ mzigo ambao uliambatatana na matusi kutoka kwa baadhi ya mashabiki na wanachama wa klabu.

Goli 11 za Kichuya na saba za Mavugo walizofunga hadi sasa kuelekea michezo mitatu ya mwisho ya klabu yao, bado wawili hao hawajafikia magoli aliyofunga Kiiza msimu uliopita wakati kama huu alikuwa tayari na magoli 19.

Kiiza ilikuwa ni muendelezo wa usajili ‘mbovu’ usiozingatia mahitaji ya timu. Aliachwa Amis Tambwe wakati akiwa mfungaji bora wa klabu, wakiamini katika Elias Maguli wakati wote wawili walipaswa kucheza hata kama si katika kikosi kimoja mchezoni.

Nilishasema Masvugo hawezi kufikia nusu ya magoli aliyofunga Kiiza msimu uliopita kwa sababu niliamini atahitaji muda, ndiyo maana nilitaka kuona Kiiza anasalia hata kama Mavugo angesajiliwa. Neno lilolowahi kumkera Rage ni pale nilipomwambia, Yusuph Manji ni mtihani wake wa kwanza mkubwa kwake na klabu kiujumla Julai, 2012.

Japo hajafanikiwa kwa kiasi kikubwa sana nje ya uwanja ila kati ya Agosti 2012 hadi sasa Manji ni mshindi wa kweli vs Simba ndani na nje ya uwanja. Mwenyekiti huyu wa Yanga amepevuka katika maeneo ya kibiashara na jambo pekee alilotaka kuona ni klabu ikishinda mataji ya ndani ya nchi na kupambana ‘kupenya’ katika soka la Afrika.

Chini ya Manji kama mwenyekiti, Yanga wamekuwa wamoja nje ya uwanja, wamekuwa washindi wa vikombe vitatu vya ligi kuu na huenda wakaenda kushinda kikombe cha nne ndani ya msimu wa tano Mei mwaka huu. Manji amewapa uhuru makocha kufanya sajili zile walizotaka na jambo hilo limeifanya timu kuwa bora ndani ya uwanja na kutawala soka la ndani.

Amefanya kazi na makocha wanne huko nyuma, Tom Saintfiet ambaye alimfukuza ndani ya siku 76 baada ya kusaini mkataba wa miaka miwili Julai, 2012. Raia huyu wa Ubelgiji alimwambia Manji ‘amuache afanye kazi yake’ huku pia akimpiga kijembe kwa kumwambia, ‘wewe ni mfanya biasha, ila si mfanyabiashara wa kimataifa’

Akamleta Mholland, Ernie Brandts, kisha Babu Hans van der Pluijm, Mbrazil, Marcio Maximo kwa miezi 6, Hans na sasa Lwandamina. Ndani ya makocha hao licha ya kukosea mara kadhaa, Manji alijifunza kitu kuwa ili pesa anazozitoa zifanye kazi anayotaka ni lazima azipe uhuru. Ndiyo maana Hans alisema ‘toa milioni 200 kwa Obrey Chirwa aje hapa’ na Manji kama mwenyekiti alisema ‘pesa itolewe’

Lakini kwa Simba kila wakati wa usajili timu inakuwa haina kocha, hapo ndipo Poppe hufanya kazi yake na hajawahi kufanikiwa kwa sababu huwezi kumuacha mfungaji kama Kiiza kwa kutegemea mfungaji kutoka ligi kuu ya Burundi moja kwa moja. Kuna mechi nyingi msimu huu Simba imeangushwa na washambuliaji, na yote kwa sababu haikuwa na mbadala katika ufungaji kama Kiiza.

Leo hii, Basrcelona hawezi kumuuza Lionel Messi eti kwa sababu watakuwa na uwezo wa kumsaini Edinson Cavani kutoka PSG! Usajili wa Kamati ya usajili Simba ni sababu ya yote haya yanayotokea sasa upande wa timu hiyo. Sasa wanataka hadi ‘kuandamana’ hii ni kali sana, uandamane wakati wewe ni mfalme wa Top 6? Fikirini kabla ya kusema.

KOCHA OMOG

Nimekuwa shabiki wa klabu ya Simba kwa maisha yangu yote ya ufahamu na kamwe siwezi kuwa shabiki wa klabu nyingine hapa Tanzania japokuwa siridhishwi na mwenendo wa klasbu hii tangu msimu wa 2012/13.

Sijawahi kuona tumaini la kunyanyuka kwa Simba chini ya utawala huu wa rais Evance Aveva na makamu wake Kaburu. Na niliwahi kumwambia Ismail Aden Rage Jualai, 2012 kuwa ‘anaipeleka Simba katika anguko kubwa’ na hiki ndicho kinachoendelea kutokea.

SIMBA walimpa kazi Omog kwa sababu ni rafiki wa mmoja wa viongozi wa klabu hiyo wakati akipewa nafasi iliyokuwa imeachwa wazi Dylan Kerr. Omog anaweza kuwa amefanikiwa kwa maana ya kushinda mataji akiwa AFC Leopard ya Congo Brazaville, na Azam FC lakini ukiniambia kocha ambaye Simba ilipaswa kumsaini ni Mganda, Jackson Mayanja chini yake Salum, Mayanga.

Mayanja alishathibisha ubora wake wakati aliposhika kwa muda nafasi iliyoachwa wazi na Kerr. Kama si sababu za kiutawala Mganda huyu angeipa Simba taji la VPL msdimu uliopita. Alishinda game 7 mfululizo huku timu ikicheza vile alivyotaka yeye.

Kumleta Omog ilikuwa ni sawa na kuanza upya kabisa huku mifumo yake ikihitaji wachezaji wapya zaidi na bahati mbaya alikuta timu imeshasajili. Vuta picha kama usajili wa Simba ungesimamiwa na Mayanja na Mayanga Juni, 2016 Simba ingekuwa na kikosi cha aina gani.

Bado siwezi kumsema kabisa Omog kwa sababu kama kocha amefanikiwa kwa kiasi kikubwa kulingana na namna hali ilivyokuwa wakati akichukua kibarua hicho, ila naamini Mayanja na Mayanga wangekuwa mbali zaidi kama wangepewa timu hiyo.

UTAWALA

Nilisema kati ya fimbo zangu tatu za kuiangusha Simba msimu huu-utawala niliuzungumzia kama sababu ya kuanguka. Licha ya kwamba katika sababu zangu mbili za mwanzo uongozi unahusika ila hapa nitazungumzia ni kwa namna gani unahusika kuiangusha timu ndani ya uwanja.

Furaha yote ya Simba imeishia katika mchezo wao wa kwanza tu walipotembelea kanda ya Ziwa. Licha ya watawala wote hao kuambatana na timu Kagera-walichapwa 2-1 na wenyeji wao Kagera Sugar, wakashinda kiajabu vs Mbao FC, wakaangusha pointi mbili mbele ya Toto Africans.

‘Uongozi ni matendo si kujionesha’ inashangaza sana kuona msemaji wa klabu hiyo anaitisha mkutano na waandishi wa habari halafu anazungumzia kuhusu ‘ukabila’ Hii ni sumu ambayo haipaswi kutumika katika nchi yetu. Kuzaliwa mjini si kujua kila jambo. Kama unafahamu ukubwa wa Simba kwanini sasa wewe mwenyewe unaenda mbele ya wanahabari na kuzungumzia ukabila?

Kushindwa kutoa kauli yoyote rasmi kwa uongozi wa Aveva kuhusu kile alichokisema Haji Manara ni sawa na kuiaminisha jamii kuwa uongozi wa timu hiyo ulimtuma Haji kuzungumzia ukabila, na kama ni hivyo basi hilo ni kosa kubwa ambalo wamelifanya na kwa hakika linathibitisha kile nisemacho mara kwa mara kuhusu watu hao wanaoongoza klabu kama ‘genge la wahuni’

Msimu uliopita Manara huyu huyu anayejiita mtu wa mpira alishinikiza timu yake isicheze hadi Yanga na Azam FC wacheze michezo yao ya viporo. Nilishangaa sana kwa sababu Simba ilikuwa katika moto na kila timu ilikuwa inahofu kukutana nao. Leo hii Manara huyuhuyu anatupa ‘shimoni’ Simba katika wakati mbaya, lakini maalumu kwa wapinzani wao katika ubingwa. Simba wamepata matokeo stahili ndani ya uwanja na hawawezi kunyimwa haki yao mezani kama wangefuata kanuni.

Simba hawakuwa na sababu ya kusema yote waliyosema kupitia Manara, kitendo cha uongozi wa klabu kukaa kimya hadi sasa ni ishara kuwa ‘msimu kwao umeishia’ kanda ya Ziwa ndiyo maana walijaribu kulazimisha kupata pointi za ‘mezani’ wakati walipoteza uwanjani.

Wiki iliyopita nilisema, ‘muda’ ni suala lililowaangusha Polisi Dar FC wakati walipokata rufaa ‘nje ya muda’ kupinga ushindi wa 2-0 ambao Simba waliupata dhidi yao ndani ya uwanja. Polisi Dar FC walitaka ushindi baada ya Simba kumchezesha mchezaji Novalty Lufunga akiwa ndani ya adhabu ya kutumikia kadi nyekundu katika michuano ya FA Cup.

Nilisema, rufaa ya Simba dhidi ya Kagera kuhusu kadi tatu za njano za Mohamed Fakhi ilikuwa ‘nje ya muda’ hivyo haikuwa na nguvu tena japo kuna baadhi ya watu walibadilisha ukweli huo kwa maslai yao binafsi. Simba walifahamu kuwa walipeleka rufaa bila ada ya rufaa na ilikuwa nje ya muda, sasa kitu gani kilimfanya Manara ( Mr. Povu) kulalamika wanaonewa.

Nilimsikia aklisema kuna kiongozi wa juu wa TFF alijaribu kuzuia maamuzi ya Kamati ya saa 72 ambayo iliwapa ushindi wa mezani vs Kagera. Mimi nadhani mtu huyo mkubwa wa TFF alijaribu kuzuia kwa sababu alijua kanuni zimekiukwa hivyo hakutaka itangazwe ili kuhofia kutokea mkanganyiko kama uliopo sasa.

Manara kama unajua Simba ni kubwa, basi ‘umeitukanisha’ klabu kubwa kwa jamii na bila kuomba radhi wewe ‘ni mkabila’

Hata kama ni mimi ningekuwa katika nafasi ya Mohamed Dewji ningeanza kujiuliza ni kwanini timu imeshindwa ndani ya uwanja licha ya kujitolea kiasi kikubwa cha pesa. Ningekuwa katika nafasi ya MO Dewji ningejiuliza, huyu Manara aliisemea klabu au? na kutafakari kauli yake ‘ya kikabila’ na kutazama kuhusu ufadhili wangu na faida zinazopatikana klabuni.

Karibu Mbappe, Tumeona Nyama Alizokula Ronaldo, Tunawaza Mifupa Utakayoitafuna.

$
0
0

Usiku wa tarehe 12 April, kinda huyu aliyewahi kuruka hatimaye aliweka rekodi ya kuwa mchezaji mdogo zaidi kuwahi kufunga mabao mawili katika mchezo mmoja kwenye hatua ya mtoano. Ndio, anaitwa Mbappe huyu ambaye anafananishwa na Thierry Henry ingawa moyo wake upo Madeira akijaribu kuyaishi maisha magumu kwenye soka ya Cristiano Ronaldo. Mbappe amepitia ukuaji wake akizibusu na kupiga magoti mbele ya picha za Cristiano Ronaldo, akiomba kila usiku unaopita aweze kuwa kama yeye.

Pengine Mbappe anaweza asiwe mbali na moja ya matukio ya ndotoni mwake, inawezekana kabisa akatupa shuka na kuanza kuzitumikia ndoto zake. Lakini kama mchezaji Lebron James alivyowahi kusema juu ya Michael Jordan kuwa anafukuza Zimwi, basi Mbappe naye kaingia katika mbio hizo, anafukuza Zimwi ambalo limekua, limeishi na likaifahamu damu inayoitwa mafanikio.

Haikuwahi kuwa rahisi kwa Cristiano kufika hapo, hakikuwa kitu rahisi kumfanya mwanamitindo Irina Shayk kumfanya ajute kuachana nae na wala sio jambo jepesi kwa mwanafasheni Georgina Rodriguez kuamua kuacha kazi kwenye kampuni kubwa kama Prada kwa sababu ya jina la Cristiano Ronaldo.

Haya ni maisha aliyoyapigania, ameyajenga na amestahiki kuwa hapo. Ikiwa katika usiku huo huo wa Mbappe, Cristiano Ronaldo akiubadili kuwa wake kwa kufikisha mabao 100 kwenye mashindano ya Ulaya anabaki kuwa jina la kipekee ambalo wino utatumika wa moto kuliandika kwenye vitabu vya soka.

Huyu ambaye wengi wanamfahamu Jorge Mendes kama binadamu anayemwongoza lakini ukweli unabaki kuwa kuna mwanaume anayeitwa Ricky Regufe ambaye aliamua kuachana na soka ili akasome namna ya kuendesha maisha kama ya akina Ronaldo na akafanikiwa kuokota almasi hii ya Madeira na kuifuta vumbi.

Huyu ndiye haswaa anayeamua mpaka mtindo wa kunyoa wa Ronaldo, huyu ambaye Ureno ilibidi wamuweke kwenye orodha ya watendaji wao ili aende kwenye mashindano ya mataifa Ulaya na Ronaldo. Anaishi Ronaldo, anapumua na kula Ronaldo.

Lakini ni Ronaldo huyu ambaye vitabu itabidi viandike kuwa ni mwanadamu pekee aliyezisalimu nyavu kwenye mashindano ya kombe la dunia ya 2006, 2010, 2014 na mashindano ya mataifa ya Ulaya ya 2004, 2008, 2012 na 2016 ambako alikuwa bingwa. Hakuna binadamu mwingine anayepumua aliyefanya hili.

Dunia imesahaulishwa na mabao 100 ya Ulaya kuwa huyu ndiye mwanadamu anayeongoza kwa hattricks kwenye La Liga alizofunga kwa wakati mfupi kuliko mtu mwingine yoyote, anazo 32 juu ya wote.

Kama kuna upande Mbappe atatakiwa kuuwaza pia ni kuwa mwanaume huyu amesimamisha dunia kwenye mitandao ya kijamii, watu wanamfuata kuliko mwanamichezo yoyote Yule, alipewa na muonekano huyu.

Aliishi kwenye historia za kina Figo, Nuno Gomes, Pauleta, na Eusebio lakini alivuka bahari ya shamu na fimbo ya Musa na kuzitenganisha zote hizi na kuweka zake, anaongoza kwa magoli kwa nchi hiyo.

Mashabiki wa Madrid waliishi katika zama za Raul, Alfredo Di Stefano na akina Carlos Santillana ambao wote waliishi Madrid kwa zaidi ya miaka 10 wakifunga wanavyojisikia, Ronaldo alifika na hakuacha hata jiwe moja likiwa halijageuka, ilimchukua miaka 6 tu kuwa mfalme.

Lakini huyu ndiye mchezaji aliyeshinda vikombe vyote katika ngazi ya klabu, na tuzo zote zinazohusu wachezaji akiwa na vilabu viwili tofauti, hakuna mwingine aliyewahi kufana hili. Ni huyu Ronaldo ambaye mama Dolores aliyekuwa mpishi na mzee Dinis ambaye alikuwa mtunza bustani waliamua kuongeza mtoto wa mwisho katika familia kumbe hawakujua wanaongeza malaika kwenye soka.

Bahati mbaya hata baba yake aliyepoteza imani na maisha na kufa kutokana ulevi na kuathiri hakufanikiwa kushuhudia ubora wa huyu malaika, hakufanikiwa kuziona nyakati mabazo hotel maarufu za Pescana ni za mwanae, nyakati ambazo sanamu maarufu Hispania ni ya mwanae na nyakati ambazo hata uwanja wa ndege wa kimataifa umepewa jina la mwanae.

Inawezekana Ronaldo akawa na makumbusho nchini Ureno lakini Mbappe anatakiwa kufahamu kuwa makumbusho ya kudumu Ronaldo amejenga vichwani mwetu na hilo la mabao 100 ni mojawapo tu. Ronaldo alikula nyama alivyojisikia, tungependa uende mbali zaidi ule na mifupa, lakini nina mashaka kama meno thabiti unayo.

Kumuishi huyu sio jambo dogo, Mbappe ana miguu inayofaa, ana ubongo wenye rutuba na ana kila kitu cha kuwa mchezaji bora. Lakini kuna jambo moja tu ambalo huwa ni gumu siku zote, kufuta mhuri wa moto na Ronaldo ameshaweka huu. Ahsante Ronaldo na Karibu Kylian Mbappe, macho yetu yatakuwepo kwenye Tv kwa miaka 15 ijayo.

Viewing all 676 articles
Browse latest View live


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>