Quantcast
Channel: Makala – ShaffihDauda
Viewing all articles
Browse latest Browse all 676

Mchawi wa Zidane na Perez ni Kinyago cha Gazzaniga

$
0
0

Kule Rhodes magharibi mwa ufaransa alizaliwa jamaa mmoja alikuwa na akili sana.

Jamaa huyu alikuwa akichonga vinyago vyake ambavyo vingi vilikuwa na muonekano wa umbo la mwanamke. Jamaa huyu aligundua kinyago chake ambacho aliiga muonekano wa kinyago cha kigiriki kijulikanacho kama Nike ya Samothrace ambacho hapo awali kiligundulika karne ya pili wala hakikukamilika.

Image result for nike samothrace

Kinyago kile cha Nike kilikuwa na Mabawa lakini kichwa kilikuwa kimekatwa.

Mchongaji huyu sio mwingine bali ni bwana Abel Lafleur. Kinyago kile kikapewa jina la Jules Rimet maana alipigania kuhakikisha kuwa kinyago kile kinapata heshima kubwa dunia.

Image result for abel lafleur sculpteur

Tukiachana na kinyago mwaka huu mwezi wa 5 tarehe 23 kule Mjini Kyiv wanaume watahangaika kupigania kinyago cha bwana Hugo Meisl. Hugo Meisl zamani sana alianzisha kombe la Challenge ambalo kwa sasa mnaliita uefa champions league au kwa kingereza Ligi ya mabingwa barani.

Related image

Sasa tuendelee na kinyago cha Lafleur. Baada ya kinyago cha kwenda Uruguay, kisha baadae kikapelekwa Italia, Ujeruman magharibi kisha mwaka 1958 kikaplekwa Brazil. Mwaka 1966 kinyago kile kikapelekwa England. Kikiwa nchini kule wadokozi wakakiiba.

Related image

Kinyago kile baadae kilipatikana na mbwa ajulinae kama Pickles ndiye aliye aligundua mahali kilipofichwa na mwizi. Baadae kwa mara ya pili kinyago kilipelekwa brazil mwaka 1970 kiliibiwa na hakikupatikana kabisa.

Related image
Pele akiwa na Kinyago cha Bwana Abel Lafleur

Cristaino Ronaldo (33) ni Mreno, Ramos Sergio (32(, Tony Kroos (28), Dany Carvajal (27), Rafael Varane (25), Luka Modric (32), Casamero (26), Marcelo (30). Hawa ni wachezaj tegemezi kwenye vikosi vyao vya timu za taifa. Hawa tunatarajia kuwaona katika michuano ya kombe la dunia wakiwa kama wachezaji muhimu . Nchi kama Brazil, Ufaransa, Ujerumani na Hispania ukiachilia mbali Ureno hizi ni nchi ambazo zinatarajiwa kupigania kombe la dunia tena kila timu ikiwa na uhakika wa kombe hilo.

Image result for abel lafleur sculpteur

Baada ya kinyago cha Lafleur kupotea kabisa, alijitokeza muitaliano mwingine Silvio Gazanigga ambaye alipeleka vinyago viwili kule uswisi.

Image result for silvio gazzaniga

Kinyago kimoja kilikubaliwa na kingine kikakataliwa. Kinyago hiki kinawatoa udenda Messi na Ronaldo.

Kinyago cha awali kilikuwa kilogramu 5 za dhahabu.

Related image

Kinyago hiki kipo kule Urusi mwaka huu

Kama kuna fainali za uefa zimekaa kinafiki sana ni hizi za mwaka huu. Asilimia 90 ya wachezaji wa kikosi cha kwanza cha Real Madrid wana nafasi kubwa katika timu zao za taifa kutwaa kinyago cha Gazzaniga. Kumetokea sintofahamu mbaya zaidi ambayo imesababishwa na wachezaji muhimu kupata majeraha. Chamberlain, Koscienly pamoja na Alves huenda wakaleta hofu kubwa kwaa baadhi ya wachezaji katika mchezo huu,

Image result for liverpool vs real madrid

Ni dhahiri kwamba kombe UEFA ndilo kombe rahisi Zaidi kwa wachezaji wa Madrid na Liverpool kulipata kuliko kombe lingine lolote kuanzia sasa mpaka mwakani tarehe kama leo.

Related image

Namaanisha kuwa kombe la dunia utacheza takribani michezo saba kulipata lakini kwa tarehe 23 watacheza dakika 90 tu na za nyongeza.

Kimahesabu ni rahisi Zaidi kwa baadhi ya wachezaji waliverpool kujituma kuliko hawa wa Madrid ambao wamelitwaa kwa miaka miwili mfululizo tena na wengine wakiwa wamekwisha litwaa mara 3 huku wakijua wazi huenda kombe la dunia la mwaka huu likawa kombe lao la mwisho.

Related image

Wachezaji wa kihispania tayari wamekwisha kutwaa kombe la dunia na hapa namzungumzia Ramos.

Hawa wengine ndio kombe lao la kwanza au la pili. Sioni kama kuna wachezaji wengi ndani ya Liverpool ambao tunaweza kusema watacheza kwa tahadhari ili kuzipigania timu zao za taifa. Mchezaji ambaye kidogo ana uhakika na taifa lake kwamba sio wasindikizaji ni Roberto Firmino na Brazil yake. Waliobakia wote hawa wanajua kabisa hawawezi kutwaa kombe la dunia na hata kama wakishiriki nafasi hiyo ni ndogo kwao huku baadhi ya wachezaji tegemezi wakiwa hawapo kabisa kombe la dunia.

Jina Nchi Mshiriki Nafasi KD Nafasi yake
Mo Salah Misri Ndiyo Finyu sana Tegemezi
Roberto firmino Brazil Ndiyo kubwa Kawaida
Virgi V. Djik Uholanzi hawapo 0 0
Sadio Mane Senegal Ndiyo Finyu mno anategemewa
Wijnaldum Uholanzi hawapo 0 0
Dejan Lovren Uholanzi hawapo 0 0

Vijana wengine ni kama Andrew Robertson, pamoja na Alexander Arnold ambao timu zao za taifa hazina nafasi katika kombe la dunia. Roberto Firmino, Emre Pamoja na Jordan Henderson hawa ni moja ya watu watakaocheza kwa tahadhari kwani timu zao za taifa zina nafasi kubwa pia.
James Milner hategemewi katika kikosi cha England tena. Kilichobaki ni kwa Liverpool kujitoa kwa damu na moto.

lakini Real Madrid bado wana uzoefu mkubwa.

Image result for liverpool vs real madrid

Nimeona Ronaldo akiwekwa benchi baadhi ya michezo. Mwalimu Zidane ana akili sana. Anajua wazi kuwa hata Ronaldo mwenyewe hawezi kubeti kuwa Ureno atatwaa ubingwa huo wa Dunia. Anaamini kuwa Ronaldo atajitoa kuhakikisha kuwa anatwaa taji la 3. Ronaldo analenga Ballon d’Or na anajua fika pia Argentine ni tia maji tia hivyo hahofii kama Messi atampiga bao kwa kunyakua taji hilo

Image result for liverpool vs real madrid

Haoni kama Messi anaweza kutwaa kinyago cha Gazzaniga. Ni kazi kidogo hasa kwa Argentine hii iliyohaa vitimbwi kila uchao. Anajua mbaya wake ni Mo Salah na sio Messi kwa sasa. Perez na Zidane wala hawana wazo lolote kuhusu Kombe la Dunia, wao fikra zao ni UEAF tu. ni kweli maana kama watakosa UEFA mwaka huu itakuwa wametoka kapa. Ni aibu kwao. Hata kama Hispania au Ureno itatwaa Ubingwa wa Dunia au Ufaransa itakuwa fedheha kwa Madridi kutoka mikono mitupu. Lakini wachezaji wake watakiwaza kinyago hiki. Huenda Ronaldo hana hata wasiwasi lakini vipi kuhusu wachezaji wengine? mimi sijui ila tutaona mengi katika fainali hizo.

Makala hii imeandaliwa na Privaldinho unaweza pia kunifollow Instagram kwa jina hilo hilo.


Viewing all articles
Browse latest Browse all 676

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>