Quantcast
Channel: Makala – ShaffihDauda
Viewing all articles
Browse latest Browse all 676

Guardiola amsifia Zlatan

$
0
0

Sehemu ya 9

simulizi ya maisha ya Zlatan

Ibra alipoona kiwango chake kitaoza alituma barua ya kuomba kuuzwa. Lakini Guardiola alitaka kuficha ficha mambo kwa kudai kuwa Ibra haondoki. Ibra akatamka hadharani kuwa kama hatomruhusu kuhama atampiga teke waziwazi.

Baada ya Vitisho vile mkurugenzi msaidizi wa Barcelona Bwa. Carles Villarubi akasema Kumsajili Zlatan ilikuwa kosa kubwa mno. Zlatan akajibu kuwa kama walinisajili kimakosa kwanini Laporta hakusema hayo tokea mwanzo?

Najua wanajua wazi kuwa shida yangu kubwa ilikuwa ni ugomvi na mwanafilosofia wao waliyemuita kocha. Sikuwa na muda kupoteza nikiwa benchi, nilimpa nafasi achague moja, nimvunje au aniruhusu niondoke zangu.

Gaurdiola hakuwa mtu wa waandishi wa habari sana. Maisha yake ya ndani ya klabu yalibakiwa uwa ndani ya klabu. Hakutaka kabisa kuweka mambo wazi.

Alipoulizwa kuhus Ibra alisema kuwa

Ibra ni mchezaji wa muhimu katika kikosi changu wala siwezi kusema kuwa sithamini mchango wake. Amesaidia timu kupata alama 99, tumefika hatua ya nusu fainali ya UEFA ni jambo la keri kwetu. Kabla Zlatan haja hapa nilijua tayari ni mchezaji mkubwa na mwenye uwezo mkubwa, alipofika hapa niligundua kuwa ni mchezaji mwenye kiwango cha hali ya juu, zaidi ya hata nilivyokuwa nadhania hapo awali.

Amekamilika kwa kila idara na anajituma sana. Kila mara amekuwa na uchu wa kutaka kufanikiwa.
Shida kubwa aliyokutana nayo hapa labda nisema tu presha za media na kadhalika. Na si rahisi kufanana na kila mtu. Kupishana ni sehemu kubwa ya wanaume. Nikisema sio mchezaji mzuri nitakuwa mnafiki. Maisha ya hapa Uhispania ni tofauti kidogo na kule italia itsoshe hii ni klabu kubwa.

Pia aliongeza kuwa:

Ukiwa mshambuliaji ukipoteza mpira ukiwa ligi ya italia ni tofauti kidogo na ukipoteza mpira hapa kwetu. Mshambuliaji hapa kwetu anacheza kama kiungo ili kuondoa magepu uwanjani hasa kwenye suala la kukaba. Sisi tunakaba kama timu na sio kama jukumu la mchezaji Fulani.

Marehemu Yohan Cruyjf aliwahi kusema kuwa Zlatan haendani kabisa na mfumo wa Katalunya.

Zlatan akishangazwa sana na kauli ile akasema “naona huyu mzee nae anazeeka vibaya, kama aliona mpira wa kihispania haukunifaa kwanini hakuwashauri bodi yao isinisajili?

Unajua sielewi kabisa haya maneno yanatoka kwa mchezaji mkubwa na kocha mkubwa kama huyu mholanz. Hawa wanakaa pamoja kila mara kucheza karata, je hawakuwahi hata kushauriana kuhusu usajili wangu?Yaani badala aishauri klabu yeye anakuaja kuongea na waandishi wa habari na kunijadili mimi?

Hii ilikuwa simulizi ya njia ya mafanikio ya Zlatan. Makala ya mwisho itaelezea safafi yake kurudi italia na mwisho itakuwa sehemu ya maisha yake ufaransa na England. Makala hii imeandaliwa na Privaldinho (Instagram)


Viewing all articles
Browse latest Browse all 676

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>