Rekodi zinavyomtumbukiza Hary kane kwenye dimbwi la unafiki na uroho.
Mkurugenzi wa PFA (Shirikisho la Mpira ligi kuu England) amejikwaa kwa Familia ya Harry Kane. Waingereza ni wepesi sana kulalamikia mambo madogo kwa kujenga hoja nzito kwa kutumia njia nyepesi.
Mkurugenzi huyu Bwana Ben Purkiss alitoa boko wakati wa utoaji tuzo za ligi kuu England.
Aliongea kimasihara tu na sidhani kama alikuwa siriazi kiasi kile. Nanukuu
Harry Kane ni mchezaji wa kiwango cha juu sana, ana uwezo wa kufunga magoli kwa jitihada zake bila kutegemea magoli ya mpira uliomgusa.
Nukuu hii ililenga zaidi sakata la Harry Kane kulalamikia FA kuwa goli alilopewa Ericksen (mchezaji mwenzake) lilikuwa lake kwani aliuparaza mpira ule. Waingereza hawashindwi jambo. Wakasema msaada wa video umeshindwa kuonesha kama aliugusa au lah! Nilicheka sana. Video niliyo nayo kwenye simu yangu inaonesha wazi Kane hakuugusa mpira ule. Hauoneshi kama kuna namna yeyote ambayo Kane ameugusa mpira.
Nimemsikiliza vizuri kocha wao mkuu Mauriccio Pochettino. Ameweka unafiki pembeni. NakuuGoli limetupa sisi alama tatu, yote yaliyotokea baada ya tukio lile mimi hainihusu, nafundisha kwa manufaa ya timu, sijali nani aliyefunga, awe Delle Alli, iwe Ericksen au Son hilo kwangu sio la muhimu zaidi, ila alama tatu.
Kuhusu kukata rufaa kwa goli lile sio maamuzi yangu, ni maamuzi ya timu, wala sikushirikishwa kuhusu maamuzi hayo maana nisingechangia lolote. Nina uhakika Kane na Ericksen wamekubaliana hilo ila hawakunifuata na kuniomba ushauri. Hilo lipo kwao na kwa ajili ya klabu yao mimi hayanihusu.
Kwa kauli hizi ni wazi kwamba kuna uwezekano kukatokea mpasuko mkubwa kwa klabu na kwa timu ya taifa pia.
Maamuzi kama haya Kocha mkuu hashrikishwi maana yake inaleta hewa chafu ndani na nje ya timu. Kocha amekwisha onesha msimamo wake wazi kuwa yeye haoni umuhimu wa hayo mambo ya namna hiyo.
Harry Kane mimi nina imani kubwa ni mchezaji mkubwa mbaye anaweka maslahi ya timu mbele. sijajua kipi kimemkuta. labda ni PRESHA. Ninachokiona hapa kuna mkono wa Waingereza na watu wengine wa Pembeni. Roho zinawauma ni kwa namna gani kepteni wao ananyanyaswa na waraabu. Yeye mwenyewe anaona aibu. kvipi nahodha anateswa na wageni ndani ya Ardhi yao.
PATA KIFURUSHI
Orodha ya wafungaji Bora kutoka England tokea EPL ianzishweJina | Mwaka | Klabu | Idadi |
Teddy Sheringham | 1992-93 | Nottingham Forest / Tottenham Hotspur | 22 |
Andy Cole | 1993–94 | Newcastle United | 34 |
Alan Shearer | 1994–95 | Blackburn Rovers | 34 |
Alan Shearer | 1995–96 | Blackburn Rovers | 31 |
Alan Shearer | 1996–97 | Newcastle United | 25 |
Dion Dublin | 1997–98 | Coventry City | 18 |
Michael Owen | 1997–98 | Liverpool | 18 |
Chris Sutton | 1997–98 | Blackburn Rovers | 18 |
Kevin Phillips | 1999–’00 | Sunderland | 30 |
Harry Kane amekuwa mfungali bora kwa miaka miwili mfululizo (2016-24, na 2017-29). Inaonekana kama ana uchu mkubwa wa kufukuzia rekodi ya Alan Shearer ya kuwa mfungaji bora kwa miaka miatatu mfululizo. Aliamini hilo. mara ya mwisho England kutoa mfungaji bora ilikuwa mwaka 2000 na ilibidi wasubirie miaka 16 ndipo apatikane mfungaji bora muingereza. Lakini shida ya huyu aliyepatikana na uchu wa rekodi za hapo awali ambazo zinamfanye awe mroho hadi kwenye magoli ya wenzake.
Alifahamu fika Sergio Aguero ana kuwa na majeraha ya mara kwa mara na alijua ujio wa Gabriel Jesus utampa Aguero wakatiu mgumu. Cha ajabu amekua kidudu mtu kutoka Misri ambaye hakuna aliyemtegemea kabisa kama angeleta changamoto kubwa kiasi kile. hata kama ingekuwa ni wewe lazima uchanganyikiwe.
Nimejarbu kuangalia kwa namna gani watu wameguswa? Kila mtu ameonesha kuwa kile kilichofanywa ni kitendo cha kijinga.Vardy Jarmie licha ya kwamba ni mwingereza mwenzake aliweka vialama vya kicheko kwenye ukarasa wake wa Twitter kuonesha kuwa kile kilichofanywa ni cha kijinga.
Wachezaji wa Liverpool kama Karius na Milner nao waliweka maneno ya kashfa kwenye kurasa zao. Kosa alilolifanya Harry Kane ni kitendo cha yeye kujirekodi video na kusema kwamba
“Nina furaha na ushindi, na ninafurahia kufunga, nina apa kwa niaba ya maisha ya mwanangu lile goli ni langu, ule mpira nimeugusa, wakiamua kusikiliza maneno yangu sawa, wasiponisikiliza pia siwezi kufanya lolote.
Baada ya hapo walio wengi wamemjia juu sana
Alan Shearer “natashangaa endapo watanipa magoli yangu 9 ambayo hawakunipa” {usisahau kwamba Harry Kane alikuwa anafukuzia rekodi yake ya ufungaji bora kwa miaka mitatu mfululizo.}
Lee Nelson “Harry Kane amedai kuwa mwanangu wa kwanza ni wakwake”
Mo Salah “waoooooooo kweli?
Gary Lineker “Goli la Mandzukic amepewa Kane”
Jarmier Vardy “akacheka tu”
Athari kubwa ipo sana kwa huyu nahodha wa Uingereza. wanajiandaa na kombe la dunia lakini vituko vya namna hii vinaleta dosari kubwa. Ni wazi anachowaza sio kile ambacho sisi tuna waza.
Mbaya zaidi baada ya kushindwa kufunga goli lolote katika mchezo wa nusu fainali ya kombe la FA dhidi ya Man United, shirikisho la Soka England (FA) liliweka picha ya utani iliyomuonesha Smalling huku ikiambatanishwa na maneno kwamba kuna nini mfukoni mwako Chris?kisha inaonekana kama Smalling anashangaa
Pochettino aliwajia juu sana FA akidai ule ni udhalilishaji kwa Harry Kane, kabla FA hawajaomba msamaha. Tayari Vardy ameingia vita ya chini kwa chini na Kane, kilichobaki ni vita kwenye vyumba vya kubadilishia nguo.
Mwisho ni hili la mkurugenzi wa FA ambalo nimeanza nalo hapo mwanzo. Mkurugenzi huyu ameonekana kumtania Kane katika sherehe za utoaji Tuzo. Familia ya Harry Kane imemjia juu kwani haikupendezwa kabisa na Purkiss. Baadhi ya wadau wa soka walimshutumu Purkiss na walimtaka aombe radhi hadharani lakini aligoma. Alijibu akasema
“siwezi kuomba msamaha hadharani, mimi na Kane tunaongeamara kwa mara. Nimekwisha kutana nae, nimeshamweleza dhamira yangu ilikuwa wapi? Aliridhika kwa maelezo yangu na tumekwisha malizana katika hilo.
Nilimwambia kuwa ile ilikuwa heshima kubwa sana kwake mmi kumtaja katika hotuba yangu kwani nimeheshimu mchango wake kwa taifa hil. Nilionesha ni kwa namna gani yeye ni bora.
Nilimsihi kuwa lengo langu lilikuwa kumuonesha mimi nimemjua yeye kabla hajawa mchezaji mkubwa, nilimfahamu akiwa anafunga magoli mengi ambayo hata FA hawakukaa kujadili kama ni lake au sio lake.
Nilimkumbusha kuwa yeye ni mchezaji mkubwa England, lengo sio kumkwaza ila nilichukizwa sana kwa namna mchezaji wetu bora analeta gumzo kwa goli moja tu.
Makala hii imeandaliwa na Privaldinho unaweza pia kunfollow Instagram kwa jina hilo.
Je unamtazamo wowote kuhusu mchezo wa Simba dhidi ya Yanga? basi nitumie kwa ufupi jina lako unapotokea na ushauri wako kipi kifanyike ili timu yako ishinde katika pambano hilo kisha nitazipost hapa hapa. kwa ufupi sana kwenye namba 0763370020.