Quantcast
Channel: Makala – ShaffihDauda
Viewing all articles
Browse latest Browse all 676

Juventus wamchanganya Zlatan

$
0
0

Hii ni sehemu ya saba ikiwa ni mwendelezo wa makala kuhusu Historia ya Maisha ya Zlatan.

Baada ya migogoro ya Muda mrefu Ajax Zlatan atimkia Juventus.

Fabio Capello alipokuwa As Roma alimfukuzia sana Zlatan alipokuwa Malmo lakini juhudi ziligonga mwamba. Ugumu wa maisha ya Zlatan klabu Ajax yalimpa Capello upenyo wa kumpata Zlatan. Wakati huu Fabio Capello alikuwa mkufunzi wa Juventus. Juhudi zake za kunasa kalamu ya Zlatan zilizaa matunda. Mnamo mwaka 2004 Zlatan alijiunga Juventus kwa ada ya Euro 16.

Maisha yake Juventus msimu wa kwanza hayakuwa magumu ukilinganisha na klabu yake ya zamani ya Sjax. Msimu wa kwanza alitia kimyani magoli 16. Real Madrid walitangaza kitita cha Paundi Milioni 70 kupata huduma za Ibra. Mino Raiola alisema kiasi kile kisigetosha hata kumlipia gharama zake za usafiri ili kukamilisha dili hivyo aliwakebehi kuwa ada ile ndogo mno. Capello aliwaambia wandishi wa habari kuwa Zlatn alipotua Juventus alikuwa hawezi kupiga kwa nguvu mashuti.

Alimpa jukumu la kuwa na muda wa zaida kujifunza kupiga mashuti akiwa pekee yake kwa muda wa masaa mawili kila mara baada ya mazoezi ya ujumla. Mwaka 2006 Juventus waliingia kwenye kasumba mbaya sana ya upangaji wa matokeo. Madhara yake yalikuwa makubwa kiasi cha kushushwa daraja.

Habari za chini ya kaptea zilifumua siri kuwa Mino Raiola hakuwa tayari mteja wake kuendelea kucheza Serie B. Fununu zile zilipomfikia Mino alikanusha madai hayo na kusema kwamba makubaliano ya kuuzwa kwa Zlatan yalishafanywa miezi 6 kabla ya hapo.

“November 2 2005 Juventus iliifunga Bayern magoli 2-1, Zlatan alitolewa nje kwa kadi nyekundu dakika ya 89, Luciano Moggi Mkurugenzi wa Juventus alitoka kwa hasira kwenye jukwaa lake, akaenda moja kwa moja mpaka vyumba vya kubadilishia nguo, akamfokea sana Ibra na kumweleza kuwa aondoke klabuni kwake mara moja, kisha akanitafuta mimi akaniambia mwambie Ibra hatumtaki klabuni hapa na anaweza kuvunja mkataba wake mara moja” alisema Raiola.

Raiola hakumwambia chochote Ibra, kwa sababu alijua tu kwamba Zlatan wangegombana mkataba ungevunjwa kwa makubaliano ya pamoja hivyo wasingepata kitu, lakini kama Juventus wangevunja wenyewe mkataba basi wangemlipa Zlatan Milioni 90.

Nilinyamaza makusudi kama sijui kuna kitu kinaendelea kwani nilifahamu ukorofi wa Zlatan wangegombana na bosi na dili lingeharibika. Nilijua Inter wapo tayari kutoa kiasi kikubwa kumnasa. Sikutaka mambo yaende kwa fujo”

Alisema Raiola

PATA KIFURUSHI

 

Jina Kamili Lucciano Moggi
Kuz, Mahali Monticiano Siena
Cheo Mkurugenzi Mtendaji Juventus (1994-2006)
skendo Ya Upangaji wa matokeo 2005
Adhabu Kifungo cha maisha kutokujihusisha na soka

 

Mino anathibitisha kuwa hakuna mnyama anayeweza kumzuia Zlatan kufanya anachojisikia. Baada ya Juventus kushusha daraja Mino aliitishia kuifungulia kesi kwakuwa walikuwa hawataki kumuuza.

Matatizo waliyoyapata yangewafanya kupoteza wachezaji wengi. Ni Moggi tu aliyekuwa tayari Zlatan aondoke. Bodi nzima ilianza kuvurugana. Kesi ya Moggi ilimchanganya zaidi maana alijua wazi atafungiwa kujihusisha na soka maisha yake yote. Alichotaka ni Zlatan aondoke Juve kabla ya hukumu haijatoka.

Baada ya skendo ya Calciopoli Moggi alikuja kwenye mkutano na wachezaji, alikuwa amevaa vizuri sana, alionekana dhaifu, kwanza kila mtu klabuni alikuwa anamuogopa, ni mtu mwenye ushawishi na nguvu kubwa klabuni hapo, cha ajabu alipoanza kuongea alilia sana, nilishangazwa sana, sijawahi kuona mtu mwenye heshima kama Yule akilia, alinikata sana maini, niliogpa sana hadi tumboni langu lilianza kuvurga, nilihisi nimepigwa ngumi za tumboni. 

Kilichoniuma ni kwamba mimi siamini kama tulitwaa mataji au kushinda michezo kwa sababu ya tulibebwa na waamuzi, hapana, tulikuwa na uwezo na tulishinda kwa sababu tulijituma na si vinginevyo.

Hayo yalikuwa maneno ya Zlatan alipoulizwa kuhusu Moggi.

Takwimu za Zlatan Juventus.

Mwaka Michezo/dakika Magoli/assisti Njano Nyekundu
2004-05 45/ 3,927 16/5 7 0
2005-06 47/ 3,271 10/2 5 1

msimu wa kwanza alicheza michezo 10 ya UEFA bila kufunga bao lolote.

KIKOSI CHA JUVENTUS WAKATI ULE 2005

Position Player
1 Italy GK Gianluigi Buffon
2 Italy DF Alessandro Birindelli
3 Italy DF Giorgio Chiellini
4 France MF Patrick Vieira
6 Croatia DF Robert Kovač
7 Italy DF Gianluca Pessotto
8 Brazil MF Emerson
9 Sweden FW Zlatan Ibrahimović
10 Italy FW Alessandro Del Piero (NAHODHA)
11 Czech Republic MF Pavel Nedvěd
14 Italy DF Federico Balzaretti
15 Italy DF Domenico Criscito
16 Italy MF Mauro Camoranesi
17 France FW David Trezeguet
18 Romania FW Adrian Mutu
No. Position Player
19 Italy MF Gianluca Zambrotta
20 Italy MF Manuele Blasi
21 France DF Lilian Thuram
22 France GK Landry Bonnefoi
23 Italy MF Giuliano Giannichedda
24 Uruguay MF Rubén Olivera
25 Uruguay FW Marcelo Zalayeta
27 France DF Jonathan Zebina
28 Italy DF Fabio Cannavaro
32 Italy GK Christian Abbiati (Mkopo kutoka Milan)
43 Italy GK Claudio Scarzanella
44 Italy FW Michele Paolucci
50 Cuba MF Samon Reider Rodríguez
60 Italy MF Claudio Marchisio

Amini usiamini hakuna dhuluma inayodumu. Unajua kwanini Zlatan alimvunja kwa makusudi Raphael Van Da Vaart pale Ajax? Basi Lucciano Moggi ndiye mhusika mkuu. Kivipi? Tukutane makala ijayo.

Makala hii imeandaliwa na Privaldinho Pia unaweza kunifollow Instagram kwa jina hilo hilo. usisahau pia kusubscirbe Youtube Chanel ya Dauda TV

 


Viewing all articles
Browse latest Browse all 676

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>