Kumeanza minong’ono na ukosoaji kuhusu kocha wa Yanga George Lwandamina kutokana na matokeo ya timu hiyo siku za hivi karibuni, baadhi ya wadau wa soka wanaonekana kutoridhishwa na mwenendo mabingwa watetezi wa taji la VPL.
Lwandamina alitambulishwa rasmi na makamu mwenyekiti wa klabu hiyo mbele ya waandishi wa habari baada ya kusaini mkataba wa kuitumikia Yanga akirithi nafasi ya Hans van Pluijm ambaye alipewa nafasi ya ukurugenzi wa ufundi ndani ya klabu hiyo.
Lwandamina alichukua timu katikati ya msimu wakati huo yanga ikiwa nafasi ya pili ikiwa na pointi 33 nyuma ya Simba kwa pointi mbili na aliisaidia Yanga kutetea taji la VPL na kuweka rekodi ya kulitwaa kombe hilo kwa mara ya tatu mfululizo.
Wakati Lwandamina anachukua mikoba ya Hans pale Yanga tayari mechi za mzunguko wa kwanza zilikuwa zimemalizika na yeye alianza kucheza ligi kuanzia raundi ya pili ya msimu uliopita.
Mechi tano za Lwandamina za mwanzo wa msimu mpya (2017/2018)
Msimu huu ndio mpya kwa Lwandamina tayari ameshakiongoza kikosi hicho katika mechi tano za msimu huu ambapo amefanikiwa kushinda mechi mbili, sare tatu huku akiwa bado hajapoteza mchezo. Timu ipo nafasi ya sita ikiwa na pointi tisa ikiwa imefunga magoli manne na kuruhusu magoli mawili.
- 27/08/2017 Yanga 1-1 Lipuli
- 10/09/2017 Njombe Mji 0-1 Yanga
- 16/09/2017 Majimaji 1-1 Yanga
- 23/09/2017 Yanga 1-0 Ndanda
- 01/10/2017 0-0 Mtibwa
Mechi ya sita Yanga watacheza ugenini dhidi ya Kagera Sugar (14/10/2018) uwanja wa Kaitaba, Bukoba mkoani Kagera.
Kagera Sugar ?? Yanga
Mechi tano za Hans van Pluijm za msimu mpya (2016/2017)
Ktika mechi sita za kwanza za Yanga msimu mpya wa 2016/2017 ambapo timu hiyo ilikuwa chini ya Pluijm, timu ilikuwa imeshinda mechi tatu, sare moja na kupoteza mchzo mmoja. Hans alikusanya pointi 10 katika michezo mitano, timu ilifunga magoli nane na kuruhusu bao moje pekee.
- 28/08/2016 Yanga 3-0 African Lyon
- 07/09/2016 Ndanda 0-0 Yanga
- 10/09/ 2016 Yanga 3-0 Majimaji
- 17/09/2016 Mwadui 0-2 Yanga
- 25/09/2016 Stand United 1-0 Yanga
Mechi ya sita Hans aliiongoza Yanga kucheza dhidi ya Simba na kulazimishwa sare ya kufungana 1-1 uwanja wa taifa.
01/10/2016 Yanga 1-1 Simba
Kwa aina ya kikosi cha Yanga kilivyokuwa enzi za Pluijm na kilivyo sasa wakati wa Lwandamina kwa kuzingatia wachezaji waliokuwepo enzi za Pluijm na waliopo sasa, pamoja na hali ya majeruhi, unadhani yupi ni kocha bora kati yao?
Unaweza kuchangia maoni yako kwa kudondosha comment yako hapo chini juu ya kile unachokiamini kuhusu ubora wa makocha hao (Lwandamina vs Hans van Pluijm)