Na Baraka Mbolembole
Kocha huyu raia wa Zambia aliisimamia Yanga kwa mara ya kwanza katika mchezowa ligi kuu. Lwandamina aliyechukua nafasi ya Mholland,Hansvan der Pluijm ambaye sasa ni Mkurugenzi wa ufundi klabuni hapo alianzana kikosi kile kile ambacho kimezoeleka.
Deo ‘Dida’, Juma Abdul, Mwinyi Hajji,Kelvin Yondan, Vicent Bossou, Thaban Kamusoko,SaimonMsuva, Haruna Niyonzima, Amis Tambwe,Donald Ngoma na Deus Kaseke walianza vs JKT Ruvu na kumsaidia kocha huyo kuanza VPL na ushindimzuri wa 3-0 dhidi ya ‘vibonde’hao wa ligi.
Nilichokiona kutoka kwa kocha huyo ni uwezo wa kuusoma mchezo, kuwasoma wapinzani wake na kufuatilia ufanyaji kazi wa wachezaji wake ndani ya uwanja. Sub yake ya kumtoa mshambulizi,Tambwe na kumpa nafasi kiungo,Said Juma Makapu awali ilionekana kama vile alichemsha lakini alijua alichofanya.
Haruna Niyonzima alisogea juu zaidi kutoka namba 8 na kwenda namba 10. Alifanya hivyo baada ya kugundua kipaji cha upigaji wa pasi za mwisho alichonacho Mnyarwanda huyo ambaye alipiga pasi mbili za magoli yaliyofungwa na Msuva mara baada ya kupelekwa namba kumi. Nadhani bado ana mengi ya kuifanyia Yanga lakini mechi yake ya kwanza VPL ilikuwa nzuri kwa kila shabiki wa timu yake.
Juma Kaseja
Nahodha wa zamani wa timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’na klabu ya Simba SC, golikipa Juma Kaseja alicheza mchezo wake wa kwanza wa ligi kuu Tanzania Bara akiwa na timu yake mpya-Kagera Sugar FC siku ya Jumamosi iliyopita katika uwanja wa Sokoine, Mbeya na kuonesha kiwango cha juu.
Mshindi huyo wa mataji 7 ya ligi kuu, alikuwa ‘kizuizi’ kikubwa dhidiya washambuliaji wa timu yake ya zamani-Mbeya City FC katika mchezo uliomalizika kwa suluhu-tasa. Licha ya baadhi ya watu kuhoji usajili wake na wengine kufikia hatua ya kusema ‘mlinzi huyo wa goli amezeeka’, Kaseja mwenye miaka 31 hivi sasa aliwajibu kwa kiwango chake bora ndani uwanja.
Alikuwa makini muda wote wa mchezo, aliwapanga vizuri walinzi wake na hakuacha kuwapigia kelele pindi alipoona wakifanya makosa. City walishindwa kumtumia Kaseja msimu huu kufuatia kipa huyo kugoma kujiunga na kikosi hicho kwa madai hakuwa amelipwa stahiki zake-pesa za usajili.
Kumaliza bila kuruhusu goli tena dhidi timu yake ya zamani ni jambo zuri kwake lakini kocha Mecky Mexime atakuwa na furaha zaidi kwa sabababu amempata kipa bora ambaye ataweza kuongoza vyema safu yake ya ulinzi ambayo iliruhusu magoli 16 katika michezo ya mzunguko wa kwanza.
Daniel Agyei
Nashangaa baadhi ya watu kusema Simba haikustahili kumuacha golikipa Muivory Coast,Vicent Angban wakati kipa huyo alikuwa na makosa mengi kiuchezaji licha ya kuruhusu magoli 8 katika michezo 15 ya mzunguko wa kwanza.Wiki iliyiopita niliuponda usajili wa mshambulizi, Pastory Athanas na uwepo wa makipa wawili wakigeni katika timu hiyo.
Sikuona sababu ya Simba kusaini makipa wawili wakigeni wakati nafasi hiyo wangeweza kuicha wazi au kusaini mchezaji wa nafasi nyingine. Kuachwa kwa Angban kulikuwa ni sahihi kwa maana hakuwa mchezaji mzuri wa mipira ya wazi-krosi,kona na hata mikwaju ya faulo. Pia alikuwa na ‘dharau’ kwa maana mara kwa mara alikuwa akitoka nje ya maeneo yake ya hatari na kucheza mbalina goli lake.
Katika mchezo wake wa kwanza wa ligi kuu siku ya Jumapili, golikipa raia wa Ghana, Daniel Agyei alionesha kiwango kizuri. Mwanzoni mwa mchezo huo dhidi ya Ndanda FC katika uwanja wa Nangwanda, Mtwara, Agyei ilimbidi kufanya kazi ya ziada ili kuzuia timu yake isifungwe goli la mapema kufuatia maelewano’ hafifu’ ya walinzi wake wa kati, Abdi Banda na Mzimbabwe, Method Mwanjali.
Licha ya kuwa na siku chache katika timu hiyo,nyada huyo aliweza kuelewana haraka na safu yake ya ulinzi huku kila shambulizi lililofika kwake alizuia kwa ustadi. Hatemi hovyo mpira, anauwezo wa kucheza krosi,na mipira ya ‘ana kwa ana’. Mchezo wake wa kwanza VPL ulikuwa bora kwa maana uliambatana na ushindi wa 2-0 kwa timu yake.
Abdi Banda
Banda alitishia kuondoka katika timu kama ataendelea kufanywa ‘mchezaji’ wa benchi. Kiraka huyo mwenye uwezo wa kucheza bekinamba 3,4,5 na kiungo namba 6 hakuweza kupata nafasi ya kudumu katika mzunguko wa kwanza na jambo hilo halikuwa akilipenda kwa sababu alikuwa fiti kimwili na kiakili.
Kocha Mcameroon, Joseph Omog alimpanga mchezaji huyo katika beki namba 4 na alichokifanya katika mchezo wa Jumapili dhidi ya Ndanda ni kielelezo tosha ni kwanini mchezaji huyio wa zamani wa Coastal Union alikuwa akilazimisha kuchezeshwa.
Mwanzoni mwa mchezo alionekana kupoteza mawasiliano na patna wake Mwanjali lakini baada ya muda mfupi akatulia na kuonyesha uwezo wake wa kukaba na kuanzisha mashambulizi kwa pasi zakendefu. Kiwango chake kilikuwa bora, alikuwa mtulivu, na alisaidia sana kuwafanya wenzake kucheza kwa umakini wakati ambao Ndanda walikuwa wakifanya mashambulizi.