Quantcast
Channel: Makala – ShaffihDauda
Viewing all articles
Browse latest Browse all 676

Mtazamo VPL: ‘Mkata Umeme’ umewaona Kamusoko, Niyonzima, wewe unakuja vipi?

$
0
0

mkata-umeme-1

Na Athumani Adam

Nilipata nafasi ya kuitazama Yanga kwenye mechi yake ya mzunguko wa pili ligi kuu Tanzania bara siku ya Jumamosi dhidi ya Jkt Ruvu, mchezo ambao Yanga waliibuka na ushindi wa mabao 3-0. Kiungo wa Yanga Haruna Niyonzima alihusika kwenye mabao yote, pia alicheza kwenye kiwango cha hali ya juu.

Pasi yake  ndefu kwenda kwa Msuva ambaye alipiga krosi iliyozaa bao la kwanza baada ya beki wa JKT kushindwa kuokoa mpira na kujifunga  ilikuwa maridadi sana. Bao la pili alipiga krosi kutoka upande wa kulia mwa uwanja, kuelekea upande wa kushoto, kisha mpira ukarudishwa katikati na kumkuta Msuva aliyefunga kwa kichwa cha kuogelea “Diving header”.

Pasi kama hizi ambazo zinalekea kuzalisha mabao wazungu wanaziita “Key Pass”. Kwenye mechi  ya Jumamosi Niyonzima alikuwa na Key Pass takribani sita pamoja na pasi ya bao moja, “Assist”.

Niyonzima alicheza vizuri sana kwenye eneo la katikati akishirikiana na Kamusoko ambaye alicheza kama kiungo wa chini. Kwenye eneo hili la kiungo wa chini au kiungo mkabaji mara nyingi wamezoeleka kucheza wachezaji wenye kutumia nguvu nyingi, wababe uwanjani.

Lakini mpira wa kisasa tumeshuhudia wachezaji laini laini wenye kutumia akili nyingi kuliko nguvu wakicheza kwenye eneo hili. Siku hizi hawaitwi tena viungo wakabaji yaani  “Defensive Midfield”. Jina lao wanaitwa Deep Laying Midfields.

Kazi yao kubwa ni kuanzisha mashambulizi kuelekea mbele, mfano alivyokuwa Andrea Pirlo pale Juventus. Au Michael Carrick pale Man United na wengine wengi kwenye timu tofauti duniani. Kamusoko ni aina ya “Deep Laying” pia anaweza kusogea mbele kucheza kama kiungo mshambuliaji.

Nafasi hii ambayo anacheza Kamusoko, Yanga kwenye dirisha dogo la usajili  imemleta kiungo kutoka Zambia anaitwa Justine Zulu. Jina la utani ambalo linavuma kwenye vyombo vya habari habari hapa nchini anaitwa “Mkata umeme”

Kutokana na jina hili inaonekana Zulu ni aina ya wachezaji walewale tuliwazoea wakicheza kwa kutumia nguvu nyingi kwenye eneo la kiungo. Kama Zulu yupo hivyo bila shaka atakuwa na kazi kubwa kuingia kwenye kikosi cha Yanga.

Wachezaji haina ya kina Zulu mara nyingi wanakuwa na faida hususani timu inapotaka kujilinda zaidi kuliko kushambulia, au timu inapozidi kwenye umiliki wa mpira. Yanga kwenye ligi kuu ya Vodacom inaweza kucheza kwa kujilinda kwenye mechi mbili tu, labda dhidi ya Simba au Azam tena vya vipindi kadhaa na sio muda wote wa mchezo.

Staili ya mpira wa Yanga bado haijabadilika, wanacheza kwa kushambulia hata kwenye mechi za kimataifa. Kumbuka michezo dhidi ya Al-Ahly kwenye mashindano ya klabu bingwa yaliyopita.

Kwa kombinesheni hii ya Niyonzima na Kamusoko, naona nafasi finyu kwa Zulu kumnayang’anya namba mmoja wao kama hatokuwa na vitu vya ziada kuwazidi viungo hawa kutoka Rwanda na Zimbambwe.

Niyonzima amerudi kwenye kiwango chake baada ya kukosekana  kwenye mechi nyingi za mzungo wa kwanza, Kamusoko yupo vizuri akitimiza majukumu yake vizuri uwanjani. Kulia kuna Msuva na kushoto yupo  Deus Kaseke.

Bahati nzuri  Zulu alikuwepo jukwaani jana wakati kina Niyonzima wakitakata kwenye eneo la kiungo, sijui yeye atakujaje? Tusubiri tuone…


Viewing all articles
Browse latest Browse all 676

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>