Baada ya mchezo wa Timu Samatta Vs Timu Ali Kiba nilipata nafasi ya kuongea na Kocha Julio. Nikamuuliza anaonaje kiwango cha Ali Kiba. Akasema Ali Kiba ana kipaji kizuri kuliko hata baadhi ya wachezaji wanaolipwa fedha nyingi hapa ligi kuu bara. Vilabu vikubwa vinampuuzia tu lakini Ali Kiba ana uwezo.
Binafsi nilipomuona ukiachilia ile penati yake ya mwendokasi mpira ana ujua naweza kusema amekosa tu mwalimu mzuri wa kumwelekeza baadhi ya mambo ya kiufundi akamilike kuwa mchezaji wa kulipwa.
Je muda/ Unamruhusu?
Mwezi Novemba King Kiba anafikisha miaka 32. Kisoka huyu mtu tunasema ni mzee. Ila hapa Afrika ana miaka 23 kwenye fomu ya mkataba wake. Hajachelewa sana. Kimafanikio amechelewa lakini kwa kuwa anataka kutimiza ndoto yake ni muda muafaka kwake. Mpira ni ndoto ya kila anaupenda kuucheza.
Mwaka 1979 kabla hajapoteza maisha Bobby Marley alisema kucheza mpira ni “uhuru wa mtu binafsi” Tena anakiri kwamba kama sio miundo mbinu mibovu ya soka nchini Jamaica basi angeachana na mziki ajiunge kwenye soka. Huenda na sisi tukasema kama sio miundo mbinu mibovu ya soka basi Ali Kiba angekuwa mbali.
Huu ni muda Ali Kiba kutetea kauli ya Julio kwamba yeye anawazidi uwezo baadhi wachezaji wakubwa hapa bongo.
Ali Kiba anakwenda kuchezea klabu ambaye Shemeji yake mtarajiwa Abdi Banda aliwahi kuichezea. Abdi Banda inasemekana ana mahusiano na dada yake Ali Kiba ajulikane kama Zabibu Kiba. Huenda Banda akawa mmoja wa washauri wa Kiba kisoka kwa maana kwamba wapo karibu.
Ushauri wangu ni upi?
Kuna mambo ambayo huwezi kupingana nayo kwamba soka ni mchezo mgumu sana ambao huwezi kuuchanganya na kitu kingine kabisa. Wapo watu kama akina Clint Dempsey walikuwa wasanii wazuri, yupo Memphis Depay ambaye pia ni msanii. Wameshindwa kuwika kimuziki kwa sababu ya soka.
Ali Kiba ni Msanii mkubwa sana Afrika Mashariki. Kwa wenzetu ulaya soka linalipa kuliko muziki, lakini sisi hapa Tanzania wanamuziki ndio wana mafanikio zaidi. Hayupo mchezaji mwenye jina kubwa zaidi masikioni mwa watanzania wengi kuliko Ali Kiba. Hata Mbwana Samatta hana umaarufu wa Ali kiba. Kiba amepatia umaarufu kwenye sanaa ya mziki wa bongo fleva. Bongo fleva imempa umaarufu mkubwa. Lakini kwa sasa anapswa kuuweka mziki pembeni kwa muda. Unaweza kuba mziki hata ukiwa na miaka 60 lakini soka mhh.
Changamoto!
Kuna kauli ilinitia wasiwasi sana. Kauli ga Julio. alisema hivi “Alikiba ni mchezaji mzuri sana, mimi binafsi huwa namwambia ‘nataka nikusajili’, kama hawezi kuja kule mkoani lakini tukija hapa Dar aje acheze, ana uwezo mkubwa sana kuliko wachezaji wengi wa Simba na Yanga ambao wanalipwa mishahara ya bure
Yaani kama hawezi kuja kule mkoani. Yaani Julio mwenyewe anaona umuhimu wa kazi ya Ali Kiba na anajua mziki unamlipa zaidi kuliko soka hivyo akawa anahofia kwamba Kiba atakuwa bize sana na mziki.
Ali Kiba anajua wazi kwamba itabidi azunguke Tanzania bara kwenye viwanja zaidi ya 17 tofauti ndani ya miezi 8. Anaelewa wazi kwamba Coastal Unioni sasa itapata mashabiki wengi kwa sababu yake. Na anapaswa kuwaridhisha mashabiki hao kwa kiwango Murua. Lakini hapo hapo anaelewa viwanja mbalimbali na kumbi za muziki zitamhitaji kwa ajili ya shoo. Xxl watahitaji sauti yake kwa ajili ya kupamba vipindi vyao kwa ajili ya maendeleo ya muziki wa kizazi kipya. Najua kabla hajafanya maamuzi haya alishauriana na watu mbalimbali hajakurupuka hivyo itabidi akubaliane na changamoto zote hizo.
Simaanishi kwamba Ali Kiba amekosea. La Hasha naamanisha anapaswa kujifunza kwa Rob Stewart. Rod Stewart “Rod the Mod” alizaliwa jijini London. Alikuwa nahodha wa timu yao ya shule ya mpira ya Middlesex Schoolboys. Baada ya kumaliza shule alikwenda dafaja la 3 kufanya majaribio katika klabu ya Brentford lakini hakufanikiwa kupewa mkataba. Wakati ule alikuwa pia anafanya muziki. Rod anasema hivi “Soka na muziki ni mambo nayoweza kufanya bila tatizo lolote, ingawa muziki ni rahis kidogo, naweza kunywa pombe kiasi cha kuelewa na bado nikaimba lakini soka huwezi kufanya hivyo. Soka unahitaji kutuliza akili na kufanya kitu kimoja.”
Hata Tom Cruise alipenda soka. Hata alipoumia goti na kushauriwa kwamba akafanyiwe upasuaji aweze kuendelea na soka akasema hapana naomba niendelee na uigizaji ili niwe huru. Maneno yale yale ya Bobby Marley kwamba mpira unapaswa kuwa huru. Ali Kiba nae anapaswa kwenda pembeni na muziki. Najua kuna ushindani wa timu huko mitandaoni n.k. Najua atakumbana na changamoto za hizo timu. Nafahamu kiba anaweza kuishi katika mazingira ya kusemwa vibaya n.k. Huenda akacheza mwaka mmoja akamaliza haja yake kisha akaendelea na muziki. Hata hivyo Ali Kiba ni msanii ambaye anaweza akatoa wimbo mmoja kisha akatuachia sauti yake mwaka mmoja ndipo arudi tena.
Siamini kama amefuata hela kwenye soka. Sio kweli. Amekuja tu kutimiza ndoto zake za kucheza soka. Haimaanishi kwa kiwa halipwi hela nyingi kama kwenye mziki basi asijitume. Kwenye mpira mekapu ni nasa sana ajikaze apambane aisaidie Coastal aondoke na rekodi yeyote tutamkumbuka huko baadae kwa hilo.
Ali kiba kuja kwenye soka hakumpi yeye tu furaha ya kutimiza ndoto zake. Ila kuna maana kubwa sana kwetu. Ronaldo alipokwenda Madrid amekwenda na rundu kubwa la mashabiki nyuma yake. Ali Kiba nae anawafuasi wengi sana nyuma yake. Hata wale wasiopenda michezo watakwenda viwanjani ili kumona King. Mr Yeeoh anapendwa kila engo la taifa hili. Kuna watu kule mbamba bay na kule ushirombo hawajawahi kumuona. Hivyo Coastal wakikutana na Mwadui au Mbeya City watu watajaa uwanjani kumuona. Nilitegemea kusikia kuna makampuni yatajitokeza kwa ajili ya kumvalisha Kiba viatu au hata kumlipia usafiri au Makampuni ya Hoteli kujitokeza kuwalaza Coastal kwa sababu tu Kiba ni Brand. Ni ngumu sana lakini Coastal wamelamba dume. Hatujakomaa tu kisoka lakini Kiba ataleta hamasa kubwa sana kisoka. Atatuangusha sana pale tutakaposikia mara leo hayupo kesho atacheza au acheze tu mechi za Tanga na Dar. kuliko
Karibu Ali Kiba na kila la kheri….
Makala na Privaldinho unaweza pia kunifollow (instagram)