Quantcast
Channel: Makala – ShaffihDauda
Viewing all articles
Browse latest Browse all 676

El classico Messi na Ronaldo nani kiboko?

$
0
0

Kwani mdau wewe upande gani? Upande wa La purga au Cr7 mnyamaa? Unaamini nani atafanya poa zaidi kati ya hawa miamba wa soka?
Basi sawaa…. Ngoja mimi nikuletee takwimu za hawa jamaa walipokutana katika El classico na rekodi zao.

Mechi walizoshinda
Mechi Ushindi Poteza sare
Messi 37 17 12 8
Ronaldo 29 8 14 7
vurugu la Mashabiki sasa

Kwa hapa Messi ameonekana kumbwaga mfalme huyu wa Ureno mwenye shabaha zake. Messi ameshinda michezo 17 huku akiwa amecheza michezo mingi zaidi kuliko Ronaldo takribani michezo 8. Ameshinda michezo 13 ambayo ni ya la liga. Ronaldo alijiunga Marid mwaka 2009 ndiyo maana amezidiwa baadhi ya mechi na mzee kiroboto. Hakuna mchezaji wa ulaya aliyeifunga Barcelona magoli mengi kama Ronaldo.

Ronaldo ni mchezaji pekee duniani, narudia tena, mchezaji pekee duniani au niseme mwanadamu pekee, tena kwa herufi kubwa MCHEZAJI PEKEE DUNIANI mwenye magoli 11 ndani ya Camp Nou. Pale Camp Nou watu si wanasema pale ni shimoni sijui KORONGONi kwamba ukienda pale mweleka unakuhusu? sasa Mwanaume huyu hajuagi hayo.

kwenye hii picha kuna wadau wameshindwa kujizuia imebidi wamtukane tu kwa kumnyooshea kidole.
Magoli waliofunga
Mechi Magoli mashuti
Messi 37 25 129
Ronaldo 29 17 122

Bila shaka hapa mzee mwenye tambo zake wakati wa ushangiliaji ambaye inasemekana kina dada wengi wanamkubali zaidi kuliko kale kamtu kafupi amezidiwa magoli na mzee kirikuu. Kirikuu ameonakana kuwaotea sana ndugu zake hawa jiji wa Madrid.

kesho usikose kufika Escape One kucheki mpambano huo na mashindano ya play station

Hata hivyo kijana huyu mreno ana wastani mzuri sana wa mashuti akiwa amezidiwa mashuti 7 tu pia akiwa nyuma akiwa michezo 8. Cr7 ze goli mashine amekuwa na uchu sana wa kuchungulia lango ndiyo ameonakana kuwa mashuti mengi ukilingana na usawa wa mechi zake.

Ronaldo ndiye mchezaji pekee aliyefunga magoli kwenye mechi 6 mfululizo za el classico
wanaume wenye Ballon d’Or zao

Nani Fundi wa asisti?
Kwanza kwa taarifa yako, hakuna kiumbe chochote kilichotengeneza magoli mengi zaidi ya Messi. Yaani tokea Adamu mpaka Messi hatuna taarifa ya kiumbe chochote kile. Labda wakati wa zama za mawe.

Asisti Nafasi
Messi 14 65
Ronaldo 1 15

hiki kajamaa kafupi khaa? kufunga kafunge chenyewe, kutengeneza magoli awe yeye daah? ana roho mbaya. kila kitu chake?
Kwenye jukumu hili la kulisha wengine Ronaldo ameonekana kukipenda zaidi kijiko chake kuliko sahani za wengine. Muargentine amefanya vyema zaidi katika nafasi hii hasa ukiangalia majukumu yake na nafasi yake uwanjani imempa uwanja mpana wa kulisha wengine.

March 22, 2015.

Messi amekosa michezo miwili tu El Classico akiwa kikosi cha kwanza tokea mwaka 2004. Mwaka 2005-06 ambapo aliumia na mwaka 2007-08 pia alikuwa majeruhi.

Nidhamu
Njano Njano mbili Nyekundu
Messi 11 0 0
Ronaldo 10 1 0

Kwenye michezo yote Ronaldo ametolewa nje mchezo mmoja tu mwaka 2009 dakika ya 65 na ametokea benchi mchezo michezo miwili mwaka 2013 aliingia dakika ya 57 na mwaka 2017 ambapo aliingia na kutolewa kwa kadi nyekundu.

picha yenye Ballon d’Or 10

Asanteni sana Messi na Ronaldo kizazi pekee bora duniani chenye ushindani kuwahi kutokea. saluti

Makala hii imeandaliwa na Privaldinho (instagram).


Viewing all articles
Browse latest Browse all 676

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>