Haya yalikuwa maneno ya mchambuzi nguli mzaliwa wa Wrexham Wales Bw. Robbie William Savage.
Huenda utabiri au mawazo na mtizamo wa Savage unatimia. Southampton baada ya kulaghaiwa na Liverpool kwa kuwauzia wachezaji takribani 6.
Jina | thamani | mwaka |
Adam lallana | £25m | July 1, 2014 |
Dejan Lovren | £20m | July 27 2014 |
Nathaniel Clyne | £12.5m | July 1, 2015 |
Sadio Man | £30m | June 28, 2016 |
Rickie Lambert – | £4m | June 2, 2014 |
Virgil van Dijk | £75m | Dec 2017 |
Jumla | £166 |
Tokea mwaka 2014 wana wastani wa kupoteza mchezaji wao muhimu mmoja kwenye kikosi chao hasa hasa kwa majogoo wa Liverpool. Siwezi kusema moja kwa moja kwamba Soton inaporomoka kwa sababu hiyo lakini ukajaribu kuiangalia Liverpool inafanya vyema sana hasa ukiangalia wachezaji wao muhimu pia ni wale walitokea Southampton. Soton wanahitaji maombi ya ziada kuwazuia kwenda kuzimu (kushuka daraja).
Soton wapo nafasi ya 18 kwenye msimamo wa Ligi kuu. Wapo hatarini kabisa kushuka daraja wakiwa na alama 28 sawa na Stock City waliopo nafasi ya 19.
Timu | M | W | D | L | GF | GA | GD | P |
Crystal Palace | 34 | 8 | 10 | 16 | 36 | 54 | -18 | 34 |
Swansea City | 33 | 8 | 9 | 16 | 27 | 46 | -19 | 33 |
Southampton | 33 | 5 | 13 | 15 | 33 | 53 | -20 | 28 |
Stoke City | 34 | 6 | 10 | 18 | 31 | 64 | -33 | 28 |
West Browmwich | 34 | 4 | 12 | 18 | 27 | 52 | -25 | 24 |
Kwa takwimu hizo hapo juu ni wazi kuwa Soton wana hali ngumu.
Hakika wanahitaji kubakia ligi kuu. Wana kikosi kizuri sana. Wana wachezaji wenye uzoefu mkubwa. Sawa wachezaji muhimu wameondoka lakini hata hawa waliopo ni wazuri kuliko wale waliopo Brighton. Shida ni mipango mibovu ndani ya klabu na kwa jinsi gani mwalimu anatengeneza mikakati ya kuijenga timu kwa malengo ya muda mrefu.
Mtazamo wangu ni upi?
Kocha wa hapo awali Mauricio Pellegrino alilipa fadhila za Southampton kwa kuwapiga mateke ya tumbo baada ya kushinda mchezo mmoja tu katika michezo 17 ya hapo awali. Mark Hughes aliipokea Southampton ikiwa na na alama 1 tu kushuka daraja, lakini kwa sasa mgonjwa wetu hata maji ya kunywa inabidi atafuniwe kwani yupo kwenye hatari ya kushuka daraja baada ya michezo 3.
West Ham United | 3–0 | Southampton |
Arsenal | 3–2 | Southampton |
Southampton | 2–3 | Chelsea |
Mnamo tarehe 14 mwezi wa tatu Mark Hughes aliingia mkataba wa kuinoa Sotoni. Bila propaganda watakatifu hawa wa Britannia Rd walifanya uamuzi sahihi kabisa kumnasa Mark Hughes kuwa kocha wao mkuu licha ya kuwa hatarini. Ukijaribu kutazama michezo yao ya mwisho hapo juu utagundua timu kwa kiasi Fulani imeinuka.
- Angalia kwa namna walivyoweza kupata magoli kwenye michezo migumu. Hata hivyo waliwatawala hata Chelsea nusura wapate ushindi.
-
Southampton Chelsea Umiliki 58% 42% Mashuti 10(7) 17 (5) kona 4 7 faulo 13 14 - walijitahidi kadiri ya uwezo wao lakini bahati haikuwa yao. Tena ukiachilia mbali makosa ya hapa na pale basi michezo yao dhidi ya Arsenal na huo Chelsea walikuwa na uwezekano mkubvwa wa kushinda.
PATA KIFURUSHI
Jina Kamili; Southampton Football Club |
Kuanzishwa; 21 November 1885; 132 |
Jina la utani; the saints (Watakatifu) |
Uwanja; St Mary’s Stadium |
Wamiliki; Gao Jisheng (80%), Katharina Liebherr (20% |
Kombe kubwa; FA (1976) |
Hii ni timu ya sita ya Mark Hughes kuifundisha katika ligi kuu England, Blackburn, Fulham, Manchester City, QPR na Stoke City (Ni Sam Allardyce pekee aliyefundisha vilabu vingi kumzidi (saba)). Katika Historia yake tokea mwaka 2004 mpaka 2017 ameweza kucheza michezo 444 na amekuwa na wastani wa alama 1.32 kwa kila mchezo
Kama atawazea kupambana bila shaka Soton inahitaji angalau kufikia alama 38 ili wawe na uhakika wa kubaki ligi kuu yaani alama 10 kutoka sasa ambazo naziona kwenye michezo ifuatayo
Tarehe | Mpinzani | Mahali |
19 April 2018 | Leicester city | Ugenini |
28 April 2018 | Bournemouth | Nyumbani |
5 May 2018 | Everton | Ugenini |
8 May 2018 | Swansea | Ugenini |
13 May 2018 | Man City | Nyumbani |
Mark Hughes anapaswa kuhakikisha anashinda michezo mitatu au kuwaombea Palace na Swansea kupoteza angalau michezo mitatu iliyobakia.
Hapaswi kuchafua heshima yake kwani takwimu zinaonesha kuwa Mark Hughes hajawahi kumaliza msimu akiwa na timu ambayo inashikilia nafasi za mwisho.
15 | 6 | 10 | 7 | 10 | 8 | 17 | 9 | 9 | 9, 13. |
Soton wamejitahidi msimu huu kwa kiasi chake. Ni moja ya timu ambazo zimecheza takolini nyingi zaidi msimu ikiwa nafasi ya 5. Istoshe ukiacha zile timu 6 za juu hii ndiyo timu pekee iliyotengeneza nafasi nyingi za kufunga kuliko timu yeyote wakiongozwa na Mshambuliaji wao hatari Charlie Austin mwenye magoli 7. Tatizo ni Safu yao ya ushambuliaji imekuwa na ubutu sana kwenye kumalizia magoli kwani kwa ujumla safu hii ina jumla ya magoli 13 pekee.
Kiufupi kuna hali mbaya sana kwa Mark Hughes ambaye amewatelekeza Stoke City wanaoshuka daraja. Huenda timu mbili zikashuka daraja kwa kupitia mikononi mwake ndani ya msimu mmoja. Hughes anadai kuwa Stoke ilimhujumu na baadhi wachezaji walikuwa hawajitumi. Mashabiki wengi wa Stoke walimtaka Hughes kutimuliwa lakini najiuliza sasa hivi wapo wapi?
Hughes ni mchezaji wa zamani wa Soton ambaye anawajua vyema sana. Ameikuta klabu kwenye nusu fainali ya FA ambapo watakutana na Chelsea. Wapo dakika 90 kabla ya kufika fainali ya Wembley. Ni mchezo mkubwa sana kwao hasa ukiangalia Chelsea hii ambayo huenda ikatoka kapa. Wanapaswa kujitoa kwa jasho na damu angalau kupata matokeo ambayo kwa namna fulani yanaweza kuwapa ubingwa wa kufuta machozi yao.Bila shaka hii ni kazi kubwa sana kwa Hughes na ni kipimo tosha kwake na kinaweza kumjengea sifa mbaya sana kama atashindwa kupigania kibarua chake. Kwa kuangalia takwimu za huko juu na uzoefu wa Hughes anapaswa kubaki ligi kuu. Nina imani hakika anaweza kubaki kama timu za juu yaani Palace na Swansea zitakwama.
Uwezekano Palace kubakia ligi kuu ni mdogo sana kuliko Soton Kwani Palace ana mechi na timu zinazoshuka daraja West Bromwich, na Stoke na hii ni michezo migumu sana. karata ya mwisho ipo kwa Swansea ambaye ana mechi ngumu sana ikiwa ni pamoja na mechi yao dhidi ya Soton na Stoke. kwa ubovu wa Swansea nina imani hii ndio nafasi ya pekee ya Hughes kubakia ligi kuu.
Hughes ana kazi sana hasa katika michezo ya Everton na Bournemouth na hasa ule wa mpinzani wake mkubwa Swansea na hiyo ndiyo michezo ya yeye kubaki EPL
Makala hii imeandaliwa na Privaldinho unaweza pia kunifollow Instagram kwa jina hilo hilo na usisahau kusubscribe channel ya youtube ya Dauda Tv