Sehemu ya 6
Ilipoishia….
“Nilipoingia uwanjani tulikuwa chini magoli mawili. Nilikuwa namfokea kila mchezaji uwanjani. Hata nilipomfokea Zlatan nae alinifokea. Nikachukia sana kitendo cha Zlatan kunijibu vibaya. Nilikuwa nagombana na kila mtu nikitaka wajitume tupate matokeo.
Nilipewa mpira na Zlatan alikuwa kwenye nafasi nzuri ya kufunga ila sikumpa pasi makusudi. Zlatan nae alipopata mpira aligoma kunipa pasi. Kuna wakati nilitoa mpira nje makusudi. Mpira ulipoisha nilimtukana Zlatan matusi ya nguoni, Zlatan nae alimrudishia matusi yale yale” alisema Hassan Mido.
Baada ya majibizano Mido akakasirika kwa ghadhabu akamrushia usoni Zlatan mkasi aliokuwa ameushikilia. Zlatan anasema aliukwepa ule mkasi maana ulimjia kichwani kwa kasi ya ajabu. Mkasi ulienda ukatoboa ukuta na ukanasa pale pale. Baada ya dakika kumi Mido alikwenda kwenye jakuzi. Aliporudi alimkuta Zlatan amekaa. Wakaangaliana kwa dakika kadhaa kisha wote wakaiishia kuchekana. Mido akamwambia Zlatani ningekuua leo, Zlatan akamwambia ndiyo ila ungeozea jela.
Baada ya Hapo Mido alitolewa kwa mkopo na kwenda Celta Vigo. Mido anasema licha tukio lile lakini bado yeye na Zlatan ni maswahiba wakubwa tu.Baada ya Mido Kuondoka Zlatan alipata uhuru wa kucheza. kiwango kiliimarika sana na kufunga magoli 11 katika michezo 13.
Mido anena;
Mimi ni mchezaji mkubwa sana Misri, wakati ule nilikuwa ndiye mchezaji pekee niliyekuwa ligi kubwa kutoka taifa langu. Watu walikuwa hawaijui hata ligi ya Uholanzi lakini walikuwa wanaifuatilia kila mara Ajax ilipocheza ili tu wanione mimi. Sasa kitendo cha kushangaza nilikuwa sipati nafasi ya kuanza na hii iliwafehedhesha wana Misri wote maana walikuwa wanajaa vilabuni ili tu wanione. Hali ile ilinijengea jeraha akilini mwangu na hii ilisababisha madhara ambayo yangeondoa uhai wa Zlatan.
Michezo | Magoli | Asisti | Krosi | Paasi | Mashuti |
94 | 22 | 6 | 74 | 1,180 | 102 |
Maisha ya Ajax katika michuano ya UEFA yalitia nanga baada ya kushinda mchezo mmoja katika michezo 6 kwenye kundi. Licha ya kwamba alicheza kwenye klabu ambayo ilikuwa ikisuasua alitajwa kwenye orodha ya wachezaji 49 bora ulaya akiwa namba 20 baada ya kufunga magoli 21 kwenye michezo 41 akiwa na umri miaka 21 tu.
Alifedheheshwa sana na kipigo kutoka kwa Utrecht hasa pale kocha alipomtoa nje. Zlatan akakumbuka kuna jamaa alikuwa anamsumbua sana (Mino Raiola). Akaamua kumpigia simu na kumtukana matusi mengi huku akimsisitiza amfanyie mpango wa uhaimisho la sivyo atafanya tukio la kijinga.
SAJILI KUBWA 5 ZA MINO RAIOLA
Jina | kutoka | Kwenda | Bei | mwaka |
P. Pogba | Juventus | Man United | €105 mil
|
2016 |
R. Lukaku | Everton | Man United | €85 mil
|
2017 |
Z. Ibrahimovic | Barcelona | Inter | €46 mil
|
2009 |
Robinho | R. Madrid | Man City | €35 mil
|
2010 |
P. Nedved | Juventus | Lazio | €41 mil
|
2001 |
Siku 10 baadae Mnamo tarehe 18 agasti 2004 ilisemekana Zlatan alimvunja mchezaji mwenzake kwa makusudi kwenye mchezo wa kimataifa dhidi ya Uholanzi. Inasemekana Zlatan alikuwa na ugomvi na Raphael Van Da Vaart na magazeti mengi yalimshtumu kuwa alimuumiza kwa kudhamiria.
PATA KIFURUSHITakwimu zake mwaka wake wa mwisho 2003/04
Mashindano | Mechi | Magoli | Asisti | Dakika |
Ligi kuu | 22 | 13 | 7 | 1,408 |
uefa | 6 | 1 | – | 451 |
Kufuzu UEFA | 2 | 2 | – | 146 |
Toto KVNB | 1 | – | 90 | |
Jumla | 31 | 15 | 7 | 2,095 |
Tukio lile liliibua ugomvi mkubwa kati yake yeye na Raphael Van Da Vaart pamoja na Lois Van Gaal. Walipokwenda kambini Ureno mwaka 2004 walikwaruzana sana na Van Gaal. Van Gaal alisema Zlatan ni mzembe, mzito na hajitumi mazoezini. Bila shaka damu ya Zlatan na Van Gaal hazikuivana. walikuwa wakitupiana vijembe mara kwa mara. mara ya mwisho Paul Scholes alitamka waziwazi kuwa Zlatan asingeweza kujiunga na Man United wakati Van Gaal alipokuwa kocha wa Man United
Zlatan nae akajibu akasemaKila mara Van Bastern alikuwa akimshauri Zlatan aina ya uchezaji, na alikuwa tayari kusikiliza maelekezo ya Bastern kuliko madikteta wengine klabuni hapo (akimaanisha Van Gaal). Van Gaal alikuwa ananipigia simu na kunipa maelekezo ambayo yalikuwa yanakinzana na ushauri wa Van Basten, nikamuuliza nimsikilize nani? wewe au Van Basten kisha nikamkatia simu.
Aliongeza kuwa Van Gaal ni mtu wa ajabu na wa ovyo sana. Huwa hangalii mchezaji anataka nini ila anajithamini yeye tu. Yaani kiufupi HASHAURIKI. Zlatan akamkashifu Van Gaal kwa maneno ya kebehi kwa kusema kuwa “Van Gaal hajawahi kuwa mshambuliaji atamwambia nini? Bora Bastern amewahi kucheza eneo hilo sio yeye”.
Kwanza zlatan akadai huyo mtu anaitwa Van Gaal hawakuwahi kuonana uso kwa uso alikuwa anasikia taarifa zake. Zlatan alikuwa akipokea malalamiko kutoka kwake mara kwa mara lakini hawakuwahi kukaa meza moja na kuongea.
je baada ya ugomvi wake na Van Gaal kipi kiliendelea? usikose makala ijayo
imeandaliwa na Priva Abiud. Pia unaweza kunifollow Instagram kwenye account yangu ya Ptivaldinho na usisahau Kusubscribe Youtube Channel yetu ya Dauda TV.