England wameshinda ubingwa wa kombe la dunia la vijana chini ya umri wa miaka 17 baada ya comeback ya kutoka nyuma kwa magoli 2-0 na kwenda kushinda 2-5 dhidi ya Spain katika mchezo wa fainali uliopigwa Kolkata nchini India.
Kikosi cha U17 kinaungana na U20 kama mabingwa wa dunia – England imekuwa taifa la pili kushikilia mataji hayo mawili ya dunia kwa wakati mmoja.
Timu za vijana za England ni hazina inayoweza kuiondoa aibu ya Three Lions ya wakubwa kutokufanya vizuri kwenye mashindano makubwa. Mafanikio ya vijana hawa ni jambo lilowatengenezea kufahamika kwa vijana hawa lakini haya ndio mambo matano 5 ambayo inabidi uyafahamu kuhusu Waingereza hawa.
Like Father Like Son
Baba mzazi wa nahodha wa U17 Angel Gomes, Gil Gomes alikuwa kwenue kikosi cha Ureno cha mwaka 1991, kilichokusanya vipaji kama
Luis Figo, Rui Costa na Joao Pinto, kilibeba ubingwa wa 1991 Fifa World Youth Championship.
Hata Gil hakufanikiwa sana katika soka la ukubwani, aliishia kutumikia vilabu kama
Hendon, Middlewich, Salford na Hyde katika ligi za nchini katika soka la Uingereza.
Ilikuwa wakati huu ndio Gill alikutana na mama yake Angel, ndio kijana huyu akazalowa jijini London.
Kiungo mshambuliaji anayekipiga katika klabu ya Manchester United tangu alipokuwa na miaka 13. Hata hivyo, amekuwa mtembezi pale Carrington tangu akiwa mdogo sana, kwasababu alikuwa akienda kumtembelea uncle wake – winga wa zamani wa United, Nani.
Gomes aliingia kuchukua nafasi ya Wayne Rooney katika dakika 2 za mwisho za mchezo wa mwisho wa Premier League msimu uliopita na kuweka rekodi ya kuwa mchezaji mdogo zaidi kuwahi kuitumikia United tangu Duncan Edwards mwaka 1953.
Kipigo cha 23-0 kwenye mechi ya kwanza
Golikipa wa Manchester City Curtis Anderson ameruhusu magoli manne katika mechi 5 za mashindano ya dunia. Haya ni mafanikio makubwa – kwenye mchezo wake alikubali kipigo cha magoli 23-0 akiitumikia Crookland Casuals dhidi ya Furness Rovers.
Baada ya hapo alisainiwa na Blackpool kabla ya kwenda Manchester City mwaka 2012 kwa ada ya £15,000 akiwa na miaka 11.
Anderson alifunga na kucheza penati katika mchezo wa raundi ya 16 bora dhidi ya Japan.
DNA ya soka
DNA ya Sessegnon ina nguvu sana.
Steven Sessegnon, mtoa assist mbili kwenye fainali ya jana, pia aliisaidia saba U17 katika mechi za mtoano, lakini Steven sio mwanasoka bora hata kwenye familia yake.
Pacha wake Twin Ryan Sessegnon – ambaye hakuwepo India – alikuwa sehemu muhimu ya kikosi cha Fulham kilichomaliza msimu wa Championship vizuri, akifunga magoli 5 katika mechi 25 za ligi na baada ya hapo akaenda kuwa mfungaji bora pacha katika michuano ya U19 ya Euro mwezi July wakati England walipoifunga Ujerumani na kubeba ubingwa. Spurs waliripotiwa kutuma ofa £25m ambayo ilikataliwa na Fulham mwezi August.
Unamkumbuka Stephane Sessegnon – mshambuliaji wa zamani wa Sunderland, West Brom na Benin – huyu ni mpwa wao.
Kinda lilomuacha mdomo wazi Pep Guardiola
Sifa za Phil Foden zimekuwa zikitoka kwa watu mbalimbali – lakini wote wana maono yanayofanana.
Mnamo June 2008, Reddish Vulcan – timu ya vijana ya huko Stockport – ilitangaza kwamba Foden, akiwa na miaka 8 kipindi hicho alikuwa anaelekea Manchester City.
Miaka 9 baadae mpaka July 2017 kocha wa Manchester City Pap Guardiola amemuongelea Foden kwa sifa za hali ya juu.
“Ni kipindi kirefu sijaona mchezaji wa aina yake. Kiwango ni cha juu sana. Sina maneno sahihi ya kumuelezea na kile nikichokiona,” – Pep aliongea maneno haya baada ya mchezo wa Pre Season vs Manchester United nchini Marekani.
Foden pamoja na Brahim Diaz na Jadon Sancho (kabla kuondoka) walitajwa na mwenyekiti wa City Khaldoon al-Mubarak kuwa miongoni wa wachezaji wa Academy ambao watapata nafasi katika kikosi cha wakubwa msimu huu.
Foden alifunga magoli mawili katika mchezo wa fainali na akatajwa kuwa mchezaji bora wa mashindano.
The Boss
Kocha Steve Cooper – uzoefu wake wa kucheza katika anga za kimataifa umeishia mwisho kwenye Europa League.
Hata hivyo, baba yake Keith alifanya kazi ya urefa katika michuano ya European Championship hatua ya kufuzu na miaka 3 katika Premier League.
Keith Cooper, baba yake Steve, akimpa kadi Gary Gillespie wa Coventry katika Premier League game vs Leicester mnamo October 1994.
Steve alikuwa mmoja wa makocha wenye umri mdogo zaidi kuwahi kupewa leseni ya ukocha ya UEFA akiwa na miaka 27, na baada ya kuwa kufundisha soka katika vilabu vya Wrexham na Liverpool, alichaguliwa kuwa kocha wa kikosi cha England U16 mnamo mwaka 2014. Leo hii ni mshindi wa kombe la dunia.