Na Thomas Ng’itu
Achana na matokeo ya sare ya bila kufungana dhidi ya Azam na Simba,jambo kubwa lililokuwepo katika mchezo huo ni bato la aina yake katika dimba la kati.
Katika safu ya kiungo ya Azam iliyokuwa ikiongozwa na Himid na Kingue, waliweza kukata spidi ya viungo wa Simba James Kotei,Mzamiru na Niyonzima takribani dakika 15 za kipindi cha kwanza.
Lakini hata hivyo viungo wa Simba nao hawakuwa nyuma kwani walimfanya Niyonzima atembee anavyotaka,baada ya kukabiwa vilivyo na Mzamiru pamoja na Kotei.
Bato hili la viungo lilizidi kuwa kali zaidi Mao alipopata kadi ya njano mapema tu, alipomfanyia faulo Kotei kwani ushindani katika eneo la katikati ndio ulizidi kupindukia na kufanya mpira usichezwe katika duara la kati.
Fomesheni ya Cioba ya kuwachezesha viungo wakabaji wawili ilikuwa na mantiki katika kipindi cha kwanza kwasababu waliweza kuendana na spidi ya viungo wa Simba,ambao wameimarika zaidi.
Katika kipindi cha kwanza Azam walitumia mchezo wa 4-2-3-1,ambapo nyuma kulikuwa na Aggrey Morris,Yakub Mohammed,Daniel Amoah na Bruce Kangwa,Viungo Himid Mao na Stephen Kingue ambao walikuwa viungo wakabaji,Salum Abubakar,Mbaraka Yusuph,Enock Agyei wakiwa viungo wachezeshaji huku Yahya Mohammed akiwa amesimama mbele peke yake.
Hata hivyo katika kipind cha pili walibadilika na kucheza 4-5-1 baada ya kumuingiza Yahya Zayd,Domayo na Singano.
Kwa upande wa Simba wao walianza kwa fomesheni ya 3-5-2 kwa kusimamisha Mwanjali,Mbonde na Nyoni nyuma,kisha kujaza viungo watano katikati lakini hata hivyo katika kipindi cha pili walijikuta katika kipindi kigumu baada ya Azam nao kujaza viungo.
Viungo wala kadi
Katika mchezo huo kudhihirisha bato iliyokuwepo,vuingo James Kotei na Mzamiru Yassin walipata kadi za njano na kwa upande wa Azam Himid Mao,Stephen Kingue na Salum aboubakary nao walipata kadi za njano.
Kwa hali hii inaonyesha dhahiri kuwa katika eneo la viungo wa timu zote mbili, kulikuwa na patashika nguo kuchanika.