Quantcast
Channel: Makala – ShaffihDauda
Viewing all articles
Browse latest Browse all 676

Usajili wa Neymar PSG: Qatar, Siasa za Mashariki ya kati, biashara zilivyochangia uhamisho wa Neymar

$
0
0

Ulimwengu wa soka unasubiri kwa hamu kukamilika kwa uhamisho wa mshambuliaji wa kibrazil Neymar kutoka FC Barcelona kwenda Paris Saint Germain (PSG) kwa adabya uhamisho ambayo itavunja rekodi ya £198m – kama ambavyo kipengele chake cha kuvunja mkataba wa Barca kinavyosema.

Hiki ndio kiasi cha pesa ambacho kinazungumziwa, kiasi hiki kitakuwa zaidi ya mara 2 ya kile ambacho kililipwa na Manchester United kwenda Juventus kwa ajili ya usajili wa Paul Pogba – £89m, mnamo mwaka 2016.

Kwa miezi kadhaa nyuma kulikuwepo na tetesi kwamba Neymar hana furaha kucheza chini ya kivuli cha Lionel Messi. Pia kumekuwepo na taarifa kwamba Neymar amekuwa hana mahusiano mazuri na baadhi ya wachezaji wenzake – mfano mdogo ni juzi alivyoshikana mashati na Nelson Semedo mazoezini. Yote haya yanatajwa kwa sehemu ya sababu ya kufikia maamuzi ya kwenda Paris.

Yote yamezungumza kuhusu sababu za ndani ya uwanja, lakini kiuhalisia Neymar kwenda PSG kuna sababu nyingi za nje ya uwanja.. PSG ilinunuliwa kampuni ya Qatar Sports Investments (QSI) mwaka 2011, wakiwa na lengo ya kuitengeneza klabu hiyo kuwa kubwa na bora zaidi ulimwenguni. Wakati mafanikio ya nyumbani yakiwa yamepatikana, vikombe vya kimataifa limekuwa tatizo linazozuiwa ukuaji wa klabu katika anga za kimataifa na ukuaji wa biashara kiujumla.


Usajili wa Neymar unaweza kutafsiriwa kwamba ni kamari kubwa iliyochezwa na QSI. Lakini kwa misimu miwili iliyopita klabu hiyo imewasajili wachezaji wawili wa daraja la juu (Julian Draxler kutoka Schalke na Angel Di Maria kutoka Manchester United), lakini hawa wote wawili wapo kwenye level ya Neymar, Messi au Cristiano Ronaldo.
Kushindwa kusajili wachezaji wenye majina makubwa kulitokana na kuyumba kwa biashara kuu ya nchi ya Qatar, kushuka kwa bei ya mafuta. Hili lilipelekea mpaka kupinguzwa kwa bajeti ya maandalizi ya michuano ya kombe la dunia – kulikopelekea watu wengi kupoteza ajira zao. Kuyumba kwa uchumi wao kulipelekea pia kuanza kwa mjadala wa kuanzisha mfumo wa kodi (wananchi na biashara zinazofanyika Qatar hazilipiwi kodi). Hivyo matumizi haya makubwa ya kumsajili Neymar ni jambo ambalo limewashangaza wana uchumi wengi.

SIASA ZA MASHARIKI YA KATI
Sababu nyingine kuu ya usajili wa Neymar ni ya kisiasa zaidi. Neymar anaweza kutumika katika kuitangaza nchi hiyo na vivutio vyake hasa wakati huu ambapo nchi hiyo ipo kwenye hali mbaya kutokana kutengwa na majirani zao. Kwa miezi takribani miwili iliyopita Qatar imekuwa kwenye msuguano mkubwa na nchi jirani zinazoizunguza nchi hiyo – Saudi Arabia, the United Arab Emirates, Egypt na Bahrain, kutokana na tuhuma mbalimbali za kwamba nchi hiyo inasaidia na kusapoti ugaidi na pia inaingilia siasa za nchi jirani.
Msuguano huu umepelekea nchi kadhaa kukata ushirikiano wa kidiplomasia na serikali ya Doha, mipaka ya nchi zote za karibu imefungwa na mpaka pekee wenye njia ya ardhi wa nchi hiyo baina yake na Saudia Arabia, pia umefungwa kwa wiki kadhaa sasa.
Katika kukabaliana na vikwazo hivi, Qatar imeamua kukaza misuli na kutokubali kuendeshqa na vikwazo vya majirani na kuimarisha mahusiano na Iran pamoja na Uturuki – huku nchi hiyo ikiendelea kujiimarisha na mipango mengine ya kiuchumi. Nchi hiyo ina hifadhi kubwa sana ya fedha, ipo katika kuongeza uzalishaji wa gas na kuacha kutegemea biashara ya mafuta – mipango yao ya uzalishaji mkubwa wa Gas ikikamilika nchi hiyo itakuwa mzalishaji mkubwa zaidi wa Liquafied Gas.

BIASHARA
Usajili wa Neymar utakuwa na faida kubwa kwa PSG, mpaka kwa wamiliki wa klabu – Qatar. Kwa wakati ambao nchi kama Saudia zinaiongelea vibaya Qatar, Doha imejitengenezea ukubwa wa kuzungumzia sana kwenye mchezo pendwa zaidi ulimwenguni.
Inaweza kuonekana Neymar anatumika kama chambo katika vita ya kisiasa ya mashariki ya kati. Lakini Neymar ana uwakilishi mzuri wa watu wanaojua kujadili biashara ya kumnufaisha mteja wao, inaaminika atalipwa zaidi ya billion 1.9 za kitanzania kwa wiki.
Nia ya Qatar kusimama nchi yenye nguvu Zaidi ya kiuchumi kuliko maadui zake ndio inapelekea ukamilikaji wa dili hii kubwa kuliko zote katika historia ya soka. Ingawa wengi wanatoa hoja kwamba soka na siasa zisichanganywe – uhamisho wa Neymar unaonyesha wazi kwamba soka la karne ya 21 na michezo kwa ujumla ni sehemu ya siasa.

Kwa hakika Neymar hajali kuhusu tuhuma za Saudia kwamba Qatar inasapoti vikundi vya Muslim Brotherhood, al-Qaeda na Islamic State, ataelekea bank meno 32 nje kwa kusaini mkataba tajiri zaidi katika soka.
Neymar atakuwa akilipwa zaidi ya £24m kwa mwaka kwa mshahara tu baada ya kodi na kabla ya marupurupu mengine.
Kwa wiki atakuwa anaondoka na £515,000 baada ya kodi – haya ni malipo makubwa zaidi kwa mchezaji mmoja barani ulaya.
Kwa upande wa PSG, na mashabiki zake watakuwa na furaha jwa matumaini ya kuelekea kwenye kilele cha mafanikio ya soka barani ulaya kiujumla.


Viewing all articles
Browse latest Browse all 676

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>