Quantcast
Channel: Makala – ShaffihDauda
Viewing all articles
Browse latest Browse all 676

Keita, Van Dijk na ‘mla bata’ Emerick Aubameyang watavyompa ubingwa wa EPL Klopp

$
0
0

Na Salym Juma, Arusha

Liverpool ni timu kongwe nchini Uingereza na Ualaya kwa ujumla. Mataji ya Ulaya iliyochukua ukijumlisha na yale ya ligi kuu ya Uingereza yanaifanya timu hii kuheshimika zaidi Duniani. Liver wana deni kubwa kwa mashabiki wake, deni ambalo mkongwe Steve Gerrald ameshindwa kulilipa licha ya makubwa aliyofanya Merseyside. Taji la EPL ndio linalowaumiza Liver. Makocha na wachezaji wengi wamepita Anfield ila wameambulia kustaafu bila kutwaa taji hili.

Japo Liver imejaribu mara kadhaa kushindana kiume kupigania kombe hili, mwisho wa siku wamejikuta wakijikwaa dakika za mwisho na kuambulia kuwapa wapinzani ubingwa. Baada ya kuja kwa Jurgen Klopp ‘JK’ Liver imekuwa ikijitahidi kurejesha matumaini kwa mashabiki wake, leo hii tutazame namna gani Liver itaboreka zaidi endapo ikikamilisha usajili wa Naby Keita Virgil van Dijk na Pierre-Emerick Aubameyang  wachezaji watatu ambao wapo sokoni kwa sasa.

RB Leipzig huenda muda wowote ikapokea kiasi cha £70 million au zaidi kutoka kwa vijogoo wa Anfield kwaajili ya kumuuza kiungo wao anaejulikana kama Naby Keita. Liverpool ya ‘JK’ imekuwa ikimuwania mchezaji huyu wa kimataifa kutoka Guinea. Japokuwa safu ya kiungo ya Liver haikusua sua msimu uliopita ila ‘JK’ anataka kuboresha eneo hili ambalo mara nyingi limekuwa kama daraja kwa mabeki na washambuliaji. Keita ni kiungo ambaye Klopp hapaswi kukata tamaa kutafuta saini yake.

Naweza kusema hadi sasa Liver haina ‘Box to Box midfielder’ anayeweza kucheza kama Keita. JK anataka saini ya Nabby kwasababu anahitaji ulinzi mkubwa kwa mabeki na wakati huo huo anahitaji akina Coutinho, Mane, Sallah na Firmino wawe huru zaidi na wasiwe na mzigo mkubwa wa kukaba. Keita huenda akaongeza nguvu ya Liver kupigania taji la EPL kwa nguvu zote kwani vijogoo watahitaji kikosi kipana ili kuanza mapambano kwa kujiamini.

Japokuwa amaekuwa akifananishwa na Ngolo Kante wa Chelsea ila naweza kusema Keita amejaaliwa kitu cha ziada ambacho mkata umeme wa Chelsea amekikosa ambacho ni kufunga magoli. Hadi sasa akiwa na michezo 138 pekee Keita amefunga mara 32, idadi ya magoli ambayo viungo wengi wanaocheza nafasi yake hawajawahi kufunga. Miaka yake 22 huenda ikamfanya acheze vizuri na mchawi mwingine pale kati (Jordan Henderson).

Virgil van Dijk ni beki wa kati wa Southampton ambaye kiumri tumelingana naye (26) ila kimaumbile naweza kujichanganya nikamwambia ‘shikamoo’. Eneo la kati la Liverpool lilikuwa na makosa mengi mno hali ambayo iliwafanya muda mwingi wamlaumu mlinda mlango wao. Japo beki huyu amekuwa akiwaniwa na Chelsea na Everton ila ‘JK’ anapaswa kukomaa ili kupata saini yake hasa kutokana na uwezo mkubwa alionao mholanzi huyu ambaye amevaa jezi ya Uholanzi mara 12.

Ukuta wa Liver unahitaji mwanaume wa kazi ambaye atakwenda kushirikiana vyema na Nathaniel Clyne upande wa kulia huku kushoto ukipambwa na usajili mpya wa Andy Robertson. Endapo vijogoo watanasa saini hii muhimu huenda Joel Matip akapata wakati mwepesi katika idara hii ambayo imeonekana kupwaya tangu walivyoondoka Daniel Agger, Martin Skrtel na Sami Hyypia. “Virgil van Dijk is one of the best central defenders in the Premier League” haya ni maneno ya mshambuliaji wa zamani wa England na Southampton Matt Le Tissier wakati akizungumza na Sky Sport.

Liverpool inaweza kuwa na ukuta mgumu zaidi na endapo watafanikiwa kwa hili huenda ukame wa vikombe ukawa mwisho kwani idara ya ushambuliaji ya Liver ni hatari pengine kuliko timu yoyote pale London ukiacha Spurs. Van Daik kama wanavyotamka waholanzi anahitajika kwa udi na uvumba pale Anfield hasa kutokana na kutokuwepo kwa mabeki wengi sokoni katika kipindi hiki cha usajili ambacho kitafikia ukingoni ukingoni wiki kadhaa zijazo.

Mla Bata Pierre-Emerick Aubameyang pia amekuwa akihusishwa na kujiunga na Liverpool hasa baada ya Chelsea kujiondoa kwenye mbio. Mshambuliaji huyu ana kasi, anajua kupiga vyenga na uwezo wake wa kufunga ni mkubwa ila idara ya ushambuliaji ya Liver ipo vizuri sana chini ya Mane, Sallah, Firmino, Coutinho na bwana mdogo Dominick Solanke. Klopp ni kocha wa Liverpool aliyekabidhiwa mikoba na mashabiki na viongozi kwahiyo lazima ameona kitu cha ziada kutoka kwa Pierre.

Kutokana na staili ya ufundi ya ‘JK’ huenda akazidi kuikomalia saini ya mshambuliaji huyu ambaye ni Chotara wa Kifaransa. Upeo wangu mdogo wa uchambuzi unaona Pierre haitajiki sana Liverpool ila suala la ‘rotation’ huenda likanishawishi usajili huu ambao utawafanya Liver waonekane vidume baada ya kuburuzwa kwenye usajili mara kadhaa na vilabu vikubwa pale England. Aubameyang alisajiliwa na Klopp akitokea Saint-Étienne timu ambayo alifanya makubwa.

Miaka yake 28 inavifanya vilabu vingi vikubwa kujiondoa kwenye mbio za kumuwania licha kipaji cha kufunga. Liver wanayo nafasi kubwa ya kumsajili kwasababu kubwa mbili. Moja ni uwepo wa Mbape sokoni umeharibu soko la Aubameyang katika vilabu vikubwa Ulaya. Pili mahusiano mazuri ya Klopp na Mgabon huyu yanachagiza Pierr kwenda kuwasha moto licha ya pesa kubwa inayohitajika pale Dortmund ili kumng’oa mchezaji huyu.

Kutokana na idara hizi tatu kwenye kikosi cha Klopp, naweza kuandika kwa kujiamini kuwa Liverpool itakuwa timu hatari ambayo itafanya makubwa licha kutozungumzwa sana kama ilivyo kwa Man U, Man City na Chelsea ambao tumezoea kuwaona kwenye Kamera kila kukicha. Natamani kuwa mmoja wa watu watakaoshuhudia mechi za Liver hasa baada ya kukamilisha usajili wa wachezaji hawa ambao wapo sokoni kwa sasa na muelekeo wa kuwapata ni mkubwa.


Viewing all articles
Browse latest Browse all 676

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>