Quantcast
Channel: Makala – ShaffihDauda
Viewing all articles
Browse latest Browse all 676

FIFA na wanachama wake wakizingatia haya, ubaguzi tutausoma kwenye vitabu vya historia

$
0
0

Na Salym Juma, Arusha

Mshambuliaji bora kabisa Duniani kuwahi kutokea baada ya Pele, Diego Maradona amekaririwa akisema kuwa aliwahi kubaguliwa akiwa Napoli. Kumbuka huyu ni Mzungu ila amewahi kukutwa na tatizo hili ambalo linawaumiza sana watu wenye ngozi nyeusi. Sulley Muntari msimu uliopita alichukua maamuzi magumu ya kutoka nje ya uwanja baada ya kusikia kelele za ubaguzi kisa rangi yake. Urusi ni nchi itakayoandaa michuano ya Kombe la Dunia mwakani chini ya FIFA.

Matukio ya ubaguzi barani Ulaya yanazidi kushamiri licha ya kelele na adhabu mbalimbali kwa timu, wachezaji na mashabiki pale wanapokutwa na hatia. FIFA isipokuwa makini huenda mwakani watu weusi wakadhalilika hadharani kwani warusi sio watu wazuri kwa watu weusi na ushahidi wa hili wanafahamu akina Eto’e na Willian. Ili kuzika sakata hili la ubaguzi nazani FIFA na mashirikisho ya vyama vya soka yanapaswa kuwa ‘serious’ kupambana kwa vitendo juu ya suala hili.

September 2012 Chama cha Soka cha Uingereza kilimkuta na kashfa ya ubaguzi wa rangi aliyekuwa nahodha wa Chelsea John Terry. Terry alikutwa na hatia ya ubaguzi dhidi ya Anton Ferdinand katika mechi iliyowakutanisha Waingereza hawa iliyochezwa October 2011.  Baada ya hatia hii Terry alifungiwa mechi 4 na kupigwa faini ya pound 220,000. Mfano wa adhabu hii ni nyepesi mno kwani pesa sio tatizo kwa wazungu ila kurefusha kifungo ni jambo ambalo litaiathiri klabu na mchezaji pia.

Kifungo kirefu alichopewa mshambuliaji wa Barcelona Luis Suarez baada ya kumng’ata Giorgio Chiellini ni mfano wa adhabu sahihi ambazo zinapaswa kuhamia kwenye suala la ubaguzi wa rangi. Miezi 4 aliyofungiwa Suarez ni kipimo kizuri cha mchezaji kujifunza kwani ni rahisi kiwango cha mchezaji kudorora au hata timu husika kuathirika. Urefu wa kifungo utavifanya vilabu, mashabiki na wachezaji wawe makini au kuacha kabisa suala la ubaguzi.

Waamuzi wapewe nguvu uwanjani. Nilifurahishwa na michuano ya mabara iliyofanyika Urusi kwani marefa walipewa mamlaka ya kuahirisha mechi endapo ubaguzi ungetokea. Urusi ni moja ya nchi zinazosifika kwa ubaguzi wa rangi na hili FIFA waliliona mapema na walifanikiwa kwa kiwango kikubwa katika hili. Endapo mchezaji au mashabiki wakitoa ishara ya ubaguzi basi mwamuzi anatakiwa aahirishe mchezo husika bila kujali matokeo au dakika tukio lilipotokea.

Uamuzi huu utawafanya mashabiki wawe na nidhamu kwani mpira ni starehe ambayo watu huenda kujumuika na familia zao, hivyo linapokuaja suala la mpuuzi mmoja au kikundi fulani kuwasitishia starehe itawauma na timu pia zitapata hasara kwa mechi kusitishwa. Muntari aliwahi kutoka uwanjani kutokana na kubaguliwa ila mwamuzi hakuonesha ushirikiano katika mechi ile. Jambo hili pia litainufaisha FIFA katika michuano ya Kombe la Dunia mwakani.

Vyama vya soka kuwa mfano katika mapambano haya. “Sikuwahi kusikia kitu kama hicho nchini England kwasababu kitendo hiki hakivumiliki pale England” haya ni maneno ya Sulleh Muntari mara baada ya kubaguliwa. England ni taifa lenye ligi maarufu na wachezaji wengi wenye asili ya Kiafrika wanacheza pale ila matukio ya mashabiki kubagua watu weusi ni mara chache sana kutokea. FA ipo ‘serious’ kiasi fulani katika masuala ya kibaguzi endapo mchezaji/shabiki akikutwa na hatia.

John Terry na Luis Suarez wamewahi kukutwa na hatia katika suala la ubaguzi wakafungiwa na kutozwa faini pia. Mikel Obi aliwahi kumshutumu mwamuzi kuwa amembagua kwenye mchezo dhidi ya United ila baadae FA ilichunguza na kugundua Mikel hakubaguliwa na hivyo rungu kumgeukia Mnigeria huyu. Sijui ni kwasababu ya kuwepo kwa wachezaji wengi weusi ndani kikosi cha timu ya taifa ya England au laah ila FA inapaswa kuigwa na vyama vingine Barani Ulaya.

Timu zicheze bila mashabiki uwanjani. Inawezekana hii ni miongoni mwa sababu itakayosaidia kutokomeza suala hili kwani mashibiki ni watu wenye nguvu ya kubadilisha matokeo na kuna msemo wa soka kwamba shabiki ni mchezaji wa 12. Kufungiwa kwa mashabiki kutarudisha heshima kwani ubaguzi mara nyingi huanzia majukwaani na mara chache wachezaji wamekuwa wakibaguana wao kwa kwa wao. Suala hili linatakiwa kuhimizwa na FIFA.

Timu kunyang’anywa pointi. Hakuna kitu kinachoumia mashabiki na wachezaji kama kupata matokeo uwanjani alafu baadae eti kisa mtu/kikundi mamlaka husika zinawanyang’anya pointi. Jambo hili litawafanya Wazungu wawe makini sana katika suala hili ambalo mara zote limekuwa likiwaandama watu wenye ngozi nyeusi. Endapo FIFA wapo ‘serious’ katika hili wao ndio wanatakiwa kutoa mwongozo kwenye Mashirikisho ya Soka Ulimwenguni hasa barani Asia na Ulaya.


Viewing all articles
Browse latest Browse all 676

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>