Na Athumani Adam
Si jambo rahisi kufunga mabao matatu kwenye mechi moja yaani hat- trick kwenye michuano migumu ya ligi ya mabingwa barani Ulaya. Kuthibitisha hilo mshambuliaji wa Arsenal Lucas Perez amekuwa mchezaji wa sita kwa upande wa Arsenal kuingia kwenye orodha ya wachezaji ambao wamewahi kuifungia timu hiyo mabao matatu.
Perez aliisaidia kuivusha timu yake kuingia hatua ya 16 bora baada ya kuifungia mabao matatu kwenye ushindi wa 4-1 ugenini dhidi ya klabu ya FC Basel ya Uswisi. Ushindi huo umeifanya Arsenal kumaliza nafasi ya kwanza kwenye Kundi A wakiwa na pointi 14 huku PSG ikiwa nafasi ya pili na pointi 12.
Ukiachana na Lucas Perez ambaye jana aliondoka na mpira kule Uswisi, makala hii inakupa wachezaji wengine sita ambao wamewahi kuondoka na mpira kwa kufunga hat-trick kwenye michuano ya ligi ya mabingwa Ulaya.
Thiery Henry vs As Roma, November 2002
Ilikuwa kwenye uwanja wa Stadio Olimpico kule jijini Roma, siku hiyo wenyeji timu ya As Roma walipata goli la kuongoza kupitia kwa Antonio Cassano. Lakini hat-trick ya Thiery Henry usiku huo ilitosha kupindua matokeo na Arsenal kuibuka na ushindi wa 3-1 kwenye mchezo wa Kundi B.
Nicklas Bendtner vs Fc Porto, March 2010
Arsenal ilikuwa kwenye wakati mgumu baada ya kupoteza mechi ya kwanza nyumbani hatua ya 16 ligi ya mabingwa Ulaya kwa mabao 2-1 dhidi ya Porto ya Ureno. Kwenye mechi ya marudiano Porto hawakuamini kilichotokea pale walipopokea kipigo cha mabao 5-0 wakiwa nyumbani. Mshambuliaji wa Arsenal Nicklas Bendtner alifunga hat-trick usiku huo.
Danny Welbeck vs Galatasaray, October 2014
Kwenye uwanja wa Emirates mshambuliaji Danny Welbeck alitoa zawadi kwa kocha Arsenal Wenger ya kusherekea miaka 18 tangu ajiunge na klabu hiyo mwaka 1996. Kwenye ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya Galatasaray, Danny Welbeck alifanikiwa kufunga matatu peke yake.
Giroud vs Olympiacos , December 2015
Arsenal ilihitaji Ushindi wowote isipokuwa matokeo ya 1-0 au 2-1 ili kusonga mbele kwenye hatua ya 16 bora michunao ya mabingwa Ulaya kwa msimu huo. Alikuwa ni Oliver Giroud ambaye aliibuka shujaa pale alipofunga matatu pekee yake kwenye ushindi wa 3-0.
Mesut Ozil vs Ludogorets, 2016
Hii ni hat-trick ya kwanza kwa msimu huu wa michuano ya ligi ya mabingwa Ulaya. Timu ya Ludogorates ambayo ipo Kundi A sambamba na Arsenal walikubali kupoteza kwa mabao 3-2 nyumbani dhidi ya Arsenal. Shukrani kwa Ozil ambaye aliifungia Arsenal mabao yote.
Kumbuka Arsenal ipo sawa na klabu ya Manchester United kwa kufunga hat-trick kwenye michuano ya ligi ya mabingwa Ulaya. Hadi sasa timu zote zimefanikiwa kuandika historia kufunga hat-trick sita kwenye michuano hiyo mikubwa kwa upande wa vilabu kwa bara la Ulaya.