Moja ya mechi kubwa katika ulimwengu wa soka inachukua nafasi yake leo usiku katika uwanja wa Camp Nou – mabingwa watetezi wa La Liga FC Barcelona wataikaribisha Atletico Madrid.
Kiuhalisia pambano hili litaamriwa na sehemu ya mashambulizi – MSN vs Vijana wa kifaransa Antoine Griezmann na Kevin Gameiro, ambao watakuwa wakipewa sapoti na Mkongwe Fernando Torres.
Kabla ya kuingia dimbani usiku wa leo tuangalie takwimu za safu hizi mbili katika michezo iliyowakutanisha miamba hii.
Mhispaniola huyu anaingia uwanjani akiwa na magoli 11 dhidi ya Blaugrana. Torres anaingia uwanjani leo akiwa na magoli mawili ya dakika za mwisho vs Gijon. Kurudia kile alichokifanya dhidi ya Barcelona mwaka 2006 ni jambo analolipa kipaumbele usiku wa leo.
Antonie Griezmann
Mshambuliaji huyu wa kifaransa aliwanyoosha Barca hivi karibuni – kwenye mchezo wa Champions League msimu uliopita, atakuwa anaingia kwenye mchezo wa leo akiwa ametoka kupiga goli mbili vs Real Sociedad wikiendi iliyopita.
Baada ya kuondoka Sevilla, Gameiro sasa anaitumikia safu ya ushambuliaji ya Atletico. Ameshaifunga Barcelona magoli mawili katika sare ya 2-2 akiwa Sevilla miaka kadhaa iliyopita, pia aliwatungua katika 2015 UEFA Super Cup.
Leo Messi
Lionel Messi ana wastani wa goli moja kwa kila mchezo vs Atletico tangu alipoanza kuwatungua katika mchezo wa ushindi wa 6-0 msimu wa 2006/07, Kiujumla Messi amefunga magoli 21 katika michezo 20 aliyokutana na Los Rojiblancos.
Neymar
Kijana huyu mwenye umri wa miaka 24 alishawatungua Atletico kwa goli la ushindi katika mchezo wa 2013 Supercopa de Espana, na msimu uliopita aliifungia Barca goli lingine la ushindi katika mchezo wa La Liga ambao uliisha kwa 2-1 katika dimba la Estadio Vicente Calderon.
Luis Suarez
Hakuna ubishi kwamba Luis Suarez amekuwa tegemeo sana katika ufungaji kwenye kikosi cha Blaugrana. Msimu uliopita katika mchezo wa robo fainali wa Champions League.