Mchezo wa soka haukwemo kwenye mashindano haya mara mbili tu, mwaka 1896 na 1932.
Kuelekea mashindano ya Olympic ya mwaka huu vifuatavyo ndio vitu unavyopaswa kujua kuhusu mchezo wa soka katika Rio Olympic Games.
4-20 huku kukiwa na mataifa 16 yaliyogawanywa katika makundi manne. Timu mbili za juu kwenye kila kundi zikienda kwenye hatua ya mtoano. Kwa upande wa wanawake kuna jumla ya timu 12 na hivyo wanaunda makundi 3 ya timu 4 kila kundi, timu 6 zinafuzu moja kwa moja – mbili kutoka kwenye kila kundi, pia best losers wawili wanaungana na timu sita kwenda robo fainali.
Mfumo wa mashindano haya pia unatoa nafasi ya kupatikana kwa mshindi wa 3 ambaye huenda kubeba medali ya shaba kwa upande wa wanawake na wanaume.
Maracanã
Fainali kwa upande wa wanaume ya kutafuta mshindi wa medali ya dhahabu itachezwa katika dimba la kihistoria la Maracana. Kwa wenyeji Brazil, wameshashinda ubingwa wa America ya Kusini mara 8, ubingwa wa dunia mara 5, Medali ya dhahabu ya Olympic ndio ambayo imekosekana kwenye mafanikio ya Selecao.
Wameshashinda medali ya silver mara 3 wakiwa na vizazi vya akina Ronaldo, Ronaldinho na Neymar..
Mshambuliaji wa Barcelona Neymar — ambaye hakushiriki kwenye Copa America mwezi June — anarejea kuongoza kikosi imara cha Brazil kujaribu kuvunja mwiko wao kutopata mafanikio katika Olympic japo watakabiliwa na ushindani wa vikosi kama vya Ujerumani na Argentina.
Neymar
Neymar atakuwa miongoni mwa wachezaji watatu wenye umri zaidi ya miaka 23 wanaoruhusiwa kushiriki. Kizingiti cha umri kilianza kutumika mwaka 1992 katika michuano iliyofanyika Barcelona na ilikuwa ni muafaka uliofikiwa baina ya FIFA na Kamati ya Olimpiki (IOC) ili kuwaruhusu wanasoka kushiriki michuano hiyo bila kuathiri mashindano ya FIFA ya kombe la dunia.
Lionel Messi alishinda medali yake ya dhahabu pekee akiwa na Argentina katika michezo iliyofanyika Beijing 2008, wakati Cristiano Ronaldo aliiwakilisha nchi yake mwaka 2004 jijini Athens.
Sheria ya katazo la umri ipo kwa upande wa mashindano ya wanaume tu, timu za wanawake hushirikisha vikosi kamili.
Viwanja
Viwanja vingi vilivyotumika katika kombe la dunia miaka miwili iliyopita ndivyo vitakavyotumika kwa mechi za pande zote mbili za wanawake na wanaume.
Maracanã — utatumika katika mechi za fainali zote za wanawake na wanaume, viwanja vingine vitakavyotumika ni Sao Paulo, Brasilia, Salvador, Belo Horizonte na Manaus, ambacho kipo karibu kilomita 3,000 kutoka Rio ndani ya misitu ya Amazon.
Mashindano ya muda mrefu zaidi ya World Cup
Ingawa sio mashindano makubwa zaidi kwa upande wa soka, lakini soka imekuwa mojawapo ya michezo katika Olimpiki tangu mwaka 1896 na 1932. Mara ya kwanza ilikuwa kabla ya kombe la dunia la kwanza na mabadiliko ya kanuni kwa miaka yote kuliruhusu kupatikana mabingwa wa tofauti.
Timu 18 za mataifa tofauti zimeshashinda medali ya dhahabu – Hungary na Great Britain wakiongoza kwa kushinda mara 3 kila timu.
Kwa mara ya kwanza soka la wanawake lilianza kwenye mashindano ya Olimpiki mnamo mwaka 1996 na tangu wakati huo yamekuwa yakitawaliwa na Marekani, ambao wameshashinda mara 4 medali za dhahabu na medali moja ya Silva.