Quantcast
Channel: Makala – ShaffihDauda
Viewing all articles
Browse latest Browse all 676

‘MECHI 3 YANGA SC WEWE BADO UNAMSUBIRIA TU OBREY CHIRWA?’

$
0
0

IMG_0207

Na Baraka Mbolembole

LICHA ya kusajili kwa matarajio makubwa katika klabu ya Yanga SC akitokea FC Platnum ya Zimbabwe, kiungo-mshambulizi raia wa Zambia, Obrey Chirwa ni kama tayari ‘amejiweka’ katika presha kubwa. Niliwahi kuzungumzia tofauti zilizopata kutokea kati ya washambuliaji wawili wa Yanga, Mzimbabwe, Donald Ngoma na raia wa Burundi, Amis Tambwe.

Kuanza kukosa umoja na upendo kwa wachezaji hao waliofunga jumla ya magoli 38 katika ligi kuu msimu uliopita upande wangu nilichukulia/nitaendelea kuamini ni tatizo jipya katika timu hiyo kwa maana Ngoma alimwambia Tambwe, ‘Muda wako wa kutamba umekwisha.’

Hii ni kauli inayoweza kuchukuliwa ni ya kawaida lakini kiukweli ni ‘wivu’ ambao tayari Ngoma ameuonyesha kutokana na mafanikio ya Tambwe msimu uliopita ambao alikuwa ni mfungaji bora wa ligi kuu na klabu yake.

Ngoma alikuwa akimpigia debe Chirwa na kumuona ni mtu mwenye thamani kwake zaidi ya Tambwe. Inashangaza sana, kwa maana mshambulizi huyo wa Zimbabwe alitaja jina la Chirwa katika ugomvi wake na Tambwe kule Uturuki walipokuwa katika kambi ya maandalizi kabla ya kuwavaa TP Mazembe katika game yao ya pili katika Confederation Cup 2016.

Kuhusika kwa jina la Chirwa katika ugomvi wa Ngoma na Tambwe hakukuonekana tatizo kwa Mzambia huyo na aliendelea kuonekana kama ‘matarajio makubwa’ ya Yanga katika michuano ya Caf kwa maana Tambwe hajapata kufunga hata goli tangu kuanza kwa michuano ya Caf msimu huu. Presha bila shaka ilikuwa kubwa sana.

Yanga iliyokosa makali Caf ilianza hatua ya makundi kwa kipigo cha 1-0 kutoka kwa MO Bejaia ya Algeria (ugenini,) ikafuatia na kipigo kingine kama hicho kutoka kwa Mazembe (nyumbani,) kabla ya kuongeza ubora kidogo na kufunga goli lao la kwanza katika hatua hiyo walipotoka sare ya kufungana 1-1 nyumbani na Medeama SC ya Ghana.

Jana wakapigwa kipigo kikubwa cha kwanza katika michuano ya Caf tangu walipofungwa 3-0 na Al Ahly ya Misri mwaka 2009.

Katika game zote 3 za mwisho za mabingwa wa Tanzania Bara (Yanga 0-1 Mazembe, Yanga 1-1 Medeama, Medeama 3-1 Yanga, Chirwa alikuwa ‘mtu wa mashabiki’ wa Yanga na baada ya dakika zake 71′ vs TP Mazembe, jina la Chirwa ‘halikubanduka’ midomoni mwetu.

Mshambuliaji aliyesajiliwa kwa zaidi ya milioni 200, tena akiwa na miaka 22 tu ameonekana ‘kupwaya’ hata alipoonekana kugusa tu mpira! Mzee Akilimali ambaye sidhani kama ni mtaalamu sana wa ufundi yeye hakuwa na subira.

Alisema wazi ‘Chirwa anaruka ruka tu uwanjani.’ Nilitaraji kumwona ‘kiboko wa Tambwe’ na pengine ‘Chirwa halisi akiibeba Yanga katika mchezo dhidi ya Medeama, lakini kilichotokea ni kushuhudia kiwango kingine cha kufadhaisha wakati mchezaji huyo aliposhindwa kufunga katika moja ya nafasi za wazi.

Inawezekana mchezaji huyo anahitaji muda zaidi kama wanavyoamini wakufunzi wa timu hiyo, lakini katika hali halisi ni wazi game zake mbili alizopangwa sambamba na Ngoma katika safu ya mashambulizi zimetoa mwelekeo kuwa mshambulizi huyo ana kazi kubwa sana ya kuthibitisha thamani yake.

Tambwe ni presha yake ya kwanza, mashabiki wasio wavumilivu walichangia kushindwa kutulia kwa Mbrazil, Geilson Santos ‘Jaja.’ Chirwa apambane hasa na kufunga magoli zaidi ya Amis Tambwe vinginevyo, huyu jamaa ni ‘gharasa ghali zaidi katika kandanda la Tanzania.’ ‘Mechi 3 Yanga SC wewe bado unamsubiria tu Obrey Chirwa?’

Kwa ukaribu zaidi, tafadhali unaweza ku-LIKE PAGE yangu #BSports. Utapata Updates za michuano mbalimbali.


Viewing all articles
Browse latest Browse all 676

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>